“Aprili 27–Mei 2: ‘Kazi Yangu Itasonga Mbele’: Mafundisho na Maagano 3–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 3-5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Januari 27–Februari 2: “Kazi Yangu Itasonga Mbele”
Mafundisho na Maagano 3–5
Wakati wa miaka yake michache ya kwanza kama nabii wa Bwana, Joseph Smith, bado hakujua kila kitu kuhusu “kazi ya ajabu” aliyoitwa kufanya. Lakini kitu kimoja uzoefu wake wa awali ulichomfundisha ilikuwa kwamba ili kufanya kazi ya Bwana, ni lazima jicho lake liwe “kwenye utukufu wa Mungu pekee” (Mafundisho na Maagano 4:1, 5). Kwa mfano, kama Bwana alimshauri kufanya kitu ambacho yeye hakuwa na uhakika kama alitaka kufanya hilo, yeye alihitaji kufuata ushauri wa Bwana. Na hata kama alikuwa amepata “mafunuo mengi, na … uwezo wa kufanya kazi kuu nyingi,” kama alihisi kwamba kile alichotaka yeye kilikuwa muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Bwana, yeye, “lazima angeanguka” (Mafundisho na Maagano 3:4). Lakini Joseph alijifunza kitu kingine muhimu kuhusu kufanya kazi ya Mungu: “Mungu ni mwenye rehema,” na kama Joseph angetubu kwa dhati, yeye alikuwa “bado mteule” (mstari wa 10). Kazi ya Mungu, hata hivyo, ni kazi ya ukombozi. Na kazi hiyo “haiwezi kubatilishwa” (mstari wa 1).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ninaweza kumtumaini Mungu.
Mapema katika huduma ya Joseph Smith, marafiki wema walikuwa wagumu kupatikana—hususani marafiki kama Martin Harris, aliyeheshimika, mtu mwenye mafanikio, ambaye alifanya dhabihu kubwa ili kusaidia kazi ya Joseph. Hivyo Martin alipoomba ruhusa ili kuonyesha kurasa za kwanza 116 za mswada wa tafsiri ya Kitabu cha Mormoni kwa mke wake, kwa kawaida Joseph alitaka kuheshimu ombi lake, ingawa Bwana alimwonya dhidi ya hilo. Kwa masikitiko makubwa, kurasa zile zilipotea wakati zikiwa mikononi mwa Martin, na Joseph na Martin walirudiwa kwa ukali sana na Bwana (ona Watakatifu, 1:51–53).
Unaposoma Mafundisho na Maagano 3:1–15, tafakari Bwana anataka ujifunze nini kutokana na uzoefu wao. Kwa mfano, unajifunza nini kuhusu:
-
Kazi ya Mungu? (ona mstari wa 1–3, 16).
-
Matokeo ya kumwogopa mtu kuliko kumtumaini Mungu? (ona mstari wa 4–8).
-
Baraka ambazo zinakuja kutokana na kubaki waaminifu? (ona mstari wa 8).
-
Njia ambayo Bwana alimuadhibu na kumtia moyo Joseph? (ona mstari 9–16).
Katika ujumbe wake “Ni Njia Gani Wewe Unatazama?,” Mzee Lynn G. Robbins anatupatia mifano mingi ya kimaandiko ya watu waliokuwa na hofu ya Mungu na watu waliokubali shinikizo kutoka kwa wengine (Liahona, Nov. 2014, 9–11). Fikiria kusoma mifano hii katika maandiko anayoyarejelea. Je, unajifunza nini kutoka katika hadithi hizi? Ni uzoefu gani uliowahi kuupata ulipomtumainia Bwana pale ulipokabiliwa na shinikizo la kufanya kitu tofauti? Ni yapi yalikuwa matokeo ya matendo yako?
Ona pia Dale G. Renlund, “Mfumo kwa ajili ya Ufunuo Binafsi,” Liahona, Nov. 2022, 16–19; “The Contributions of Martin Harris,” katika Revelations in Context (2016), 1–9; Topics and Questions, “Seeking Truth and Avoiding Deception,” Gospel Library; “Amri Zake Mungu,” Hymns, no. 71.
Ninaweza kumtumikia Mungu kwa moyo wangu wote, uwezo, akili na nguvu.
Sehemu ya 4 mara nyingi inatumika kwa wamisionari . Hata hivyo, inapendeza kufahamu kwamba ufunuo huu ulitolewa kwanza kwa Joseph Smith Mkubwa, ambaye hakuwa ameitwa kwenye umisionari lakini bado alikuwa “anatamani kumtumikia Mungu” (mstari wa 3).
Njia moja ya kusoma sehemu hii ni kuifikiria kama maelezo ya kazi kwa ajili ya mtu anayetaka kufanya kazi ya Bwana. Je, Bwana anatafuta nini? Ni faida gani Yeye anatoa?
Unajifunza nini kuhusu kumtumikia Mwokozi kutokana na ufunuo huu?
Rais Russell M. Nelson amesema kukusanywa kwa Israeli “ni changamoto kubwa, ni kusudi kubwa, na ni kazi kubwa duniani” (“Tumaini la Israeli” [worldwide youth devotional, Juni 3, 2018], Maktaba ya Injili). Ni kipi unachopata katika hotuba yake ambacho kinakuvutia wewe kushiriki katika kazi hii?
Kupitia Roho Mtakatifu ninaweza kupata ushahidi juu ya Kitabu cha Mormoni.
Mnamo Machi 1829, mke wa Martin Harris, Lucy, alifungua madai mahakamani kwamba Joseph Smith alikuwa anadanganya watu kwa kusingizia kuwa anatafsiri mabamba ya dhahabu (ona Watakatifu, 1:56–58). Kwa hiyo Martin alimwomba Joseph ushahidi zaidi kwamba mabamba ya dhahabu yalikuwa ya kweli. Mafundisho na Maagano 5 ni ufunuo katika kujibu ombi la Martin. Unajifunza nini kutoka sehemu hii kuhusu yafuatayo:
-
Ni nini Bwana anasema kingetokea kama mabamba ya dhahabu yangeonyeshwa kwa walimwengu ili waone (ona Mafundisho na Maagano 5:7). Kwa nini unafikiri ingelikuwa hivyo?
-
Wajibu wa mashahidi katika kazi ya Bwana (ona mstari wa 11–15; ona pia 2 Wakorintho 13:1).
-
Jinsi ya kupata ushuhuda wa Kitabu cha Mormoni kwa ajili yako mwenyewe (ona mstari wa 16; ona pia Moroni 10:3–5).
Yesu Kristo alitoa neno Lake kupitia Joseph Smith.
Ni nini Mafundisho na Maagano 5:1–10 inakufundisha kuhusu wajibu wa Joseph Smith katika siku yetu—na katika maisha yako? (Ona pia 2 Nefi 3:6–24.)
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mafundisho na Maagano 3:5–10; 5:21–22
Ninaweza kuchagua mema wakati wengine wanapojaribu kunifanya nitende mabaya.
-
Ili kuanzisha majadiliano kuhusu kujifunza kumtumaini Baba wa Mbinguni, ungeweza kutaka kurejelea hadithi ya kupotea kwa kurasa za mswada (ona Hadithi za Mafundisho na Maagano, 18–21). Mngeweza kisha kuigiza pamoja na watoto wako mazingira ambapo wanaweza kujaribiwa kufanya kitu wanachojua kuwa siyo sahihi. Ni maneno gani au kirai gani katika Mafundisho na Maagano 3:5–8; 5:21–22 ambacho kingeweza kuwasaidia katika mazingira hayo.
Bwana ananialika kusaidia katika kazi Yake.
-
Kila mstari katika Mafundisho na Maagano 4 una kweli za thamani ambazo zinaweza kuwasaidia watoto wako kujifunza kuhusu kumtumikia Mungu. Hapa kuna baadhi ya mawazo ya kuwasaidia kugundua kweli hizo.
-
Mngeweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 4:1 na onyesha picha ambazo zinaonyesha kazi ya Mungu ya “ajabu” katika siku za mwisho (kama vile wamisionari, mahekalu na Kitabu cha Mormoni).
-
Watoto wako wangeweza kufikiria matendo au kuchora picha zikielezea kirai “mtumikie kwa moyo wenu wote, uwezo, akili na nguvu” (Mafundisho na Maagano 4:2).
-
Mngeweza kutafuta pamoja zana ambazo zinatumika kufanya kazi shambani. Ni kwa jinsi gani zana hizi hutusaidia sisi? Kisha watoto wako wangeweza kutafuta vitu katika Mafundisho na Maagano 4:5–6 ambavyo ni sawa na zana za kufanyia kazi ya Mungu.
-
Watoto wakubwa wangeweza kupekua Mafundisho na Maagano 4 wao wenyewe na kutengeneza orodha ya mambo wanayojifunza kuhusu kile inachomaanisha kumtumikia Mungu.
-
Mngeweza kuimba pamoja wimbo kuhusu kazi ya umisionari, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168).
-
Mafundisho na Maagano 5:1–7, 11, 16, 23–24
Ninaweza kuwa shahidi kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli.
-
Ili kufundisha watoto wako kuhusu mashahidi, ungeweza kuwaomba kufikiria kwamba rafiki amewaambia kwamba wamemwona paka akitembelea miguu ya mbele. Je, wao wataamini? Itakuwaje kama rafiki mwingine atawaambia kitu hicho hicho? Zungumzeni pamoja kuhusu “shahidi“ ni nani na kwa nini mashahidi ni muhimu. Ungeweza kisha kuwasaidia watoto wako kupekua Mafundisho na Maagano 5:1–3, 7, 11 kwa ajili ya majibu ya maswali kama haya:
-
Je, Martin Harris alitaka kujua nini?
-
Joseph Smith angeweza kumwonyesha nani yale mabamba ya dhahabu?
-
Kwa nini kuona mabamba pengine kusingeweza kumshawishi mtu kuwa Kitabu cha Mormoni ni cha kweli?
-
Tunaweza kufanya nini ili kuwa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni? (ona Mafundisho na Maagano 5:16; Moroni 10:3–5).
-