Njoo, Unifuate
Mei 26–Juni 1: “Mwaminifu, Mwenye Haki, na Mtumishi Mwenye Hekima”: Mafundisho na Maagano 51–57


“Mei 26–Juni 1: ‘Mwaminifu, Mwenye haki na Mtumishi mwenye Hekima’: Mafundisho na Maagano 51–57,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 51–57,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

mwanamume akilima shamba

Mfuo wa Kwanza, na James Taylor Harwood

Mei 26–Juni 1: “Mwaminifu, Mwenye Haki na Mtumishi mwenye Hekima”

Mafundisho na Maagano 51–57

Kwa waumini wa Kanisa mnamo miaka ya 1830, kuwakusanya Watakatifu na kuujenga mji wa Sayuni ilikuwa kazi ya kiroho na ya kimwili vilevile, ikiwa na maswala mengi ya kiufundi ya kushughulikia: Mtu alihitajika kununua ardhi ambapo Watakatifu wangeweza kuishi. Mtu alihitajika kuchapisha vitabu na machapisho mengine. Na mtu alihitajika kusimamia ghala ili kutoa bidhaa kwa watu waliokuwa Sayuni. Katika ufunuo ulioandikwa katika Mafundisho na Maagano 51–57, Bwana aliwateua na kuwaelekeza watu kushughulikia majukumu haya.

Lakini wakati ujuzi katika mambo kama haya unahitajika Sayuni, ufunuo huu pia unafundisha kwamba Bwana anakusudia Watakatifu Wake wawe wenye kustahili kiroho ili kuitwa watu wa Sayuni—watu Wake. Anatuita kila mmoja wetu kuwa “mwaminifu, wenye haki, na mtumishi mwenye hekima,” tukiwa na roho iliyopondeka, “tukisimama imara” katika majukumu yetu tuliyopewa (ona Mafundisho na Maagano 51:19; 52:15; 54:2). Ikiwa tunaweza kufanya hivyo—licha ya ujuzi wetu wa kimwili—Bwana anaweza kututumia kuijenga Sayuni.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 51

Bwana ananitaka niwe mwaminifu, mwenye haki na mtumishi mwenye hekima.

Ikiwa ungekuwa muumini wa Kanisa mnamo 1831, ungeweza kuwa umealikwa kuishi sheria ya uwekaji wakfu kwa kutoa mali zako kwa Kanisa kupitia askofu. Kisha Yeye angerejesha kwako, mara nyingi, kile ulichotoa, wakati mwingine kikiwa na ziada. Lakini ilikuwa si tena mali yako—ilikuwa utumishi wako.

Leo hii taratibu ziko tofauti, lakini kanuni hizi bado ni muhimu kwenye kazi ya Bwana. Unaposoma sehemu ya 51, fikiria kuhusu kile ambacho Mungu amekikabidhi kwako. Maneno “mtumishi” (mstari wa 19) na “iliyowekwa wakfu” (mstari wa 5) hudokeza nini kuhusu matarajio ya Mungu juu yako?

Rais Spencer W. Kimball alieleza: “Katika Kanisa utumishi ni wajibu mtakatifu wa kiroho au wa kimwili ambapo kuna kuwajibika. Kwa sababu vitu vyote ni vya Bwana, sisi ni watumishi kwa miili yetu, akili, familia, na mali zetu. (Ona Mafundisho na Maagano 104:11–15.) Mtumishi mwaminifu ni yule ambaye hutumia mamlaka kwa haki, huijali familia yake, na kuwajali masikini na wanaohitaji msaada” (“Welfare Services: The Gospel in Action,” Ensign, Nov. 1977, 78).

Ona pia “The Law of Consecration” (video), Maktaba ya Injili.

5:1

The Law of Consecration

Historians Kate Holbrook and Steven C. Harper discuss what the Law of Consecration is, the three core doctrines pertaining to it, and how we can live it today.

Mafundisho na Maagano 52:9–11; 22–27

Ninaweza kuwaalika wengine waje kwa Yesu Kristo popote niendapo.

Wakati Bwana alipowatuma viongozi kadhaa wa Kanisa kule Missouri, aliwaambia watumie muda wao safarini na “wahubiri njiani” (mistari 25–27). Ni kwa jinsi gani unaweza kushiriki injili “safarini,” au wakati wa matukio ya kawaida ya maisha yako?

Mafundisho na Maagano 52:14–19

ikoni ya seminari
Bwana hunisaidia niepuke udanganyifu.

Kukiwa na watu wengi waliodai madhihirisho ya kiroho, Watakatifu wa mwanzo walikuwa na wasiwasi kuhusu kudanganywa. Ni onyo gani Bwana aliwapa wao katika Mafundisho na Maagano 52:14? Suluhisho Lake lilikuwa lipi? (ona mistari 14–19).

Utaratibu ni kitu ambacho hujirudia rudia kila mara, njia inayoweza kutabirika. Mifano inajumuisha kuhesabu kwa namba shufwa au machweo na mawio ya jua kila siku. Je, ni mifano ipi mingine unaweza kuifikiria? Unapopekua Mafundisho na Maagano 52:14–19, tambua utaratibu wa Bwana kwa ajili ya kuepuka udanganyifu. Ingeweza kusaidia kutambua kwamba “iliyopondeka” hudokeza hisia ya unyenyekevu na toba; “upole” hupendekeza utulivu na kujithibiti mwenyewe; na “kujenga” humaanisha kuelekeza, kuboresha, au kuendeleza. Kwa nini unahisi utaratibu wa Bwana hujumuisha sifa hizi, vile vile utiifu? Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia utaratibu huu kuepuka udanganyifu?

Fafanua maneno magumu. Katika app ya Maktaba ya Injili, unaweza kugusa na kushikilia neno na kisha kuchagua “Fafanua.” Kisha utaelekezwa kwenye maelezo ya neno hilo. Jaribu hili wakati unapokutana na maneno usiyoyafahamu—au maneno ambayo yanaonekana kufahamika ambayo ungependa kuyaelewa vyema zaidi.

Ni ipi baadhi ya mifano ya udanganyifu katika siku zetu? Ni kwa jinsi gani tunaweza kujua ikiwa tunadanganywa?

Kwa mfano, ungeweza kufikiria kutathmini chaguzi zako kuhusu sinema, muziki, na mitandao ya kijamii kulingana na viwango katika “Tembea katika nuru ya Mungu” kwenye Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 16–21.

Ona pia Gary E. Stevenson, “Usinidanganye,” Liahona, Nov. 2019, 93–96; “Niongoze,” Nyimbo za Dini, na. 49; Topics and Questions, “Seeking Truth and Avoiding Deception,” Maktaba ya Injili.

Mafundisho na Maagano 54

Ninaweza kumgeukia Bwana wakati ninapoumizwa na chaguzi za wengine.

Je, umewahi kuvunjika moyo wakati mtu fulani unayemtegemea alipoacha kutimiza ahadi zake? Hili liliwatokea Watakatifu kutoka Colesville, New York, ambao walitarajia kuweka makazi kwenye shamba la Leman Copley huko Ohio. Ili kujifunza kutokana na uzoefu huu, zingatia kupitia tena kichwa cha habari cha sehemu ya 54 (ona pia Saints,, 1:125–28; “A Bishop unto the Church,” Revelations in Context,, 78–79). Kama ungekuwa na rafiki miongoni mwa Watakatifu wa Colesville, ni ushauri upi ungeupata katika sehemu ya 54 wa kushiriki nao?

Shamba la Leman Copley

Shamba la Leman Copley

Mafundisho na Maagano 56:14–20

Heri wenye moyo safi.

Katika mistari hii, Bwana alizungumza kwa wote matajiri na masikini; ingeweza kuwa ya kuvutia kulinganisha ushauri Wake kwa makundi haya mawili. Ni kipi katika mistari hii kinaonekana kuhusika kwako binafsi?

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana..

ikoni ya 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 51:9

Ninaweza kuwa mwaminifu.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wajifunze kile inachomaanisha kuwa mwaminifu, mngesoma pamoja Mafundisho na Maagano 51:9 na kushiriki hadithi za watoto ambao walikabiliana na maamuzi ya kuwa waaminifu. Ungeweza kutumia picha, vikaragosi vya soksi, au wanasesere wa karatasi ili kuzifanya hadithi ziwe za kuvutia zaidi. Ni kwa jinsi gani Bwana anatubariki tunapojitahidi kuwa waaminifu?

  • Fikiria kucheza mchezo na watoto wako. Baadaye, jadilini jinsi ambavyo mchezo ungekuwa tofauti ikiwa mtu angefanya udanganyifu. Kwa nini ni muhimu “kutenda kwa uaminifu” kwa kila mmoja?

Mafundisho na Maagano 52:10; 53:3; 55:1

Ninapokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono.

  • Kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono kumetajwa mara kadhaa katika Mafundisho na Maagano 51–57. Hii inaweza kuwa fursa nzuri ya kuwafundisha watoto wako kuhusu ibada hii. Kwa mfano, wangeweza kutazama picha ya mtoto akithibitishwa na kuelezea nini kinatendeka katika picha hiyo. Waombe wapige makofi wakati wanaposikia “kuwekea mikono” au “kuweka mikono” wakati unaposoma Mafundisho na Maagano 52:10; 53:3; 55:1.

  • Mngeweza pia kuimba “The Holy Ghost,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,105) au wimbo unaofanana. Wasaidie watoto wapate maneno na virai kwenye wimbo ambavyo vinafundisha kuhusu kipawa cha Roho Mtakatifu.

    mvulana akithibitishwa

Mafundisho na Maagano 52:14–19

Mungu ana utaratibu kunisaidia nisidaganywe.

  • Ili kufundisha kuhusu utaratibu wa Bwana kwa ajili ya kuepuka udanganyifu, ungeweza kuanza kwa kuwasaidia watoto wapate mifano ya utaratibu—katika asili, katika blanketi nguo za rangi nyingi, au katika maisha ya kila siku. Wasaidie wapate utaratibu Bwana alioutoa katika Mafundisho na Maagano 52:14–15. Hakikisha wanaelewa maneno yoyote yasiyofahamika katika mistari hii. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia utaratibu huu kutambua ukweli?

Mafundisho na Maagano 54:4–6

Ninapaswa daima kushika maagano yangu.

  • Kwa maneno yako mwenyewe, shiriki na watoto wako kile kilichotokea kwa Watakatifu ambao walikuja kuishi kwenye shamba la Leman Copley (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 54). Watoto wako wangeweza kujifanya kuwa muumini wa Kanisa ambaye amewasili kutoka Ohio. Wangehisi vipi baada ya Leman kuvunja agano lake? Hii inatufundisha nini sisi kuhusu kushika maagano yetu au kutunza ahadi zetu? Someni pamoja Mafundisho na Maagano 54:6 ili kugundua baraka kwa ajili ya watu wanaoshika maagano yao.

Mafundisho na Maagano 55:1–4

Ninaweza kutumia baraka alizonipa Mungu kuwabariki wengine.

  • Ili kutambulisha sehemu ya 55, unaweza kutaka kuelezea kwamba William W. Phelps alikuwa mchapishaji wa magazeti ya habari ambaye alijifunza kuhusu injili na kujiunga na Kanisa. Soma pamoja na watoto wako Mafundisho na Maagano 55:1–4, na uwasaidie wagundue kile Mungu alichomtaka William afanye. Ni kwa jinsi gani Yeye alipanga kutumia talanta za William? Hii ingeweza kuongoza kwenye majadiliano kuhusu jinsi ambavyo Mungu anaweza kutualika tutumie talanta zetu kuwabariki watoto Wake.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

Watakatifu wakiweka wakfu bidhaa zao

Askofu Partridge Anapokea Bidaa Zilizowekwa Wakfu, na Albin Veselka

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto