“Agosti 11–17, ‘Ijengeni … Nyumba ya Mungu’: Mafundisho na Maagano 88,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 88,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Agosti 11–17: “Ijengeni … Nyumba ya Mungu”
Mafundisho na Maagano 88
Kila mara, Bwana hutupa mtazamo mdogo wa “ukuu na uweza” Wake usio na mipaka (Mafundisho na Maagano 88:47) kupitia mafunuo ya kushangaza. Mafundisho na Maagano 88 ni aina hiyo ya ufunuo—mmoja unaohusu nuru na utukufu na falme ambazo zinaweza kufanya mahangaiko yetu ya duniani kuonekana hayana maana kwa kulinganisha. Hata kama hatuwezi kutambua yote, tunaweza angalau kuhisi kwamba kuna zaidi kwenye umilele kuliko kile tunachoweza kuelewa sasa. Bila shaka, Bwana hashiriki kweli hizi kuu kututisha au kutufanya tuhisi duni. Hakika, Yeye aliahidi, “Siku itakuja mtakayomjua Mungu” (mstari wa 49; msisitizo umeongezwa). Pengine ilikuwa ni kwa mwisho huo mtukufu kwamba Bwana aliwaamuru Watakatifu Wake huko Kirtland kuunda Shule ya Manabii. “Jiandaeni wenyewe,” Yeye alisema. “Tayarisheni kila kitu kinachohitajika; na ijengeni … nyumba ya Mungu” (mstari wa 119). Zaidi kuliko mahala pengine popote, ni ndani ya nyumba takatifu ya Mungu—na katika nyumba zetu—ambapo Yeye anaweza kuinua uoni wetu juu ya ulimwengu huu, “kuufichua uso wake [kwetu],” na kutuandaa “kustahimili katika utukufu wa selestia” (mistari 68, 22).
Ona Saints, 1:164–66.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Yesu Kristo hunipa mimi amani
Siku kadhaa baada ya onyo kwamba vita “vitamwagika juu ya mataifa yote” (Mafundisho na Maagano 87:2), Bwana alitoa ufunuo ambao Joseph Smith aliuita “tawi la mzeituni,” ambalo kwa kawaida ni ishara ya amani” (Mafundisho na Maagano 88, kichwa cha habari cha sehemu, ona pia Mwanzo 8:11). Kote katika kujifunza kwako kwa sehemu ya 88 wiki hii, tafuta ujumbe wa amani wa Bwana kwa ajili yako.
Nuru na sheria huja kutoka kwa Yesu Kristo.
Maneno nuru na sheria yamerudiwa mara nyingi katika sehemu ya 88. Wekea alama au andika mistari pale unapopata maneno haya katika mstari wa 6–67, na andika kile unachojifunza kuhusu nuru na sheria—na kumhusu Yesu Kristo. Ni nini unahisi kupata mwongozo kufanya ili upokee nuru na kuishi “sheria ya Kristo”? (mstari wa 21).
Ona pia Isaya 60:19; Yohana 1:1–9; 3 Nefi 15:9; Timothy J. Dyches, “Nuru Huambatana na Muru,” Liahona, Mei 2021, 112–15; Sharon Eubank, “Kristo: Nuru Ing’aayo Gizani,” Liahona, Mei 2019, 73–76.
Mafundisho na Maagano 88:62–64
“Songeeni karibu nami.”
Ni uzoefu upi umekuonesha kwamba ahadi katika mistari hii ni za kweli? Hatua yako inayofuata ni ipi katika “kusogea karibu na” Kristo? Fikiria kuufanya wimbo “Karibu Na Ewe, Mungu Wangu!” (Nyimbo za Dini, na. 48) kuwa sehemu ya kujifunza kwako na kuabudu kwako.
Mafundisho na Maagano 88:67–76
Ninaweza kuwa msafi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.
Amri ya Bwana ya “jitakaseni” inapatikana mara mbili katika sehemu ya 88 (mistari 68, 74). Unadhani kishazi hiki kinamaanisha nini? Ungeweza kupitia tena baadhi ya vifungu hivi chini ya “Utakaso” katika Mwongozo wa Maandiko (Maktaba ya Injili). Ni kwa jinsi gani tunatakaswa? Acha swali hili liongoze kujifunza kwako Mafundisho na Maagano 88: 67–76, na andika umaizi wa kiroho wowote unaoupokea.
Mafundisho na Maagano 88:77–80, 118–26
“Tafuteni maarifa, hata kwa kujifunza na pia kwa imani.”
Bwana aliwaambia Watakatifu waanzishe “shule ya manabii” huko Kirtland (Mafundisho na Maagano 88:137). Mengi ya maelekezo katika sehemu ya 88 yaliwafundisha jinsi ya kufanya hivyo. Maelekezo haya yangeweza pia kukusaidia wewe “kuijenga … nyumba ya kujifunza” (mstari wa 119) katika maisha yako mwenyewe. Hakika, ungeweza kuchukulia mstari wa 77–80 na 118–26 kama mpango makini wa “kuikarabati tena nyumba yako [au maisha yako kuwa kituo cha kujifunza injili” na “kimbilio la imani” (Russell M. Nelson, “Kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Liahona, Nov. 2018, 113). Ingekuwa ya kuvutia kuchora vile ambavyo “ukarabati wako mpya” ungeweza kuwa, ikijumuisha virai kutoka katika mistari hii ambavyo unahisi unahitaji kuvitumia.
Ingeweza pia kusaidia kuchunguza maswali haya: Kwa nini kujifunza na elimu ni muhimu kwa Bwana? Ni kipi Yeye anataka nijifunze? Ni kwa jinsi gani Yeye anataka nijifunze? Tafuta majibu ya maswali haya katika mstari wa 77–80 na katika “Ukweli Utakuweka Huru” (Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 30–33.)
Unadhani inamaanisha nini kujifunza “kwa kusoma na pia kwa imani”? (mstari wa 118). Ni umaizi upi unaupata kutoka kwenye ujumbe wa Mzee Mathia Held “Kutafuta Maarifa kupitia Roho”? (Liahona, Mei 2019, 31–33).
Ona pia Topics and Questions, “Seeking Truth and Avoiding Deception,” Gospel Library; “A School and an Endowment,” katika Revelations in Context, 174–82.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Baba wa Mbinguni hutoa zawadi nzuri.
-
Ungeweza kuanza mjadala kuhusu Mafundisho na Maagano 88:33 kwa kuwaomba watoto wako wazungumze kuhusu zawadi ambazo wamepewa—zote zile walizopokea kwa shangwe na zingine ambazo hawakupokea kwa shangwe. Pengine wangeweza kuigiza wakipokea zawadi kwa shangwe. Kisha ungeweza kuzungumza kuhusu zawadi Baba wa Mbinguni alizotupatia sisi (kama vile kipawa cha Roho Mtakatifu). Ni kwa jinsi gani tunapokea zawadi hizi kwa shangwe?
Kama nikimtafuta Mwokozi, nitampata.
-
Mafundisho na Maagano 88:63 ina maneno ya vitendo ambayo yangeweza kuwa mwongozo kwa shughuli za burudani ili kuwatia moyo watoto wako watafute uwepo wa Bwana katika maisha yao. Kwa mfano, je, wewe na watoto wako mnaweza kufikiria mchezo kwa ajili ya kujadili kirai “nitafuteni kwa bidii nanyi mtanipata” (msisitizo umeongezwa) au “bisheni, nanyi mtafunguliwa”?
-
Ili kusisitiza mwaliko wa Mwokozi wa “sogeeni karibu nami,” ungeweza kumuomba mtoto mmoja ashikilie picha ya Yesu (picha kama ile iliyopo mwisho wa muhtasari huu) kwenye upande mmoja wa chumba huku watoto wengine wakisimama kwenye upande mwingine. Watoto wako wanapofikiria juu ya vitu wanayoweza kufanya ili kusogea karibu na Mwokozi, wanaweza kupiga hatua kuelekea picha ile, na mtoto anayeshikilia picha ile angeweza kupiga hatua kuwaelekea wale watoto wengine. Zungumza na watoto wako kuhusu jinsi unavyosogea karibu na Mwokozi na jinsi Yeye anavyosogea karibu nawe. Ungeweza pia kuimba pamoja nao wimbo kuhusu mada hii, kama vile “I Feel My Savior’s Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75).
Mafundisho na Maagano 88:77–80, 118
Baba wa Mbinguni ananitaka nijifunze.
-
Waombe watoto wako wakuambie kuhusu kile wanachojifunza shuleni au kwenye Darasa la Watoto. Ungeweza pia kushiriki baadhi ya vitu unavyojifunza. Kisha ungeweza kuwaonesha watoto wako maneno nini, kwa nini, na kwa jinsi gani. Wasaidie watafute Mafundisho na Maagano 88:77–79 ili kupata kile Bwana anachotutaka tujifunze kukihusu. Kisha pamoja angalieni katika mstari wa 80 ili kujua kwa nini Yeye anatutaka sisi tujifunze na katika mstari wa 118 ili kujua ni kwa jinsi gani tunapaswa kujifunza.
Nyumba yetu inaweza kuwa takatifu kama hekalu.
-
Unapowasomea watoto wako Mafundisho na Maagano 88:119, wangeweza kutengeneza mnara wa hekalu kwa mikono yao kila mara wanaposikia neno “nyumba.” Eleza kwamba Baba wa Mbinguni alimtaka Joseph Smith na Watakatifu wajenge hekalu, au “nyumba ya Mungu.”
-
Ungeweza kuwaomba watoto wako wachague maneno saba ambayo yanaelezea nyumbani kwao. Kisha wasaidie watafute, katika Mafundisho na Maagano 88:119, maneno saba Bwana anayoyatumia kuielezea nyumba Yake. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuifanya nyumba yetu iwe “nyumba ya Mungu”?