Hadithi za Maandiko
Yaredi na Familia Yake


“Yaredi na Familia Yake,” Hadithi za Kitabu cha Mormoni (2023)

Etheri 1–46

Yaredi na Familia Yake

Safari iliongozwa na Bwana

Mnara unajengwa, na Yaredi na kaka yake wanawatazama watu karibu nao wakibishana.

Yaredi na familia yake waliishi katika Babeli maelfu ya miaka kabla Yesu hajazaliwa. Walimtii Bwana. Lakini watu wengi katika Babeli hawakumtii Bwana. Watu wale walianza kujenga mnara ili kujaribu kufika mbinguni. Bwana alibadilisha lugha ya watu ili wasiweze kuelewana.

Mwanzo 11:4–9; Etheri 1:33

kaka wa Yaredi anasali, na Yaredi anaangalia mji

Yaredi alikuwa na kaka. Bwana alimwamini kaka yake Yaredi. Yaredi alimuomba kaka yake asali kwa Bwana kwa ajili ya msaada. Katika sala yake, kaka wa Yaredi alimwomba Bwana asibadili lugha ya familia yake na marafiki. Kwa njia hiyo bado wangeweza kuelewana.

Etheri 1:33–36

Yaredi na kaka yake wanazungumza na familia zao

Bwana alikuwa mwenye upendo na mkarimu. Hakubadilisha lugha ya familia na marafiki wa Yaredi. Baadaye, Bwana alimwambia kaka wa Yaredi kwamba Alikuwa ametayarisha nchi maalumu kwa ajili yao. Bwana alisema angewaongoza huko.

Etheri 1:35–42

Yaredi, kaka yake, na familia zao wanaondoka kwenye mji, na kuchukua wanyama wengi pamoja nao

Yaredi na kaka yake walikusanya familia na marafiki zao. Pia walikusanya wanyama wao na kila aina ya mbegu. Kisha waliacha nyumba zao na kusafiri kupitia nyikani. Bwana aliwaongoza kwa kuzungumza nao kutoka kwenye wingu.

Etheri 1:40–43; 2:1–6

familia zikiwasili baharini

Baada ya kusafiri kwa muda mrefu, walifika baharini. Waliishi kwenye ufuko kwa miaka minne. Kwa muda mrefu, kaka wa Yaredi hakusali kwa Bwana.

Etheri 2:13–14

kaka wa Yaredi anasali

Bwana alimwambia kaka wa Yaredi kusali tena. Kaka wa Yaredi alitubu na alisali kwa Bwana. Bwana alimsamehe.

Etheri 2:14–15

kaka wa Yaredi akitengeneza merikebu ndogo

Bwana alimfundisha kaka wa Yaredi kutengeneza merikebu zilizoitwa mashua. Familia zingeweza kutumia mashua kuvuka bahari hadi nchi ya ahadi.

Etheri 2:15–17

kaka wa Yaredi akiangalia mashua, hema, na bahari

Kaka wa Yaredi na familia yake walitengeneza mashua. Aliona kwamba hakukuwa na mwanga ndani ya mashua. Alimuuliza Bwana kama wangelazimika kusafiri kuvuka bahari gizani. Bwana alimwambia kaka wa Yaredi afikirie njia ya merikebu kuwa na nuru.

Etheri 2:16–19; 22–25

Yesu Kristo anaonekana kidogo, na mkono Wake ukinyooshwa kugusa mawe katika mikono ya kaka wa Yaredi

Kaka wa Yaredi alichonga mawe madogo 16 yanayoakisi mwanga. Alimwomba Bwana ayaguse na kuyafanya yang’ae. Bwana alinyoosha mkono Wake na kugusa mawe moja baada ya jingine kwa kidole Chake. Kaka wa Yaredi aliweza kuona kidole cha Bwana. Alishangazwa kwamba Bwana alikuwa na mwili kama wa kwake.

Etheri 3:1-8

Yesu Kristo anazungumza na kaka wa Yaredi

Bwana alisema kwamba kaka wa Yaredi alikuwa na imani kubwa. Kisha Bwana akatokea na kuonyesha mwili Wake wa kiroho kwa kaka wa Yaredi. Bwana alisema, “Mimi ni Yesu Kristo.” Alisema kwamba Alichaguliwa kuwa Mwokozi. Alimfundisha kaka wa Yaredi vitu vingine vingi.

Etheri 3:9–20, 25–27

kaka wa Yaredi anaandika, na mawe yakiwa kwenye bakuli lililofunikwa karibu naye

Kaka wa Yaredi alirudi kwa familia yake na marafiki. Aliandika kile alichojifunza alipokuwa pamoja na Bwana. Pia aliweka mawe kwenye mashua. Sasa walikuwa na nuru kwa ajili ya safari yao.

Etheri 4:1; 6:2–3

mashua zikisafiri kwenye bahari yenye dhoruba

Familia ziliingia ndani ya mashua ili kuvuka bahari. Walimwamini Bwana kuwalinda. Kulikuwa na dhoruba nyingi na mawimbi. Wakati mwingine, maji yalifunika mashua kabisa. Lakini walisali, na Bwana akawarudisha juu ya maji tena. Waliimba nyimbo nyingi za shukrani kwa Bwana.

Etheri 6:4–10

Yaredi, kaka yake, na familia zao wanawasili katika nchi mpya

Baada ya karibu mwaka mmoja, walifika nchi ambayo Bwana aliwaahidi. Walilia kwa shangwe na kumshukuru Yeye.

Etheri 6:11–12