Njoo, Unifuate
Julai 28–Agosti 3 “Nguvu za Uchamungu”: Mafundisho na Maagano 84


“Julai 28–Agosti 3, ‘Nguvu za Uchamungu’: Mafundisho na Maagano 84,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 84,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Joseph Smith akipokea Ukuhani wa Melkizedeki

Utondoti kutoka Urejesho wa Ukuhani wa Melkidezeki, na Liz Lemon Swindle

Julai 28–Agosti 3: “Nguvu za Uchamungu”

Mafundisho na Maagano 84

Tangu ukuhani uliporejeshwa mnamo 1829, Watakatifu wa mwanzo walikuwa wamebarikiwa kwa nguvu takatifu za Bwana. Walibatizwa, kuthibitishwa, na kuitwa kutumikia kwa mamlaka ya ukuhani, kama vile ilivyo kwetu leo. Lakini kuweza kufikia nguvu ya ukuhani si sawa na kuielewa kikamilifu, na Mungu alikuwa na mengi zaidi ambayo Yeye alitaka Watakatifu Wake wayaelewe—hasa kwa urejesho uliokuwa ukija wa ibada za hekaluni. Ufunuo wa mwaka 1832 juu ya ukuhani, sasa Mafundisho na Maagano 84, uliongeza ono la Watakatifu juu ya kile ukuhani ulicho hasa. Na unaweza kufanya kitu sawa na hicho kwetu leo. Kwani, kuna mengi ya kujifunza kuhusu nguvu takatifu ambayo inashikilia “ufunguo wa ufahamu wa Mungu,” ambayo hufanya “nguvu za uchamungu,” zidhihirike,” na ambayo hututayarisha “kuuona uso wa Mungu, hata Baba, na kuishi” (mstari wa 19–22).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 84:17–32

ikoni ya seminari
Ninaweza kufikia nguvu ya ukuhani na baraka za Mungu.

Unapofikiria neno ukuhani, nini huja akilini mwako? Ni kwa jinsi gani nguvu ya ukuhani wa Mungu inashawishi maisha yako?

Baada ya kutafakari maswali haya, ungeweza kujifunza Mafundisho na Maagano 84:17–32, ukitafuta kile Bwana anachokutaka ujue kuhusu nguvu ya ukuhani Wake. Fikiria jinsi gani ungeweza kutumia mistari hii kumwelezea mtu juu ya ukuhani na madhumuni yake.

Kitu kimoja utakachopata ni kwamba kupitia ibada za ukuhani, “nguvu za uchamungu hujidhihirisha” (ona Mafundisho na Maagano 19:21). Pengine ungeweza kuorodhesha ibada za ukuhani ulizozishiriki (orodha katika Kitabu cha Maelezo Jumla, 18.1, 18.2, inaweza kusaidia). Ni kwa jinsi gani ibada hizi—na maagano husika—vimekuletea nguvu za Mungu katika maisha yako? Je! Maisha yako yangekuwaje bila hizo?

Rais Russel M. Nelson alifundisha: “Kila mwanamke na kila mwanamume anayefanya maagano na Mungu na kuyatunza maagano hayo, na anayeshiriki kwa kustahili katika ibada za ukuhani, ana fursa ya moja kwa moja kwenye nguvu za Mungu.” (“Hazina za Kiroho,” Liahona, Nov. 2019, 77). Zingatia kijifunza ujumbe wa Rais Nelson, ukitafuta njia ambazo kupitia kwazo unaweza “kuvuta nguvu ya Mwokozi katika maisha [yako].”

Ona pia Mafundisho na Maagano 25:10, 13, 15; 121:34–37, 41–46; Topics and Questions, “Priesthood,” “Mafundisho ya Joseph Smith kuhusu Ukuhani, Mahekalu, na Wanawake,” Maktaba ya Injili; Kitabu cha Maelezo Jumla, 3.6, Maktaba ya Injili.

Mafundisho na Maagano 84:31–44

Ukuhani hutunukiwa kwa kiapo na agano.

Kiapo na agano la ukuhani (ona Mafundisho na Maagano 84:31–44) vina matumizi maalumu kwa wana wa Baba wa Mbinguni ambao wametawazwa kwenye ofisi ya ukuhani, lakini nyingi kati ya baraka zilizoahidiwa katika mistari hii zinapatikana kwa watoto wote wa Mungu. Ahadi hizi ni gani, na ni nini Mungu anatuomba sisi tufanya ili kuzipokea?

Mzee Paul B. Pieper alifundisha: “Ni ya kupendeza kwamba katika kiapo na agano la ukuhani [ona Mafundisho na Maagano 84:31–44], Bwana anatumia vitenzi pata na pokea. Yeye hatumii kitenzi tawaza. Ni hekaluni ambapo wanaume na wanawake—kwa pamoja—hupata na kupokea baraka na nguvu za Ukuhani wa Haruni na Melkizedeki” (“Uhalisia Uliofunuliwa wa Maisha ya Duniani,” Ensign, Jan. 2016, 21).

Unapojifunza Mafundisho na Maagano 84:31–44, tafakari kile inachoweza kumaanisha “kupata” na “kupokea” ukuhani. Ni kwa jinsi gani hii ni tofauti na kutawazwa katika ofisi ya ukuhani? Ni nini kingine Bwana anakualika upokee katika mistari hii? Ni kwa jinsi gani unafanya hivyo?

Ni kipi unapata ambacho kinakupa msukumo wa kuwa mwaminifu zaidi katika kumpokea Mwokozi, Baba Yake, watumishi Wake, na nguvu ya ukuhani Wake?

Ona pia Mafundisho na Maagano 121:36–46.

Mafundisho na Maagano 84:43–61

Kuishi kwa neno la Mungu huleta nuru na kweli katika maisha yangu.

Ni kweli zipi unazipata katika Mafundisho na Maagano 84:43–61 ambazo zinakusaidia uelewe kwa nini unahitaji kujifunza neno la Mungu kwa uthabiti? Ona tofauti kati nuru na giza katika mistari hii; ni kwa jinsi gani “kufanya bidii ya usikivu kwa maneno ya uzima wa milele” kumeleta nuru, kweli, na “Roho ya Yesu Kristo” kwenye maisha yako? (mstari wa 4345).

Ona pia 2 Nefi 32:3.

Linganisha kanuni za injili na vitu vinavyofahamika. Je, unaweza kufikiria analojia ambayo ungetumia kuonesha kweli katika mstari wa 43–44? Kwa mfano, ni kwa jinsi gani kufuata hatua zote katika mapishi ni kama “kuishi kwa kila neno … la Mungu”?

mwanamke akisoma maandiko

“Fanya bidii ya kuwa msikivu kwenye maneno ya uzima wa milele.”

Mafundisho na Maagano 84:62–91

Bwana atakuwa pamoja nami wakati ninapokuwa katika huduma Yake.

Unaposoma mistari hii, ungeweza kubainisha njia ambazo kupitia kwazo Bwana alisema angewasaidia watumishi Wake. Ni kwa jinsi gani ahadi hizi zinatumika kwenye kazi ambayo Yeye ametuomba tuifanye? Kwa mfano, ni kwa jinsi gani ahadi katika mstari wa 88 zimetimizwa katika maisha yako?

Mafundisho na Maagano 84:106–110

Kila mtu anaweza kuchangia kwenye kazi ya Mungu.

Je, tunajifunza nini kutoka katika mistari hii kuhusu jinsi ambavyo Bwana hutimiza kazi Yake? Je, ni ushauri upi na baraka zipi unazipata? Ungeweza pia kufikiria jinsi ambavyo “umeelekezwa katika unyenyekevu kamili” kwa sababu ulitumikia pamoja na mtu fulani ambaye alikuwa “imara katika Roho,” ikijumuisha watu katika familia yako.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni ya 02 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 84:4–5

Ibada za hekaluni zinanisaidia nijitayarishe kuishi na Baba wa Mbinguni tena.

  • Ili kuwasaidia watoto wako watazamie kwenda hekaluni, ungeweza kutengeneza chemsha bongo ya picha ya hekalu. Nyuma ya kila kipande, ungeweza kuandika kitu fulani tunachokifanya hekaluni, kama vile kubatizwa kwa niaba ya mababu, kuunganishwa pamoja na wanafamilia wetu, na kufanya maagano na Mungu. Soma Mafundisho na Maagano 84:4 pamoja na watoto wako, na waombe wasikilize kile Bwana alichowaamuru Watakatifu wajenge. Wewe na watoto wako mnapofanyia kazi chemsha bongo pamoja, shirikini mmoja na mwingine mambo tunayoweza kufanya ili kujiandaa kuingia hekaluni.

Mafundisho na Maagano 84:19–22

Ninaweza kupokea nguvu ya Baba wa Mbinguni kupitia ibada za ukuhani.

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe ibada ni nini, zingatia kuangalia pamoja nao picha za ibada kadhaa za ukuhani, kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 103–8, au ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waombe waelezee ni kitu gani kinafanyika katika kila picha. Kisha mngeweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 84:19–22. Ni kwa nini Baba wa Mbinguni anatutaka tupokee ibada hizi? Waambie watoto wako jinsi ambavyo umehisi nguvu ya Mungu kwa sababu ya ibada ulizopokea na maagano uliyoyafanya. (Ona pia “Nguvu ya Ukuhani, Mamlaka, na Funguo” katika kiambatisho A au kiambatisho B.)

Young Couple Going to the Temple; GAK 609; GAB 120; Primary manual 2-32; Doctrine and Covenants 131:1-3; 132:4-7, 19-20
watoto wakipokea sakramenti

Mafundisho na Maagano 84:77

Mimi ni rafiki wa Yesu ninapomfuata Yeye.

  • Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 84:77 pamoja, waulize watoto wako kuhusu kile inachomaanisha kuwa rafiki. Ungeweza kuzungumza kuhusu marafiki wazuri uliowahi kuwa nao. Ni kwa jinsi gani Yesu anatuonesha kwamba Yeye anataka sisi tuwe marafiki Zake? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonesha kwamba tunataka hivyo pia? Wimbo kama “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79) ungeweza kusaidia katika mazungumzo haya.

Mafundisho na Maagano 84:88

Baba wa Mbinguni huwasaidia watumishi Wake.

  • Watoto wako wangeweza kufurahia kusikia kuhusu jinsi wamisionari walivyokusaidia wewe, familia yako au mababu zako kupokea injili. Kisha wewe ungeweza kusoma kuhusu ahadi maalumu Bwana alitoa kwa wamisionari katika Mafundisho na Maagano 84:88. Labda watoto wako wangeweza kufikiria juu ya matendo ambayo yanaendana na mstari huu. Fikiria kushiriki kuhusu wakati ulipokuwa unamtumikia Bwana na ukahisi kwamba Yeye alikuwa pamoja nawe, kama ilivyoelezwa katika mstari wa 88. Ungeweza pia kuwasaidia watoto wako wafikirie jinsi wanavyoweza kuwa wamisionari sasa. Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anatusaidia tujue nini cha kusema wakati tunapozungumza na wengine kuhusu Yesu Kristo.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

hekalu katika machweo

Hekalu la Italia Roma

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto