“Januari 13–19: ‘Niliona Nguzo ya Mwanga’: Joseph Smith—Historia ya 1:1–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Joseph Smith—Historia ya 1:1–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Joseph Smith—Historia ya 1:1319: “Niliona Nguzo ya Mwanga”
Joseph Smith—Historia ya 1:1–26
Ungeweza kusema kwamba Mafundisho na Maagano ni kitabu cha majibu kwa sala: mengi ya mafunuo matakatifu katika kitabu hiki yalikuja kama majibu ya maswali. Swali ambalo lilianzisha haya yote—lile ambalo lilizua kumiminika kwa ufunuo wa siku za mwisho—liliulizwa na mvulana wa umri wa miaka 14. “Vita vya maneno na makelele ya maoni” (Joseph Smith—Historia ya 1:10) yalimwacha Joseph Smith achanganyikiwe kuhusu dini na uhusiano wake na Mungu. Labda unaweza ukahusisha na hilo. Tunapata migongano mingi ya mawazo na sauti za ushawishi katika siku yetu. Tunapotaka kuzichambua jumbe hizi na kupata ukweli, tunaweza kufanya kile ambacho Joseph alifanya. Tunaweza kuuliza maswali, kujifunza maandiko, kutafakari na hatimaye kumuuliza Mungu. Katika kujibu sala ya Joseph, nguzo ya mwanga ilishuka kutoka mbinguni. Mungu Baba na Yesu Kristo walimtokea na wakajibu maswali yake. Ushuhuda wa Joseph wa uzoefu ule wa kimiujiza kwa ujasiri unatangaza kwamba yeyote “ambaye [amepungukiwa] na hekima aombe dua kwa Mungu, naye atapewa” (Joseph Smith—Historia ya 1:26). Tunaweza wote kupokea, kama sio ono la kimbingu, angalau ono la wazi zaidi, lililoangazwa na nuru ya mbinguni.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Joseph Smith—Historia ya 1:5–26
Joseph Smith ni Nabii wa Urejesho.
Azma ya historia ya Joseph Smith ilikuwa kutuweka sisi “katika kuupata ukweli” kwa sababu ukweli kuhusu Joseph mara nyingi umepotoshwa (Joseph Smith—Historia ya 1:1). Unaposoma Joseph Smith—Historia ya 1:1–26, ni nini kinaimarisha ushuhuda wako wa wito wake mtakatifu?
Ona pia Watakatifu, 1:3–19.
Joseph Smith—Historia ya 1:5–25
Ninawezaje kupokea majibu ya sala zangu?
Je, Umewahi “kupungukiwa na hekima” au kuhisi kukanganyikiwa kuhusu uamuzi uliohitaji kufanya? (Joseph Smith—Historia ya 1:13). Uzoefu ambao Joseph Smith aliupata mnamo 1820 unaweza kutumika kama mpangilio mzuri kwako kwa ajili ya ufunuo binafsi. Kwa mfano, unapopekua Joseph Smith—Historia ya 1:1–25, tafuta matukio unayoweza kuhusisha na hilo? Unajifunza nini kuhusu:
-
Jinsi gani Joseph alivyojitayarisha kwa ajili ya jambo hili takatifu katika sala? (ona mstari wa 8, 11, 14–15).
-
Kazi ya kujifunza maandiko katika kutafuta ufunuo? (ona mstari wa 11–12).
-
Ni nini cha kufanya unapokabiliwa na upinzani? (ona mstari wa 15–16, 21–26).
-
Kukubali na kufanyia kazi majibu unayopokea? (ona mstari wa 18–25)
Ni umaizi gani wa ziada unaweza kuupata kutoka katika makala ya Rais HenryB. Erying “Ono la Kwanza: Mpangilio wa Ufunuo Binafsi”? Liahona, Nov. 2020, 12–17.
Ungeweza pia kutafuta mifano mingine katika maandiko juu ya watu wanaowasiliana na Mungu. Picha katika Kitabu cha Sanaa ya Injili au vitabu vingine vya Njoo, Unifuate vinaweza kukupa mawazo. Jaribu kujibu maswali yaliyoorodheshwa awali kwa kila mfano unaoupata. Ni uzoefu gani umekuwanao wa kupokea majibu ya sala? Unaweza kufanya nini ili kuwasaidia wengine kuwa na uzoefu mzuri pia?
Ona pia Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 88–92; Mada na Maswali, “Ufunuo Binafsi,” Maktaba ya Injili.
Joesph Smith—Historia ya 1:15–20
Joseph Smith alimuona Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo.
Joseph Smith aliamini kwamba Mungu angejibu sala yake, bali hakutarajia jinsi jibu lile lingebadili maisha yake—na ulimwengu. Unaposoma kuhusu tukio la Joseph, tafakari jinsi gani Ono la Kwanza lilivyobadili maisha yako.
Kwa mfano, Ono la Kwanza limefunua kweli kadhaa kuhusu Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo, ambazo zilikinzana na yale ambayo wengi katika siku za Joseph waliyaamini. Unaposoma Joseph Smith—Historia ya 1:15–20, kumbuka kuandika njia tofauti za kukamilisha maelezo kama mfano huu: “Kwa sababu Ono la Kwanza lilitokea, ninajua kwamba …”
Ni hisia gani unazo unapotafakari tukio la Joseph na kila kitu kilichotokana na tukio hilo?
Ona pia (video) ya “Ask of God: Joseph Smith’s First Vision” (video), Maktaba ya Injili; “Asubuhi Ile Njema,” Nyimbo za Dini, na. 15.
Joseph Smith—Historia ya 1:15–20
Kwa nini kuna simulizi tofauti za Ono la Kwanza?
Wakati wa uhai wake, Joseph Smith alirekodi uzoefu wake katika Kijisitu Kitakatifu takribani mara nne, mara kwa mara akitumia mwandishi. Kwa kuongezea, simulizi kadhaa ziliandikwa na watu wengine waliomsikia Joseph akizungumza kuhusu ono lake. Ingawa simulizi hizi zinatofautiana katika baadhi ya taarifa, kutegemeana na mwandishi, wasikilizaji na mpangilio, vinginevyo ziko sawa. Na kila simulizi inaongeza taarifa ambayo inatusaidia kuelewa vyema uzoefu wa Joseph Smith, sawa sawa na kila moja ya Injili nne zinavyotusaidia kuelewa vyema huduma ya Mwokozi.
Ona pia Mada na Maswali, “Simulizi za Ono la Kwanza,” Maktaba ya Injili.
Joseph Smith—Historia ya 1:21–26
Ninaweza kubaki mkweli kwa kile ninachokijua, hata kama wengine watanikataa.
Baada ya Ono lake la Kwanza lisilo na kifani Joseph Smith kwa kawaida alitaka kushiriki tukio hilo na watu wengine. Upinzani aliokabiliana nao ulimshangaza. Unaposoma simulizi yake, kitu gani kinakuvutia wewe kubaki mkweli kwenye ushuhuda wako? Ni mifano gani mingine—kutoka kwenye maandiko au mhenga, au watu unaowajua—inakupa ujasiri wa kubaki mkweli kwenye uzoefu wa kiroho ulio nao?
Ona pia Gary E. Stevenson, “Kulisha na Kutoa Ushuhuda Wako,” Liahona,Nov. 2022, 111-14
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Joseph Smith—Historia ya 1:3–14
Joseph Smith aliandaliwa kuwa nabii wa Mungu.
-
Kujifunza kuhusu ujana wa Joseph Smith kungeweza kuwasaidia watoto wako kujifananisha naye wanapojifunza kutokana na uzoefu wake. Pengine wangeshikilia picha ya Joseph Smith na kushiriki wanachojua kuhusu yeye. Kama inahitajika unaweza kuongezea baadhi ya kweli kuhusu yeye kutoka katika Joseph Smith—Historia ya 1:3–14 (ona pia “Sura ya 1: Joseph Smith and His Family,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 6–8, au video inayofanana nayo katika Maktaba ya Injili). Joseph alipata uzoefu gani ambao ulimwandaa yeye kuwa nabii? Ni kitu gani Mungu anatuandaa sisi kufanya?
Joseph Smith—Historia ya 1:10–13
Mungu anaweza kujibu maswali yangu kupitia maandiko.
-
Fikiria kuwaonyesha watoto wako aina mbalimbali ya vitabu, ikijumuisha maandiko. Wasaidie kufikiria maswali ambayo vitabu hivi vinaweza kuyajibu. Kisha mngeweza kusoma pamoja Joseph Smith—Historia ya 1:10–11 kutafuta ni maswali gani Joseph Smith alikuwa nayo na majibu gani aliyapata katika maandiko.
-
Watoto yawezekana wakaweza kupata maneno katika mstari wa 12 ambayo yanaelezea jinsi kusoma Yakobo 1:5 kulimwathiri Joseph. Kisha mngeweza kushiriki uzoefu na kila mmoja katika kifungu cha maandiko kilichokuwa na ushawishi wa nguvu kwenu. Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu kusoma maandiko, kama vile “Search, Ponder, and Pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,109). Je,wimbo unafundisha nini kuhusu kusoma maandiko?
Joseph Smith—Historia ya 1:10–17
Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zangu.
-
Ili kuanzia majadiliano kuhusu jinsi gani ya kuwasiliana na Baba wa Mbinguni, labda wewe au watoto wako wanaweza kuulizana maswali ukitumia mbinu mbalimbali za mawasiliano, kama kutuma ujumbe kwa simu, kupiga simu au barua ya kuandika kwa mkono. Ni kwa jinsi gani tunauliza maswali kwa Baba wa Mbinguni? Ni kwa jinsi gani tunamwonesha Yeye kwamba tunampenda na tunamheshimu katika sala zetu? Someni pamoja Joseph Smith–Histioria ya 1: 16–19 na jadilini jinsi gani Baba wa Mbinguni alijibu sala ya Joseph Smith. Wewe na watoto wako mngeweza kisha kushiriki uzoefu wakati mlipomwomba Mungu msaada na kupokea jibu.
Joseph Smith—Historia ya 1:17–19
Joseph Smith aliwaona Baba wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo.
-
Watoto wadogo wanaweza kufurahia kusimama mikono ikiwa imenyoshwa wakiifanya kuwa ni miti katika Kijisitu Kitakatifu wakati ukiwaambia kuhusu Ono la Kwanza. Waombe watoto wayumbe yumbe kama vile wanapulizwa na upepo wakati wewe ukizungumza kuhusu sala ya Joseph Smith. Kisha waambie wasimame wima na kimya wakati unawaambia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtokea Joseph Smith.
-
Watoto wakubwa wanaweza kufurahia kutumia picha moja au zaidi katika muhtasari huu kukuambia kile wanachojua kuhusu Ono la Kwanza. Wahimize kurejelea kwenye Joseph Smith—Historia ya 1:14–17 na kueleza mawazo yao na hisia kuhusu uzoefu wa Joseph (ona pia “Sura ya 2: Ono la Kwanza la Joseph Smith,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 9–12, au video inayofanana nayo katika Maktaba ya Injili).