“Februari 17–23: ‘Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu’: Mafundisho na Maagano 12–17; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani:Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 12–17: Joseph Smith—Historia ya 1:66–75,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Februari 17–23: “Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu”
Mafundisho na Maagano 12–17; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75.
Watu wengi ulimwenguni kote labda kamwe hawajasikia Harmony, Pennsylvania. Bwana mara nyingi huchagua mahali pasipokuwa muhimu kwa ajili ya matukio mengi muhimu katika ufalme Wake. Katika eneo la msitu karibu na Harmony mnamo Mei 15, 1829, Yohana Mbatizaji aliwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery. Aliweka mikono yake juu ya vichwa vyao na kutunuku Ukuhani wa Haruni juu yao, akiwaita “watumishi wenzangu” (Mafundisho na Maagano 13:1).
Yohana Mbatizaji, alikuwa mtumishi wa Mungu mwenye kuaminika aliyembatiza Mwokozi na kutayarisha njia kwa ajili ujio Wake (ona Mathayo 3:1–6, 13–17)). Kwa hawa vijana wawili wakiwa katika umri wa miaka ya ishirini, lazima ilikuwa ya kunyenyekeza, labda hata kuzidiwa, kuitwa watumishi wenza wa Yohana. Wakati ule, Joseph na Oliver kwa kiasi walikuwa hawajulikani, kama vile Harmony ilivyokuwa haijulikani. Lakini huduma katika kazi ya Mungu daima imekuwa kuhusu jinsi tunavyohudumu, sio kuhusu nani anatambua. Licha ya udogo au kutoonekana kwa mchango wako kunavyoweza kuonekana wakati mwingine, wewe pia ni mtumishi mwenza katika “kazi kuu na ya ajabu” ya Bwana (Mafundisho na Maagano 14:1).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ninaweza kushiriki katika “kazi kuu na ya ajabu” ya Mungu.
Joseph Night na David Whitmer wote wawili walitaka kujua jinsi gani wangeweza kusaidia katika kazi ya Bwana. Unaposoma jibu la Bwana kwao (Mafundisho na Maagano 12; 14), fikiria kuhusu inamaanisha nini kwako “kuanzisha na kustawisha kusudi la Sayuni” (12:6; ona pia 14:6). Ni kanuni gani na sifa kama za Kristo unazipata katika sehemu hizi ambazo zinaweza kukusaidia wewe kufanya hili?
Ona pia “The Knight and Whitmer Families,” katika Revelations in Context, 20–24.
Yesu Kristo alimtuma Yohana Mbatizaji kurejesha Ukuhani wa Haruni.
Yohana Mbatizaji aliwaita Joseph Smith na Oliver Cowdery “watumishi wenzake.” Unadhani inamaanisha nini kuwa mtumishi mwenza waYohana Mbatizaji? (ona Mathayo 3:13–17; Luka1:13–17; 3:2–20).
Unaposoma kile Yohana Mbatizaji alichosema kuhusu Ukuhani wa Haruni katika sehemu ya 13, tafakari jinsi gani funguo za ukuhani huu zinasaidia kukamilisha misheni ya Yohana ya kutengeneza njia ya Bwana. Kwa mfano:
-
Je, “Huduma ya malaika” ni nini? (ona 2 Nefi 32:2–3; Moroni 7:29–32; Mwongozo wa Maandiko, “Malaika,” Maktaba ya Injli).
-
Je, “injili ya toba” ni nini? (ona Mafundisho na Maagano 84:26–27; Dale G. Renlund, “Ukuhani na Nguvu ya Mwokozi ya Kulipia Dhambi,” Liahona, Nov. 2017, 64–67).
Je, ni kwa jinsi gani ibada za Ukuhani wa Haruni (kama vile ubatizo na sakramenti) zinasaidia kutayarisha njia kwa ajili ya kumpokea Mwokozi katika maisha Yako?
Funguo za ukuhani ni nini?
Mzee Dale G. Renlund na mkewe, Ruth, walitoa maelezo haya kuhusu funguo za ukuhani:
“Neno funguo za ukuhani hutumika kwa njia mbili tofauti. Ya kwanza inaelezea haki maalumu au haki inayotunukiwa juu ya wale wote wanaopokea Ukuhani wa Haruni au Melkizedeki. … Kwa mfano, wenye Ukuhani wa Haruni hupokea funguo za huduma za malaika na funguo za injili ya matayarisho ya toba na ubatizo kwa uzamisho kwa ajili ya ondoleo la dhambi (ona Mafundisho na Maagano 13:1; 84:26–27). Wenye Ukuhani wa Melkizedeki hupokea ufunguo wa siri za ufalme, ufunguo wa ufahamu wa Mungu, na funguo za baraka zote za kiroho za Kanisa (ona Mafundisho na Maagano 84:19; 107:18). …
“Njia ya pili neno funguo za ukuhani hutumika kurejelea uongozi. Viongozi wa ukuhani hupokea funguo za ziada, haki ya kuongoza kitengo cha kimuundo wa Kanisa au akidi. Kuhusu swala hili, funguo za ukuhani ni mamlaka na nguvu za kuelekeza, kuongoza, na kutawala katika Kanisa” (The Melchizedek Priesthood: Understanding the Doctrine, Living the Principles [2018], 26).
Joseph Smith—Historia ya 1:66–75
Ibada hunifanya kupokea nguvu za Mungu.
Je, Umewahi kujiuliza ingekuwaje kuwa na Joseph Smith na Oliver Cowdery wakati wa matukio haya makubwa ya Urejesho? Unaposoma Joseph Smith—Historia ya 1:66–75, ikijumuisha muhtasari mwishoni mwa mstari wa 71, ungeweza kuelewa angalau baadhi ya kile walichohisi. Je, ni kitu gani kinakuvutia kuhusu maneno yao? Kumbuka, hasa, baraka walizozipokea kwa sababu walipokea ukuhani na kubatizwa. Je, ni baraka gani Mwokozi amekupatia wewe kupitia ibada za ukuhani?
Ili kujifunza zaidi, zingatia kutengeneza jedwali lenye vichwa vya habari Ibada na Baraka. Kisha ungeweza kupekua maandiko kama haya ili kuorodhesha ibada na baraka ambazo huja: Yohana 14:26; Matendo ya Mitume 2:38; Mafundisho na Maagano 84:19–22; 131:1–4; Joseph Smith—Historia ya 1:73–74. Je, ni baraka gani nyingine ungeweza kuongeza kwenye orodha hii? Je, ni kwa jinsi gani ibada ulizopokea zimekuletea nguvu za Mwokozi katika maisha yako?
Ona pia David A. Bednar, “Kwa Nguvu za Mungu katika Utukufu Mkuu,” Liahona, Nov. 2021, 28–30; Saints, 1:65–68; “God of Power, God of Right,” Hymns, no. 20; Topics and Questions, “Covenants and Ordinances,” Maktaba ya Injili.
Kuleta nafsi kwa Kristo ni jambo la thamani kubwa.
Je, umewahi kujiuliza kama vile John na Peter Whitmer walivyofanya, ni kitu gani “kingekuwa cha thamani kubwa” katika maisha yako? (Mafundisho na Maagano 15:4; 16:4). Unaposoma Mafundisho na Maagano 15–16, tafakari kwa nini kuleta nafsi kwa Kristo ni jambo la thamani kubwa. Je, wewe unafanya nini ili “kuleta nafsi” kwa Kristo?
Ona pia Saints, 1:68–71.
Bwana anawatumia mashahidi kuanzisha neno Lake.
Shahidi ni nini? Kwa nini Bwana anawatumia mashahidi katika kazi Yake? (Ona 2 Wakorintho 13:1). Tafakari maswali haya unaposoma maneno ya Mungu kwa Mashahidi Watatu katika Mafundisho na Maagano 17. (Ona pia “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” katika Kitabu cha Mormoni. Ni kwa jinsi gani mashahidi wanasaidia kutimiza “madhumuni ya haki” ya Mungu? (mstari wa 4).
Je, unaweza kutoa ushahidi juu ya nini?
Ona pia Saints, 1:73–75; “A Day for the Eternities” (video), Maktaba ya Injili.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mafundisho na Maagano 13; Joseph Smith—Historia ya 1:68–74
Yohana Mbatizaji alirejesha Ukuhani wa Haruni.
-
Kazi ya sanaa katika muhtasari huu ingeweza kuwasaidia watoto wako kuona taswira ya urejesho wa Ukuhani wa Haruni (ona pia “Sura ya 6: Joseph and Oliver Are Given the Priesthood,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 26–27, au video inayohusiana na hiyo katika Maktaba ya Injili). Je, wangefurahia kuchora picha ya tukio hili kulingana na kile unachosoma na wao katika Joseph Smith—Historia ya 1:68–74?
-
Ungeweza pia kuonyesha picha ya Yohana Mbatizaji wakati mkisoma pamoja Mathayo 3:13–17; Joseph Smith—Historia ya 1:68–70. Je, ni kwa nini ilikuwa muhimu kwamba Bwana amtume Yohana Mbatizaji kumpatia Joseph Smith mamlaka ya ukuhani ya kubatiza?
Baba wa Mbinguni ananibariki kupitia Ukuhani wa Haruni.
-
Ili kuchochea majadiliano kuhusu funguo ambazo zimetajwa katika Mafundisho na Maagano 13, wewe na watoto wako mngeweza kutazama jozi ya funguo na kuzungumza kuhusu kile funguo zinaturuhusu sisi kufanya. Labda ungeweza kuwasaidia kutafuta neno funguo katika sehemu ya 13. Je, ni maneno gani mengine au virai katika Mafundisho na Maagano 13 vinaelezea baraka za Ukuhani wa Haruni? Watoto wako wangeweza pia kutambua njia ambazo Baba wa Mbinguni anatubariki kupitia ukuhani katika video “Blessing of the Priesthood’ (Maktaba ya Injili).
Mafundisho na Maagano 15:4–6, 16:4–6
Kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo ni jambo la “thamani kubwa zaidi.”
-
John na Peter Whitmer walitaka kujua ni kitu gani “kingekuwa cha thamani kubwa zaidi” kwao (ona Mafundisho na Maagano 15:4; 16:4). Pengine wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu vitu ambavyo ni vya thamani kubwa kwenu. Unaposoma Mafundisho na Maagano 15:6 au 16:6, waombe watoto wako kuinua mkono juu wanaposikia Bwana alichosema ni “cha thamani kubwa.”
-
Inamaanisha nini “kuleta nafsi kwa [Yesu kristo]”? Wasaidie watoto wako kutengeneza orodha ya mawazo, kama vile kuwa marafiki kwa watu wengine, kushiriki maandiko na marafiki au kumwombea mtu aliye katika shida. Watoto wako wangeweza kutafuta picha ya vitu hivi katika majarida ya Kanisa au kwenye Kitabu cha Sanaa za Injili. Au wangeweza kuchora picha zao wenyewe. Waalike wachague kitu fulani kutoka kwenye orodha zao ambacho watafanya. Mngeweza pia kuimba kwa pamoja ubeti wa nne wa mstari wa “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75).
Ninaweza kuwa shahidi wa Kitabu cha Mormoni.
-
“Sura ya 7: Witnesses See the Gold Plates” (katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 31–33, au video inayohusiana na hilo katika Maktaba ya Injili) inaweza kuwasaidia watoto wako kujifunza kuhusu wale Mashahidi Watatu. Baada ya Kusoma Mafundisho na Maagano 17:5–6, wasimulie watoto wako jinsi wewe umejua kwamba Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni?