Njoo, Unifuate
Oktoba 6–12: “Nitayapanga Mambo Yote kwa Faida Yenu”: Mafundisho na Maagano 111–114


“Oktoba 6–12: ‘Nitayapanga Mambo Yote kwa Faida Yenu’: Mafundisho na Maagano 111–114,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 111–114,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Joseph Smith akifundisha katika Hekalu la Kirtland

Oktoba 6–12: “Nitayapanga Mambo Yote kwa Faida Yenu”

Mafundisho na Maagano 111–114

Je, umewahi wakati wowote kuwa na uzoefu wa kiroho ambao ulikufanya ujisikie kujiamini na salama katika imani yako kwa Kristo—lakini kisha mateso ya maisha yakajaribu imani yako, na ukajikuta ukipambana kuipata tena amani uliyoihisi kabla? Kitu fulani kama hicho kilitokea kwa Watakatifu huko Kirtland. Chini ya mwaka mmoja baada ya bubujiko za kiroho zilizohusishwa na kuwekwa wakfu kwa Hekalu la Kirtland, matatizo yaliibuka. Mgogoro wa kifedha, mzozo ndani ya Akidi ya Wale Kumi na Wawili, na majaribu mengine yalisababisha baadhi ya Watakatifu kuyumba katika imani yao licha ya uzoefu wao wa awali.

Hatuwezi kuepuka majaribu, kwa hiyo ni kwa jinsi gani tunaweza kuyazuia kutishia imani na ushuhuda wetu? Huenda sehemu ya jibu inaweza kupatikana katika ushauri wa Bwana katika Mafundisho na Maagano 112, uliotolewa wakati dhiki huko Kirtland ilikuwa inazidi kuvimba. Bwana alisema, “Itakaseni mioyo yenu mbele zangu” (mstari wa 28), “Msiasi” (mstari wa 15), “Fungeni viuno vyenu kwa ajili ya kazi” (mstari wa 7), na “Jinyenyekeze” (mstari wa 10). Tunapofuata ushauri huu, Bwana “atatuongoza [sisi] kwa mkono” kuipitia dhiki yote na kuingia kwenye uponyaji na amani (ona mistari 10,13).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 111

Bwana anaweza “kupanga mambo yote kwa ajili ya faida [yangu].”

Ilipofika mwaka wa 1836, Kanisa lilikuwa limelimbikiza madeni makubwa katika kufanya kazi ya Bwana. Joseph Smith na wengine walikuwa na wasiwasi kuhusu madeni haya na kufikiria njia za kuyalipa (ona kichwa cha habari cha sehemu cha Mafundisho na Maagano 111).

Unaposoma Sehemu ya 111, fikiria jinsi maneno ya Bwana kwa Joseph yanavyotumika kwako—na mambo yanayokutia wasiwasi. Kwa mfano, ni lini ulihisi upendo wa Mungu “licha ya ujinga wako” (mstari wa 1)? Je, ni kwa jinsi gani Bwana amekusaidia upate “hazina” zisizotegemewa (mstari wa 10)? Yeye amefanya nini ili “kupanga mambo yote kwa faida yako” (mstari wa 11)? Je, kirai “haraka kadiri mtakavyoweza kuyapokea” kinakufundisha nini kuhusu Baba wa Mbinguni?

Ona pia Mathayo 6:19–21, 33; “Hazina Nyingi Zaidi ya Moja,” Ufunuo katika Muktadha, 229–34.

Mafundisho na Maagano 112:3–15, 22

ikoni ya seminari
Bwana ataniongoza niwapo mnyenyekevu na mwenye kutafuta mapenzi Yake.

Thomas B. Marsh, Rais wa Akidi ya Wale Kumi na Wawili, alikasirika kwamba Joseph Smith, pasipo kushauriana naye, aliwaita washiriki wawili wa akidi yake kwenda kuhubiri injili huko Uingereza. Alikutana na Nabii, ambaye alipokea ufunuo ambao ulimsaidia Thomas kuweka kando hisia zake za maumivu. Ufunuo huo umeandikwa katika Mafundisho na Maagano 112.

Weka muktadha huu akilini unapojifunza Mafundisho na Maagan 112. Ni kitu gani umekipata ambacho yawezekana kiliponya hisia za maumivu ya Thomas? Katika mistari 3–15 na 22, ungeweza katafuta majibu ya maswali kama haya: Je, unyenyekevu ni nini? Inamaanisha nini kwa Bwana kukuongoza “kwa mkono”? Kwa nini unafikiri kuwa mnyenyekevu kunakusaidia upokee mwongozo wa Bwana? Ungeweza kupata majibu ya ziada katika “Mpangilio wa Unyenyekevu” katika ujumbe wa Mzee Joseph W. Sitati “Mipangilio ya Ufuasi” (Liahona, Nov. 2022, 87–88).

Mfikirie mtu unayemfahamu ambaye ni mnyenyekevu. Mtu huyu anafanya nini kuonyesha unyenyekevu? Unajifunza nini kutoka kwa Mwokozi kuhusu kuwa mnyenyekevu? Pengine unaweza kutafuta picha za nyakati katika maisha Yake wakati alipoonyesha unyenyekevu.

Ni lini wewe ulihisi kuongozwa na Bwana ulipojinyenyekeza mwenyewe?

Ona pia Ulisses Soares, “Uwe Mnyenyekevu na Mpole wa Moyo,” Liahona, Nov. 2013, 9–11; “The Faith and Fall of Thomas Marsh,” katika Ufunuo katika Muktadha, 54–60; Topics and Questions, “Humility,” Maktaba ya Injili; “Nyenyekea,” Nyimbo za Dini, na. 63.

Shirikisha Wanafunzi Fikiria kuhusu jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kwa ukamilifu washiriki katika kijifunza kweli katika maandiko. Kwa mfano, ili kuwasaidia waelewe kile Bwana alichosema katika Mafundisho na Maagano 112:10, ungeweza kumziba macho mtu na kwa uangalifu mwongoze kwa kumshika mkono kuzunguka kizuizi cha viti au vitu vingine. Tunaweza kujifunza nini kuhusu unyenyekevu kutokana na onyesho hili?

Mafundisho na Maagano 112:12–26, 28, 33–34

Wale ambao wameongoka kwa dhati huja kumjua Yesu Kristo.

Ukweli kwamba baadhi ya mitume katika mwaka 1837 waligeuka dhidi ya Nabii ni ukumbusho mzuri kwamba licha ya wito wetu katika Kanisa ambao tunao au ni kwa kiasi gani tunaijua injili, lazima binafsi tuhakikishe kuwa tumeongoka kwa Kristo. Pengine mngeweza kusoma Mafundisho na Maagano 112:12–26, 28, 33–34 na kutafuta kweli ambazo zinaweza kuwasaidia kushinda majaribu ya imani au kuwa wenye kuongoka kikamilifu zaidi kwa Bwana. Unaweza kujisikia kushawishika kushiriki kile ulichokipata ili kumsaidia mtu mwingine kuimarisha uongofu wao kwa Kristo.

Mafundisho na Maagano 113

Joseph Smith alikuwa “mtumishi katika mikono ya Kristo.”

Nabii Isaya alimtaja mmoja wa wazao wa Yese kama “chipukizi” na “mzizi” (Isaya 11:1, 10). Katika sehemu ya 113, Bwana anaelezea kwamba mzao huyu, mtumishi wa Kristo, angekuwa chombo katika kuwakusanya watu wa Bwana katika siku za mwisho (ona Mafundisho na Maagano 113:4, 6). Unabii huu unamwelezea Nabii Joseph Smith vizuri sana. Ni jinsi gani unabii huu na kweli zingine katika sehemu ya 113 vimekuwa vikiwatia moyo Watakatifu wakati wa misukosuko waliyokuwa wanaipitia huko Kirtland? Unapata nini katika ufunuo huu ambacho kinakuvutia kubaki imara na kuendelea kushiriki katika kazi ya Bwana hivi leo?

Ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Yese,” Maktaba ya Injili; 2 Nefi 21:10–12; Joseph Smith—Historia ya 1:40.

kielelezo cha Isaya 11:1

Isaya aliandika juu ya “chipukizi” na “mizizi” inayotoka kwenye “shina la Yese” (Isaya 11:1).

Kwa mawazo zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya 01 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 111:2, 10–11

Mambo ya Mungu yanaweza kuwa hazina kwangu.

  • Wewe na watoto wako mngeweza kuchora kile kinachokuja akilini mnaposikia neno hazina. Kisha mngeweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 111:2, 10–11, na kulinganisha hazina za duniani na vitu ambavyo Bwana huviona kuwa ni hazina. (Ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii.) Ni kwa jinsi gani tunaweza kuyaona mambo ya Mungu kuwa ni hazina zaidi?

Mafundisho na Maagano 112:10

Bwana ataniongoza kwa mkono, na kujibu sala zangu.

  • Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 112:10 pamoja, wewe na watoto wako mngeweza kuimba pamoja “Nyenyekea” (Nyimbo za Dini, na. 63). Mngeweza pia kucheza mchezo ambao unahusisha kuongozana “kwa mkono” (kama ule wa njia yenye vizuizi). Je, Ni kwa jinsi gani Bwana anatuongoza “kwa mkono,” ingawa Yeye kimwili hayupo pamoja nasi? Je, ni kwa nini tunahitaji Bwana atuongoze sisi? Ni lini tumehisi mkono wa Bwana ukituongoza sisi?

  • Wewe au watoto wako mngeweza kuandika maneno ya Mafundisho na Maagano 112:10 na kupigia mstari baraka atupazo Bwana tunapomgeukia Yeye kwa unyenyekevu. Wahimize watoto wako kushiriki nyakati ambapo kwa unyenyekevu walimwomba Bwana msaada na kupokea majibu ya sala zao au wakaongozwa kufanya kitu chema (ona Moroni 7:13, 16).

Yesu anamponya mtoto

Maelezo kutoka Inuka na Utembee, na Simon Dewey

Mafundisho na Maagano 112:11

Yesu anataka nimpende kila mmoja.

  • Wewe na watoto wako mnaweza kupeana zamu ya kusoma kutoka “Sehemu ya 41: Matatizo Kirtland” (katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 158–60). Je, ni nani katika hadithi alifanya matatizo katika Kirtland kuwa mabaya zaidi? Je, ni nani alikuwa akijaribu kuyaboresha zaidi? Halafu mngeweza kusoma Mafundisho na Maagano 112:11 na zungumzeni kuhusu kwa nini Mwokozi anatutaka tumpende kila mtu. Ni lini Yeye alionyesha upendo kwa watu ambao hawakuwa wakarimu Kwake? (Kwa mfano, ona Luka 23:34). Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu kuwapenda wengine, kama vile “I’ll Walk with You” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41).

2:20

Chapter 41: Trouble in Kirtland: 1837–1838

Mafundisho na Maagano 112:11–14, 24–26.

Wale ambao wameongoka kwa dhati huja kumjua Yesu Kristo.

  • Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 112:24–26, wewe na watoto wako mngeweza kuzungumza kuhusu tofauti kati ya kujua jina la mtu na kuwajua watu hao. Ni mafundisho gani kutoka mistari 11–14 yanatusaidia tuelewe inamaanisha nini kumjua Bwana?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki .

Thomas B. Marsh anaandika ufunuo aliopewa kupitia Joseph Smith.

Kuwa Mnyenyekevu, na Julie Rogers.

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto