Njoo, Unifuate
Oktoba 13–19: “Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake”: Mafundisho na Maagano 115–120


Oktoba 13–19: ‘Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake’: Mafundisho na Maagano115–120,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 115–120,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

picha ya kuchoro ya Far West, Missouri

Far West, Missouri, na Al Rounds

Oktoba 13–19: “Dhabihu Yake Itakuwa Takatifu Zaidi Kwangu Mimi Kuliko Mafanikio Yake”

Mafundisho na Maagano 115–120

Kulikuwa na sababu ya Watakatifu kuwa na matumaini mema kuhusu sehemu yao mpya kabisa ya kukusanyika, Far West, Missouri. Jiji lilikuwa linakua haraka, ardhi ilionekana kuwa yenye neema, na jirani kulikuwa na Adam‑ondi‑Ahman, sehemu yenye umuhimu mkubwa mno kiroho katika siku za nyuma na katika siku zijazo (ona Mafundisho na Maagano 107:53–56116). Bado, lazima ilikuwa vigumu kwa Watakatifu kutofikiria kuhusu kile walichopoteza. Licha ya kufukuzwa kutoka Independence, mahali pa kitovu cha Sayuni, Watakatifu ilibidi pia waikimbie Kirtland, wakiacha hekalu lao walilolipenda baada ya miaka miwili tu. Na wakati huu haikuwa tu maadui nje ya Kanisa waliokuwa wanasababisha matatizo—waumini wengi mashuhuri walikuwa wamegeuka dhidi ya Joseph Smith, ikijumuisha washiriki wanne wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Badala ya kufokasi juu ya kile walichokipoteza, waaminifu waliendelea tu na ujenzi wa Sayuni, wakati huu huko Far West. Walifanya mipango kwa ajili ya hekalu jipya. Mitume wapya wanne waliitwa. Walielewa kwamba kufanya kazi ya Mungu haina maana kwamba hutaanguka; inamaanisha “unainuka tena.” Na ingawa itabidi ufanye dhabihu, dhabihu hizo ni takatifu kwa Mungu, hata “takatifu zaidi … kuliko mafanikio [yako]” (Mafundisho na Maagano 117:13).

Ona Watakatifu,, 1:296–99.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 115:3–6

Jina la Kanisa ni muhimu kwa Bwana.

Rais Russell M. Nelson alisema kwamba jina la Kanisa ni “jambo lenye umuhimu mkubwa” (“Jina Sahihi la Kanisa,” Liahona, Nov. 2018, 87). Fikiria kuhusu kwa nini hii ni kweli unaposoma Mafundisho na Maagano 115:4–6. Jina la Kanisa linahusika vipi na kazi na misheni yake?

Ona pia 3 Nefi 27:1–11.

Mafundisho na Maagano 115:5–6

Sayuni na vigingi vyake vinatoa “kimbilio kutokana na tufani.”

Unapojifunza taswira yenye nguvu katika Mafundisho na Maagano 115:5–6, zingatia kazi ambayo Bwana anakutaka wewe, kama muumini wa Kanisa Lake, uitimize. Kwa mfano, unaweza kufanya nini ili, “kuinuka na kuangaza” au “uwe bendera kwa mataifa”? (mstari wa 5). Ni dhoruba gani za kiroho unaziona zimekuzunguka? Ni kwa jinsi gani unapata “kimbilio” kupitia kukusanyika? (mstari wa 6).

Ona pia “Brightly Beams Our Father’s Mercy,” Nyimbo za Dini, na. 335.

mnara wa taa

Kanisa la Mwokozi linaweza kuwa mnara wa taa na kimbilio katika dhoruba.

Mafundisho na Maagano 117

Dhabihu zangu ni takatifu kwa Bwana.

