Njoo, Unifuate
Mei 12–18: “Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”: Mafundisho na Maagano 46–48


“Mei 12–18: ‘Takeni Sana Karama Zilizo Kuu’: Mafundisho na Maagano 46–48,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 46–48,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani 2025

kukutana kando ya mto

Mkutano wa Kambi, na Worthington Whittredge

Mei 12–18 “Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”

Mafundisho na Maagano 46–48

Wakati Parley P. Pratt, Oliver Cowdery, Ziba Peterson, na Peter Whitmer Mdogo walipoondoka Kirtland na kuhama ili kuendelea kuhubiri injili, waliacha zaidi ya waumini wapya wa Kanisa 100 ambao walikuwa na ari kubwa lakini uzoefu mchache au maelekezo kidogo. Hawakuwa na vitabu vya maelekezo, hakuna mikutano ya mafunzo ya uongozi, hakuna matangazo ya mkutano mkuu—kwa kweli, hawakuwa hata na nakala nyingi za Kitabu cha Mormoni za kuwagawia watu. Wengi wa hawa waaminio wapya walikuwa wamevutwa kwenye injili iliyorejeshwa kwa ahadi ya madhihirisho ya kustaajabisha ya Roho, hasa yale yaliyoelezwa katika Agano Jipya (ona kwa mfano, 1 Wakorintho 12:1–11). Lakini wengi walipata wakati mgumu kutambua madhihirisho ya kweli ya Roho. Alipoona mkanganyiko, Joseph Smith aliomba kwa ajili ya usaidizi. Jibu la Bwana lina thamani leo, wakati watu wanapokana na kupuuzia mambo ya Roho. Yeye alithibitisha kwamba madhihirisho ya kiroho ni halisi. Yeye pia alifafanua yalikuwa ni nini: karama kutoka kwa Baba wa Mbinguni mwenye upendo, “zilizotolewa kwa manufaa ya wale ambao wanampenda [Yeye] na kushika amri [Zake] zote, na yule ambaye hutafuta kufanya hivyo” (Mafundisho na Maagano 46:9).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 46:1–7

Mwokozi huwakaribisha wote ambao wanataka kuabudu katika Kanisa Lake.

Je, unahisi kwamba marafiki zako na watu katika ujirani wako wanahisi kukaribishwa kwenye ibada za kata yako? Je, ni kipi unatenda ili kufanya mikutano yako ya Kanisa iwe mahali ambapo watu wanataka kurejea tena? Tafakari jinsi unavyoweza kutumia ushauri wa Bwana katika Mafundisho na Maagano 46:1–7 (ona pia 2 Nefi 26:24–28; 3 Nefi 18:22–23).

Ungeweza pia kufikiria kuhusu wakati ambapo ulihudhuria ibada za Kanisa—au mkutano wa kikundi kingine—kwa mara ya kwanza. Watu walifanya nini ili kukusaidia uhisi kukaribishwa?

Ona pia Moroni 6:5–9; “’Yavutia Kuuimba,” Nyimbo za Dini, na. 96; “Welcome” (video), Maktaba ya Injili.

1:17

Karibu ComeUntoChrist.org

Karibu kwenye jumuiya ambayo kila mtu anajitahidi kuishi kama Yesu alivyofundisha. Njoo uone kile tunachoamini kwenye ComeUntoChrist.org.

Mafundisho na Maagano 46:7–33

ikoni ya seminari
Baba wa Mbinguni hunipa vipawa vya roho ili kuwabariki wengine.

Watakatifu wa mwanzo waliamini katika vipawa vya roho lakini walihitaji msaada kuvitambua na kuelewa madhumuni yake. Unapojifunza kuhusu vipawa vya Roho katika Mafundisho na Maagano 46:7–33, tafakari madhumuni ambayo “[kwayo] vinatolewa” (mstari wa 8). Je, unajifunza nini kumhusu Mungu—mtoaji wa vipawa hivi?

Unaweza kufikiria mifano uliyoiona ya watu wakitumia vipawa hivi au vipawa vingine vya roho? Ni kwa jinsi gani vinakuwa na “manufaa … kwa watoto wa Mungu”? (mstari wa 26). Ungeweza pia kuona kama unaweza kutambua mifano mbalimbali ya vipawa vya roho katika maandiko kama haya: 1 Wafalme 3:5–15; Danieli 2:26–30; Matendo ya Mitume 3:1–8; Helamani 5:17–19; Mormoni 1:1–5; Etheri 3:1–15; Mafundisho na Maagano 6:10–12; Musa 7:13.

Kujifunza kwako juu ya vipawa vya roho kunaweza kukuongoza kwenye kutafakari ni kipawa kipi Mungu amekupatia. Je, ni kwa jinsi gani unaweza kutumia vipawa hivi kuwabariki watoto Wake? Kama una baraka ya patriaki, pengine inaonesha vipawa ulivyopewa. Kusoma ujumbe wa Mzee John C. Pingree Mdogo “Nina Kazi Kwa Ajili Yako,” kungeweza pia kufungua akili yako kwa vipawa ambavyo hujavifikiria (Liahona, Nov. 2017, 32–35).

Kama ungependa kujifunza kuhusu jinsi ya kukuza vipawa vya kiroho, analojia mwanzoni wa ujumbe wa Mzee Juan Pablo Villar “Kufanyia Mazoezi Misuli Yetu ya Kiroho” ungeweza kusaidia (Liahona, Mei 2019, 95). Ni “mazoezi” gani yangeweza kusaidia kukuza vipawa vyako vya kiroho?

Ona pia Topics and Questions, “Holy Ghost,” Maktaba ya Injili.

Mafundisho na Maagano 47

Bwana anataka Kanisa Lake litunze historia.

Wito wa John Whitmer wa kutunza historia ya Kanisa uliendeleza utamaduni wa muda mrefu wa watunza historia miongoni mwa watu wa Mungu. Kwa nini unadhani kutunza historia ni muhimu sana kwa Bwana? Tafakari hili unaposoma sehemu ya 47, vile vile maelekezo yanayofanana na hayo katika 2 Nefi 29:11–12; Musa 6:5; Ibrahimu 1:28, 31. Unahisi Bwana anakutaka wewe uweke rekodi ya nini kuhusu maisha yako?

Kwenye FamilySearch, unaweza kurekodi kumbukumbu na uzoefu kutoka kwenye maisha yako—na maisha ya mababu zako (ona FamilySearch.org).

Ona Henry B. Eyring, “Ee Kumbuka, Kumbuka,” Liahona, Nov. 2007, 66–69.

John Whitmer

John Whitmer

Mafundisho na Maagano 47

Roho Mtakatifu anaweza kunielekeza wakati ninapotimiza wito wangu.

Labda unaweza kujihusisha na kile ambacho John Whitmer alihisi wakati alipohitaji hakikisho kwamba wito wake ulitoka kwa Mungu. Je, Bwana alisema nini katika Mafundisho na Maagano 47 kwa John Whitmer—na kwako—ili kukupa kujiamini katika kutekeleza miito ambayo Yeye huitoa?

Kazi ya mwalimu. Kufundisha ni zaidi ya kuwasilisha taarifa. Kunajumuisha kutengeneza mazingira ambapo washiriki wa darasa wanaweza kujifunza na kugundua kweli wao wenyewe na kushiriki kile ambacho wamejifunza pamoja na wengine (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi26).

ikoni ya 02 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 46:2–6

Ninaweza kuwasaidia wengine wajisikie wanakaribishwa kanisani.

  • Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 46:5 pamoja na watoto wako, zungumza kuhusu jinsi Mwokozi anavyotaka watu wahisi wakati wanapokuja kwenye Kanisa Lake. Waalike watoto wako wafikirie kwamba wamemwona mtu fulani kanisani kwa mara ya kwanza. Wasaidie wafanyie mazoezi jinsi wanavyoweza kumsaidia mtu huyu kujisikia anakaribishwa.

Mafundisho na Maagano 46:7–26

Baba wa Mbinguni hunipa vipawa vya kiroho ili kuwabariki wengine.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wajifunze kuhusu vipawa vya kiroho vilivyoelezwa katika Mafundisho na Maagano 46:13–26, zingatia wazo hili. Ungeweza kuandika vipawa hivi kwenye vipande vya karatasi na vifiche chumbani. Watoto wako wanapokipata kila kipande cha karatasi, wasaidie wapate mahali kipawa hicho kilipotajwa katika sehemu ya 46. Kwa kila kipawa, zungumza nao kuhusu jinsi kinavyotumika kuwabariki wengine (maelezo kwenye “Sura ya 20: Vipawa vya Roho,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 77–80, yanaweza kusaidia).

    2:19

    Chapter 20: Gifts of the Spirit: 8•March 1831

  • Waambie watoto kuhusu vipawa ambavyo wewe unahisi Baba wa Mbinguni amewapa wao, na waruhusu wazungumze kuhusu vipawa wanavyovigundua kwa kila mmoja. Kulingana na Mafundisho na Maagano 46:8–9–26, kwa nini Baba wa Mbinguni anatupatia sisi vipawa vya roho? Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia vipawa vyetu kuwasaidia wengine?

Mafundisho na Maagano 47:1, 3

Ninaweza kuandika historia yangu.

  • Waruhusu watoto wako wagundue kile ambacho Bwana alimtaka John Whitmer afanye katika Mafundisho na Maagano 47:1, 3. Mngeweza pia kushiriki mmoja na mwingine hadithi zingine pendwa kutoka kwenye maandiko. Sema wazi kwamba tunajua kuhusu hadithi hizi kwa sababu mtu fulani aliziandika.

  • Fikiria jinsi unavyoweza kuwahamasisha watoto wako waandike hadithi zao binafsi. Ungeweza kushiriki baadhi ya maingizo kutoka kwenye shajara yako binafsi au hadithi kuhusu babu aliyekwisha fariki (ona FamilySearch.org au app ya Memories). Ungeweza kutoa baadhi ya vidokezo vya shajara, kama vile “Nini kilitokea wiki hii ambacho ungependa wajukuu zako wajue kukihusu?” au “Ni kwa jinsi gani uliuona mkono wa Bwana katika maisha yako wiki hii?” Watoto wadogo wangeweza kuchora picha za uzoefu wao, au ungeweza kuwarekodi wakisimulia hadithi zao. Ni baraka zipi huja kutokana na kutunza “historia ya kila mara”? (Mafundisho na Maagano 47:1).

msichana akiandika kwenye shajara

Mafundisho na Maagano 48:2–3

Ninaweza kuwasaidia wengine kwa kushiriki kile ambacho nimepewa.

  • Unaposoma Mafundisho na Maagano 48:2–3 pamoja na watoto wako, unaweza kuhitaji kuelezea kwamba watu walikuwa wanakuja Ohio kutoka Mashariki, na hawakuwa na mahali pa kuishi. Bwana aliwaomba Watakatifu wafanye nini ili kusaidia? Wasaidie watoto wako wafikirie juu ya vitu ambavyo Mungu amewapa wao ambavyo wanaweza kuvishiriki pamoja na wengine. Ungeweza pia kuimba pamoja nao wimbo kama vile “‘Give,’ Said the Little Stream” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 236).

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

Waumini wa Kanisa wakisalimiana

Wale wote wanaotaka kumwabudu Mwokozi wanakaribishwa katika mikutano ya Watakatifu Wake.

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto