Njoo, Unifuate
Septemba 8–14: “Tulieni na Jueni Kuwa Mimi ni Mungu”: Mafundisho na Maagano 98–101


“Septemba 8–14: ‘Tulieni na Jueni Kuwa Mimi ni Mungu’: Mafundisho na Maagano 98–101,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 98–101,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

makundi yenye fujo yakiwashambulia Watakatifu huko Missouri

C.C.A. Christensen (1831–1912), Watakatifu Wakifukuzwa kutoka Jackson County Missouri, c. 1878, mafuta kwenye kitambaa cha pamba, inchi 77 ¼ × 113. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, zawadi ya wajukuu wa C.C.A. Christensen, 1970

Septemba 8–14: “Tulieni na Mjue Kuwa Mimi ni Mungu”

Mafundisho na Maagano 98–101

Kwa Watakatifu mnamo miaka ya 1830, Independence, Missouri, kiuhalisia ilikuwa nchi ya ahadi. Palikuwa “mahali pa katikati” ya Sayuni (Mafundisho na Maagano 57:3)—mji wa Mungu duniani—na kukusanyika kwa Watakatifu mahala pale ulikuwa utangulizi wa kusisimua kwa Ujio wa Pili. Lakini majirani zao sehemu ile waliona mambo kitofauti. Walipinga madai kwamba Mungu ametoa ardhi kwa Watakatifu, na walikuwa hawana raha kwa matokeo ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii ya watu wengi mno waliohamia kwa haraka mno. Kutokuwa na furaha punde kuligeuka kuwa mateso na ghasia. Mnamo 1833, ofisi ya uchapishaji ya Kanisa iliharibiwa, na Watakatifu walifurushwa kutoka kwenye nyumba zao.

Joseph Smith alikuwa umbali wa zaidi ya maili 800 huko Kirtland, na habari hizi zilichukuwa wiki nyingi kumfikia. Lakini Mungu alijua nini kilichokuwa kinatokea, na alifunua kwa Nabii Wake kanuni za amani na za kutia moyo ambazo zingewafariji Watakatifu—kanuni ambazo pia zinaweza kutusaidia wakati tunapokabiliwa na mateso, wakati matamanio yetu ya haki hayatimizwi, au wakati tunapohitaji kukumbushwa kwamba mateso yetu ya kila siku hatimaye, kwa vyovyote vile, “yatafanya kazi kwa pamoja kwa faida [yetu]” (Mafundisho na Maagano 98:3).

Ona Saints, 1:171–93; “Waiting for the Word of the Lord,” katika Revelations in Context, 196–201.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 98:1–3, 11–14, 22; 101:1–16, 22–31, 36

ikoni ya seminari
Majaribu yangu yanaweza kufanya kazi pamoja kwa faida yangu.

Baadhi ya changamoto zetu maishani zinasababishwa na chaguzi zetu wenyewe. Zingine zinasababishwa na chaguzi za wengine. Na wakati mwingine mambo hutokea tu ambayo ni sehemu ya maisha ya duniani. Bila kujali sababu, dhiki inaweza kusaidia kutimiza azma takatifu pale tunapomgeukia Mungu.

Hii ilikuwa kweli kwa Watakatifu wa Missouri mnamo 1833, na ni kweli kwetu leo. Unaposoma kile Bwana alichowaambia Watakatifu katika Mafundisho na Maagano 98 na 101, tafakari jinsi ambavyo ujumbe Wake hutumika kwenye majaribu tofauti tofauti au magumu unayoweza kuyapata. Hapa kuna baadhi ya maswali na nyenzo za kukusaidia.

Kama jaribu ni matokeo ya:

  • Chaguzi binafsi: Ni ushauri—na ahadi zipi—unazipata katika Mafundisho na Maagano 98:11–12; 101:1–9? Unajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Ni kipi unahisi Mungu angetaka wewe ufanye?

  • Chaguzi za wengine: Ni faraja ipi unaipata katika Mafundisho na Maagano 98:1–3, 22; 101:10–16, 22? Ni kwa jinsi gani Bwana anatutaka tujibu unyanyasaji, uonevu, au vurugu? (Ona pia Life Help, “Abuse,” Maktaba ya Injili; Topics and Questions, “Abuse” Maktaba ya Injili.) Ni kipi mistari hii inafundisha kuhusu jinsi ya kuweka tumaini lako katika Bwana?

  • Magumu ya maisha ya duniani: Ni mtazamo gani unaupata kutoka Mafundisho na Maagano 98:1–3; 101:22–31, 36? Ni kipi unajifunza kutokana na majaribu yako? Ni kipi unafanya ili kualika msaada wa Mungu? Ni kwa jinsi gani Yeye anakusaidia wewe?

Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi Mungu anavyoweza kufanya “mambo yote ambayo kwayo mmeteswa … yafanye kazi kwa pamoja kwa faida yenu” (Mafundisho na Maagano 98:3), fikiria kujifunza ujumbe wa Mzee Anthony D. Perkins “Wakumbuke Watakatifu Wako Wanaoteseka, Ee Mungu Wetu” (Liahona, Nov. 2021, 103–5). Ungeweza kutafuta kifungu cha maneno katika ujumbe wake ambacho kinakusaidia uelewe jinsi Mwokozi anavyokualika uzione changamoto zako. Ni kwa njia zipi majaribu yako yamefanya kazi pamoja kwa faida yako au kutimiza azma za Mungu?

Ona pia Warumi 8:28; 2 Nefi 2:2; Mafundisho na Maagano 90:24; D. Todd Christofferson, “Njooni Sayuni,” Liahona, Nov. 2008, 37–40; “Trial of Adversity,” “Feeling the Lord’s Love and Goodness in Trials,” “The Refiner’s Fire” (video), ChurchofJesusChrist.org.

2:3

Trial of Adversity

Katie, who was paralyzed in an auto accident, shares how she exercises her faith to embrace her new life.

4:17

Feeling the Lord's Love and Goodness in Trials

When Darlyn learned of her illness, she feared she would not see her children grow up. But through her trial, she felt the Lord’s love and immense goodness. How does He comfort you in times of trial?

5:2

The Refiner's Fire

The refiner’s fire is not a comfortable place to be. It involves intense heat and repeated hammering. But it is in the refiner’s fire we are purified and prepared to meet God.

Mafundisho na Maagano 98:23–48

Bwana ananitaka nitafute amani katika njia Yake.

Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Wafuasi wa Yesu Kristo wanapaswa kuwa kielelezo kwa ulimwengu wote kufuata. Ninawasihi mfanye yote muwezayo kumaliza mizozo binafsi ambayo kwa sasa inapamba moto mioyoni mwenu na katika maisha yenu” (“Nguvu ya Msukumo wa Kiroho,” Liahona, Mei 2022, 97).

Wakati si kila kitu katika Mafundisho na Maagano 98:23–48 kitatumika kwenye michangamano yako na wengine, je, ni kanuni zipi unazozipata ambazo zinaweza kukuongoza umalize mizozo binafsi katika maisha yako? Unaweza kupata kweli za ziada katika wimbo kuhusu amani au msamaha, kama vile “Truth Reflects upon Our Senses” (Nyimbo za Kanisa,, na. 273).

mchoro wa Yesu Kristo

Utondoti kutoka Kristo na Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hofman

Mafundisho na Maagano 99–100

Bwana huwatunza watu ambao wanamtumikia Yeye.

Mafunuo katika sehemu ya 99 na 100 yalitolewa kwa watu ambao walikuwa na majukumu muhimu ya Kanisa lakini walikuwa pia na wasiwasi kuhusu familia zao. Unapata nini katika mafunuo haya ambacho kingeweza kuwasaidia? Ni ujumbe upi Bwana anao kwa ajili yako katika mafunuo haya?

Ona pia “John Murdock’s Missions to Missouri” katika “‘I Quit Other Business’: Early Missionaries” na “A Mission to Canada,” in Revelations in Context, 87–89, 202–7.

Mafundisho na Maagano 101:43–65

Kufuata ushauri wa Mungu husaidia kuniweka salama.

