Njoo, Unifuate
Machi 10–16: “Kuinuka kwa Kanisa la Kristo”: Mafundisho na Maagano 20–22


“Machi 10–16, ‘Kuinuka kwa Kanisa la Kristo’: Mafundisho na Maagano 20–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 20–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Joseph Smith akihubiri kwenye chumba kilichojaa watu

Machi 10–16: “Kuinuka kwa Kanisa la Kristo”

Mafundisho na Maagano 20–22

Kazi ya Mwokozi ya kukileta Kitabu cha Mormoni sasa ilikuwa imekamilika. Lakini kazi Yake ya Urejesho ilikuwa ndio imeanza tu. Katika nyongeza ya kurejesha mafundisho na mamlaka ya ukuhani, Bwana aliliweka wazi kupitia mafunuo ya awali kwamba Yeye pia alitaka kurejesha taasisi rasmi—Kanisa Lake (ona Mafundisho na Maagano 10:53; 18:5). Mnamo Aprili 6, 1830, zaidi ya waaminio 40 walisongamana kwenye nyumba ya magogo ya familia ya Whitmer huko Fayette, New York, kushuhudia kuanzishwa kwa Kanisa la Yesu Kristo.

Baadhi ya watu wanajiuliza kwa nini Kanisa lililopangwa ni muhimu?? Jibu linaweza kupatikana, angalau kwa sehemu, katika mafunuo yaliyohusiana na mkutano ule wa kwanza wa Kanisa mnamo 1830. Yanaelezea baraka ambazo zisingewezekana kama Kanisa la kweli la Yesu Kristo lisingekuwa “limeundwa na kuanzishwa” katika siku za mwisho (Mafundisho na Maagano 20:1).

Ona pia Saints, 1:84–86; “Build Up My Church,” katika Revelations in Context, 29–32.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 20–21

Yesu Kristo Amerejesha Kanisa Lake

Kwa nini tuna Kanisa lililopangwa? Labda jibu bora zaidi ni “Kwa Sababu Yesu Kristo amelipanga.” Unapojifunza Mafundisho na Maagano 20–21, unaweza gundua mifanano kati ya lile ambalo Yeye alillianzisha kalei na hili alilolirejesha leo. Tumia mistari ifuatayo ili kujifunza kuhusu Kanisa la Mwokozi katika nyakati za kale: Mathayo 16:15–19; Yohana 7:16–17; Waefeso 2:19–22; 3 Nefii 11:23–26; Moroni 4–5. Tumia mistari hii ili kujifunza kuhusu Kanisa lililorejeshwa: Mafundisho na Maagano 20:17–25, 60, 72–79; 21:1–2. Ungeweza kuandika kile ambacho umekipata katika mchoro kama huu:

Mafundisho

Ibada

Mamlaka ya ukuhani

Manabii

Kanisa la kale la Kristo

Mafundisho

Ibada

Mamlaka ya ukuhani

Manabii

Kanisa la Kristo lililorejeshwa

Mafundisho

Ibada

Mamlaka ya ukuhani

Manabii

Je, unajifunza nini kutoka kwenye shughuli hii kuhusu kwa nini Yesu Kristo alilianzisha—na kurejesha—Kanisa Lake?

Ona pia Dallin H. Oaks, “Hitaji la Kanisa,” Liahona, Nov. 2021, 24–26.

Alika kushiriki. Unapowaalika watu kushiriki kile walichokuwa wakijifunza wao wenyewe, watahisi kutiwa moyo kuendelea na kujifunza kwao binafsi. Ungeweza kuwaalika wengine kushiriki nini?

Mafundisho na Maagano 20:37, 75–7922

Ibada takatifu hunisaidia kuwa kama Mwokozi.

Wakati Kanisa lilipoundwa, Bwana aliwafundisha Watakatifu Wake kuhusu ibada takatifu, ikijumuisha ubatizo na sakramenti. Unaposoma kuhusu ibada hizi, tafakari jinsi gani zinakusaidia wewe kuhisi kuunganika na Mwokozi? Kwa mfano, ibada hizi zinakusaidiaje wewe kudumisha “uamuzi wako wa kumtumikia Yesu Kristo hadi mwisho”? (mstari wa 37). Ungeweza pia kusoma sala za sakramenti (mstari wa 77, 79) na fikiria kwamba unazisikia kwa mara ya kwanza. Je, ni umaizi gani unaoupokea?

Ona pia D. Todd Christofferson, “Kwa Nini Njia ya Agano,” Liahona, Mei 2021, 116–19.

mvulana akipitisha sakramenti

Mafundisho na Maagano 20:38–60.

Huduma ya Ukuhani inabariki waumini wa Kanisa na familia zao.

Je, umewahi kufikiria kuhusu ni kwa nini ilikuwa muhimu kwa Mwokozi kurejesha ukuhani katika Kanisa Lake? Kusoma kile ambacho Yeye aliwaagiza wenye ukuhani kufanya katika Mafundisho na Maagano 20:38–60 kunaweza kukupa baadhi ya umaizi. Je, Mwokozi amekubariki vipi wewe na familia yako kupitia kazi zilizoelezewa katika mistari hii?

Kwa nyongeza kwa wale waliotawazwa katika ukuhani, wanawake ambao wamesimikwa katika Kanisa pia wanatumia mamlaka ya Mungu wanaposhiriki katika kazi Yake. Ili kujifunza ni kwa namna gani, ona ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Funguo na Mamlaka ya Ukuhani” (Liahona, Mei 2014, 49–52).

Ona pia Topics and Questions, “Joseph Smith’s Teachings about Priesthood, Temple, and Women,” Maktaba ya Injili.

Mafundisho na Maagano 21

ikoni ya seminari
Kutii neno la Mungu kupitia manabii Wake kutanipa ulinzi wa kiungu.

Mafundisho na Maagano 21:4–9 inajumuisha mialiko ya kumfuata nabii wa Bwana na ahadi madhubuti kwa wale wanaofanya hivyo. Mawazo yafuatayo yanaweza kukusaidia kutafakari mistari hii:

  • Ni maneno gani katika mstari wa 4–5 yanaelezea kile Mwokozi anakutaka wewe ufanye kwa maneno ya manabii Wake walio hai? Kwa nini unafikiri “uvumilivu na imani” vinahitajika ili kufanya hili?

  • Tafakari taswira ambayo Mwokozi anaitumia katika mstari wa 6 ili kuelezea baraka ya kumfuata nabii Wake. Unadhani inamaanisha nini kwa “milango ya jehanamu”? Je, Bwana “anatawanyaje nguvu za giza” kwa ajili yako? Je, inamaanisha nini kwa “mbingu zitetemeke kwa ajili yenu”?

  • Bwana anakutaka wewe ufanye nini kupitia Rais wa sasa wa Kanisa? Bwana ametimizaje ahadi Zake kwa kuwa umefuata ushauri Wake?

Orodhesha umaizi wa ziada unaoupata kutoka kwenye sehemu zifuatazo za ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Nabii wa Mungu” (Liahona, Mei 2018, 24–27):

  • Kwa nini Tunamfuata Nabii:

  • Mlinzi Juu ya Mnara:

  • Msishangae:

Ona pia “Watchman on the Tower” (video), ChurchofJesusChrist.org; Topics and Questions, “Prophets,” Maktaba ya Injili; “Sauti ya Nabii,” Nyimbo za Dini, na. 13.

4:17

Watchman on the Tower

(Ezekiel 33:1-7) The Lord calls prophets to be the "watchmen" on the tower.

Kwa mawazo zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni 02 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 20–21

Kanisa la Yesu Kristo limerejeshwa.

  • Fikiria kutumia kichwa cha habari cha sehemu kwa ajili ya Mafundisho na Maagano 21, Sura ya 9 ya Hadithi za Mafundisho na Maagano, au video “Organization of the Church” (ChurchofJesusChrist.org) ili kusaidia watoto wako kuelewa nini kilitokea siku ya kuanzishwa Kanisa.

    1:35

    Chapter 9: Organization of the Church of Jesus Christ: 6•April 1830

  • Labda watoto wako wangeweza kulinganisha picha za Yesu Kristo, mtu anayehudumu, ubatizo na sakramenti pamoja na mistari katika sehemu ya 20 (ona mstari ya 21–23, 47, 72–74, 75–79). Tumia picha hizi na mistari ili kujadili baraka tulizonazo kwa sababu Yesu Kristo amerejesha Kanisa Lake.

Mafundisho na Maagano 20:37, 41, 71–74

Wakati ninapobatizwa na kuthibitishwa, ninaahidi kumfuata Yesu Kristo.

  • Watoto wako wanaweza kuona picha ya mtoto akibatizwa na kuthibitishwa. Wanaweza kuonyesha jinsi gani inalingana na maelekezo katika Mafundisho na Maagano 20:41, 71–74. Tunajifunza nini kutoka Mafundisho na Maagano 20:37 kuhusu watu wanaotaka kubatizwa? Mngeweza pia kuimba “When I Am Baptized”kwa pamoja (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,103), au angalieni video “The Baptism of Jesus” (Maktaba ya injili).

    2:54

    The Baptism of Jesus

    Jesus seeks out John the Baptist and is baptized in order to fulfill all righteousness.

    Msichana anabatizwa na msichana anathibitishwa
  • Kama watoto wako tayari wamebatizwa na kuthibitishwa, waulize kuhusu uzoefu wao. Je, wanazo picha ambazo wangeweza kuonyesha? Zungumza nao kuhusu kile wanachofanya ili kumfuata Yesu Kristo na jinsi gani Yeye amewabariki.

Mafundisho na Maagano 20:75–79

Ninaweza kujichukulia juu yangu jina la Yesu na daima kumkumbuka Yeye

  • Watoto wako wangeweza kutafuta neno “radhi” katika mistari yote miwili ya Mafundisho na Maagano 20:37 (kuhusu ubatizo) na mstari wa 77 (sala ya sakramenti). Je, Bwana anatutaka sisi tuwe radhi kufanya nini? Pengine watoto wako wangeweza kuangalia kitu ambacho kina jina juu yake (kama vile jina la bidhaa au jina la mtu). Jina linatuambia nini kuhusu kitu hicho? Je, inamaanisha nini kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo?

  • Fikiria kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 20:77 na waombe watoto wako kutambua ahadi tunazofanya kama sehemu ya sakramenti. Pengine wangeweza kupeana zamu ya kuigiza kitu wanachoweza kufanya ili “daima kumkumbuka” Mwokozi na kubashiri matendo ya kila mmoja yalivyo. Kulingana na mstari wa 77, ni kwa jinsi gani tunabarikiwa wakati daima tunapomkumbuka Mwokozi?

Mafundisho na Maagano 21:4–6

Yesu ananibariki ninapomfuata nabii Wake.

  • Baada ya kugundua mialiko na ahadi katika Mafundisho na Maagano 21:4–6, watoto wako wangeweza kuangalia kwenye picha ya nabii wa sasa na kuelezea kitu walichojifunza au kusikia kutoka kwake. Shiriki na kila mmoja njia ambazo Yesu Kristo amekubarki kwa kumfuata nabii Wake.

Rais Nelson

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

Joseph Smith akisimikwa na Oliver Cowdery

Oliver Cowdery Akimtawaza Joseph Smith, na Walter Rane

ukurasa wa shughuli ya watoto