Njoo, Unifuate
Agosti 25–31: “Mpokee Utimilifu Wake”: Mafundisho na Maagano 93


“Agosti 25–31, ‘Mpokee Utimilifu Wake’: Mafundisho na Maagano 93,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 93,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo

Utondoti kutoka Namwona Mwana wa Mtu, na Walter Rane

Agosti 25–31: “Mpokee Utimilifu Wake”

Mafundisho na Maagano 93

“Unapopanda ngazi,” Joseph Smith alifundisha, “lazima uanze kutoka chini, na kupanda hatua kwa hatua, mpaka unafika juu; na ndivyo ilivyo kwa kanuni za injili—lazima uanze na ya kwanza, na kuendelea mpaka ujifunze kanuni zote za kuinuliwa” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 268).

Wakati mwingine ngazi ile ya kuinuliwa inaonekana ni ya juu sana kuifikia, lakini tulizaliwa kuipanda mpaka juu kwa msaada thabiti wa Mwokozi. Mapungufu yoyote yale tunayoweza kuyaona ndani yetu, Baba wa Mbinguni na Mwanawe wanaona kitu fulani kitukufu ndani yetu, kitu fulani cha kiungu. Kama vile ambavyo Yesu Kristo “alikuwa hapo mwanzo na Baba,” vivyo hivyo “ninyi pia mlikuwepo” (Mafundisho na Maagano 93:21, 23). Kama vile Yeye “alivyoendelea kutoka neema hadi neema, mpaka alipopokea utimilifu,” ndivyo pia “mtakavyopokea neema juu ya neema” (mstari wa 13, 20). Injili iliyorejeshwa inatufundisha kuhusu asili ya kweli ya Mungu, na kwa hiyo inatufundisha pia kuhusu asili yetu ya kweli na hatma yetu. Wewe ni mtoto halisi wa Mungu mwenye uwezekano wa “kupokea utimilifu wake kwa wakati wake” (mstari wa 19).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 93

Kama vile Yesu Kristo, ninaweza kutukuzwa na kupokea utimilifu wa Mungu.”

Nabii Joseph Smith alifundisha, “Kama watu hawawezi kuelewa sifa ya Mungu, hawajielewi wao wenyewe” (Mafundisho: Joseph Smith40). Unapojifunza kuhusu Mwokozi kwa kujifunza Mafundisho na Maagano 93, tafuta pia kile unachojifunza kuhusu wewe mwenyewe. Kwa mfano, unajifunza nini kuhusu Yeye kutoka mstari wa 3, 12–13, 21, na 26? Ni kweli zipi zinazofanana unazozipata kuhusu wewe mwenyewe katika mstari wa 20, 23, na 28–29? (Ona pia 1 Yohana 3:2; 3 Nefi 27:27). Maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia uelewe na utumie kweli katika sehemu hii:

  • Unahisi inamaanisha nini kupokea “neema juu ya neema” na kuendelea “kutoka neema hadi neema”? (mistari 12–13). Kama itasaidia, ungeweza kusoma “Neema” katika Mwongozo wa Maandiko (Maktaba ya Injili).

  • Unagundua nini kutoka kwenye ufunuo huu kuhusu jinsi ambavyo Mungu hutusaidia tukue na tujifunze? Ni kwa jinsi gani kujua hili kunaathiri jinsi unavyowatendea wengine—na wewe wenyewe?

  • Ni kipi unajifunza kuhusu “jinsi ya kuabudu, na … kile unachokiabudu”?mstari wa 19; ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Kuabudu,” Maktaba ya Injili).

Mafundisho na Maagano 93:1–39

ikoni ya seminari
Utukufu wa Mungu ni nuru na kweli.

Unaweza kuona kwamba maneno utukufu, nuru, na kweli yanatokea mara kwa mara katika ufunuo huu. Unapojifunza mstari wa 20–39 hasa, tengeneza orodha ya kweli unazojifunza kuhusu dhana hizi. Kutengeneza jedwali kama hili kunaweza kusaidia:

Mstari

Kile ninachojifunza

Maswali ya kutafakari

Mstari

24

Kile ninachojifunza

Maswali ya kutafakari

Kuna udanganyifu mwingi ulimwenguni. Ni kwa jinsi gani naweza kujua ukweli? (ona pia Yakobo 4:13).

Mstari

28

Kile ninachojifunza

Maswali ya kutafakari

Mstari

36

Kile ninachojifunza

Mungu ni mtu wa nuru na kweli.

Maswali ya kutafakari

Mstari

37

Kile ninachojifunza

Maswali ya kutafakari

Ni nani ninamfahamu ambaye anaonekana kuweza kukinza ushawishi wa uovu? Kwa nini wanaweza kufanya hivi?

Mstari

Kile ninachojifunza

Maswali ya kutafakari

Mstari

Kile ninachojifunza

Maswali ya kutafakari

Mstari

Ona pia: Mafundisho na Maagano 50:24

Kile ninachojifunza

Maswali ya kutafakari

Ni kipi unachopata katika mistari hii ambacho kinakutia msukumo wa kutafuta nuru kuu na ukweli? Kwa nini nuru na ukweli ni majina mazuri kwa ajili ya Yesu Kristo? (ona Yohana 8:12; 14:6). Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinaathiri maisha yako?

Pia ungeweza kuandika ahadi kuhusu hatma yako ya milele katika mstari wa 20, 22, 28, 33–35. Kuna uhusiano gani kati ya ahadi hizi na kupokea nuru?

Fikiria kuchunguza “Tembea katika nuru ya Mungu” (Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi, 18–21) ili kujua nini unaweza kufanya ili kupata nuru na jinsi Bwana anavyoahidi kukubariki. Video za “Light and Truth, Part 1” na “Part 2” (Maktaba ya Injili) ninaweza kutoa mawazo ya ziada.

Ona pia “Nifundishe Mwenendo wa Nuru,” Nyimbo wa Dini, na. 194; Topics and Questions, “Holy Ghost,” Maktaba ya Injili.

6:39

Light and Truth, Part 1

(D&C 88:6-13) This video examines God's attributes of light and truth as explained in section 88 of the Doctrine and Covenants.

6:49

Light and Truth, Part 2

(D&C 93:28,36-40) This video examines God's attributes of light and truth as explained in section 88 of the Doctrine and Covenants.

dirisha katika hekalu

“Utukufu wa Mungu ni … nuru na kweli.”

Mafundisho na Maagano 93:40–50

“Iweke sawa sawa nyumba yako mwenyewe.”

Amri ya “kuiweka sawa sawa nyumba yako mwenyewe” (mstari wa 43) siyo kuhusu kupanga makabati na vyumba vya faragha bali kuhusu kufundisha—na kujifunza—“nuru na kweli” (mstari wa 42). Fikiria jinsi unavyojaribu kufuata ushauri huu. Ni changamoto zipi unakabiliana nazo? Ni kweli zipi katika Mafundisho na Maagano 93 zinaweza kusaidia?

Ni umaizi upi unaoupata kutoka kwenye mafundisho haya ya Mzee David A. Bednar?

“Katika ofisi yangu kuna mchoro maridadi wa shamba la ngano. Mchoro huo ni mkusanyiko mkubwa wa alama—ambazo hakuna ambayo ikiwa peke yake inavutia wala kupendeza. Kwa kweli, ukisimama karibu na mchoro, yote unayoweza kuona ni wingi wa mistari ya njano na ya rangi ya dhahabu na kahawia ambayo inaonekana kutohusiana na kutovutia. Hata hivyo, unaposogea taratibu mbali na picha hiyo, kila mpako wa rangi moja inajumuishwa na zingine na kuzaa mazingira ya kupendeza ya shamba la ngano. Nyingi za alama za kawaida, kila moja hufanya kazi pamoja ili kuumba mchoro unaovutia na maridadi.

“Kila sala ya familia, kila tukio la kujifunza maandiko kama familia, na kila jioni ya familia nyumbani ni alama kwenye mchoro wa nafsi zetu. Hakuna tukio moja linaloweza kuonekana kuwa la kuvutia sana ama la kukumbukwa. Lakini kama vile tu alama za rangi ya njano na dhahabu na kijivu zinavyokamilishana vyema na kuzalisha picha inayovutia, ndivyo pia msimamo wetu wa kufanya mambo yanayoonekana kuwa madogo unavyoweza kusababisha matokeo muhimu ya kiroho. ‘Kwa hiyo, msichoke kutenda mema, kwa kuwa mnaijenga misingi ya kazi kubwa. Na kutokana na mambo madogo huja yale yaliyo makuu” [Mafundisho na Maagano 64:33]. Uthabiti ni kanuni muhimu tunapouweka msingi wa kazi kuu katika maisha yetu binafsi na tunapokuwa wenye bidii na kuwajibika katika nyumba zetu wenyewe” (“Wenye Bidii Zaidi na Kuwajibika Zaidi Nyumbani,” Liahona, Nov. 2009, 19–20).

Ona pia Henry B. Eyring, “Nyumba Ambapo Roho wa Bwana Hukaa,” Liahona, Mei 2019, 22–25

familia wakiomba pamoja

Bwana anawaamuru wazazi “kulea watoto wao katika nuru na kweli.”

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni ya 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 93:2–21

Yesu Kristo ndiye Nuru na Uzima wa Ulimwengu.

  • Fikiria kuonesha picha ya Mwokozi na kuwaliza watoto wako kwa nini ni muhimu kujifunza kumhusu Yesu Kristo na kumfuata Yesu Kristo. Kisha mngeweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 93:19 ili kugundua sababu moja muhimu.

  • Unaweza kutaka kuchagua kweli kadhaa kuhusu Kristo katika sehemu ya 93 ambazo zinakupatia msukumo na wasaidie watoto wako wazigundue na wazielewe (ona pia “Sura ya 33: Ufunuo kuhusu Yesu Kristo,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 126–27, au video inayohusiana nayo katika Maktaba ya Injili). Kwa kila ukweli unaochagua, ungeweza kuwapa watoto wako neno au kirai cha kusikiliza pale mnapousoma mstari huu pamoja. Kwa mfano, Yesu Kristo:

    1:18

    Chapter 33: A Revelation about Jesus Christ: May 1833

mchoro wa Kristo

Utondoti kutoka Nuru ya Ulimwengu, na Howard Lyon

Mafundisho na Maagano 93:23, 29, 38

Niliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani.

  • Mwokozi amesisitiza mara tatu katika sehemu ya 93 kwamba sisi tuliishi pamoja na Mungu “hapo mwanzo” (mstari wa 23, 29, 38). Ili kuwasaidia watoto wako wagundue hili, ungeweza kuwaalika wasome Mafundisho na Maagano 93:23, 29, 38 na watafute ukweli kuhusu wao wenyewe ambao unarudiwa katika mistari hii. Ni kwa nini Baba wa Mbinguni anatutaka tujue ukweli huu? Ungeweza pia kuwauliza watoto wako kile wanachojua kuhusu maisha yetu pamoja na Baba wa Mbinguni kabla ya kuzaliwa. Ili kuwasaidia wajifunze zaidi, soma pamoja nao kifungu kimoja au zaidi vifuatavyo: Yeremia 1:5; Mafundisho na Maagano 138:53–56; Musa 3:5; Ibrahimu 3:22–26.

  • Mngeweza pia kuimba pamoja “I am a Child of God” au:I lived in heaven: (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3, 4)., na mjadili kweli tunazojifunza kutoka kwenye nyimbo hizi kuhusu dhumuni letu la kuja duniani.

Mafundisho na Maagano 93:24–39

Ninapokea nuru na kweli ninapomtii Mungu.

  • Ili kuwasaidia watoto wako watumie kweli kuhusu utiifu katika Mafundisho na Maagano 93, fikiria kuandika marejeleo machache ya maandiko kutoka katika sehemu hii juu ya kipande cha karatasi. Kwenye vipande tofauti vya karatasi, andika kweli ambazo kila moja ya mistari hii inazifundisha. Watoto wako wangeweza kufanya kazi pamoja kusoma mistari hii na kuoanisha kweli na marejeleo ya maandiko. Mifano ingeweza kujumuisha:

    • Mstari wa 24: Ukweli ni kujua mambo halisi yaliyopita, ya sasa, na ya baadaye.

    • Mstari wa 28: Ninaweza kupokea nuru na ukweli ninapotii amri.

    • Mstari wa 37: Ninapokuwa na nuru na kweli, ninaweza kukinza uovu.

    • Mstari wa 39: Ninapoteza nuru ba kweli ninapokuwa si mtiifu.

    Unaweza kutaka kushiriki mifano ya kweli ambazo umepata kuzijua unapotii amri za Bwana.

Tohoa kulingana na umri wa watoto wako. Unayajua mahitaji na uwezo wa watoto wako; kuwa huru kutohoa mawazo ya shughuli ili kukidhi mahitaji yao. Kwa mfano, katika shughuli hii, kama unawafundisha watoto wadogo, inaweza kuwa vyema kufokasi kwenye ukweli mmoja rahisi kutoka kwenye sehemu ya 93

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

mchoro wa Kristo akihubiri kutoka kwenye Torati

Nuru na Kweli, na Simon Dewey

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto