“Machi 24–30: ‘Mambo Yote Lazima Yafanyike kwa Utaraibu’: Mafundisho na Maagano 27–28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 27-28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Machi 24–30: “Mambo Yote Lazima Yafanyike katika Utaratibu”
Mafundisho na Maagano 27–28
Neno ufunuo lilikuwa bado kwa kiasi ni wazo jipya kwa Watakatifu wakati Urejesho ukiendelea kutokeza. Waumini wa mwanzo wa Kanisa walijua kwamba Nabii Joseph Smith angeweza kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa. Lakini wengine je? Maswali kama haya yakawa ya ukosoaji wakati Hiram Page, mmoja wa Mashahidi Wanane wa mabamba ya dhahabu, alipoamini alikuwa amepokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa. Watakatifu wengi waaminifu waliamini kwamba mafunuo haya yalikuwa kutoka kwa Mungu. Bwana alijibu kwa kufundisha kwamba katika Kanisa Lake “mambo yote lazima yafanyike katika utaratibu” (Mafundisho na Maagano 28:13). Hii ilimaanisha kuwa amekuwa na mtu mmoja tu “aliyeteuliwa kupokea amri na mafunuo kwa ajili ya Kanisa zima (Mafundisho na Maagano 28:2). Wengine, hata hivyo, wangeweza kupokea ufunuo binafsi kwa ajili ya sehemu zao katika kazi ya Bwana. Kwa kweli, maneno ya Bwana kwa Oliver Cowdery ni ukumbusho kwetu sote: “itatolewa kwako … juu ya nini utakachofanya” (Mafundisho na Maagano 28:15).
Ona pia “All Things Must Be Done in Order,” katika Revelations in Context, 50–53.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Ninapokea sakramenti kwa ukumbusho wa Yesu Kristo.
Sally Knight na Emma Smith walibatizwa Juni 1830, lakini uthibitisho wao ulivurugwa na kundi la wahuni. Miezi miwili baadae, Sally na mumewe, Newel, waliwatembelea Emma na Joseph, na iliamuliwa kwamba sasa wathibitishwe na kwamba kundi lile lishiriki sakramenti pamoja. Wakati akiwa njiani kuchukua divai kwa ajili ya sakramenti, Joseph alisimamishwa na malaika.
Soma Mafundisho na Maagano 27:1–4 ili kugundua kitu ambacho malaika alimfundisha kuhusu sakramenti. Mistari hii inakufundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyokutaka wewe kuikaribia sakramenti? Unafikiri inamaanisha nini kuipokea “jicho lako llikiwa katika utukufu [Wake] pekee”? Tafakari hili—na kutafuta umaizi mwingine kuhusu sakramenti—unaposoma Luka 22:19–20 na 3 Nefi 18:1–11. (Ona pia the videos “The Last Supper,” “Jesus Christ Blesses Bread in Remembrance of Him,” and “Jesus Christ Blesses Wine in Remembrance of Him,” Maktaba ya Injili).
Ili kujifunza kuhusu kuifanya sakramenti kuwa tukio la kuabudu, fikiria kujifunza ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Mkate Ulio Hai Ambao Ulishuka Kutoka Mbinguni” (Liahona, Nov. 2017, 36–39). Mzee D.Todd Christofferson alifundisha nini ambacho kinaweza kukusaidia kuhisi muunganiko mkubwa na Mwokozi kupitia sakramenti? Tafakari unaweza kufanya nini vyema zaidi ili kujitayarisha kupokea alama za Upatanisho wa Mwokozi na kuzichukulia kwa unyenyekevu au kusudi zaidi.
Fikiria kuimba, kusikiliza au kusoma nyimbo za sakramenti, kama “Twapokea Sakramenti” (Nyimbo za Dini, na. 90), na kuandika hisia zako kuhusu kushiriki katika ibada hii takatifu.
Ona pia Mafundisho na Maagano 20:77, 79; 59:9–13; Topics and Questions, “Sacrament,” Maktaba ya Injili; “Obtaining and Retaining a Remission of Sins through Ordinances,” katika David A. Bednar, “Daima Shikilia Ondoleo la Dhambi Zako,” Liahona, Mei 2016, 60–62.
Bwana huwapa watumishi Wake ukuhani ili kuelekeza kazi Yake.
Tunajua nini kuhusu manabii waliotajwa katika mistari hii? Ungeweza kuchunguza taarifa kuwahusu wao katika Mwongozo wa Maandiko. Ni baraka gani zimefunguliwa kwa ajili yetu kupitia funguo ambazo manabii hawa walizishikilia?
Mafundisho na Maagano 27:15–18
Deraya ya Mungu hunisaidia kusimama dhidi ya uovu.
Rais M. Russell Ballard alisema: “Hakuna hata kitu kimoja kilicho kikuu na muhimu tunachoweza kufanya ili kujilinda wenyewe kiroho. Nguvu ya kweli ya kiroho ipo katika vitendo kadhaa vidogo sana vilivyofumwa pamoja katika kitambaa cha kiroho kilichoimarishwa ambacho kinalinda na kukinga dhidi ya uovu wote” (“Kuwa Imara katika Bwana,” Ensign, Julai 2004, 8).
Unapojifunza kuhusu deraya ya Mungu katika Mafundisho na Maagano 27:15–18, ungeweza kutengeneza jedwali kama hili hapa. Unafanya nini ili kuvaa kila kipande cha deraya ya Mungu?
Kipande cha deraya |
Sehemu ya mwili inalindwa |
Kile kinachowakilishwa na sehemu hiyo ya mwili |
---|---|---|
Kipande cha deraya Dirii ya haki | Sehemu ya mwili inalindwa Moyo | Kile kinachowakilishwa na sehemu hiyo ya mwili Matamanio yetu na mapendeleo |
Kipande cha deraya Chepeo ya wokovu | Sehemu ya mwili inalindwa Kichwa au akili | Kile kinachowakilishwa na sehemu hiyo ya mwili |
Kipande cha deraya | Sehemu ya mwili inalindwa | Kile kinachowakilishwa na sehemu hiyo ya mwili |
Kipande cha deraya | Sehemu ya mwili inalindwa | Kile kinachowakilishwa na sehemu hiyo ya mwili |
Ona pia Waefeso 6:11–18; Jorge F. Zeballos, “Kujenga Maisha Kinzani Dhidi ya yule Adui,” Liahona, Nov. 2022, 50–52.
Yesu Kristo huongoza Kanisa Lake kupitia manabii Wake walio hai.
Fikiria vile ambavyo ingekuwa kama mtu yeyote angeweza kupokea amri na ufunuo kwa ajili ya Kanisa lote. Wakati Hiram Page alipodai kuwa amepokea ufunuo kama ule, waumini wa Kanisa walichanganyikiwa. Katika Mafundisho na Maagano 28, Bwana alifunua utaratibu kwa ajili ya ufunuo katika Kanisa Lake. Unajifunza nini kutoka sehemu hii kuhusu wajibu maalumu wa Rais wa Kanisa? Unajifunza nini kutoka sehemu hii kuhusu jinsi Mungu anavyoweza kukuelekeza?
Ona pia Dale G. Renlund, “Mfumo wa Ufunuo Binafsi,” Liahona, Nov. 2022, 16–19.
Kwa nini misheni kwa Walamani ilikuwa ya kipekee?
Kusudi moja la Kitabu cha Mormoni ni “kwamba Walamani waweze kuja katika ufahamu wa baba zao, na kwamba waweze kujua ahadi za Bwana” (Mafundisho na Maagano 3:20). Hii ilikuwa kulingana na ahadi Bwana alizofanya kwa manabii wengi wa Kitabu cha Mormoni (ona, kwa mfano, 1 Nefi 13:34–41; Enoshi 1:11–18; Helamani 15:12–13). Waumini wa mwanzo wa Kanisa waliwafikiria Wahindi wa Amerika kuwa ni wazao wa watu wa Kitabu cha Mormoni. (Msimamo rasmi wa Kanisa leo ni kwamba Walamani “ni miongoni mwa mababu wa Wahindi wa Amerika” [Dibaji ya Kitabu cha Mormoni].)
Kusoma zaidi kuhusu misheni ya Oliver kwa Wahindi wa Amerika, ona “A Mission to the Lamanites,” Revelations in Context, 45–49. Je, misheni hii inakufundisha nini kuhusu Bwana na kazi Yake?
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Sakramenti inanisaidia kumkumbuka Yesu Kristo.
-
Watoto wanaweza kujiuliza kwa nini tunatumia maji kwa ajili ya sakramenti wakati Yesu alitumia divai (ona Luka 22:19–20; 3 Nefi 18:1–11). Mngeweza kusoma Mafundisho na Maagano 27:1–2 kwa pamoja na kujadili inamaanisha nini kupokea sakramenti “jicho lako likiwa kwa utukufu wa [Mungu] pekee” (mstari wa 2). Tunaweza kufanya nini ili kufokasi umakini wetu kwa Mwokozi wakati tunapopokea sakramenti?
-
Labda kuwa na picha, mistari ya maandiko au mashairi ya wimbo kuhusu Mwokozi kungeweza kuwasaidia watoto wako kumkumbuka Yeye wakati wanapopokea sakramenti. Yawezekana wakafurahia kutengeneza kijitabu cha baadhi ya picha hizi, mistari na mashairi. Wangeweza kuchora picha zao wenyewe au kutafuta baadhi kwenye jarida la Rafiki.
Mafundisho na Maagano 27:15–18
Deraya ya Mungu hunilinda mimi.
-
Ungeweza kuwaonyesha watoto wako picha ya deraya kama ile katika muhtasari huu au katika ukurasa wa shughuli katika muhtasari wa Waefeso katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2023. Unaposoma Mafundisho na Maagano 27:15–18, wasaidie watoto kutafuta vipande vya deraya katika picha. Je, deraya ya Mungu inatusaidiaje sisi “kushinda siku ya uovu”? (mstari wa 15).
Mafundisho na Maagano 28:2, 6–7
Nabii hupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa; mimi naweza kupokea ufunuo kwa ajili ya maisha yangu.
-
Kama unao watoto kadhaa, ungewaalika kucheza “mfuate kiongozi,” lakini waombe watoto wawili au zaidi kuwa kiongozi kwa wakati huo huo. Kunatokea nini inapokuwa kuna viongozi zaidi ya mmoja? Kisha mnaweza kujifunza kuhusu Hiram Page (ona “Sura ya 14: The Prophet and Revelations for the Church,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano,” 56–57, au video inayofanana nayo katika Maktaba ya Injili; au sehemu ya kichwa cha habari cha Mafundisho na Maagano 28). Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni alisahihisha mkanganyiko wa waumini wa Kanisa wa mwanzo? Ni kwa jinsi gani Yeye analiongoza Kanisa leo? (ona Mafundisho na Maagano 28:2.) Toa ushuhuda wako kwamba nabii wa sasa ameitwa na Bwana ili kuliongoza Kanisa Lake katika siku yetu.
-
Wakati ufunuo kwa ajili ya Kanisa daima utatolewa kupitia nabii, sisi sote tunaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu. Ungeweza kuwasaidia watoto wako kupekua baadhi ya maandiko yafuatayo na kutengeneza orodha ya njia ambazo Roho Mtakatifu anaweza kutuongoza sisi: Mafundisho na Maagano 28:1, 4, 15; Yohana 14:26; Moroni 8:26; 10:4–5. Shiriki na kila mmoja jinsi ulivyoongozwa na Roho Mtakatifu.