Fikiria kuwa wewe ni Newel K. Whitney au mke wake, Elizabeth, ambao walikuwa wakipitia mafanikio katika maisha huko Kirtland na halafu wanaamuriwa kuondoka. Unapata nini katika Mafundisho na Maagano 117:1–11 ambacho kingeweza kukusaidia ufanye dhabihu hii? Je, ni dhabihu zipi unazifanya kwa ajili ya Mungu? Mistari hii inakufundisha nini kuhusu Mungu ni nani na Yeye anafanya nini?

Dhabihu iliyoombwa kwa Oliver Granger ilikuwa tofauti na ile ya Whitney: Bwana alimpangia abaki Kirtland na kulipa madeni yote ya Kanisa. Wakati akiliwakilisha Kanisa kwa uadilifu, hatimaye hakuwa mwenye mafanikio sana. Fikiria jinsi gani maneno ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 117:12–15 yanaweza kutumika katika vitu ambavyo Bwana amekutaka wewe ufanye.

Ona pia “Far West na Adam-ondi-Ahman,” katika Ufunuo katika Muktadha, 239–40.

Mafundisho na Maagano 119–20

ikoni ya seminari
Zaka yangu inasaidia kuujenga ufalme wa Mungu.

Maelekezo katika sehemu ya 119 na 120 yanafafanua zaka ni nini: tunachangia “sehemu moja ya kumi” ya faida (au mapato) kila mwaka (ona Mafundisho na Maagano 119:4). Lakini mafunuo haya yanafanya zaidi ya kutoa maana. Bwana aliwaambia Watakatifu kwamba zaka “itaitakasa nchi ya Sayuni.” Na bila sheria hii, Yeye alisema, “haitakuwa … Sayuni kwenu ninyi” (mstari wa 6). Je, umewahi kuifikiria zaka katika njia hii? Jinsi gani kulipa zaka kunakusaidia wewe kutakaswa zaidi, na kuwa aliye tayari zaidi kwa ajili ya Sayuni?

Unajifunza nini kutokana na mafunuo haya kuhusu jinsi watumishi wa Bwana wanavyotumia fedha za zaka? Ni nini cha maana kwako kuhusu kirai “na kwa sauti yangu mwenyewe kwao” katika Mafundisho na Maagano 120?

Mzee David A. Bednar ametoa maelezo yenye msaada juu ya jinsi gani zaka inatumika na baraka zinazokuja kutokana na kutii sheria hii katika “Madirisha ya Mbinguni” (Liahona, Nov. 2013, 19–20). Maswali yafuatayo yanaweza kusaidia unapojifunza ujumbe wake:

16:55

The Windows of Heaven

Spiritual and temporal blessings come into our lives as we live the law of tithing.

  • Ni nani anaamua jinsi zaka inavyotumika baada ya kulipwa kwa Kanisa?

  • Zaka hutumiwa kwa ajili gani?

  • Ni baraka gani zinazokuja kama matokeo ya kulipa zaka? Kwa mfano, ni kwa njia gani kulipa zaka kunaimarisha uhusiano wako na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

  • Unaweza kujifunza nini kutokana na mwaliko wa Mzee Bednar?

  • Unawezaje kuwasaidia wengine kuzidisha imani yao katika sheria ya Bwana ya zaka?

Ona pia Malaki 3:8–12; “Zaka ya Watu Wangu,” katika Ufunuo katika Muktadha, 250–55.

Wasaidie wengine watumie kile wanachojifunza. Hata wakati mtu anapotaka kulipa zaka, wakati mwingine hawajui namna ya kufanya hilo. Kama unaifundisha familia yako au darasa, zingatia kuchukua muda kuelezea jinsi ya kulipa zaka, iwe mtandaoni au kwa slipu ya Zaka na Matoleo Mengine. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 27.)

Kwa mawazo zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya 02 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 115:4–5

Mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wajifunze jina la Kanisa na waelewe kwa nini ni la muhimu, zingatia kuwauliza kama yeyote kati yao anaweza kusema jina kamili la Kanisa. Kisha ungeweza kuwaonyesha jina hilo kutoka Mafundisho na Maagano 115:4 na kisha walirudie pamoja na wewe. Unapofanya hivyo, zingatia kuonyesha maneno muhimu na kwa nini ni muhimu. Ungeweza pia kurejelea “Sehemu ya 43: Yesu Kristo anatoa jina la Kanisa Lake” (katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 164, au video inayohusiana nayo katika Maktaba ya Injili) au imbeni “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77).

0:37

Chapter 43: Jesus Christ Names His Church: April 1838

Mafundisho na Maagano 115:4–6

Mfano wangu unaweza kuwasaidia wengine waje kwa Kristo na wapate usalama.

  • Watoto wako yawezekana wanawajua watu ambao wanapambana na wanahitaji “kimbilio” kutokana na “dhoruba za maisha” (mstari wa 6). Wanawezaje kuwasaidia watu hawa? Zingatia kuwaalika watoto wako kusimama wakati unaposoma neno inukeni katika Mafundisho na Maagano 115:5. Wangeweza kunyosha vidole vyao kama miale ya jua unaposoma muangaze. Wakumbushe watoto wako kwamba nuru yetu inakuja kutoka kwa Yesu Kristo, na wasaidie wafikirie juu ya jinsi wanavyoweza “kuangaza” kama Yeye anavyoangaza.

  • Watoto wako wangeweza kuchora picha inayofafanua Mafundisho na Maagano 115:6. Kwa mfano, wanaweza kuchora picha ya dhoruba, pamoja na watu wakikimbilia katika jengo la Kanisa. Dhoruba inaweza kuwakilisha nini? Ni kwa jinsi gani Kanisa la Mwokozi linatoa msaada? Wasaidie watoto wafikirie juu ya rafiki, mwanafamilia, au jirani aliye katika shida. Je, tunawezaje kuwasaidia watafute msaada katika Kanisa la Yesu Kristo?

Mafundisho na Maagano 117

Dhabihu zangu ni takatifu kwa Bwana.

  • Waalike watoto wako wajifanye wao ni Newel K. Whitney. Wangejisikiaje kama Bwana angewataka waache kazi zao zenye mafanikio na kuhamia sehemu nyingine mpya? (Inaweza kusaidia kurejelea “Sehemu ya 41: Matatizo huko Kirtland,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 158–60, au video inayohusiana katika Maktaba ya Injili.) Mnaposoma pamoja Mafundisho na Maagano 117:1–11, waombe watoto wakusimamishe wakati wanaposikia kitu ambacho kingewasaidia wao wawe na imani ya wamtii Bwana. Je, ni dhabihu gani tunafanya ili kumtii Bwana? Ni kwa jinsi gani Yeye anatubariki sisi?

2:20

Chapter 41: Trouble in Kirtland: 1837–1838

Mafundisho na Maagano 119–20

Baba wa Mbinguni hutumia zaka ili kuwabariki watoto Wake.

  • Wengi wa watoto unaowafundisha yawezekana ni wadogo sana kuweza kujipatia pesa na kulipa zaka, lakini ni vyema kwao kuelewa ni kwa namna gani zaka huchangia kwenye kazi ya Bwana kote ulimwenguni. Zingatia kutumia picha na ukurasa wa shughuli mwishoni mwa muhtasari huu ili kuwasaidia waelewe zaka ni kitu gani. (Ona pia “Sehemu ya 44: Zaka,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 165–66, au video inayohusiana nayo katika Maktaba ya Injili.) Je, Baba wa Mbinguni anatumiaje zaka kuwabariki watoto Wake? Shiriki hisia zako kuhusu sheria ya zaka na jinsi ilivyokubariki wewe.

1:33

Chapter 44: Tithing: July 1838

mtoto akilipa zaka

Wakati tunapolipa zaka, tunaonyesha imani yetu katika Yesu Kristo.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.