Njoo, Unifuate
Machi 3–9: “Jifunze kutoka Kwangu”: Mafundisho na Maagano 19


“Machi 3–9, ‘Jifunze kutoka Kwangu,’ Mafundisho na Maagano 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Yesu anatembea kando ya njia karibu na mti

Maelezo kutoka Njia ya Gethsemane, na Steve McGinty

Machi 3–9: Jifunze kutoka Kwangu

Mafundisho na Maagano 19

Iliwachukua Martin na Lucy Harris miaka kujipatia mojawapo ya mashamba mazuri sana huko Palmyra, New York. Lakini mnamo mwaka 1829 ilikuwa wazi kwamba Kitabu cha Mormoni kingeweza kuchapishwa tu kama Martin angeweka rehani shamba lake ili kumlipa mchapishaji. Martin alikuwa na ushuhuda juu ya Kitabu cha Mormoni, lakini Lucy hakuwa nao. Kama Martin angeweka rehani shamba lake na Kitabu cha Mormoni hakingeuzika vizuri, angepoteza shamba lake na kuhatarisha ndoa yake na kuharibu hadhi yake katika jumuiya. Ingawa hali zetu ziko tofauti na ya Martin, kwa wakati fulani au mwingine sisi sote tunakabiliana na maswali magumu kama hayo aliyokabiliana nayo: Je, injili ya Yesu Kristo ina thamani gani kwangu? Ni nini niko tayari kutoa dhabihu ili kusaidia kujenga ufalme wa Mungu? Martin Harris mwishowe aliamua kwamba angeweka rehani shamba lake ili nakala za kwanza 5,000 za Kitabu cha Mormoni ziweze kupigwa chapa. Lakini hata dhabihu hii—na dhabihu nyingine yoyote tunayoweza kufanya—ni ndogo ukilinganisha na ile dhabihu ya Yesu Kristo, “mkuu kuliko wote” (Mafundisho na Maagano 19:18), ambaye alitokwa damu kutoka kila kinyweleo ili kuwaokoa wenye kutubu.

Kwa maelezo zaidi kuhusu uchapishwaji wa Kitabu cha Mormoni, ona Saints, 1:76–84.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 19:1–12

“Mimi, Mungu, sina mwisho.”

Joseph Smith alielezea kwamba ufunuo katika sehemu ya 19 ni “amri … kwa Martin Harris, iliyotolewa na yeye ambaye ni Milele” (sehemu ya kichwa cha habari). Tafuta sehemu katika mstari wa 1–12 ambapo Bwana anasisitiza asili Yake ya Milele. Kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu kwa Martin Harris kujua hili kumhusu Bwana? Kwa nini ni muhimu kwako kujua hili?

Kwa nini unafikiri Yesu Kristo anaitwa “mwanzo na mwisho”? (mstari wa 1).

Mafundisho na Maagano 19:15–20.

ikoni ya seminari
Yesu Kristo aliteseka ili kwamba mimi niweze kutubu na kuja Kwake.

Agano Jipya linaelezea mateso ya Mwokozi katika Gethsemane katika mtazamo wa watu walioyaona. Katika Mafundisho na Maagano 19:15–20, Yesu Kristo alisema kuhusu mateso yake kutokana na mtazamo Wake Yeye mwenyewe. Unaposoma hadihi binafsi takatifu, tafuta jinsi gani Mwokozi alielezea mateso Yake. Fikiria kile kila neno au kirai vinakufundisha wewe. Kwa nini Mwokozi alikuwa radhi kuteseka? Unaweza kugundua zaidi katika Yohana 15:13; Mosia 3:7; Alma 7:11–12; Mafundisho na Magano 18:10–13.

Hisia ulizonazo unapojifunza mateso ya Mwokozi zinaweza kuchochea maswali kama haya: Kwa nini Mwokozi alipaswa kuteseka kwa ajili ya dhambi zangu? Ni kwa nini ninahitaji kutubu ili kupokea baraka timilifu za dhabihu Yake? Yawezekana ukapata umaizi kuhusu maswali haya na mengine katika ujumbe wa Mzee Ulisses Soares “Yesu Kristo: Mtunzaji wa Nafsi Zetu” (Liahona, Mei 2021, 82–84). Unapojifunza, ni misukumo gani inayokuja akilini mwako? Fikiria kuandika hisia zako kuhusu Yesu Kristo na dhabihu Yake kwa ajili yako.

Kama sehemu ya kujifunza na kuabudu kwako, yawezekana ukatafuta wimbo wa dini ambao wewe unaweza kuusikiliza au kuuimba ambao unaelezea shukrani yako kwa Mwokozi kwa mateso Yake kwa niaba yako. “Nastaajabu” (Nyimbo za Dini, na.106) ni mfano mzuri.

Je, unahisi Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wangependa ufanye nini kama matokeo ya kile ulichokihisi na kujifunza?

Ona pia “Yesu Kristo atakusaidia,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi (2022), 6–9; Mada na Maswali, “Upatanisho wa Yesu Kristo,” “Toba,” Maktaba ya Injili; D. Todd Christofferson, “Zawadi Takatifu ya Toba,” Liahona, Nov. 2011, 38–41;“Jesus Suffers in Gethsemane” (video), Maktaba ya Injili.

8:30

The Savior Suffers in Gethsemane

Jesus, Peter, James, and John retire to the Garden of Gethsemane. Jesus submits to the Father's will and begins to suffer for the sins and afflictions of mankind. He is then betrayed and arrested. Matthew 26:36–57

Mafundisho na Maagano 19:23

Amani inakuja kutokana na kujifunza juu ya Yesu Kristo na kumfuata.

Fikiria mwaliko wa Mwokozi “Jifunze kutoka Kwangu.” Unajifunza nini kuhusu Yesu Kristo katika Mafundisho na Maagano 19? Andika mawazo yako, na tafakari jinsi kweli hizi kuhusu Mwokozi zinavyokusaidia kupata amani. Inamaanisha nini kwako “kuenenda katika unyenyekevu wa Roho [Yake]”?

Ona pia Henry B. Eyring, “Kutafuta Amani Binafsi,” Liahona, Mei 2023, 29–31; “Peace in Christ” (video), Maktaba ya Injili.

4:9

Peace in Christ

Mafundisho na Maagano 19:26–41

Baraka za Mungu ni kuu kuliko hazina za duniani.

Kitabu cha Mormoni hakikuuzika vizuri sana huko Palmyra Kama matokeo yake, Martin Harris aliishia kuuza sehemu kubwa ya shamba lake ili kulipia deni kwa mpiga chapa (ona “The Contributions of Martin Harris,” Revelations in Context, 7–8). Tafakari juu ya dhabihu ya Martin—na baraka ulizopokea kwa sababu hiyo—unaposoma Mafundisho na Maagano 19:26–41. Ungeweza pia kufikiria kuhusu ni kitu gani Bwana amekutaka utoe dhabihu. Unapata nini katika mistari hii ambacho kinakuvutia kufanya dhabihu hizi kwa “shangwe” na “furaha”? (Ona pia mstari wa 15–20).

mchoro wa shamba huko Palmyra

Maelezo kutoka kwenye Shamba la Martin Harris, na Al Rounds

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 19:16–19

Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yangu.

  • Unaweza kuwasaidia watoto wako kuhisi unyenyekevu na shukrani kwa ajili ya Mwokozi kwa kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 19:16–19 au “Sura ya 51: Jesus Suffers in the Garden of Gethsemane,” in Hadithi za Agano Jipya, 129–32, au video inayoambatana katika Maktaba ya Injili. Fikiria kutua kidogo ili kuhakikisha watoto wako wameelewa na kuwaacha waonyeshe hisia zao. Kwa mfano, katika mstari wa 16, ni “mambo gani haya” ambayo Yesu aliteseka kwa ajili yetu sisi? (ona Mosia 3:7; Alma 7:11–12). Tunajifunza nini kutokana na maelezo Yake juu ya mateso Yake? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonesha shukrani zetu kwa ajili ya kile alichokifanya kwa ajili yetu?

1:46

Chapter 51: Jesus Suffers in the Garden of Gethsemane

Wasaidie watoto wajifunze kutoka kwenye maandiko. Baadhi ya watoto hupata wakati mgumu kusoma maandiko. Kufokasi kwenye mstari mmoja au kirai kunaweza kuwasaidia.

  • Wewe na watoto wako mnaweza kutafuta katika Nyimbo za Dini au kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto kwa ajili ya nyimbo ambazo zinawasaidia kuelezea hisia zenu kuhusu Yesu Kristo (ona vielezo vya mada katika vitabu hivi).

Yesu akisali Gethsemane

Mafundisho na Maagano 19:18–19, 24

Yesu Kristo alimtii Baba wa Mbinguni, hata wakati ilipokuwa vigumu.

  • Kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu ilikuwa vigumu sana, lakini Yesu Kristo alikuwa radhi kufanya hivyo ili kumtii Baba Yake na kuonyesha upendo Wake Kwake na kwetu sisi. Mngeweza kuangalia pamoja picha ya Yesu Kristo akiteseka huko Gethsemane (kama zile zilizoko katika muhtasari huu) na waulize watoto wako wakuambia kile wanachokijua kuhusu nini kinatokea katika picha. Mnaweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 19:18–19, 24 ili kusisitiza kwamba kuteseka kwa ajili yetu kilikuwa ni kitu kigumu zaidi ambacho mtu yeyote amewahi kufanya, lakini kwa sababu Yesu alimpenda Baba Yake na sisi, alitii mapenzi ya Mungu. (Ona pia Mosia 3:7). Ni mambo gani magumu ambayo Mungu anatutaka sisi tufanye? Tunawezaje kupata ujasiri wa kumtii Yeye?

Mafundisho na Maagano 19:23

“Jifunze kutoka kwangu, na sikiliza maneno yangu.”

  • Unaweza kuwasaidia watoto wako kufikiria juu ya matendo rahisi ambayo yanakwenda sambamba na virai katika Mafundisho na Maagano 19:23. Soma mstari mara kadhaa wakati wao wakifanya matendo. Je, ni baadhi ya njia gani tunaweza kujifunza juu ya Kristo na kusikiliza maneno Yake?

Mafundisho na Maagano 19:38

Baraka za Mungu ni kuu kuliko hazina za duniani.

  • Wewe na watoto wako mngeweza kupeana zamu kushikilia nakala ya Kitabu cha Mormoni na kuelezea ni kitu gani unakipendea kukihusu. Kwa ufupi zungumza kuhusu dhabihu ya Martin Harris ili Kitabu cha Mormoni kiweze kuchapishwa (ona Hadithi za Mafundisho na Maagano, 33). Bwana alimwambia nini Martin katika Mafundisho na Maagano 19:38 ambacho kingeweza kumsaidia kuwa mwaminifu na mtiifu? Wasaidie watoto wako kufikiria juu ya kitu wanachoweza kutoa dhabihu ili kumtii Mungu au kusaidia katika kazi Yake.

    2:7

    Chapter 7: Witnesses See the Gold Plates: 1829–1830

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

mchoro wa Yesu Kristo akiwa Gethsemane

Kristo Anasali katika Bustani ya Gethsemane, na Hermann Clementz

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto