Njoo, Unifuate
Juni 10–16: “Je, Mmeshuhudia Mabadiliko Haya Makuu Katika Mioyo Yenu?” Alma 5–7


“Juni 10–16: ‘Je, Mmeshuhudia Mabadiliko Haya Makuu Katika Mioyo Yenu?’ Alma 5–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)

“Juni 10–16. Alma 5–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)

Alma Mdogo akiwafundisha Wazoramu

Alma Mdogo akiwafundisha Wazoramu

Juni 10–16: “Je, Mmeshuhudia Mabadiliko Haya Makuu Katika Mioyo Yenu?”

Alma 5–7

Alma hakujua kuhusu tiba ya upasuaji wa kisasa ili kuokoa maisha kwa kupandikiza moyo, ambapo unabadili moyo ulioharibika au uliougua na kuwekewa ule ulio na afya nzuri. Lakini alijua kuhusu muujiza mkubwa wa “mabadiliko ya moyo” (Alma 5:26)—ambapo Mwokozi anatupatia upya wa maisha ya kiroho, kama vile “kuzaliwa upya” (ona Alma 5:14, 49). Alma angeweza kuona kwamba mabadiliko haya ya moyo ndicho hasa Wanefi wengi walichokihitaji. Baadhi walikuwa matajiri na wengine masikini, baadhi walikuwa na kiburi na wengine walikuwa wanyenyekevu, baadhi yao wadhalimu na wengine waliteseka kwa mateso (ona Alma 4:6–15). Lakini wote walihitaji kuja kwa Yesu Kristo ili kuponywa—kama vile sote tunavyohitaji. Iwe tunatafuta kushinda kiburi au kuvumilia mateso, ujumbe wa Alma ni ule ule: “Njooni na msiogope” (Alma 7:15). Acha Mwokozi abadili moyo ulioshupazwa, wenye dhambi au uliojeruhiwa kuwa moyo mnyenyekevu, safi na mpya.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Alma 5:14–33

Ni lazima nihisi—na niendelee kuhisi—badiliko kuu la moyo.

Rais M. Russell Ballard alisema: “Ninahitaji mara kwa mara kuchukua muda kujiuliza, “ninaendeleaje?’ … Kama mwongozo kwangu wakati wa usaili huu binafsi, wa siri, ninapenda kusoma na kutafakari maneno ya kujichunguza yanayopatikana katika mlango wa tano wa Alma” (“Kurudi na Kupokea,” Liahona, Mei 2017, 64).

Fikiria kusoma Alma 5:14–33 kama vile unajifanyia usaili mwenyewe na kuuchunguza moyo wako. Unaweza kutaka kuandika majibu yako kwa maswali hayo. Je, unajifunza nini kuhusu wewe mwenyewe? Je, unahisi kushawishika kufanya nini baada ya usaili wako?

Ona pia Dale G. Renlund, “Preserving the Heart’s Mighty Change,” Liahona, Nov. 2009, 97–99.

msichana akiomba pembeni ya kitanda

Tunapomgeukia Mungu, tunaweza kupata uzoefu wa “mabadiliko ya moyo.”

Alma 5:44–51

Ninaweza kupata ushahidi wangu mwenyewe juu ya Mwokozi na mafundisho Yake kupitia Roho Mtakatifu.

Katika Alma 5, wakati Alma alipoeleza jinsi alivyopata ushuhuda wake juu ya Mwokozi, hakutaja tukio lake la kumwona malaika (ona Mosia 27:10–17). Je, ni kwa namna gani Alma alikuja kujua ukweli yeye mwenyewe? Pengine ungeweza kutumia kile unachokipata kwenye Alma 5:44–51 kuandika “maelezo ya upishi” kwa ajili ya kupokea ushuhuda juu ya Yesu Kristo na mafundisho Yake. Je, ni “vitu gani” (kweli za injili) na “maelekezo” (vitu tunavyoweza kufanya kutafuta ukweli) ambavyo Alma alivijumuisha? Ni “vitu” gani na “maelekezo gani” wangeweza kuongeza kwenye maelezo yao ya upishi kutoka kwenye uzoefu wao wenyewe au uzoefu mwingine katika maandiko?

Alma 7

“Ninaona kwamba mko katika njia za haki”

Wakati mwingine tunakuwa kama watu wa Zarahemla, ambao walihitaji kuitwa kwenye toba (ona Alma 5:32). Wakati mwingine tu zaidi kama watu wa Gideoni, ambao walikuwa wakijaribu kutembea “kwenye njia za haki” (Alma 7:19). Je unapata kipi kutoka katika ujumbe wa Alma huko Gideoni (katika Alma 7) ambacho ni sawa na kile alichokisema huko Zarahemla (katika Alma 5)? Je, ni tofauti zipi unaziona? Tafuta vitu alivyovifundisha Alma ambavyo vinaweza kukusaidia ubakie “kwenye njia ambayo inaelekea kwenye ufalme wa Mungu” (Alma 7:19).

ikoni ya seminari

Alma 7:7–16

Mwokozi alijichukulia juu Yake dhambi zangu, maumivu na mateso.

Je, umewahi kuhisi kwamba hakuna anayeelewa mapambano au changamoto zako? Kama ni hivyo, kweli alizofundisha Alma zinaweza kusaidia. Unaposoma, tafakari mistari hii inafundisha nini kuhusu lengo la dhabihu ya Mwokozi. Ungeweza kutengeneza chati yenye kichwa cha habari Ni nini Mwokozi aliteseka na Kwa nini Aliteseka na orodhesha kile unachokipata kwenye Alma 7:7–16 (ona pia Isaya 53:3–5). Je unaweza kufikiria nyakati maalumu Alipoteseka mambo haya? Hapa kuna baadhi ya mifano kutoka kwenye maandiko: Mathayo 4:1–13; 26:55–56; 27:39–44; Marko 14:43–46; Luka 9:58. Je, unaweza kuongeza chochote kwenye orodha yako kutoka kwenye mistari hii?

Ni jambo moja kuamini kwamba Mwokozi aliteseka kwa ajili yako. Lakini ni kwa namna gani mateso Yake yanaleta tofauti kwenye maisha yako ya kila siku? Hapa kuna baadhi ya maandiko ambayo yanaonesha jinsi gani Yesu Kristo anaweza kukusaidia au “kukuokoa”: Enoshi 1:5–6; Mosia 16:7–8; 21:15; 24:14–15; 3 Nefi 17:6–7; Etheri 12:27–29; Mafundisho na Maagano 121:7–10. Umejifunza nini kutoka kwenye mistari hii? Je, ni zipi baadhi ya njia zingine ambazo kwazo Yeye anakusaidia? Je, ni wakati gani umepata uzoefu wa usadizi Wake?

Wimbo kama “Ninakuhitaji” au “Najua Kristo Yu Hai” (Nyimbo za Dini, na. 47, 68) zingeweza kukuza shukrani zako kwa ajili ya Msaada wa Mwokozi. Ni vifungu gani vya maneno kwenye nyimbo hizi za dini vinaeleza hisia zako juu Yake?

Ona pia Mada za Injili, “Upatanisho wa Yesu Kristo,” Gospel Library; “His Grace” (video collection), Gospel Library.

Shuhudia juu ya Yesu Kristo. Fikiria njia unazoweza kushiriki ushuhuda wako juu ya Mwokozi na uungu Wake, rehema na upendo. Unaweza kuwahamasisha watu unaowafundisha washuhudie juu Yake kwa kuwauliza maswali ambayo yanawapa msukumo wa kushiriki ni kwa namna gani wao wanahisi kuhusu Yeye.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Alma 5:44–48

Ninaweza kupata ushuhuda wangu mwenyewe kupitia Roho Mtakatifu.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wajifunze kukuza shuhuda zao wenyewe, ungeweza kuwaonesha picha iliyo hapa chini na uwaulize jinsi tunavyoweza kuwasaidia watoto wa wanyama wakue. Kisha ungeweza kufananisha hili na kuzitunza shuhuda zetu. Je, ni matunzo yapi shuhuda zako zinayahitaji? Tunawezaje kujua kama zinakua?

    wavulana wawili pamoja na watoto wa wanyama

    Tunapoikubali injili, ni kama kuanza maisha mapya.

  • Je, Alma alipataje ushuhuda wake imara juu ya Yesu Kristo? Ungeweza kusoma Alma 5:44–46 pamoja na watoto wako ili kupata majibu ya swali hili. Pengine watoto wako wangeweza kuandika mpango wa kufanya jambo moja wiki hii ili kuimarisha shuhuda zao.

11:17

Nguzo na Miale

Mzee Dushku anatufundisha kwamba uzoefu wa kiroho wa kustaajabisha ni nadra na kwamba Bwana kwa kawaida anatupa sisi mwale mmoja wa nuru kwa wakati.

Alma 7:10–13

Mwokozi alijichukulia juu Yake dhambi zangu, maumivu na mateso.

  • Unawezaje kuwasaidia watoto wako waelewe Alma 7:10–13 ili kwamba waweze kujua kuwa Yesu Kristo anajali kuhusu wao na Anaweza kuwasaidia? Pengine ungeweza kuwaomba washiriki uzoefu wakati walipokuwa wakiumwa au walipokuwa na tatizo lingine lililowafanya wahisi huzuni. Je, ni jinsi gani wengine waliweza kuwafanya wahisi vizuri? Toa ushuhuda wako kwamba Mwokozi ameteseka mambo hayo pia, na zungumza kuhusu wakati ambapo Alikupa faraja na kukusaidia.

  • Wakati wewe na watoto wako mkisoma Alma 7:11–13, tafuteni vitu ambavyo Yesu Kristo aliteseka kwavyo. Waalike watoto watumie maneno na vifungu vya maneno wanavyovipata ili kukamilisha sentensi hii: “Yesu aliteseka ili aweze kunisaidia mimi.” Ni jinsi gani inatusaidia sisi kujua kwamba Yesu anaelewa masumbuko yetu? Je tunapokeaje msaada Wake? Shiriki ushuhuda wako juu ya Yesu Kristo.

Alma 5:14; 7:19–20

Kumfuata Yesu Kristo huniweka katika njia iliyonyooka ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

  • Waruhusu watoto wako waangalie kwenye kioo wakati ukisoma Alma 5:14 (ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Je, inamaanisha nini kupokea mfano wa Mwokozi katika nyuso zetu?

  • Unawezaje kutumia maelezo ya Alma ya njia ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni ili kuwasaidia watoto wako wajifunze kufanya chaguzi nzuri? Ungeweza kuwasomea Alma 7:19–20 na kisha waruhusu waigize wakitembea kwenye “njia isiyo nyoofu” na katika njia iliyo nyoofu Wasaidie wafikirie kuhusu chaguzi ambazo hutusaidia tubakie kwenye njia na chaguzi zingine ambazo hututoa kwenye njia. Mngeweza pia kuangalia picha za Yesu pamoja na mzungumze kuhusu vitu Alivyovifanya ili kutuonesha njia ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Wimbo kama “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79) ungeweza kutoa baadhi ya mawazo.

Kwa ajili ya mawazo zaidi ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Yesu akiwa amevaa joho jekundu

Mtetezi Wetu, na Jay Bryant Ward