Njoo, Unifuate
Mei 5–11: “Ahadi … Zitatimizwa”: Mafundisho na Maagano 45


“Mei 5–11: ‘Ahadi … Zitatimizwa’: Mafundisho na Maagano 45,’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 45,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani 2025

familia hekaluni

Mei 5–11: “Ahadi … Zitatimizwa”

Mafundisho na Maagano 45

Ufunuo katika sehemu ya 45 ulipokelewa, kulingana na kichwa cha habari cha sehemu, “kwa shangwe ya Watakatifu.” Na kuna mambo mengi ya kuwa na shangwe kuyahusu katika ufunuo huu. Ndani yake Mwokozi anatoa ahadi Yake nyororo ya kusihi kwa ajili yetu mbele ya Baba (ona mistari 3–5). Yeye anazungumza juu ya agano Lake la milele linalosambaa kote ulimwenguni, kama “mjumbe … atakayeitengeneza njia mbele [Yake]” (mstari wa 9). Na anatoa unabii wa Ujio Wake wa Pili mtukufu. Mwokozi hufanya haya yote huku pia akitambua kwamba hizi ni nyakati zenye shida (ona mstari wa 34), kwa sehemu kwa sababu ya hatari ambazo zitatokea kabla ya ujio Wake. Lakini hatari hiyo, giza hilo si thabiti sana kuzima nuru ya tumaini. “Kwani amini ninawaambia,” Bwana alitangaza, “kwamba Mimi ni … nuru ile ing’aayo gizani” (mstari wa 7). Hiyo pekee ni sababu ya kupokea ufunuo huu—ulio na ushauri na maonyo na ukweli wowote ule Yeye anaotaka kutupatia—kwa shangwe.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 45:1–5

ikoni ya seminari
Yesu Kristo ndiye Mwombezi wangu kwa Baba.

Wakati tunapohisi hatutoshi au hatustahili mbele za Mungu, tunaweza kupata hakikisho kutoka kwenye maneno ya Mwokozi katika Mafundisho na Maagano 45:1–5. Unapopekua mistari hii, zingatia maswali kama haya:

  • Ni maneno au virai gani katika mistari hii unahisi vina maana kwako hasa?

  • Mwombezi ni mtu ambaye anamuunga mkono au kumpendekeza mtu au jambo waziwazi. Kulingana na mistari hii, ni kwa jinsi gani Yesu Kristo anafanya hili kwa ajili yako? Ni nini kinamstahilisha Yeye kufanya hivyo?

  • Je, ni kitu gani kinakuvutia kuhusu maneno ya Mwokozi kwa Baba? (mistari 4–5).

Ungeweza pia kujifunza kile Mzee Dale G. Renlund alichofundisha kuhusu Yesu Kristo, Mwombezi wetu katika “Chagueni Hivi Leo” (Liahona, Nov. 2018, 104–5). Kulingana na Mzee Renlund, dhumuni la Mwokozi lilikuwa lipi ikilinganishwa na la Lusiferi?

Vifungu vifuatavyo vinaweza kuongeza kwenye uelewa wako wa jukumu la Mwokozi kama Mwombezi. Unapojifunza, fikiria kuandika virai au kweli ambazo ungeweza kushiriki na wengine: 2 Nefi 2:8–9; Mosia 15:7–9; Moroni 7:27–28; Mafundisho na Maagano 29:5; 62:1. Kwa nini virai hivi ni muhimu kwako?

Ona pia “Nastaajabu,” Nyimbo za Dini, na 106; Topics and Questions, “Atonement of Jesus Christ,” Maktaba ya Injili; “The Mediator” (video), Maktaba ya Injili.

10:47

The Mediator

A portrayal of the analogy Elder Boyd K. Packer used in his April 1977 general conference address. A young man who fails to pay a debt is saved from the grasp of justice through the mediation of a friend.

Mafundisho na Maagano 45:9–10

Injili ni bendera kwa mataifa.

Siku za kale, bendera ilikuwa ni bango lililochukuliwa kwenda nalo vitani ili kuyaleta pamoja na kuyaunganisha majeshi. Bendera pia ni mfano au sheria ambayo vitu vingine vinaweza kupimwa dhidi yake. Unaposoma Mafundisho na Maagano 45:9–10, tafakari jinsi ambavyo maagano yako na Bwana yamekuwa bendera kwako.

Mafundisho na Maagano 45:11–75

Yesu Kristo atarudi katika utukufu.

Ujio wa Pili wa Bwana umeelezwa kama ulio “mkuu” na wa “kuogofya” (Malaki 4:5). Katika Mafundisho na Maagano 45, maelezo yote yanaonekana kufaa. Ufunuo huu unajumuisha vyote, maonyo ya busara na ahadi zenye tumiani kuhusu ujio wa Bwana. Unapojifunza mistari 11–75, tafakari jinsi unavyoweza kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili kwa imani katika Kristo badala ya kuogopa. Andika kile ambacho umegundua katika jedwali kama hili:

Unabii au ahadi

Kile ninachoweza kufanya

Unabii au ahadi

Nuru (injili) itakuja kwa wale wanaoketi gizani (mstari wa 28)

Kile ninachoweza kufanya

Pokea nuru—na uishiriki (mstari wa 29)

Unabii au ahadi

Kile ninachoweza kufanya

Unabii au ahadi

Kile ninachoweza kufanya

Unabii au ahadi

Kile ninachoweza kufanya

Katika video “Men’s Hearts Shall Fail Them” (Maktaba ya Injili), ni ushauri upi Rais Russell M. Nelson aliutoa ili kutusaidia sisi kukabiliana na hali za kuogofya kwa amani?

3:24

Men's Hearts Shall Fail Them

Elder Russell M. Nelson shares a personal story to give encouragement for when we feel "weak in the heart."

Mafundisho na Maagano 45:31–32; 56–57

Ninaweza “kusimama katika mahali patakatifu” na wala sitaondoshwa.

Unajifunza nini katika Mafundisho na Maagano 45:31–32, 56–57 kuhusu kujitayarisha kwa ajili ya ujio wa Bwana? “Mahali pako patakatifu” ni wapi? Je, inamaanisha nini “kutoondoshwa”? Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya pale ulipo pawe patakatifu zaidi?

Kumbuka kwamba Bwana alirejelea mfano wa wanawali 10, akilinganisha mafuta katika mfano na ukweli na Roho Mtakatifu. Fikiria kusoma mfano huo katika Mathayo 25:1–13 ukiwa na hilo akilini. Je, ni umaizi upi unaupata?

Ona pia David A. Bednar, “Kama Mngalinijua Mimi,” Liahona, Nov. 2016, 102–5.

wanawali watano wenye busara

Mfano wa Wanawali Kumi, na Dan Burr

Mafundisho na Maagano 45:11–15; 66–71

Sayuni ni mahali pa usalama kwa ajili ya Watakatifu wa Mungu.

Watakatifu katika kipindi cha Joseph Smith walikuwa na shauku ya kuijenga Sayuni, Yerusalemu Mpya (ona Etheri 13:2–9); Musa 7:18, 62–64). Unajifunza nini kuhusu Sayuni—mji wa kale wa siku za Henoko na mji wa siku za mwisho—kutoka Mafundisho na Maagano 45:11–15, 66–71? Leo amri ya kuanzisha Sayuni inarejelea kuanzisha ufalme wa Mungu popote tunapoishi. Unaweza kufanya nini ili kusaidia kujenga Sayuni popote unapoishi?

ikoni ya 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 45:3–5

Yesu Kristo ndiye Mwombezi wangu kwa Baba.

  • Yawezekana ukataka kuwasaidia watoto wako waelewe kwamba mwombezi ni mtu anayemuunga mkono mtu mwingine. Kisha ungeweza kuzungumza kuhusu mifano ya kuwa mwombezi ambayo wanaifahamu (kama vile kumtetea rafiki). Mnaposoma Mafundisho na Maagano 45:3–5 pamoja, wasaidie watoto wako wagundue ni nani mwombezi wetu na jinsi ambavyo Yeye hutusaidia sisi.

Mafundisho na Maagano 45:32

Ninaweza “kusimama katika mahali patakatifu.”

  • Ingeweza kuwa furaha kuweka picha za nyumba, jengo la kanisa, na hekalu ndani ya chumba. Kisha ungeweza kuwapa watoto wako vidokezo vinavyoelezea sehemu hizi na waalike wasimame karibu na picha unayoielezea. Waombe wasimame tuli wakati unaposoma mstari wa kwanza kutoka Mafundisho na Maagano 45:32. Maeneo yapi ni mahali patakatifu ambayo Mungu anatupatia? Wasaidie watoto wako waelewe kwamba “kusimama katika mahali patakatifu, na … kutoondoshwa” inamaanisha kuchagua mema wakati wote, bila kujali nini kinatokea. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuzifanya nyumba zetu ziwe mahali patakatifu zaidi?

Mafundisho na Maagano 45:9

Injili ya Yesu Kristo ni bendera kwa ulimwengu.

  • Unaweza kuwaelezea watoto wako kwamba hapo kale, bendera ilikuwa bango lililochukuliwa kwenda nalo vitani. Iliwasaidia askari kujua wapi pa kukusanyika na nini cha kufanya. Someni pamoja Mafundisho na Maagano 45:42, na mjadiliane jinsi ambavyo injili ni kama bendera. Watoto wako wangefurahia kutengeneza bendera yao wenyewe, ikijumuisha picha au maneno ambayo yanaelezea hisia zao kumhusu Mwokozi.

kuinua bendera

Injili ni kama bendera.

Mafundisho na Maagano 45:44–45

Yesu Kristo atakuja tena.

  • Maangamizo ambayo yatatokea kabla ya Ujio Wa Pili yanaweza kuwafanya watoto waogope. Kuwaelekeza kwa Yesu Kristo kunaweza kuwasaidia watazame mbele kwa imani! Fikiria kuwaalika wafikirie kuhusu jinsi wanavyohisi wakati mtu fulani maalumu anapokuja kuwatembelea, kama vile babu, bibi au rafiki. Ni kwa jinsi gani wanajiandaa kwa ajili ya ziara hiyo? Kisha ungeweza kuonesha picha ya Mwokozi, na kusoma Mafundisho na Maagano 45:44–45. Shiriki na kila mmoja jinsi unavyohisi kuhusu ujio wa Mwokozi.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wahisi kuchangamka kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi, ungeweza kuandika kwenye vipande vya karatasi baadhi ya ahadi za kutumainiwa kutoka sehemu ya 45 (ona, kwa mfano, mistari 44–45, 51–52, 55, 58–59, 66–71). Wape watoto karatasi na uwaombe wainue mkono wao wakati ahadi wanayoishikilia inapotajwa wakati mnaposoma mistari hii. Jadilini ahadi hizi zinamaanisha nini. Ungeweza pia kuimba pamoja na watoto wako wimbo kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi, kama vile “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83).

Wasaidie watoto wamtambue Roho. Unapowafundisha watoto wako, waambie wakati unapomhisi Roho Mtakatifu. Zungumza kuhusu jinsi unavyotambua ushawishi Wake. Kwa mfano, unaweza kuhisi kuwa na amani au mwenye shangwe wakati unapoimba wimbo kuhusu Mwokozi.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki

Ujio wa Pili wa Yesu Kristo

Ujio wa Pili, na Harry Anderson

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto