Njoo, Unifuate
Oktoba 20–26: “Ee Mungu, Uko Wapi?”: Mafundisho na Maagano 121–123


“Oktoba 20–26: ‘Ee Mungu, Uko Wapi?’: Mafundisho na Maagano 121–123,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 121–123,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Joseph Smith katika Gereza la Liberty

Gereza la Liberty, na Welden Andersen

Oktoba 20–26: “Ee Mungu, Uko Wapi?”

Mafundisho na Maagano 121–123

Usawa wa chini ndani ya gereza la Liberty, Missouri, ulijulikana kama “shimoni.” Kuta zilikuwa nene, sakafu ya mawe ilikuwa ya baridi na chafu, chakula haba na kilikuwa kimeoza, na madirisha mawili membamba ya chuma karibu na dari yaliruhusu mwanga mdogo sana. Hapa ndipo Joseph Smith na wengine wachache walitumia miezi minne ya baridi katika majira ya baridi ya mwaka 1838–39. Muda wote huu, Joseph alikuwa mara kwa mara akipokea habari kuhusu mateso ya Watakatifu. Amani na matumaini ya Magharibi ya Mbali yalikuwa yamedumu kwa miezi michache tu, na sasa Watakatifu walikuwa hawana makazi kwa mara nyingine tena, wakiwa wamekimbizwa kwenda nyikani kutafuta mahali pengine pa kuanza upya—wakati huu Nabii wao akiwa gerezani.

Na bado, hata katika gereza hilo baya, “ufahamu kutoka mbinguni” ulikuja “ukimwagika chini” (Mafundisho na Maagano 121:33). Swali la Joseph “Ee Mungu, uko wapi?” lilijibiwa kwa uwazi na kwa nguvu: “Usiogope … , kwani Mungu atakuwa pamoja nawe milele na milele” (Mafundisho na Maagano 121:1; 122:9).

Ona Watakatifu, 1:323–96; “Ndani ya Kuta za Gereza la Liberty,” katika Ufunuo katika Muktadha, 256–63.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 121:1–10, 23–33; 122

Nikiwa na Mungu, mateso yanaweza “kuwa kwa ajili ya faida [yangu].”

Wakati sisi au wale tunaowapenda wanateseka, ni kawaida kujiuliza kama Mungu anajua yanayotupata. Unaposoma Mafundisho na Maagano 121:1–6, fikiria kuhusu wakati ambapo ulikuwa na maswali au hisia sawa na za Joseph Smith. Unapata nini katika jibu la Bwana ambacho kingeweza kukusaidia wakati unapokuwa na maswali hayo au hisia hizo? Kwa mfano, katika mistari 7–10, 26–33, tambua baraka ambazo Yeye anaahidi. Unafikiri inamaanisha nini “kuvumilia … vyema? Ni jinsi gani Mwokozi anakusaidia wewe ufanye hili?

Unaposoma sehemu ya 122, fikiria jinsi Bwana anavyokutaka uone dhiki zako. Ungeweza kutafakari uzoefu ambao umekuja kutokana na majaribu yako na jinsi unavyoweza “kuwa kwa faida [yako]” (mstari wa 7).

Ona pia Quentin L. Cook, “Amani Binafsi katika Nyakati za Changamoto,” Liahona, Nov. 2021, 89–92; “Where Can I Turn for Peace?,” Nyimbo za Dini, na. 129.

Mafundisho na Maagano 121:34–46

ikoni ya seminari
Nguvu ya kweli na ushawishi hutegemea kanuni za haki.

Nguvu za kiulimwengu ziliwalazimisha Watakatifu kuondoka Missouri na Joseph Smith kuingia gerezani. Lakini wakati Joseph akiwa huko, Bwana alimfundisha kuhusu aina tofauti ya nguvu: nguvu Zake, “nguvu za mbinguni.” Kusoma kuhusu nguvu hizo katika Mafundisho na Maagano 121:34–46 kungekusaidia ujifunze jinsi ya kupokea nguvu hizo na jinsi ya kuzitumia kuwabariki wengine. Labda ungeweza kuandika kile unachojifunza katika jedwali lililo na safu wima zilizopewa majina Nguvu za Mbinguni na Nguvu za Kiulimwengu. Je, ni kwa jinsi gani aina hizi mbili za nguvu ni tofauti? Maelezo haya ya nguvu za Bwana yanakufundisha nini kumhusu Yeye?

Unaweza pia kutafakari neno ushawishi katika mstari wa 41. Ni zipi baadhi ya hali ambazo kwazo wewe unataka kuwa ushawishi kwa mema—labda katika uhusiano wa kifamilia, shuleni, kazini, au katika kazi za Kanisa? Unajifunza nini kutoka mistari 41–46 kuhusu jinsi Mungu anavyowashawishi watoto Wake? Unaweza kufanyia muhtasari kile ulichojifunza kwa kukamilisha sentensi kama hii: “Ili kushawishi kwa mema, mimi nita .”

Ona pia Jeffrey R. Holland, “Siyo kama Ulimwengu Utoavyo,” Liahona, Mei 2021, 35–38; David A. Bednar, “Nguvu za Mbinguni,” Liahona, Mei 2012, 48–51; “The Powers of Heaven” (video), Maktaba ya Injili.

9:13

"The Powers of Heaven"

(D&C 121:34-46) The components and processes involved in providing electricity to a home are compared to the principles the Lord outlined in section 121 for those who would exercise His priesthood in power.

Chagua kifungu cha maneno na ujifunze kwa kina. Ili kujifunza zaidi kuhusu baraka za kupendeza zilizoelezwa katika mistari 45–46, unaweza kuchagua kifungu cha maneno kinachokupendeza na ujifunze kwa kina. Kwa mfano, neno uyapambe linamaanisha nini, na ni jinsi gani wema unaweza kuyapamba mawazo yako? Au pengine unaweza kutafuta picha ya umande na jifunze kuhusu jinsi umande unavyotengenezwa juu ya mimea. Ni kwa jinsi gani hii ni sawa na vile Bwana anavyofundisha mafundisho Yake? Shiriki kile unachokigundua pamoja na familia yako au marafiki, ikijumuisha marafiki zako kanisani.

Mafundisho na Maagano 122:8

Yesu Kristo amejishusha chini ya vitu vyote ili kwamba aweze kuniinua.

Unadhani inamaanisha nini kusema kwamba Yesu Kristo “amejishusha chini … ya [Vitu] vyote”? Hapa ni baadhi ya mistari ya ziada ambayo inaweza kukusaidia uelewe kifungu hiki cha maneno: Isaya 53:3–4; Waebrania 2:17–18; 1 Nefi 11:16–33; Alma 7:11–13. Kulingana na kile unachojifunza, fikiria kuelezea upya Mafundisho na Maagano 122:8 katika maneno yako. Ni kwa jinsi gani unaweza kuonyesha shukrani zako kwa Yesu Kristo kwa kujishusha chini ya vitu vyote?

Ni kwa jinsi gani utambuzi huu kutoka kwa Rais Dallin H. Oaks unagusa uelewa wako? Tunaweza hata kusema kwamba kwa kuwa alijishusha chini ya vitu vyote, [Yesu Kristo] yupo katika nafasi nzuri zaidi ya kutuinua na kutupatia nguvu tunayohitaji ili kuvumilia mateso yetu” (“Kuimarishwa na Upatanisho wa Yesu Kristo,” Liahona, Nov. 2015, 64).

Yesu Kristo akiteseka katika Gethsemane

Maelezo kutoka Siyo Mapenzi Yangu Bali Yako, na Walter Rane

Mafundisho na Maagano 123

“Kwa furaha tufanye mambo yote yaliyo katika uwezo wdetu.”

Katika Mafundisho na Maagano 123:7–8, Joseph Smith alitaja imani potofu ambazo zilisababisha kuteseka, ikijumuisha kuteswa kwa Watakatifu. Mnamo Machi 1839, inaweza kuwa ilionekana kwamba hapakuwa na zaidi ambacho Watakatifu wangeweza kufanya kuhusu hilo. Lakini katika barua zake zilizoandikwa kutoka Gereza la Liberty, Joseph aliwaambia kile ambacho wangeweza kufanya: “[kukusanya] ufahamu wa kweli zote” na “kutulia, wakiwa na uhakika mkubwa, wa kuuona wokovu wa Mungu” (Mafundisho na Maagano 123:1, 17). Unapofikiria matatizo katika ulimwengu wa leo, fikiria kuhusu njia za kuyatatua ambazo “zipo katika uwezo [wako]” (mistari 12, 17). Na usidharau yanayoonekana kuwa “mambo madogo” (mstari wa 15). Kwa nini ni muhimu kufanya mambo haya “kwa furaha”? (mstari wa 17).

Mengi ya maelezo ambayo Joseph aliyaomba katika barua hii yaliwasilishwa kwa serikali na kuchapishwa kama mfululizo wa habari yenye sehemu 11 katika gazeti la Nauvoo, Times and Seasons (ona “A History, of the Persecution, of the Church of Jesus Christ, of Latter Day Saints in Missouri, December 1839–October 1840,” [josephsmithpapers.org]).

Kwa mawazo zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

ikoni ya 03 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 121:1–9, 122:7–9

Nikiwa na Mungu, majaribu yangu yanaweza kuwa kwa faida yangu.

  • Ili kuwasaidia watoto wako wafikirie ilikuwaje kwa Joseph Smith na marafiki zake katika Gereza la Liberty, mngeweza kusoma pamoja “Sehemu ya 46: Joseph Smith katika Gereza la Liberty” (katika Hadith za Mafundisho na Maagano, 172–74) au “Voices of the Restoration: Liberty Jail” au angalieni sehemu ya video ya “Joseph Smith: Prophet of the Restoration” (Maktaba ya Injili, kuanzia kwenye 41:30). Halafu, mnaposoma pamoja Mafundisho na Maagano 121:1–9, mnaweza kuzungumza kuhusu jinsi Mwokozi alivyomsaidia Joseph kujisikia amani. Je, tunaipataje amani katika Mwokozi, hata katika nyakati ngumu?

    1:51

    Chapter 46: Joseph Smith in Liberty Jail: November 1838–April 1839

    62:4

    Joseph Smith: The Prophet of the Restoration

    A motion picture about the life and legacy of Joseph Smith, the founding prophet of The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints.

  • Ili kuwasaidia watoto watambue kwamba majaribu yetu yanaweza “kuwa kwa faida [yetu]” (Mafundisho na Maagano 122:7), ungeweza kuzungumza nao kuhusu namna gani misuli yetu inakua wakati tunapobeba kitu kizito. Ungeweza hata kuwaalika kunyanyua kitu kizito. Kisha mngeweza kuzungumza kuhusu jinsi gani kupitia nyakati ngumu kunaweza kusaidia roho zetu kukua—tunapomgeukia Bwana kwa ajili ya msaada. Shiriki baadhi ya mifano kutoka kwenye maisha yako.

Mafundisho na Maagano 121:34–46

Uadilifu huleta “nguvu za mbinguni.”

  • Pengine mfano wa analojia ungewasaidia watoto wako waelewe “nguvu za mbingu.” Kwa mfano, ungeweza kulinganisha nguvu za Mungu na nguvu ya umeme. Kitu gani kinaweza kuzuia kifaa cha umeme kupokea nguvu? Kitu gani kinapunguza nguvu zetu za kiroho? Ni nini kinaongeza? (Tafuta maneno na vifungu vya maneno katikka Mafundisho na Maagano 121:34–46; ona pia Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 3.5, 3.6, Maktaba ya Injili.)

Mafundisho na Maagano 122:7–9

Yesu Kristo anajua ninayopitia.

  • Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano122:7–9 pamoja na watoto wako, ungeweza kushiriki uzoefu wakati ulipohisi Mwokozi yupo nawe wakati wa jaribu gumu. Mngeweza pia kuimba pamoja “Jesus Once Was a Little Child” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 55), na shuhudia kwamba Yesu Kristo anaweza kutusaidia kwa sababu anajua namna tunavyohisi.

Mafundisho na Maagano 123:15–17

Hata mambo madogo yanaweza kuleta tofauti kubwa katika huduma ya Mungu.

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe Mafundisho na Maagano 123:15–17, ungeweza kushiriki nao picha ya meli kubwa na usukani mdogo, au shiriki nao maelezo ya Mzee David A. Bednar katika “Kanuni za Injili Yangu” (Liahona, Mei 2021, 125–26) Kisha mngeweza kuzungumza kuhusu njia ndogo ndogo ambazo kupitia hizo tunaweza kuihudumia familia yetu na rafiki zetu kwa furaha.

15:0

“The Principles of My Gospel”

Elder Bednar teaches that correct gospel principles help us make wise choices and stay on the covenant path.

Kielelezo cha meli ikiwa baharini

Kama usukani mdogo wa meli kubwa, jitihada zetu ndogo zinaweza kuleta tofauti kubwa.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

Joseph Smith akiandika ufunuo katika Gereza la Liberty.

Joseph Smith katika Gereza la Liberty, na Greg K. Olsen

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto