“Machi 31–Aprili 6: ‘Yesu Kristo Atawakusanya Watu Wake’: Mafundisho na Maagano 29” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 29,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Machi 31–Aprili 6: “Yesu Kristo Atawakusanya Watu Wake”
Mafundisho na Maagano 29
Japokuwa Kanisa la Yesu Kristo lilikuwa limeanzishwa mnamo mwaka 1830, kweli nyingi za injili zilikuwa bado hazijafunuliwa, na baadhi ya waumuni wa Kanisa wa mwanzo walikuwa na maswali. Walikuwa wamesoma unabii katika Kitabu cha Mormoni kuhusu kukusanywa kwa Israeli na ujenzi wa Sayuni (ona 3 Nefi 21). Ni kwa jinsi gani hilo lingetokea? Mafunuo ambayo Hiram Page alidai kuyapokea yalibashiri juu ya mada hiyo, ambayo iliongeza tu udadisi wa waumini (ona Mafundisho na Maagano 28). Watu wengine walijiuliza kuhusu Anguko la Adamu na Hawa na kifo cha kiroho. Bwana alikaribisha maswali haya mnamo 1831, na anakaribisha maswali yetu leo. “Lo lote mtakaloomba katika imani,” Aliwaambia Watakatifu, “mkiwa mmeungana katika sala mkiamini kulingana na amri yangu, mtapokea” (Mafundisho na Maagano 29:6). Kwa kweli, kama ufunuo uliojaa mafundisho katika Mafundisho na Maagano 29 unavyoonesha, Bwana wakati mwingine anajibu maswali yetu kwa kutupatia ukweli na maarifa zaidi ya maswali tunayouliza.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Baba wa Mbinguni ana mpango kwa ajili ya wokovu wa watoto Wake.
Mafundisho na Maagano 29 inafundisha kweli nyingi kuhusu mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake. Unaposoma, tafuta kweli unazojifunza kuhusu kila moja ya sehemu zifuatazo za mpango:
-
Maisha kabla ya kuja duniani (ona mstari wa 36–37)
-
Uumbaji (ona mstari wa 31–33)
-
Anguko la Adamu na Hawa (ona mstari wa 40–41)
-
Maisha ya duniani (ona mstari wa 39, 42–45)
-
Upatanisho wa Yesu Kristo (ona mstari wa 1, 42–43, 46–50)
-
Ufufuko (ona mstari wa 13, 26)
-
Hukumu ya Mwisho (ona mstari wa 12–13, 27–30)
Ni umaizi gani mpya ulioupata? Kama ni wa msaada kwako, ungeweza kuandika katika nafasi iliyotolewa pamoja na picha mwishoni muhtasari huu. Ni kwa jinsi gani kweli hizi huathiri maisha yako?
Ona pia Mada na Maswali, “Mpango wa Wokovu,” Maktaba ya Injili.
Yesu Kristo ananialika kusaidia kukusanya watu Wake kabla ya Ujio Wake wa Pili.
Yesu Kristo anazungumzia juu ya kuwakusanya watu Wake “kama kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake” (Mafundisho na Maagano 29:2). Mlinganisho huu unakufundisha nini wewe kuhusu Yesu Kristo? Ni mawazo gani ya ziada au misukumo inayokuja unapojifunza kielelezo hiki cha kuku na vifaranga katika muhtasari huu? Fikiria kuhusu jinsi ulivyohisi Yesu Kristo akikukusanya na kukulinda wewe.
Unaposoma Mafundisho na Maagano 29:1–11, tafuta umaizi kuhusu:
-
Ni nani watakaokusanywa.
-
Inamaanisha nini “kukusanyika” kwa Kristo.
-
Kwa nini tunakusanyika Kwake.
Tafakari kwa nini unataka watu wengine wakusanyike kwa Yesu Kristo Unahisi kuvutiwa kufanya nini ili kusaidia?
Ungeweza kujiuliza mwenyewe maswali hayo hayo wakati ukiangalia video ya “A Witness of God” (Maktaba ya Injili) au kusoma au kusikiliza wimbo wa dini kuhusu kukusanya, kama vile “Israeli, Mnaitwa” (Nyimbo za Dini, no. 7). Unahisi Bwana anajaribu kukufundisha nini kuhusu kazi Yake ya kukusanya?
Rais Russell M. Nelson alisema: “Sasa kukusanyika kunafanyika katika kila taifa. Bwana ametangaza kuanzishwa kwa Sayuni katika kila eneo ambapo amewapa watakatifu Wake kuzaliwa kwao na utaifa wao” (“Kukusanyika kwa Israeli Iliyotawanyika,” Liahona, Nov. 2006, 81). Ni kwa jinsi gani kukusanyika katika njia hii kunatusaidia sisi “kujitayarisha katika mambo yote” kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi? (mstari wa 8; ona pia mstari wa 14–28).
Ona pia Russell M. Nelson na Wendy W. Nelson, “Tumaini la Israeli” (worldwide youth devotional, Juni 3, 2018), Maktaba ya Injili, D. Todd Christofferson, “Mafundisho ya Kuwa Sehemu Ya,” Liahona, Nov. 2022, 53-56; Mada na Maswali, “Kukusanyika kwa Israeli,” Maktaba ya Injili.
Mafundisho na Maagano 29:31–35
“Mambo yote kwangu ni ya kiroho.”
Unapojifunza Mafundisho na Maagano 29:31–35, jiulize mwenyewe, “inamaanisha nini amri zote ni za kiroho?” Unaweza kuorodhesha amri chache na kufikiria kweli za kiroho zinazohusiana na kila moja. Marejeleo ya Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi ungeweza kuwa wa msaada—unafundisha baadhi ya kweli za milele nyuma ya amri kadhaa za Mungu.
Ni kwa jinsi gani kujua kwamba “mambo yote … ni ya kiroho” kunaathiri jinsi tunavyozitazama amri za Mungu? Fikiria kutafuta maana ya kiroho au dhumuni katika vipengele vingine vya maisha yako vile vile.
Ona pia 2 Nefi 9:39.
Mafundisho na Maagano 29:36–50
Yesu Kristo anatukomboa kutokana na Anguko.
Ungewezaje kutumia Mafundisho na Maagano 29:36–50 ili kuelezea kwa nini tunahitaji ukombozi kupitia Yesu Kristo?
Anguko la Adamu na Hawa lilileta mauti na dhambi ulimwenguni, lakini pia lilitayarisha njia ya ukombozi na shangwe kupitia Kristo. Pamoja na wazo hilo akilini, soma mstari wa 39–43 na andika maneno na vifungu vya maneno ambavyo vinakuletea wewe shangwe. Ni kitu gani kinakuvutia wewe kuhusu kile Adamu na Hawa walisema kuhusu Anguko katika Musa 5:10–12?
Ona pia “Why We Need a Savior” (video), Maktaba ya Injili.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Baba wa Mbinguni anao mpango kwa ajili ya wokovu wa watoto Wake.
-
Ili kuanzisha maongezi kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yetu sisi, wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu wakati ambapo mlitengeneza mpango, kama vile kwa ajili ya safari au kwa ajili ya kukamilisha kazi fulani. Ungeweza pia kushiriki mifano ya mipango, kama vile kalenda yenye shughuli zilizoandikwa juu yake au maelekezo ya kutengeneza kitu. Kwa nini mipango ni muhimu? Mngeweza pia kuzungumza kuhusu kile Baba wa Mbinguni anataka kukikamilisha na ni kwa jinsi gani mpango Wake unatusaidia sisi kukikamilisha kitu hicho.
-
Ungeweza kutumia picha mwishoni mwa muhtasari huu ili kuwasaidia watoto wako kutafuta mistari katika Mafundisho na Maagano 29 ambayo inafundisha kuhusu sehemu tofauti za mpango wa Baba wa Mbinguni. Ungeweza pia kukata picha hizo na kuwauliza watoto wako kuziweka katika mpangilio sahihi. Kwa nini tunashukuru kujua kwamba Baba wa Mbinguni anao mpango kwa ajili yetu sisi? Kujua kuhusu hilo kunashawishije maisha yetu ya kila siku?
Mafundisho na Maagano 29:1–2, 7–8
Yesu Kristo anakusanya watu wake kabla ya kuja Kwake tena.
-
Kielelezo hapo chini cha kuku kukusanya vifaranga vyake au ile video ya “Chicks and Hens” (ChurchofJesusChrist.org) ingeweza kuwasaidia watoto wako kupata taswira ya analojia hii katika Mafundisho na Maagano 29:1–2. Kisha mngeweza kusoma pamoja na kuzungumza mmoja na mwingine kuhusu jinsi gani kuku analinda vifaranga vyake na ni kwa jinsi gani hilo ni sawa sawa na kile Mwokozi anachoweza kufanya kwetu sisi.
-
Ni kitu gani kingewashawishi watoto wako kutaka kumsaidia Mwokozi kuwakusanya watu Wake? Pengine wangependa kusikia uzoefu wa mtu ambaye “amekusanyika Kwake kwa kujiunga na Kanisa Lake. Kwa mfano, nani aliitambulisha familia yako Kanisani? Ni kwa namna gani tumeweza kubarikiwa kwa kukubali wito wa Mwokozi wa kukusanyika Kwake? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wengine kukusanyika Kwake? (Ona “A Message for Children from President Russell M. Nelson” [video], ChurchofJesusChrist.org.)
Yesu Kristo atakuja tena.
-
Picha ya Ujio wa Pili wa Mwokozi (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 66) au wimbo kuhusu hilo (kama vile “When He Comes Again,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83) ingeweza kukusaidia wewe na watoto wako kujadili Mafundisho na Maagano 29:11. Wasaidie watoto kugundua virai katika maandiko ambavyo vinaelezea kile wanachoona katika picha au wimbo. Shirikini mmoja na mwingine jinsi mnavyohisi kuhusu ujio wa Yesu duniani tena.