Mfano katika Mafundisho na Maagano 101:43–62 huelezea kwa nini Bwana aliruhusu Watakatifu kufukuzwa nje ya Sayuni. Unaposoma mistari hii, je, unaona jinsi yoyote ambayo wewe ni kama watumishi katika mfano huu? Ni kwa jinsi gani unamwonesha Mungu kwamba uko “tayari kuongozwa katika njia ya haki na iliyo sahihi kwa wokovu [wako]”? (ona mstari wa 63–65).

Igiza matukio au mifano. Wakati mwingine ni rahisi kujifunza na kuhusisha hadithi na mifano katika maandiko wakati tunapojiweka katika nafasi za watu ambao hadithi au mifano hiyo inawaelezea. Kama unafundisha Mafundisho na Maagano 101:43–62, ungeweza kuwaalika wanafunzi waigize mfano wakati mtu anasoma kwa sauti. Ni umaizi upi unaupata kutokana na kugeuza maneno kuwa vitendo?

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni ya 03 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 98:1–3

Yesu Kristo anaweza kugeuza majaribu yangu yawe baraka.

  • Ungeweza kuanza majadiliano kwa kuwauliza watoto wako kuhusu baadhi ya changamoto ambazo watoto wa rika lao wanakabiliana nayo. Mngeweza kisha kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 98:1–3 na kuzungumza kuhusu jinsi gani Yesu Kristo anaweza kugeuza majaribu yawe baraka. Ungeweza kushiriki na watoto wako mifano ya jinsi ambavyo Yeye amegeuza majaribu yako yawe baraka.

Mafundisho na Maagano 98:39–40

Mwokozi hunisaidia nisamehe.

Zingatia: Unapowafundisha watoto wako umuhimu wa msamaha, hakikisha pia wanaelewa kwamba kama mtu akiwaumiza, daima wanapaswa kumwambia mtu mkubwa wanayemwamini.

  • Sura ya 34 na 35 katika Hadithi za Mafundisho na Maagano (128–34) zingeweza kukusaidia ufundishe kuhusu jinsi Watakatifu walivyotendewa huko Missouri katika mwaka wa 1833. Wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu jinsi Watakatifu hawa walivyohisi. Kisha mngeweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 98:23, 39–40 ili kujua kile ambacho Bwana aliwataka wafanye. Wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu nyakati ulipohitajika kumsamehe mtu fulani na jinsi Mwokozi alivyokusaidia.

  • Ungeweza pia kuwaonesha watoto wako picha ya sura ya furaha na sura ya huzuni. Zungumza kuhusu hali ambazo kwazo mtu si mkarimu, na pendekeza jinsi ya kujibu. Wasaidie watoto wako wachague ikiwa kila jibu lingewafanya wawe na furaha au huzuni kwa kuonesha uso unaohusiana nalo. Ni kwa nini Yesu anatutaka tuwasamehe watu, hata wale ambao si wakarimu kwetu?

2:42

Chapter 34: God Warns the People of Zion: July–August 1833

2:10

Chapter 35: The Saints Leave Jackson County, Missouri: September–December 1833

Mafundisho na Maagano 101:16; 23–32

Yesu Kristo anaweza kuniletea amani.

  • Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 101:16, wasaidie watoto wako watambue hisia za amani ambazo huja tunapokuwa tumetulia na kuwaza juu ya Yesu—kwa mfano, wakati tunaposali au tunaposhiriki sakramenti. Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu staha, kama vile “Reverently, Quietly” au “To Think about Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, 26, 71). Ni kwa jinsi gani tunaweza kuhisi amani Yake katika nyumba yetu?

  • Watoto wako wangeweza kufurahia kujifunza kuhusu vile maisha yatakavyokuwa wakati Yesu atakapokuja tena. Someni Mafundisho na Maagano 101:23–32 pamoja, na zungumzeni kuhusu vitu walivyovipata katika mistari hii ambavyo vitatuletea shangwe wakati Yeye atakapokuja. Ni kwa nini inasaidia kujua kuhusu mambo haya wakati tunapokuwa na wakati mgumu?

Yesu Kristo akimkumbatia mtoto

Yesu Kristo ataleta amani na shangwe wakati atakapokuja tena.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

mchoro wa makundi ya wenye fujo yakiwatesa Watakatifu wa Siku za mwisho

Missouri Inaungua, na Glen S. Hopkinson

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto