Sura ya 48 Amani katika Amerika Baada ya Yesu kurejea mbinguni, wanafunzi Wake walianzisha Kanisa Lake nchini kote. 4 Nefi 1:1 Watu waliotubu dhambi zao walibatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. 4 Nefi 1:1 Punde Wanefi wote na Walamani waliongoka. Hawakubishana na kila mmoja wao alikuwa mkweli. 4 Nefi 1:2 Hakukuwa na tajiri wala masikini. Watu walishiriki kila kitu, na wote walikuwa na vile walivyohitaji. 4 Nefi 1:3 Wanafunzi walifanya miujiza mingi katika jina la Yesu Kristo. Waliponya wagonjwa na kuwarudishia uhai waliokufa. 4 Nefi 1:5 Watu walijenga miji mipya mahali ambapo mingine ilikuwa imeharibiwa. 4 Nefi 1:7 Walitii amri za Mungu. Walifunga na kusali na kukutana pamoja mara kwa mara kusikia neno la Mungu. 4 Nefi 1:12 Watu walikuwa na furaha. 4 Nefi 1:16 Hapakuwa na wanyang’anyi, waongo, wauaji. Watu hawakuwa tena wamegawanyika katika Wanefi na Walamani lakini wote walikuwa wamoja, watoto wa Kristo. 4 Nefi 1:16–17 Bwana aliwabariki watu katika kila kitu walichofanya. 4 Nefi 1:18 Waliishi kwa amani kwa miaka 200. Watu walikuwa matajiri sana. 4 Nefi 1:22–23