“Sauti za Urejesho: Shuhuda za ‘Ono’,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Shuhuda za ‘Ono’,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Sauti za Urejesho: Shuhuda za “Ono”
Wilford Woodruff
Wilford Woodruff alijiunga na Kanisa mnamo Desemba 1833, takribani miaka miwili baada ya Joseph Smith na Sidney Rigdon kupokea ono lililoandikwa katika Mafundisho na Maagano 76. Alikuwa akiishi New York wakati huo na alijifunza kuhusu “Ono” kutoka kwa wamisionari waliokuwa wakitumikia kwenye eneo lile. Miaka kadhaa baadaye, alizungumzia misukumo yake ya ufunuo huu:
“Nilifunzwa tangu utoto wangu kwamba kulikuwa na Mbingu moja na Jahanamu moja, na kuambiwa kwamba waovu wote walikuwa na adhabu moja na wenye haki utukufu mmoja. …
“… Niliposoma ono … , liliangaza akili yangu na kunipa shangwe kubwa, ilionekana kwangu kwamba Mungu ambaye alifunua kanuni hiyo kwa mwanadamu alikuwa mwenye busara, mwenye haki na mkweli, aliye na vyote sifa bora na hisia nzuri na ufahamu, nilihisi Yeye alikuwa na msimamo kwenye vyote upendo, rehema, haki na hukumu, na nilihisi kumpenda Bwana zaidi kuliko hapo kabla katika maisha yangu.”
“Ono [ni] ufunuo ambao unatoa mwanga zaidi, ukweli zaidi, na kanuni zaidi kuliko ufunuo wowote katika kitabu kingine chochote tulichowahi kukisoma. Unaweka wazi ufahamu wetu wa hali ya sasa, wapi tulitoka, kwa nini tuko hapa, na wapi tunakwenda. Mtu yeyote anaweza kujua kupitia ufunuo huo kile sehemu yake na hali yake itakavyokuwa.”
“Kabla sijamwona Joseph nilisema sikujali alikuwa na umri gani, au udogo wake; sikujali jinsi alivyoonekana—iwe nywele zake zilikuwa ndefu au fupi; mwanaume aliyeleta ufunuo huo [ufunuo ulioandikwa katika sehemu ya 76] alikuwa nabii wa Mungu. Nililijua hilo mimi mwenyewe.”
Phebe Crosby Peck
Wakati Phebe Peck aliposikia Joseph na Sidney wakifundisha juu ya “Ono,” alikuwa akiishi Missouri na akilea watoto watano kama mzazi mmoja. Ono lilimvutia na kumvuvia kiasi kwamba aliandika yafuatayo kushiriki kile alichojifunza yeye pamoja na ndugu zake:
“Bwana anafichua siri za Ufalme wa mbinguni kwa Watoto wake. … Joseph Smith na Sidney Rigdon walitutembelea majira ya kuchipua yaliyopita, na tulikuwa na mikutano mingi ya shangwe wakati walipokuwa hapa, na tulikuwa na siri nyingi zilizofunuliwa kwenye mtazamo wetu, ambazo zilinipa faraja kubwa. Tungeweza kuona wema wa Mungu katika kuandaa makao ya amani kwa ajili ya watoto wake. Na yule ambaye hatapokea utimilifu wa injili na kusimama kama askari jasiri katika kusudi la Kristo hawezi kuishi katika uwepo wa Baba na Mwana. Lakini kuna mahali palipoandaliwa kwa ajili ya wale wote ambao hawapokei, lakini ni mahali pa utukufu wa chini ikilinganishwa na kuishi katika ufalme wa selestia. Sitajaribu kusema zaidi kuhusiana na mambo haya kwani sasa yapo katika chapisho na yanasonga mbele ulimwenguni. Na pengine utakuwa na fursa ya kusoma wewe mwenyewe, na ukifanya hivyo, natumaini utasoma kwa moyo wa umakini na wa sala, kwani mambo haya yana thamani kukumbukwa. Na ninatamani kwamba mpekue ndani yake, kwani ni kile kinachoongoza kwenye furaha yetu katika ulimwengu huu na ulimwengu ujao.”