“Septemba 22–28, ‘Kwa Mfano wa Mwana wa Mungu’: Mafundisho na Maagano 106–108,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 106–108,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Septemba 22–28: “Kwa Mfano wa Mwana wa Mungu”
Mafundisho na Maagano 106–108
Kwa mtazamo wa kwanza, Mafundisho na Maagano 107 huonekana kuwa tu kuhusu kuratibu ofisi za ukuhani kwenye muundo wa uongozi kwa ajili ya Kanisa la Bwana. Wakati ufunuo huu ulipochapishwa, uumini wa Kanisa ulikuwa umezidi uwezo wa viongozi wachache waliokuwepo. Kueleza kwa muhtasari majukumu na wajibu wa Urais wa Kwanza, Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili, Sabini, maaskofu, na urais wa akidi kwa hakika kulikuwa kunahitajika na kulisaidia. Lakini kuna mengi zaidi kwenye maelekezo matakatifu katika sehemu ya 107 kuliko tu jinsi uongozi wa Kanisa ulivyopaswa kuratibiwa. Hapa, Bwana anatufundisha sisi kuhusu nguvu Zake na mamlaka Yake, “Ukuhani Mtakatifu, kwa mfano wa Mwana wa Mungu” (mstari wa 3). Kusudi la ukuhani ni kufungua “baraka zote za kiroho za kanisa” ili kwamba watoto wote wa Mungu waweze “kupata mbingu kufunuliwa kwao” na “kufurahia ushirikiano wao na uwepo wa Mungu Baba, na Yesu aliye mpatanishi wa agano jipya” (mstari wa 18–19). Katika kutufundisha kuhusu ukuhani Wake, Mwokozi anatufundisha kuhusu Yeye Mwenyewe na jinsi tunavyoweza kuja Kwake.
Ona “Restoring the Ancient Order,” katika Revelations in Context, 208–12.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Mafundisho na Maagano 106; 108
Bwana hunisaidia mimi wakati Yeye anaponiita nitumikie.
Katika Mafundisho na Maagano 106 na 108, Bwana alitoa ushauri na ahadi kwa waumini wawili walioitwa kutumikia katika Kanisa. Unapojifunza ushauri Wake, ungeweza kufikiria kuhusu fursa zako mwenyewe za kumtumikia Bwana—pengine jukumu la uhudumiaji, wito wa Kanisa, majukumu katika familia yako, au misukumo ya kiroho ya kutenda mema.
Je, unahisi ujumbe wa Bwana kwako ni upi katika mafunuo haya? Ni virai gani vinaonekana kuwa na maana kwako hasa? Hivi ni baadhi ya vichache vya kuzingatia:
-
Ni lini Bwana amekupa wewe “neema [au msaada wa kiungu] na hakikisho” la kukuwezesha umtumikie Yeye? (Mafundisho na Maagano 106:8).
-
Unadhani inamaanisha nini kuwaimarisha wengine “katika matendo yako yote”? (Mafundisho na Maagano 108:7).
Wakati Mzee Carl B. Cook alipopokea jukumu zito la Kanisa, alipata nguvu kutoka kwenye uzoefu wa mababu zake. Soma kuhusu nguvu hiyo katika ujumbe wake “Tumikia” (Liahona, Mei 2016, 110–12). Zingatia kuandika barua ya kuwahimiza vizazi vyako—au wewe mwenyewe siku za usoni—kukubali fursa za kumtumikia Bwana. Jumuisha katika barua yako kweli unazojifunza kutoka kwenye ujumbe wa Mzee Cook, Mafundisho na Maagano 106 na 108, na uzoefu wako mwenyewe.
Ona pia Henry B. Eyring, “Tembea pamoja Nami,” Liahona, Mei 2017, 82–85; Topics and Questions, “Serving in Church Callings,” Maktaba ya Injili; “Warren Cowdery” na “‘Wrought Upon’ to Seek a Revelation,” katika Revelations in Context, 219–23, 224–28.
Mafundisho na Maagano 107:1–4, 18–20
Ukuhani ni “kwa Mfano wa Mwana wa Mungu.”
Bwana alianza “ufunuo Wake kuhusu ukuhani” (Mafundisho na Maagano 107, kichwa cha habari cha sehemu) kwa kutufundisha jina la asili la Ukuhani wa Melkidezeki (ona mstari wa 1–4). Kwa nini unadhani ni muhimu kujua hilo? Ni kwa jinsi gani jina hili linashawishi jinsi unayofikiri kuhusu ukuhani?
Kumbuka mawazo haya pale unaposoma kuhusu ukuhani, hasa katika mstari wa 18–20. Inamaanisha nini “mbingu kufunuliwa”? Inamaanisha nini “kufurahia ushirika na uwepo wa Mungu Baba, na Yesu”? Ni kwa jinsi gani nguvu na mamlaka ya ukuhani wa Mwokozi hufanya haya yote yapatikane kwako?
Ona pia Alma 13:2, 16; Mafundisho na Maagano 84:19–27.
Watumishi wa Bwana “huungwa mkono kwa kuaminiwa, imani, na sala ya Kanisa.”
Unadhani inamaanisha nini kuwaunga mkono watumishi wa Bwana kwa kuamini kwako? kwa imani yako? kwa sala yako?
Ona pia “Mungu Mbariki,” Nyimbo za Dini, na. 12.
Mafundisho na Maagano 107:23–24, 33–35, 38, 91–92
Manabii na Mitume wanashuhudia juu ya Yesu Kristo.
Joseph Smith alishiriki sehemu ya 107 mnamo 1835 kwa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wapya (ona kichwa cha habari cha sehemu). Ni kipi Bwana aliwafundisha kuhusu wito wao katika mstari wa 23–24, 33–35, 38? Je, ni kwa jinsi gani ushahidi wako wa Yesu Kristo umeimarishwa kwa mafundisho na huduma ya Mitume Wake walio hai?
Katika mstari wa 91–92, Bwana anafundisha kuhusu Mtume Wake mkuu, Rais wa Kanisa. Ni kwa jinsi gani yeye ni “kama Musa”? (ona Mwongozo wa Maandiko, “Musa,” Maktaba ya Injli).
Ona pia David A. Bednar, “Kuchaguliwa Kushuhudia Jina Langu,” Liahona, Nov. 2015, 128–31.
Mafundisho na Maagano 107:27–31, 85–89
Mungu hutimiza kazi Yake kupitia mabaraza.
Tazama kile Bwana alichofundisha kuhusu mabaraza katika Mafundisho na Maagano 107:27–31, 85–89. Nini hufanya mabaraza yawe yenye tija? Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia kanuni hizi katika wito wako wa Kanisa, nyumbani kwako, au kwenye majukumu yako mengine?
Ona pia Russell M. Nelson, “Mabaraza ya Familia,” Liahona, Mei 2016, 63–65; Kitabu cha Maelezo Jumla, 4.3–4.4, Maktaba ya Injili.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mafundisho na Maagano 107:18–20
Yesu Kristo hunibariki kupitia nguvu Zake za ukuhani.
-
Wewe na watoto wako mnaposoma pamoja Mafundisho na Maagano 107:18–19, sisitiza kirai “baraka zote za kiroho.” Pengine wewe na watoto wako mngeweza kuorodhesha baraka ambazo zinakuja kutokana na ukuhani. Ungeweza kutengeneza mchezo wake—kuona ni nani anaweza kutengeneza orodha ndefu. Watoto wako wangeweza pia kuchora au kutafuta picha kuwakilisha baraka hizi (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Mngeweza kisha kuzungumza kuhusu jinsi ibada za ukuhani (kama vile ubatizo au sakramenti) hutusaida kupokea baraka za Mungu.
Mafundisho na Maagano 107:21–26, 33–35, 91–92
Watumishi wateule wa Bwana wanaliongoza Kanisa Lake.
-
Kila toleo la mkutano mkuu la Liahona hujumuisha ukurasa wa picha za Viongozi Wakuu wenye Mamlaka. Zingatia kuangalia picha hizi pamoja na watoto wako pale mnaposoma kuhusu majukumu yao katika Mafundisho na Maagano 107:21–26, 33–35, 91–92. Wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu kwa nini mna shukrani kwamba Bwana amewapatia majukumu haya.
-
Watoto wako wanaweza kujifunza kuhusu watumishi wa Bwana kwenye “General Church Leadership” kwenye ChurchofJesusChrist.org. Pengine kila mmoja wa watoto wako angeweza kujifunza kuhusu mmoja wa viongozi hawa na kufundishana kumhusu. Shirikini mmoja na mwingine jinsi mnavyojua kwamba viongozi hawa ni watumishi wa kweli wa Yesu Kristo.
-
Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 107:22 pamoja, wewe na watoto wako mngeweza kufanya zamu kunyanyua picha ya Urais wa Kwanza na kushiriki jinsi mnavyoweza kuwaunga mkono kama watumishi wa Bwana.
Ninaweza kuwa mwangalifu katika kuishi maagano yangu.
-
Ili kuanzisha mazungumzo kuhusu mstari huu, ungeweza kuwaalika watoto wako wafanye kitu fulani ambacho kinahitaji uangalifu makini, kama vile kujaza kikombe bila kumwaga. Je, ni kitu gani hutokea wakati tunapokuwa si waangalifu? Kisha mngeweza kusoma Mafundisho na Maagano 108:3 ili kujua kile ambacho Bwana anatutaka tufanye kwa uangalifu. Ni “viapo” (ahadi na maagano) gani tunafanya na Mungu? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa waangalifu kuhusu kuvishika? Ungeweza kushiriki sehemu za ujumbe wa Dada Becky Craven “Makini dhidi ya Kawaida” (Liahona, Mei 2019, 9–11), ambazo unahisi zingeweza kuwapa watoto wako msukumo wa kushika maagano yao. Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu kushika maagano, kama vile “I Will Be Valiant” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 162).