Njoo, Unifuate
Februari 24–Machi 2: “Thamani ya Nafsi ni Kuu”: Mafundisho na Maagano 18


“Februari 24–Machi 2, ‘Thamani ya Nafsi ni Kuu’: Mafundisho na Maagano 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani:Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Kristo Akimpa kumbatio mtoto

Februari 24–Machi 2: “Thamani ya Nafsi Ni Kuu”

Mafundisho na Maagano 18

Kuna njia nyingi tofauti za kupima thamani ya mtu. Kipaji, elimu, utajiri na muonekeno wa kimwili vyote vinaweza kuathiri jinsi gani tunamtathmini kila mmoja—na sisi wenyewe. Lakini machoni pa Mungu, thamani yetu ni jambo rahisi sana, na limeelezwa wazi kabisa katika Mafundisho na Maagano 18: “Kumbuka thamani ya nafsi ni kuu machoni mwa Mungu” (mstari wa 10). Ukweli huu rahisi unaelezea mengi zaidi juu ya kile Mungu anafanya na kwa nini Yeye anakifanya. Kwa nini Yeye aliwaelekeza Joseph Smith na Oliver Cowdery kuanzisha Kanisa la Yesu Kristo katika siku yetu? (ona mstari wa 1–5). Kwa sababu thamani ya nafsi ni kuu. Kwa nini Yeye “anaamuru watu wote kila mahali kutubu” na anawatuma Mitume kuhubiri toba? (mstari wa 9). Kwa sababu thamani ya nafsi ni kuu. Na ni kwa nini Yesu Kristo aliteseka hadi “mauti katika mwili” na “maumivu ya watu wote”? (mstari wa 11). Kwa sababu thamani ya nafsi ni kuu. Hata kama moja ya nafsi hizi inachagua kukubali zawadi ya Mwokozi, Yeye anashangilia, kwani “shangwe kubwa kiasi gani kwake katika nafsi ambayo hutubu” (mstari wa 13).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 18:1–5

“Lijengeni kanisa langu.”

Katika sehemu ya 18, Bwana alimpa Oliver Cowdery maelekezo ili kusaidia kuweka msingi wa Kanisa la Yesu Kristo. Unaona kitu gani kuhusu ushauri aliompa—hususani katika mstari wa 1–5? Ungeweza kufikiria ni kwa jinsi gani ushauri huu huu unatumika kwako “unapojenga imani yako katika Kristo Kwa mfano:

  • Je, “umetamani kujua” nini juu ya Bwana? (mstari wa 1).

  • Inamaanisha nini kwako “kutegemea juu ya mambo ambayo yameandikwa”? (mstari wa 3). Ni kwa jinsi gani Roho “amedhihirisha kwako” kwamba mambo haya ni ya kweli? (mstari wa 2; ona pia Mafundisho na Maagano 6:22–24).

  • Je, unawezaje kujenga maisha yako juu ya “msingi wa injili ya [Mwokozi] na mwamba [Wake]? (mstari wa 5).

Uliza maswali. Mafundisho na Maagano ni ushahidi kwamba maswali yanaongoza kwenye ufunuo. Unapojifunza maandiko, weka kumbukumbu ya maswali ambayo unayo. Kisha tafakari na sali kutafuta majibu.

Mafundisho na Maagano 18:10–13

ikoni ya seminari
“Thamani ya nafsi ni kuu machoni pa Mungu.”

Ni kwa jinsi gani tunaamua thamani ya kitu fulani? Kwa mfano, kwa nini bidhaa moja sokoni ni ghali kuliko nyingine? Unaposoma sehemu ya 18 wiki hii, hususani mstari wa 10–13, unaweza kutofautisha jinsi gani watu mara nyingi wanaamua thamani ya kitu kile kile kinachoamua thamani ya nafsi machoni pa Mungu. Fikiria kubadilisha jina lako katika mahali pa maneno “nafsi,” na “watu wote” Ni kwa jinsi gani mistari hii ingeweza kumsaidia mtu anayetilia shaka thamani yake?

Hapa kuna baadhi ya vifungu ambavyo vinafundisha kuhusu thamani ya nafsi: Luka 15:1–10; Yohana 3:16–17; 2 Nefi 26:24–28; Musa 1:39. Kulingana na vifungu hivi, unawezaje kufanya muhtasari wa jinsi Mungu anavyohisi kukuhusu wewe? Ungeweza pia kupekua ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf’ “Ni wa Muhimu Kwake” (Liahona, Nov. 2011, 19–22) ili kupata maneno na virai ambavyo vitakusaidia kujua kuhusu thamani yako kwa Mungu.

Ni kwa jinsi gani Mungu hukuonyesha kwamba wewe ni wa thamani kuu Kwake? Ni kwa jinsi gani ufahamu huu huathiri jinsi unavyohisi kuhusu wewe mwenyewe na wengine?

Ona pia Joy D. Jones, “Thamani kupita Kipimo,” Liahona, Nov. 2017, 13–15; Mada na Maswali, “Watoto wa Mungu,” Maktaba ya Injili.

Mafundisho na Maagano 18:11–16

Bwana anafurahi wakati ninapotubu.

Tambua ni mara nyingi namna gani maneno kama tubu na toba yametumika kote katika Mafundisho na Maagano 18. Tafakari kile unachojifunza kutokana na maneno haya kila wakati yanapotumika. Fikiria hususani mstari wa 11–16) Ni kwa jinsi gani mistari hii inaathiri jinsi unavyohisi kuhusu toba—toba yako mwenyewe na wajibu wa kuwaalika wengine kutubu na kuwa bora? Hapa kuna njia moja ya kuandika kile unachojifunza: orodhesha njia kadhaa ambazo ungekamilisha sentensi hii “Toba ni .”

Ona pia Alma 36:18–21; Mwongozo wa Maandiko, “Toba,” Maktaba ya Injili, Dale G. Renlund, “Toba: Chaguo la Furaha,” Liahona, Nov. 2016, 121–24.

baba akimpa kumbatio mwanae

Maelezo kutoka Mwana Mpotevu, na Clark Kelley Price

Mafundisho na Maagano 18:14–16

Shangwe inakuja kutokana na kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo?

Unaposoma mstari wa 14–16, tafakari inamaanisha nini “kutangaza toba”—na ni kwa nini inaleta shangwe kama hiyo. Je, ni njia gani umegundua za kuwasaidia wengine kuja kwa Mwokozi na kupokea msamaha? Je, ni kwa jinsi gani watu wengine wamefanya hivi kwako?

Ona pia Craig C. Christensen, “Hapawezi Kuwa na Kitu Kizuri Hivyo na Kitamu vile Ilivyokuwa Shangwe Yangu,” Liahona, Mei 2023, 45–47.

Mafundisho na Maagano 18:34–36

Ninaweza kusikia sauti ya Bwana katika Mafundisho na Maagano.

Kama mtu angekuuliza sauti ya Bwana ikoje, ungesema nini? Fikiria kuhusu swali hili unaposoma Mafundisho na Maagano 18:34–36. Umejifunza nini kuhusu sauti ya Bwana kutokana na kusoma Mafundisho na Maagano? Unaweza kufanya nini kusikia sauti Yake kwa dhahiri zaidi?

Ona pia:“Nisomapo Maandiko,” Nyimbo za Dini, na. 159.

Kwa mawazo zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni 03 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 18:10–13

Kila mmoja wetu ni wa thamani kuu kwa Mungu.

  • Wewe pamoja na watoto wako mnaposoma Mafundisho na Maagano 18:10–13, kumbuka kubadilisha jina la kila mmoja katika mahali pa maneno “nafsi,”na “watu wote.” Mngeweza kisha kuzungumza kuhusu jinsi gani mistari hii inavyotusaidia kuelewa jinsi gani Baba wa Mbinguni anavyohisi kuhusu kila mmoja wetu.

  • Ungeweza pia kuwauliza watoto wako kuhusu vitu ambavyo watu wanafikiri ni vyenye thamani. Au ungeweza kuwaonyesha kitu ambacho ni cha thamani kwako. Ni kwa jinsi gani tunavichukulia vitu ambavyo ni vya thamani kwetu. Kisha waruhusu wafanye zamu kujiangalia kwenye kioo. Wanapofanya hivyo, mwambie kila mtoto ni mwana wa Mungu na ni wa thamani kuu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaonesha wengine kuwa “thamani ya nafsi [zao] ni kubwa” mbele zetu?

  • Ili kusisitiza kwamba watu wote ni wa thamani kuu kwa Baba wa Mbinguni, watoto wako wangeweza kuangalia kwenye picha iliyoko mwishoni mwa muhtasari huu wakati wewe ukisoma Mafundisho na Maagano 18:10–13. Kuimba pamoja wimbo kama “Every Star is Different” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 142–43) kunaweza kusaidia kutilia mkazo hoja hii.

Kristo akiwa ameshika mtoto

Maelezo kutoka Thamani ya Nafsi, na Liz Lemon Swindle

Mafundisho na Maagano 18:13–16

Kushiriki injili kunaleta shangwe kubwa.

  • Ili kuwavutia watoto wako kushiriki injili ya Yesu Kristo, mngeweza kuzungumza ninyi kwa ninyi kuhusu uzoefu wakati mlipokuwa na kitu ambacho mlitaka kushiriki pamoja na marafiki au familia. Kwa nini ulitaka kushiriki, na kushiriki kwako kulikufanya uhisije? Kisha mngeweza kusoma Mafundisho na Maagano 18:13, 16. Ni kitu gani kinampa Bwana shangwe? Yeye anasema ni kitu gani kitatuletea shangwe? Wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu uzoefu mliokuwanao katika kushiriki shangwe ya injili ya Mwokozi.

  • Wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168), ungeweza kuwasaidia watoto wako kufikiri juu ya njia wanazoweza kushiriki injili.

Mafundisho na Maagano 18:34–36

Ninaweza kusikia sauti ya Bwana katika Mafundisho na Maagano.

  • Watoto wako yawezekana wakafurahia mchezo ambapo wanajaribu kutambua sauti tofauti za watu, kama vile wanafamilia, marafiki au viongozi wa Kanisa. Je, tunawezaje kutambua sauti ya kila mmoja wetu. Tunawezaje kutambua sauti ya Bwana? Mngeweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 18:34–36 ili kujadili swali hili. Mngeweza pia kushiriki ninyi kwa ninyi jinsi mmesikia sauti ya Bwana katika maandiko.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

mkusanyiko wa nyuso za watu kutoka tamaduni mbalimbali

Kila nafsi ni ya thamani kwa Mungu.

ukurasa wa shughuli ya watoto