“Sauti za Urejesho: Mashahidi wa Kitabu cha Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mashahidi wa Kitabu cha Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Sauti za Urejesho
Mashahidi wa Kitabu cha Mormoni
Malaika Moroni alimwonyesha Joseph Smith, Oliver Cowdery, David Whitmer na Martin Harris mabamba ya dhahabu katika msitu karibu na nyumba ya Whitmer huko Fayette, New York. Wazazi wa Joseph walikuwa wakiwatembelea akina Whitmer wakati huo. Lucy Mack Smith, mama wa Joseph, alielezea athari ambazo uzoefu huu wa kimiujiza ulileta kwa mashahidi:
“Ilikuwa kati ya saa tisa na saa kumi kamili. Bi. Whitmer na Bwana Smith na mimi mwenyewe tulikuwa tumeketi katika chumba cha kulala. Nilikaa kando ya kitanda. Wakati Joseph alipoingia, alijitupa chini karibu nami. ‘Baba! Mama!’ alisema. ‘Hamjui jinsi nilivyo na furaha. Bwana amesababisha mabamba kuoneshwa kwa watatu wengine zaidi yangu, ambao pia wamemuona malaika na watashuhudia kwenye ukweli wa kile nilichosema. Kwani wanajua wao wenyewe kwamba sizungukizunguki kudanganya watu. Na ninahisi kama vile nimepunguziwa mzigo wa kuogofya, ambao ulikuwa mzito mno kwangu mimi kuuvumilia. Lakini sasa itawabidi wabebe sehemu, na inafurahisha nafsi yangu kwamba sitakuwa tena peke yangu kabisa ulimwenguni.’ Martin Harris kisha akaingia ndani. Alionekana karibu kuzidiwa na wingi wa furaha. Kisha alishuhudia juu ya kile alichokiona na kusikia, kama walivyofanya pia wengine, Oliver na David. Ushuhuda wao ulikuwa sawa sawa katika ukweli kama ule uliopo katika Kitabu cha Mormoni. …
“Martin Harris zaidi alionekana kabisa kushindwa kuelezea hisia zake kwa maneno. Alisema, ‘Sasa nimemuona malaika kutoka Mbinguni ambaye kwa uhakika ameshuhudia juu ya ukweli wa yale yote niliyoyasikia kuhusu kumbukumbu, na macho yangu yamemuona. Pia nimeyaangalia mabamba na kuyashika kwa mikono yangu na naweza kushuhudia hayo kwa ulimwengu wote. Lakini nimepokea mimi mwenyewe ushahidi ambao maneno hayawezi kuelezea, kwamba hakuna ulimi unaoweza kuelezea, na ninambariki Mungu kwa dhati ndani ya nafsi yangu kwamba ametenda wema kwa kunifanya mimi, hata mimi, shahidi wa ukuu wa kazi yake na mipango kwa niaba [ya] watoto wa watu.’ Oliver na David pia waliungana naye katika sifa za dhati kwa Mungu kwa ajili ya wema wake na rehema. Tulirudi nyumbani [Palmyra, New York,] siku iliyofuata kundi dogo, lenye furaha na shangwe.”
Lucy Mack Smith pia alikuwepo wakati Mashahidi Wanane waliporudi kutoka kwenye tukio lao:
“Baada ya mashahidi hawa kurudi kwenye nyumba, malaika tena alijitokeza kwa Joseph; ndipo wakati huo Joseph aliyatoa mabamba na kumpa mikononi mwake. Jioni ile tulifanya mkutano, ambapo mashahidi wote walitoa ushuhuda wa mambo kama yalivyoelezwa hapo juu; na familia yetu yote, hata kwa Don Carlos [Smith], ambaye alikuwa na umri wa miaka 14, alishuhudia ukweli wa kipindi cha maongozi ya Mungu cha siku za mwisho—kwamba kilikuwa kimeanzishwa kikamilifu.”
Kwa nyongeza ya wale Mashahidi Watatu na Mashahidi Wanane, Mary Whitmer, mama wa David Whitmer, alibarikiwa pia kuwa shahidi wa mabamba ya dhahabu. Malaika Moroni alimwonyesha kama shukrani kwa dhabihu alizofanya wakati Joseph, Emma na Oliver walipokuwa wanaishi katika nyumba yake. “Wewe umekuwa mwaminifu sana na mwenye bidii katika kazi zako,” Moroni alimwambia. “Ni sahihi, kwa hiyo, kwamba unapaswa kupokea ushahidi ili imani yako ipate kuimarika.”