Njoo, Unifuate
Januari 20–26: “Mioyo ya Watoto Itawageukia Baba Zao”: Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65


“Januari 20–26: ‘Mioyo ya Watoto Itawageukia Baba Zao’: Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Joseph Smith anapokea ono la malaika Moroni

Maelezo kutoka Aliniita Mimi kwa Jina, na Michael Malm

Januari 20–26: “Mioyo ya Watoto itawageukia Mababu Zao”

Mafundisho na Maagano 2; Joseph Smith—Historia ya 1:27–65

Ilikuwa miaka mitatu tangu Mungu Baba na Mwanawe, Yesu Kristo, walipomtokea Joseph Smith katika kijisitu, na Joseph hakuwa amepokea mafunuo yoyote ya ziada tangu hapo. Alianza kujiuliza pengine Bwana hakupendezwa naye. Kama sisi sote, alikuwa amefanya makosa, na alihisi kushutumiwa kwa hayo. Bado hata hivyo Mungu alikuwa na kazi ya kufanywa na yeye. Na kazi Joseph aliyoitwa kuifanya imeunganishwa na kile Mungu anachotaka kutoka kwetu. Joseph angeleta Kitabu cha Mormoni; sisi tumealikwa kushiriki ujumbe wake. Joseph angepokea funguo za ukuhani kuigeuza mioyo ya watoto kuwaelekea baba zao; tunaweza sasa kupokea ibada kwa niaba ya mababu zetu hekaluni. Joseph aliambiwa juu ya unabii ambao punde ungetimia; sisi tumeitwa kusaidia kutimiza unabii huu. Tunaposhiriki katika kazi ya Mungu, tunaweza kutegemea kukabiliana na upinzani na hata mateso, kama vile Nabii alivyofanya. Lakini tunaweza pia kuwa na imani kwamba Bwana atatufanya vyombo katika mikono Yake, kama vile Yeye alivyofanya kwa Joseph.

ona pia Saints, 1:20–48.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Joseph Smith—Historia ya 1:27–33

ikoni ya seminari
Mungu ana kazi ya Kufanywa na mimi.

Ni kitu kimoja kuamini kwamba Mungu alikuwa na kazi kwa ajili ya Joseph Smith kufanya—sisi tunaweza kutazama nyuma kwenye maisha yake na kwa uwazi kabisa tukaona kile alichokikamilisha. Umewahi kujifikiria kwamba Mungu anayo kazi kwa ajili yako pia? Unaposoma Joseph Smith—Historia ya 1:27–33, fikiria kuhusu kazi hiyo inaweza kuwa nini? Je, inachangiaje kwenye Urejesho wa injili ya Mwokozi unaoendelea?

Mzee Gary E. Stevenson alifundisha: “Tunapokuja kwa Kristo na kuwasaidia wengine kufanya vivyo hivyo, tunashiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa, ambayo inafokasi kwenye wajibu mtakatifu ulioteuliwa. … Majukumu haya ni rahisi, yenye mwongozo wa kiungu, yenye kuhamasisha, na yanayofanyika. Ni haya hapa:

Fikiria uzoefu ambao umekuwa nao wa kushiriki katika kila moja ya majukumu haya teule ya kiungu. Je, Mwokozi angekutaka ufanye nini tena? Kuna ukurasa wa Mada na Maswali kwa ajili ya kila moja ya majukumu haya (ona “Our Role in God’s Work of Salvation and Exaltation,” Maktaba ya Injili). Ungeweza kuchunguza kurasa hizi ili kukusaidia kujibu swali hili?

Yawezekana nyakati zingine ukahisi kama Bwana hawezi kukutumia kwa sababu ya makosa uliyofanya. Tunajifunza nini kutokana na uzoefu wa Joseph Smith katika Joseph Smith—Historia ya 1:28–29? Unawezaje kujua “msimamo wako mbele za [Mungu]”?

Uliza maswali yanayohimiza mjadala wenye tija. Maswali ambayo yana zaidi ya jibu moja sahihi huwaalika wanafunzi kujibu kulingana na mawazo, hisia na uzoefu wao binafsi. Maswali yaliyoko katika muhtasari huu ni mfano wa hili.

Ona pia “Youth Responsibility in the Work of Salvation” (video), ChurchofJesusChrist.org; “Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 1.2.

3:15

Youth Responsibility in the Work of Salvation

Elder Bednar wants the youth to recognize that recent adjustments to Young Women classes and Aaronic Priesthood quorums give them operational and executional responsibility in the work of salvation. When the youth are focused, miracles will come.

Joseph Smith—Historia ya 1:34–47

Kwa kurejesha injili Yake, Mwokozi alitimiza unabii wa kale.

Wakati Moroni alipomtokea Joseph Smith, alinukuu unabii wa Agano la Kale na Jipya, kama vile Isaya 11; Matendo 3:22–23; na Yoeli 2:28–32. Unaposoma Joseph Smith—Historia ya 1:34–47, fikiria kuhusu kwa nini unabii huu yawezekana ulikuwa muhimu kwa Joseph kuujua. Kwa nini ni muhimu kwako kuujua?

Ungeweza pia kusoma kile ambacho Mzee David A. Bednar alifundisha kuhusu matembezi ya kwanza ya Moroni kwa Joseph Smith katika “Kwa Uwezo wa Mungu katika Utukufu Mkuu” (Liahona, Nov. 2021, 28).

13:16

Kwa Nguvu za Mungu katika Utukufu Mkuu

Mzee Bednar anafundisha kwamba kuheshimu maagano yetu hutusaidia kupokea nguvu ya uungu katika maisha yetu.

Ona pia “Lo! Mlimani Kumora,” Nyimbo za Dini, na. 9.

Joseph Smith—Historia ya 1:48–60

Mungu ataniandaa kufanya kazi katika ufalme Wake.

Joseph alikuwa na umri wa miaka 17 tu wakati alipoona kwa mara ya kwanza yale mabamba ya dhahabu. Hayakukabidhiwa kwake kwa utunzaji, hata hivyo, hadi miaka minne baadaye. Soma Joseph Smith—Historia ya 1:48–60, ukitafuta kitu gani kilitokea katika maisha ya Joseph wakati huo. Unafikiri matukio haya yalimwandaaje yeye kwa ajili ya kazi ambayo Mungu alimwita kuifanya? Ni uzoefu gani ulionao ambao umekuandaa wewe kumtumikia Mungu na wengine? Je, kwa sasa unapitia kitu gani ambacho kinaweza kukusaidia kujiandaa kwa ajili ya huduma ya siku za usoni?

mchoro wa Kilima Kumora, karibu na Manchester,New York

Kilima Kumora, na Al Rounds

Mafundisho na Maagano 2

Bwana alimtuma Eliya kuugeuza moyo wangu uwaelekee mababu zangu.

Ni nini maneno kama “panda,” “mioyo,” na “geuza” katika sehemu hii yanakufundisha kuhusu huduma ya Eliya na baraka za funguo za ukuhani alizozirejesha? Ni kwa jinsi gani umehisi moyo wako ukiwageukia mababu zako? Fikiria njia unazoweza kupata uzoefu wa hisia kama hizo mara nyingi zaidi. Kuwatafuta mababu zako waliofariki na kufanya ibada kwa niaba yao katika hekalu ni njia mojawapo.(ona FamilySearch.org). Je, ni njia gani nyingine unazoweza kuzifikiria?

Ona pia Mafundisho na Maagano 110:13–16; Gerrit W. Gong, “Furaha na Milele,” Liahona, Nov. 2022, 83–86.

Kwa mawazo zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Joseph Smith—Historia ya 1:28–29

Ninaweza kutubu na kusamehewa.

  • Sisi sote wakati mwingine tunahisi “hatia kwa udhaifu na kutokuwa [kwetu] wakamilifu,” kama Joseph Smith alivyohisi. Wewe na watoto wako mngeweza kusoma Joseph Smith—Historia ya 1:29 pamoja, mkitafuta kile ambacho Joseph Smith alikifanya alipohisi hivyo. Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wake ambacho kinaweza kutusaidia wakati tunapofanya makosa? Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Joseph alikuwa ameitwa na Mungu japokuwa hakuwa mkamilifu?

Joseph Smith—Historia ya 1:27–54

Baba wa Mbinguni alimwita Joseph Smith kumsaidia kufanya kazi Yake.

  • Watoto wako watahisi burudani kwa kujifanya wao ni Joseph Smith unapowasimulia hadithi ya matembezi ya Moroni katika Joseph Smith—Historia ya 1:27–54 au “Sura ya 3: Malaika Moroni na Mabamba ya dhahabu” (katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 13–17, au video inayofanana nayo katika Maktaba ya Injili). Kwa mfano, wangeweza kukunja mikono yao kama vile wanasali au kujifanya wanapanda Kilima Kumora, na kadhalika. Kisha ungeweza kuwaomba kuzungumza kuhusu kile ambacho Mungu alimwita Joseph Smith kufanya na jinsi gani sisi tumebarikiwa kama matokeo yake. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani tumebarikiwa kwa sababu Joseph Smith alitafsiri Kitabu cha Mormoni? Je, kazi yake imetusaidiaje sisi kuja karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

    NaN:NaN

Mafundisho na Maagano 2

Baba wa Mbinguni anataka familia ziunganishwe hekaluni.

  • Labda wewe na watoto wako mngefurahia kuangalia baadhi ya picha za familia yako, ikiwezekana ikijumuisha picha ya familia yenu ikiwa hekaluni (au ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 120). Kisha mngeweza kusoma Mafundisho na Maagano 2 na mshiriki mawazo yenu kuhusu kwa nini tuna mahekalu na kwa nini Baba wa Mbinguni anataka familia ziwe pamoja milele. Fikiria kuimba pamoja “Families Can Be Together Forever” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 188). Wimbo huu unasema kitu gani ambacho tunaweza kufanya ili kuwa pamoja na familia zetu milele?

Young Couple Going to the Temple, English
Hekalu la Palmyra New York

Hekalu la Palmyra New York

Mafundisho na Maagano 2

Kujifunza kuhusu mababu zangu kunaweza kuniletea shangwe.

  • Watoto wanaweza kufurahia kuhusu na kuhisi shangwe ya historia ya familia. Ili kuwasaidia, ungeweza kuwasimulia hadithi au picha za mababu zako. Zungumza na watoto wako kuhusu jinsi gani maisha yalivyokuwa kwa mababu zao walipokuwa watoto. Watoto wako wangeweza pia kufurahia baadhi ya shughuli za historia ya familia katika FamilySearch.org/discovery.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

Malaika Moroni akimwonyesha Joseph Smith mahali yale mabamba ya dhahabu yalipofichwa

Joseph Anapokea Mabamba, na Gary E. Smith

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto