“Agosti 4–10: ‘Simameni katika Mahali Patakatifu’: Mafundisho na Maagano 85–87,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 85–87,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Agosti 4–10: “Simameni katika Mahali Patakatifu”
Mafundisho na Maagano 85–87
Siku ya Krismasi kwa kawaida ni wakati wa kutafakari jumbe kama “amani duniani” (ona Luka 2:14). Lakini mnamo Desemba 25, 1832, akili ya Joseph Smith ilikuwa imetawaliwa na tishio la vita. Jimbo la Carolina Kusini katika Marekani lilikuwa limekaidi serikali na lilikuwa likijiandaa kwa vita. Na Bwana alifunua kwamba huu ulikuwa mwanzo tu: “Vita,” Yeye alitangaza, “vitamwagika juu ya mataifa yote” (Mafundisho na Maagano 87:2). Ilionekana kana kwamba unabii huu ungetimia punde tu.
Lakini kisha haukutimia. Ndani ya wiki chache tu, Carolina Kusini na serikali ya Marekani walifikia makubaliano, vita ikazuiliwa. Unabii, hata hivyo, si lazima wakati wote utimizwe katika muda au katika njia tunayoitarajia. Takribani miaka 30 baadaye, muda mrefu baada ya Joseph Smith kuuwawa kishahidi, Carolina Kusini iliasi na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilifuatia. Leo, vita kote ulimwenguni imeendelea kusababisha “dunia kuomboleza” (Mafundisho na Maagano 87:6). Thamani ya ufunuo huu ni ndogo katika kutabiri lini majanga yatakuja na kubwa zaidi katika kufundisha nini cha kufanya wakati yanapokuja. Ushauri ni uleule mwaka 1831, 1861, na 2025: “Simameni katika Mahali Patakatifu, wala msiondoshwe” (mstari wa 8).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Bwana ananitaka “nitunze historia.”
Tazama kile Bwana alichotaka kijumuishwe katika “historia” ilivyoelezwa katika Mafundisho na Maagano 85:1–2. Kwa nini unadhani Bwana anataka Watakatifu Wake watunze historia? Ni kipi ungeweza kukiwekea kumbukumbu kuhusu “namna unavyoishi, imani [yako], na matendo yako” ambavyo vingeweza kuwa baraka kwako na vizazi vijavyo? Ni kwa jinsi gani kutunza historia binafsi hukusaidia kuja kwa Kristo?
Ona pia “Journals: ‘Of Far More Worth than Gold,’” Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff (2011), 125–33; “Turning Hearts” (video), ChurchofJesusChrist.org.
Roho huzungumza kwa “sauti ndogo tulivu.”
Tafakari maneno Joseph Smith aliyoyatumia kumwelezea Roho katika Mafundisho na Maagano 85:6. Ni kwa namna gani sauti ya Roho ni “tulivu” na “ndogo”? Zingatia maelezo haya ya ziada yaliyotolewa kupitia Joseph Smith: Mafundisho na Maagano 6:22–24; 8:2–3; 9:7–9; 11:12–13; 128:1. Je, ni kwa jinsi gani Roho huzungumza nawe?
Ona pia: Luka 24:32; Mosia 5:2; Alma 32:28; Helamani 5:30; Mafundisho na Maagano 6:22–23; 11:12–13.
Wenye haki watakusanywa kwa Kristo katika siku za mwisho.
Mafundisho na Maagano 86 ina tafsiri ya Bwana ya mfano wa ngano na magugu, unaopatikana katika Mathayo 13:24–30, 37–43. Unapojifunza kuhusu maana ya mfano huu, zingatia kujaza jedwali kama hili:
Ishara |
Maana yamkini |
Maswali ya kutafakari |
---|---|---|
Ishara Mpanzi wa mbegu | Maana yamkini Manabii na mitume | Maswali ya kutafakari Ni aina gani ya “mbegu” manabii na mitume wetu wanapanda? |
Ishara Adui | Maana yamkini Shetani | Maswali ya kutafakari Ni kwa jinsi gani adui hujaribu kuzuia kazi ya Bwana? |
Ishara | Maana yamkini | Maswali ya kutafakari |
Ishara | Maana yamkini | Maswali ya kutafakari |
Hapa kuna maswali machache ya ziada ya kuzingatia:
-
Baada ya kutafsiri mfano ule, Bwana alizungumza juu ya ukuhani, urejesho, na wokovu wa watu Wake (ona mstari wa 8–11). Ni miunganiko ipi unaiona kati ya dhamira hizi na mfano wa ngano na magugu?
-
Wajibu wako ni upi katika kuwa “nuru kwa Mataifa “ na “mwokozi kwa watu wa [Bwana]”? (mstari wa 11).
Imani inapatikana katika “mahali patakatifu.”
Unabii katika sehemu ya 87 hutuonya kuhusu hatari za kimwili zinazohusiana na vita katika siku za mwisho. Lakini ushauri katika ufunuo huu pia unaweza kutumika kwa hatari za kiroho. Tafakari maswali kama yafuatayo:
-
Unabii ni ufunuo kutoka kwa Mungu kuja kwa nabii, mara nyingi kuhusu siku zijazo. Ni ipi baadhi ya mifano ya unabii ambayo manabii wa kale na wa sasa waliitoa? (ona Yohana 3:14; Mosia 3:5; Helamani 14:2–6). Ni kwa jinsi gani unabii huo ulitimizwa? (Ona Luka 23:33; Mathayo 15:30–31; 3 Nefi 1:15–21).
-
Ni zipi baraka za kukubali unabii wa manabii wa Mungu?
Ukiwa na mawazo hayo akilini, soma sehemu ya 87. (Kwa ajili ya muktadha wa kihistoria, ungeweza pia kutaka kusoma utangulizi wa muhtasari huu.) Unajifunza nini kuhusu unabii huu kutokana na ufunuo huu na jinsi ulivyotimia? Ungesema nini kwa mtu fulani ambaye anatilia shaka unabii kwa sababu haukutimia kwa haraka?
Ni ushauri upi Bwana anautoa katika mstari wa 8? Wapi ni “mahali pako patakatifu” ambapo unapata amani na usalama? Ni nini hufanya mahali kuwa patakatifu? Kwa kuongezea kwenye maeneo asili, pengine kuna nyakati takatifu, tamaduni takatifu, au mawazo matakatifu ambayo yanaweza kuleta amani. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani maneno ya manabii wa Mungu yanaweza kuwa mahali patakatifu kwako? Inamaanisha nini “kusimama” na “kutoondoshwa” kutoka mahali hapo?
Ona pia “Where Love Is,” Children’s Songbook, 138–39; Saints, 1:163–64; “Peace and War,” katika Revelations in Context, 158–64.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Roho huzungumza kwa “sauti ndogo tulivu.”
-
Watoto wako wangesema nini kama mtu fulani angewauliza ni kwa jinsi gani wanajua wakati Roho Mtakatifu anapozungumza nao? Waalike wasome kuhusu jinsi ambavyo Joseph Smith aliielezea sauti ya Roho katika Mafundisho na Maagano 85:6. Wangeweza kisha kufanya zoezi la kusikiliza na kuzungumza kwa sauti ndogo, tulivu. Ungeweza pia kushiriki uzoefu wakati Roho alipozungumza nawe katika sauti tulivu na ndogo.
-
Ili kuwasaidia watoto wako waelewe kirai “sauti ndogo tulivu,” ungecheza wimbo wa watoto kwa sauti ndogo, wimbo kama vile “The Holy Ghost” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,105). Muombe mmoja wa watoto abahatishe ni wimbo upi wakati watoto wengine wakipiga kelele za kuvuruga. Kisha ungeweza kurudia wimbo kukiwa hakuna vivuta mawazo. Ni vivuta mawazo vipi tunaweza kuondoa kutoka kwenye maisha yetu ili kumhisi Roho zaidi kila mara.
Ninaweza kusaidia kuwakusanya watu wa Mungu.
-
Ili kuwasaidia watoto wako waelewe mfano ulioelezwa katika sehemu ya 86, ungeweza kuandaa picha ndogo kadhaa au michoro ya ngano, na uifiche chumbani. Waelezee watoto wako mfano wa ngano na magugu (ona Mathayo 13:24–30), na msome pamoja maelezo ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 86:1–7. Watoto wako wangeweza kisha kukusanya picha za ngano zilizofichwa na waandike juu yake jina la mtu fulani wanayeweza “kumkusanya” kwa Yesu Kristo. Inamaanisha nini kuwakusanya watu kwa Yesu Kristo? Ni zipi baadhi ya njia ambazo kupitia hizo tunaweza kufanya hili?
Ninaweza kuwa nuru kwa Wengine.
-
Hapa kuna baadhi ya maswali unayoweza kuwauliza watoto wako wakati mnapojadili Mafundisho na Maagano 86:11: Ni kwa jinsi gani nuru hutubariki? Inakuwaje wakati hatuna nuru? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa watu wengine? Wasaidie watoto wako wafikirie njia tunazoweza “kuendelea katika wema wa [Yesu]” na kuushiriki na wengine.
Ninaweza “kusimama … katika mahali patakatifu.”
-
Someni pamoja Mafundisho na Maagano 87:6 ili kujifunza kuhusu mambo Bwana aliyosema yangetokea katika siku za mwisho. Kisha mngeweza kuzungumza kuhusu baadhi ya changamoto ambazo wewe na watoto mnakabiliana nazo. Katika mstari wa 8, ni kipi Bwana alichosema tunapaswa kufanya wakati wa nyakati ngumu?
-
Wasaidie watoto wako watengeneze orodha ya sehemu takatifu, mawazo matakatifu, na matendo matakatifu ambayo yanaweza kuwasaidia wakabiliane na hatari za kiroho. Kwa ajili ya mawazo, ona video “Standing in Holy Places” na “Stand Ye in Holy Places—Bloom Where You’re Planted” (Maktaba ya Injili).