“Februari 3-9, ‘Hii Ni Roho ya Ufunuo’: Mafundisho na Maagano 6-9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani:Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 6–9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Februari 3–9: “Hii Ni Roho ya Ufunuo”
Mafundisho na Maagano 6–9
Katika majira ya majani kupukutika ya mwaka 1828, mwalimu wa shule kijana aliyeitwa Oliver Cowdery alipata kazi ya kufundisha huko Manchester, New York, na aliishi na familia ya Lucy na Joseph Smith, Mkubwa. Oliver alikuwa amesikia kuhusu mwana wao Joseph na matukio yake yasiyo na kifani, na Oliver, ambaye alijichukulia yeye mwenyewe kama mtafuta ukweli, alitaka kujua zaidi. Akina Smith walielezea matembezi ya malaika, kumbukumbu ya kale na karama ya kutafsiri kwa uwezo wa Mungu. Oliver alivutiwa sana. Je, ingeweza kuwa kweli? Lucy na Joseph Mkubwa walimpa ushauri ambao unatumika na yeyote anayetafuta ukweli: sali na umuulize Bwana.
Oliver alifanya hivyo, na Bwana alijibu, akizungumza “amani akilini [mwake]”. (Mafundisho na Maagano 6:23). Ufunuo, Oliver aligundua, sio tu kwa manabii kama Joseph Smith. Ni kwa kila mtu anayeutaka na kuutafuta kwa bidii. Oliver bado alikuwa na mengi ya kujifunza, lakini alijua vya kutosha kuchukua hatua iliyofuata. Alijua Bwana alikuwa akifanya kitu fulani muhimu kupitia Joseph Smith, na Oliver alitaka kuwa sehemu ya hilo.
Ona pia Saints, 1:58–64; “Days of Harmony” (video), Maktaba ya Injili.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Baba wa Mbinguni huongea nami kupitia Roho Mtakatifu.
Katika majira ya kuchipua ya mwaka 1829 Oliver Cowdery alijitolea kuwa mwandishi wa Joseph Smith alipokuwa akiendelea kutafasiri Kitabu cha Mormoni. Jambo hili lilimsisimua, na alijiuliza kama angeweza pia kupokea ufunuo na karama ya kutafsiri. Jaribio lake la kwanza, hata hivyo, halikwenda vizuri.
Kama umewahi kupambana kupokea au kuelewa ufunuo, labda unaweza ukahusisha na tukio hili la Oliver na ujifunze kutokana na hilo. Unaposoma Mafundisho na Maagano 6, 8, na 9, gundua kile Bwana alichomfundisha Oliver kuhusu ufunuo binafsi. Kwa mfano:
-
Ni kitu gani Mafundisho na Maagano 6:5–7; 8:1; 9:7–8 yanapendekeza kuhusu kile Bwana anahitaji kutoka kwako kabla hajafunua mapenzi Yake?
-
Ni nini unajifunza kutoka katika Mafundisho na MaMaagano 6:14–17, 22–24; 8:2–3; 9:7–9 kuhusu njia tofauti ambazo ufunuo unaweza kuja? Ni kwa jinsi gani unaweza kuutambua?
-
Unajifunza nini cha ziada kuhusu ufunuo kutoka katika sehemu hizi?
Uzoefu wa Oliver ungeweza kukusababisha wewe “kurejesha mawazo yako” juu ya nyakati zile wakati ulipohisi kwamba Bwana alikuwa akiongea na wewe (Mafundisho na Maagano 6:22). Je, umewahi kuandika mawazo au hisia zako kuhusu uzoefu huu? Kama ndivyo, fikiria kusoma kile ulichoandika. Kama hapana, chukua muda wa kuandika kile unachokumbuka. Fikiria jinsi gani unaweza kuendelea kupata nguvu kutokana na matukio haya. Kwa baadhi ya mawazo, ona ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Kumbukumbu za Kuelezeka Kiroho” (Liahona, Mei 2020, 18–22).
Viongozi kadhaa wa Kanisa wameshiriki uzoefu wao juu ya ufunuo katika mkusanyiko wa video za “Hear Him”. Baada ya kuangalia moja au zaidi ya video hizi, yawezekana mkashawishika kuandika uzoefu wenu wenyewe, mkishiriki jinsi gani Bwana amezungumza na nanyi.
Ona pia Topics and Questions, “Personal Revelation,” Gospel Library; “Oliver Cowdery’s Gift,” in Revelations in Context, 15–19.
Mafundisho na Maagano 6:18–21, 29–37
Mtegemee Kristo katika kila wazo.
Bwana alijua kwamba Joseph Smith angepitia “hali ngumu” katika miaka inayokuja (Mafundisho na Maagano 6:18). Yeye anajua ni majaribu gani yapo katika siku zako za baadaye pia. Unapata nini katika ushauri Wake kwa Joseph na Oliver katika Mafundisho na Maagano 6:18–21, 29–37 ambao unakusaidia wewe kumtumaini Yeye?
Je, unahisi inamaanisha nini “kumtegemea [Kristo] katika kila wazo”? (mstari wa 36), Unawezaje kufanya hili kwa uendelevu zaidi—katika nyakati nzuri na “hali ngumu”? Fikiria ushauri huu kutoka kwa Rais Russell M. Nelson: “Ni jambo gumu kiakili kujitahidi kumtazamia Yeye katika kila wazo. Lakini wakati tunapofanya hivyo, wasiwasi wetu na hofu yetu hukimbia” (“Kuleta Nguvu ya Yesu Kristo katika Maisha yetu,” Liahona, 41).
Ona pia Neil L. Andersen, “Akili Yangu Ilishika Wazo Hili juu ya Yesu Kristo,” Liahona, Mei 2023, 91–94.
“Msiogope kufanya mema.”
Kwa nini wakati mwingine sisi “huogopa … kufanya mema”? (mstari wa 33). Je, unapata nini katika Mafundisho na Maagano 6:29–37 ambacho hukupa wewe ujasiri wa kutenda mema? Fikiria kuimba au kusikiliza wimbo wa dini ambao unakushawishi kuwa na ujasiri katika Kristo, kama vile “Tusonge Mbele” (Nyimbo za Dini, na. 139).
Mafundisho na Maagano 6–7; 9:3, 7–14
“Kwani ukiomba kile utakachotaka, utapewa.”
Tambua ni mara ngapi maneno kama “taka” au “matakwa” yanatokea katika sehemu ya 6 na 7. Unajifunza nini kutoka sehemu hizi kuhusu umuhimu ambao Mungu anauweka katika matamanio yako? Jiulize mwenyewe swali la Bwana katika Mafundisho na Maagano 7:1: “Wataka nini wewe?”
Mojawapo ya matamanio ya haki ya Oliver Cowdery—kutafsiri kama Joseph Smith alivyotafsiri—halikutimizwa. Unaposoma Mafundisho na Maagano 9:3, 7–14, ni misukumo gani unayopokea ambayo ingeweza kukusaidia wakati matamanio yako ya haki hayatimii kwa sasa?
Ona pia Mafundisho na Maagano 11:8; Dallin H. Oaks, “Hamu,” Liahona, Mei 2011, 42–45.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mafundisho na Maagano 6:5, 15–16, 22–23; 8:2; 9:7–9
Baba wa Mbinguni huongea nami kupitia Roho Mtakatifu.
-
Kweli ambazo Oliver Cowdery alijifunza kuhusu ufunuo binafsi zinaweza kuwasaidia watoto wako wanapokuza uwezo wao wa kumtambua Roho Mtakatifu. Ungeweza kutumia “Sura ya 5: Joseph Smith na Oliver Cowdery” (katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 22–25, au video inayohusiana nayo katika Maktaba ya Injili ili kuwafundisha kuhusu Oliver kile alichojifunza. Shiriki na kila mmoja sehemu zako pendwa za hadithi hii? Unapofanya hivi, sisitiza mambo ambayo Bwana alimfundisha Oliver jinsi gani ya kusikiliza sauti ya Mungu, na kusoma mistari inayohusiana nayo, kama vile Mafundisho na Maagano 6:23 au 9:7–9.
-
Ungeweza pia kuwaalika watoto wako kugusa vichwa vyao na vifua vyao unaposoma maneno “akili” na “moyo” katika Mafundisho na Maagano 8:2. Waambie watoto wako, kutokana na uzoefu wako, huwa inakuwaje wakati Roho Mtakatifu anapozungumza kwenye akili na moyo wako. Wasaidie kutafuta majibu ya maswali haya “Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu anazungumza na sisi?” katika mistari hii: Mafundisho na Maagano 6:15–16, 22–23; 8:2; 9:7–9.
Kwa sababu ya Yesu Kristo, siwezi “kuogopa”.
-
Bwana aliwaambia Joseph na Oliver, “msiogope, enyi kundi dogo” (Mafundisho na Maagano 6:34). Waalike watoto wako warudie kirai hiki pamoja na wewe mara kadhaa. Pia waruhusu kufurahia kujifanya kuwa kundi la kondoo wanaoogopa. Yawezekana kondoo wakaogopa kitu gani? Kisha wewe na watoto wako mngeweza kutazama picha ya Mwokozi kama mchungaji (iko moja mwishoni mwa muhtasari huu) na zungumzia kuhusu jinsi gani Yeye anavyotulinda sisi kama mchungaji anavyowalinda kondoo Wake.
-
Fikiria kucheza au kuimba wimbo kuhusu kupata ujasiri, kama vile “Dare to Do Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 158) au “Tusonge Mbele” (Nyimbo za Dini, na. 139). Wimbo unafundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyotusaidia tusiogope?
Ninaweza kumtegemea Yesu Kristo katika kila wazo.
-
Baada ya kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 6:36, wewe na watoto wako mngeweza kutengeneza michoro ili kuwasaidia kukumbuka “kumtegemea Yesu Kristo katika kila wazo.” Shiriki na kila mmoja michoro yenu na wasaidie watoto wako kufikiria kuhusu mahali wanapoweza kuiweka ili waione mara kwa mara.