“Oktoba 27–Novemba 2: “Nyumba kwa Jina Langu”: Mafundisho na Maagano 124,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 124,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Oktoba 27–November 2: “Nyumba Kwa Jina Langu”
Mafundisho na Maagano 124
Ilikuwa ni miaka sita iliyopita ya ugumu kwa Watakatifu, mambo yalianza kuonekana kuwa mazuri katika majira ya kuchipua ya 1839: Watakatifu wakimbizi walikuwa wamepata huruma miongoni mwa raia wa Quincy, Illinois. Walinzi walikuwa wamewaruhusu Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa kutoroka ufungwa huko Missouri. Na Kanisa ndio kwanza lilikuwa limenunua ardhi huko Illiois ambapo Watakatifu wangekusanyika tena. Ndiyo, ardhi ilikuwa yenye majimaji, iliyojawa na mbu, lakini ikilinganishwa na changamoto ambazo Watakatifu walikuwa tayari wamekumbana nazo, hili pengine lilionekana lenye kuhimilika. Kwa hiyo walikausha majimaji na wakatengeneza mkataba wa mji mpya, ambao waliuita Nauvoo. Inamaanisha “nzuri” kwa Kiebrania, ingawa ulikuwa zaidi ni msemo wa imani kuliko maelezo sahihi, angalau hapo mwanzo. Wakati huo huo, Bwana alikuwa akimshawishi Nabii wake kwa hisia za uharaka. Alikuwa na kweli nyingi na ibada za kurejesha, na Alihitaji hekalu takatifu ambapo angeweza “kuwavika [Watakatifu Wake] kwa heshima, kutokufa, na uzima wa milele” (Mafundisho na Maagano 124:55). Katika njia nyingi, hisia hizi hizi za imani na uharaka ni za muhimu katika kazi ya Bwana leo.
Ona Saints, 1:399–427; “Organizing the Church in Nauvoo,” katika Ufunuo katika Muktadha, 264–71.
Jifunze zaidi kuhusu maeneo ya kihistoria ya Kanisa huko Illinois.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Mafundisho na Maagano 124:2–11
Ninaweza kuwaalika wengine kuja kwa Kristo?
Bwana alimwambia Nabii Joseph Smith “kufanya tangazo la dhati la injili Yake” kwa “wafalme wote wa ulimwengu” (ona Mafundisho na Maagano 124:2–11). Kama wewe ungepokea kazi hii, tangazo lako lingesema nini kuhusu Yesu Kristo na injili Yake iliyorejeshwa? Pia tafakari jinsi gani unaweza kushiriki ushahidi wako kikawaida na kiasili na watu unaochangamana nao kila siku.
Ona pia “Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu la Maadhimisho ya Miaka Mia Mbili,” Maktaba ya Injili.
Mafundisho na Maagano 124:12–21
Ninaweza kuwa mfuasi ambaye Bwana anamwamini.
Zingatia kushiriki na wengine, kama Mwokozi alivyofanya katika Mafundisho na Maagano 124:12–21, sifa kama za Kristo unazoziona ndani yao. Je, ni kwa jinsi gani Yeye ameonyesha upendo Wake na tumaini Lake kwako?
Ona pia Richard J. Maynes, “Kupata Tumaini la Bwana na la Familia Yako,” Liahona, Nov. 2017, 75–77.
Mafundisho na Maagano 124:22–24, 60–61
Bwana ananitaka kuwakaribisha na kuwakubali wengine.
Unapotafakari maelekezo ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 124:22–24, 60–61, fikiria kuhusu jinsi wewe unavyoweza kuifanya nyumba yako na kata yako kuwa mahali kama vile Bwana alivyoiwazia Nauvoo.
Ona pia “A Friend to All” (video), ChurchofJesusChrist.org.
Mafundisho na Maagano 124:25–45, 55
Tunajenga mahekalu kwa Bwana ili tupokee ibada takatifu.
Kwa nini unahisi Bwana “siku zote amekuwa akiwaamuru” watu Wake “kujenga [mahekalu] kwa jina [Lake]”? Fikiria kutengeneza orodha ya sababu unazozipata katika Mafundisho na Maagano 124:25-45, 55. Unaweza kuzipata zingine katika wimbo wa dini kama “Bwana Nyumba Yako” (Nyimbo za Dini, na. 141) au video ya “What Is a Temple?” (Maktaba ya Injili). Je, ni kwa jinsi gani kazi ya ujenzi wa mahekalu ni ishara ya upendo wa Bwana kwako wewe?
Tangu Hekalu la Nauvoo lilipojengwa miaka ya 1840 hivi, zaidi ya mahekalu 300 yamejengwa au kutangazwa. Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Tunajua ya kwamba muda wetu katika hekalu ni muhimu kwa wokovu na kuinuliwa kwetu na kwa familia zetu. … Mashambulizi ya adui yanaongezeka kwa kasi, kwa ukubwa na kwa namna mbalimbali. Hitaji letu la kuwa hekaluni mara kwa mara halijawahi kuwa kubwa kiasi hiki” (“Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano,” Liahona, Nov. 2018, 114). Ni kwa jinsi gani hekalu limekusaidia kuhimili “mashambulizi ya adui”? Je, unahisi kutiwa msukumo kufanya nini ili kufuata ushauri wa Rais Nelson?
Ona pia “Why Latter-day Saints Build Temples,” temples.ChurchofJesusChrist.org.
Mafundisho na Maagano 124:45–55
Bwana atawabariki wale ambao wanajitahidi kutii amri zake.
