Hadithi za Maandiko
Yesu Anarudi kwa Baba Yake


“Yesu Anarudi kwa Baba Yake,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

3 Nefi 28; 4 Nefi 1

2:38

Yesu Anarudi kwa Baba Yake

Akiwahudumia wanafunzi Wake kabla ya kuondoka

Yesu Kristo anazungumza na kundi la watu

Yesu alikuwa amewafundisha watu injili Yake. Alikuwa amewafundisha kumpenda Mungu na kutumikiana. Punde, Yesu angerudi kwa Baba Yake. Aliwaomba wanafunzi kuendelea kuwafundisha watu baada ya Yeye kuondoka.

3 Nefi 11:41; 28:1

Yesu Kristo anatabasamu na kuinua mkono Wake

Kabla ya kuondoka, Yesu aliwauliza kila mmoja wa wanafunzi Wake kile ambacho wangependa Yeye awafanyie. Wengi wa wanafunzi walisema walitaka kuishi na Yesu baada ya kumaliza kumtumikia duniani. Yesu aliwapa ahadi kwamba wangeishi pamoja Naye baada ya kufa.

3 Nefi 28:1–3

wanafunzi watatu wanaonekana kuwa na wasiwasi

Watatu kati ya wanafunzi walikuwa na huzuni kwa sababu walikuwa na wasiwasi sana kumwambia Yesu kile walichotaka. Lakini Yesu alijua kile walichotaka kutoka Kwake. Walitaka kuishi mpaka Ujio wa Pili wa Mwokozi ili waweze kuwasaidia watu zaidi kuja kwa Yesu.

3 Nefi 28:4–7, 9

Yesu Kristo anazungumza na wanafunzi watatu

Yesu aliwapa ahadi kwamba hawangekufa. Wangebaki duniani na kuwasaidia watu kuja Kwake hadi Ujio Wake wa Pili.

3 Nefi 28:7–11

Yesu Kristo anainuka juu hewani na anazungukwa na nuru

Yesu alimgusa kila mwanafunzi kwa kidole Chake isipokuwa wale watatu waliotaka kubakia. Kisha Yesu akaondoka na kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

3 Nefi 28:1, 12

wanafunzi watatu wanatabasamu na kung’aa kidogo

Baada ya hili, mbingu zilifunguka na wanafunzi watatu wakatwaliwa juu mbinguni. Waliona na kusikia vitu vingi vya kushangaza na waliambiwa wasizungumzie kuvihusu. Miili yao pia ilibadilishwa ili wasife au kuhisi maumivu.

3 Nefi 28:13–15, 36–40

wanafunzi wanawabatiza watu

Wanafunzi walirudi na kuendelea kuwafundisha watu kuhusu Yesu. Watu walitaka kumfuata Yesu na walibatizwa katika Kanisa Lake. Upendo wa Mungu ulikuwa mioyoni mwao, na walishiriki kila kitu walichokuwa nacho kwa kila mmoja wao. Walikuwa na furaha, na Mungu aliwabariki. Kila mmoja aliishi katika amani kwa takribani miaka 200.

3 Nefi 28:16–18, 23; 4 Nefi 1:1–23