Sura ya 37 Nefi na Lehi gerezani Nefi na Lehi walikuwa wana wa Helamani Helamani aliwataka wao kuwa wenye haki kama Lehi na Nefi ambao walitoka Yerusalemu. Helamani 5:4–7 Helamani aliwafundisha wanawe kuamini katika Yesu Kristo. Walijifunza kwamba msamaha huja kupitia imani na toba. Helamani 5:9–12 Nefi na Lehi walikwenda kufundisha neno la Mungu kwa Wanefi na Walamani. Maelfu ya watu walibatizwa. Helamani 5:14–19 Wakati Nefi na Lehi walipokwenda kwenye nchi ya Nefi, jeshi la Walamani liliwatupa gerezani na halikuwapa chakula kwa siku nyingi. Helaman 5:20–22 Walamani walikwenda gerezani kuwauwa Nefi na Lehi lakini hawakuweza kwa sababu walikuwa wamelindwa kwa uzio wa moto ambao ungemuunguza yoyote ambaye angejaribu kuwagusa. Helamani 5:22–23 Nefi na Lehi hawakuungua kwa moto. Waliwaambia Walamni kwamba nguvu za Mungu zilikuwa zinawalinda. Helamani 5:24–26 Ardhi na kuta za gereza zilianza kutikisika. Wingu jeusi liliwazunguka watu gerezani, na waliogopa. Helamani 5:27–28 Sauti kutoka juu ya giza iliongea. Ilikuwa ni ya ukimya kama mnong’ono, lakini kila mmoja aliisikia. Helamani 5:29–30 Sauti iliwaambia watu kutubu na kuacha kujaribu kuwauwa Nefi na Lehi. Helamani 5:29–30 Sauti ilinena mara tatu, na ardhi na kuta za gereza ziliendelea kutikisika. Walamani hawakuweza kukimbia kwa sababu ilikuwa giza sana na walikuwa wakiogopa sana. Helamani 5:33–34 Mnefi ambaye alikuwa ni muumini wa Kanisa aliona kwamba nyuso za Lehi na Nefi zilikuwa ziking’aa gizani. Helamani 5:35–36 Nefi na Lehi walikuwa wakitazama kuelekea mbinguni na kuongea. Muumini yule aliwaambia Walamani wawaangalie. Walishangaa Nefi na Lehi walikuwa wakiongea na nani. Helamani 5:36–38 Muumini yule aliyekuwa akiitwa Aminadabu, aliwaambia Walamani kwamba Nefi na Lehi walikuwa wakiongea na malaika. Helamani 5:39 Walamani walimuuliza aminadabu ni kwa jinsi gani wangeweza kuondoa giza. Aliwaambia watubu na kusali mpaka wawe na imani katika Yesu Kristo. Helamani 5:40–41 Walamani walisali mpaka wingu la giza likaondoka. Helamani 5:42 Wakati giza lilipoondoka, watu waliona nguzo ya moto ikiwazunguka. Moto haukuwaunguza au kuunguza kuta za gereza. Helamani 5:43–44 Walamani walihisi shangwe kuu, na Roho wa Mungu aliijaza mioyo yao. Helamani 5:44–45 Sauti ilinong’ona, ikisema wangefarijiwa kwa sababu ya imani yao katika Yesu Kristo. Helamani 5:46–47 Walamani waliangalia juu kuona wapi sauti ilitokea. Waliwaona malaika wakishuka chini kutoka mbinguni. Helamani 5:48 Karibu watu 300 waliona na kusikia kile kilichotokea gerezani. Walikwenda na kuwaambia wengine. Helamani 5:49–50 Wengi wa Walamani waliwaamini na wakatupa silaha zao za kivita. Helamani 5:50–51 Walamani waliacha kuwachukia Wanefi na kuwarudishia ardhi yao waliyokuwa wameichukua. Walamani wakawa wenye haki zaidi kuliko Wanefi. Helamani 5:50, 52 Walamani wengi walikwenda na Nefi na Lehi na kufundisha wote Wanefi na Walamani. Helamani 6:1, 6–7