Watakatifu walikuwa wamepewa amri ya kujenga hekalu katika Wilaya ya Jackson, Missouri, lakini “walizuiliwa na maadui zao” (Mafundisho na Maagano 124:51). Mistari 49–55 ina ujumbe wenye hakikisho kwa watu ambao wanataka kutii amri za Mungu lakini wanazuiliwa kufanya hivyo kwa sababu ya familia au sababu nyinginezo. Je, ni ushauri gani wewe unaupata katika mistari hii ambao ungeweza kumsaidia mtu katika hali kama hiyo?
Mafundisho na Maagano 124:91–92
Bwana anaweza kuniongoza kupitia baraka yangu ya kipatriaki.
Muda mfupi baada ya baba wa Nabii, Joseph Smith Mkubwa kufariki dunia, Bwana alimwita Hyrum Smith katika wito ambao baba yake alikuwa ameushikilia—Patriaki wa Kanisa. Unaweza kusoma kuhusu hili katika Mafundisho na Maagano 124:91–92.
Jinsi gani wewe ungeweza kuelezea baraka ya kipatriaki kwa mtu ambaye hajawahi kusikia kuhusu hilo? Je, ungeweza kusema nini ili kumhimiza mtu kupokea hiyo baraka? Tafuta majibu ya maswali haya katika ujumbe wa Mzee Randall K. Bennett “Baraka Yako ya Kipatriaki—Mwongozo wa Kiungu kutoka kwa Baba wa Mbinguni” (Liahona, Mei 2023, 42–43) au Topics and Questions, “Patriarchal Blessings” (Maktaba ya Injili).
Kulingana na kitu ulichojifunza na kupitia, fikiria jinsi utakavyo kamilisha sentensi hii: Baraka ya kipatriaki ni kama .” Je, ni kwa nini Baba wa Mbinguni anataka watoto Wake wapokee baraka ya kipatriaki?
Kama bado hujapokea baraka ya kipatriaki, unaweza kufanya nini ili kujiandaa kwa ajili ya hilo? Kama umeshapokea baraka ya kipatriaki, unawezaje kumwonyesha Mungu kwamba unaithamini zawadi hii?
Ona pia Kazuhiko Yamashita, “Lini Upokee Baraka Yako ya Kipatriaki,” Liahona, Mei 2023, 88–90; Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 18.17, Maktaba ya Injili.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mafundisho na Maagano 124:15, 20
Yesu Kristo anapenda uadilifu.
-
Ili kuwasaidia watoto wako wakumbuke kitu wanachojifunza kutoka kwenye Mafundisho 124:15, 20, ungeweza kuwasaidia wachore na kukata mioyo ya karatasi. Juu ya mioyo hiyo, ungeweza kuwasaidia waandike vifungu vya maneno kutoka kwenye mistari hii. Wimbo kama “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159) ungeweza kusaidia kuimarisha maneno ya Bwana.
-
Baada ya kusoma pamoja Mafundisho na Maagano124:15, 20, labda ungeweza kuwasaidia watoto wako watafute kile inachomaanisha kuishi kwa uadilifu kwenye ukurasa wa 31 wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi. Bwana alisema nini mahususi kuhusu George Miller katika mstari wa 20 “kwa sababu ya uadilifu wa moyo [wa George]? Ungeweza pia kushiriki mifano ya watoto wakionyesha uadilifu kutokana na uzoefu wako mwenyewe au kutoka katika jarida la Rafiki. Waalike watoto wako waweke lengo la kuonyesha uadilifu wiki hii na wakuambie wanavyojisikia wanapofanya hivyo.
Mafundisho na Maagano 124:28–29, 39
Yesu anawaamuru watu Wake kujenga mahekalu.
-
Watoto wako yawezekana wakafurahia kutazama picha za mahekalu, ikijumuisha hekalu la kale na hekalu lililo karibu na mahali wanapoishi (ona ChurchofJesusChrist.org/temples/list). Ungeweza kutumia picha hizi na Mafundisho na Maagano 124:39 ili kuelezea kwamba Yesu Kristo siku zote amekuwa akiwaamuru watu Wake kujenga mahekalu—katika nyakati za kale na katika siku yetu (ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii).
-
Kama unaisha karibu kabisa na hekalu, fikiria kuwapeleka watoto wako hapo na kwa utulivu watembee kwenye viwanja vya hekalu. Waalike kutafuta maneno: “Utakatifu kwa Bwana— Nyumba ya Bwana” nje ya hekalu. Zungumza na watoto wako kuhusu maneno haya yanamaanisha nini.
-
Zingatia kutumia mawazo katika “Kubatizwa na Kuthibitishwa kwa niaba ya Mababu” katika kiambatisho A ili kuwasaidia watoto wako kutazamia siku ambapo wataweza kuingia hekaluni (ona pia “Hekalu na Mpango wa Furaha” katika kiambatisho B).
Mafundisho na Maagano 124:91–92
Bwana atanibariki kupitia baraka ya kipatriaki.
-
Mnaposoma pamoja Mafundisho na Maagano 124:91–92, wasaidie watoto wako watafute kile ambacho Bwana alimwita Hyrum Smith kufanya. Zungumzia kuhusu baraka ya kipatriaki ni ini: ni baraka maalumu ambamo ndani yake Bwana anatufundisha kuhusu sisi wenyewe na kile Yeye anachotaka sisi tufanye na tuwe. Zingatia kutumia sehemu ya “Kupokea Baraka ya Kipatriaki” katika kiambatisho A ili kuwasaidia watoto wako wajiandae kupokea baraka ya kipatriaki.