Njoo, Unifuate
Sauti za Urejesho: Muungano wa Usaidizi


“Sauti za Urejesho: Muungano wa Usaidizi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Muungano wa Usaidizi,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho

Muungano wa Usaidizi

Mnamo mwaka 1842, baada ya Muungano wa Usaidizi kuanzishwa huko Nauvoo, Illinois, Nabii Joseph Smith alisema, “Kanisa halikuwa limeundwa kikamilifu hadi pale wanawake walipoundiwa kikundi.” Vilevile, mafunzo juu ya Urejesho wa Kanisa la Bwana na ukuhani Wake hayakamiliki mpaka yatakapojumuisha mafunzo juu ya Muungano wa Usaidizi, ambao wenyewe ni “urejesho wa mpangilio wa kale” wa wafuasi wa kike wa Yesu Kristo.

Eliza R. Snow alifanya jukumu muhimu katika urejesho huo. Alikuwepo wakati Muungano wa Usaidizi ulipoanzishwa kwa mara ya kwanza na, kama katibu wa muungano, aliandika mihutasari wakati wa mikutano. Alishuhudia kwa macho yake kwamba Muungano wa Usaidizi ulianzishwa “kwa mpangilio wa ukuhani.” Hapa chini ni maneno yake, yaliyoandikwa wakati alipokuwa akihudumu kama Rais Mkuu wa pili wa Muungano wa Usaidizi, ili kuwasaidia dada zake kuelewa kazi takatifu iliyokabidhiwa kwa mabinti wa agano wa Mungu.

Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi gani Muungano wa Usaidizi ulivyoanzishwa, ona Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2017), 1–25; The First Fifty Years of Relief Society (2016), 3–175.

Emma Smith akiongoza mkutano wa Muungano wa Usaidizi

Picha ya jumuiya ya Muungano wa Usaidizi na Paul Mann

Eliza R. Snow

“Ingawa jina [Muungano wa Usaidizi] linaweza kuwa la kisasa, taasisi hiyo ni ya asili ya kale. Tuliambiwa na [Joseph Smith], kwamba jumuiya kama hii ilikuwepo katika kanisa hapo kale, madokezo ambayo yamefanywa katika baadhi ya nyaraka zilizoandikwa katika Agano Jipya, zikitumia jina, ‘mama mteule’ [ona 2 Yohana 1:1; Mafundisho na Maagano 25:3].

“Hii ni jumuiya ambayo haiwezi kuwepo bila ukuhani, kutokana na ukweli kwamba inapata mamlaka yake yote na nguvu kutokana na chanzo hicho. Wakati Ukuhani ulipochukuliwa kutoka duniani, jumuiya hii sawa na kila kiambatisho kingine cha utaratibu wa kweli wa Kanisa la Yesu Kristo duniani, ikawa imekufa. …

“Nikiwepo wakati wa uanzishwaji wa jumuiya ya ‘Muungano wa Usaidizi kwa Wanawake wa Nauvoo,’ … na pia nikiwa na uzoefu mkubwa katika jumuiya hiyo, pengine ninaweza kuwasilisha madokezo machache ambayo yatawasaidia mabinti wa Sayuni katika kupiga hatua mbele katika nafasi hii muhimu mno, ambayo imejaa majukumu mapya na yaliyoongezwa. Ikiwa yeyote kati ya mabinti na akina mama katika Israeli wanahisi kupungukiwa katika nafasi zao za sasa, sasa watapata uwanda wa kutosha kwa kila nguvu na uwezo wa kutenda mema kwa yale ambayo wamewezeshwa kwa nguvu kutoka juu. …

Stoo ya matofali mekundu huko Nauvoo, Illinois

Muungano wa Usaidizi ulianzishwa katika chumba cha ghorofani cha Stoo ya Matofali Mekundu.

“Swali linaweza kuja akilini, kwa yeyote, Ni nini kusudi la Muungano wa Usaidizi wa Wanawake? Ningejibu—kufanya mema—kuleta kwenye hali ya kuhitaji kila uwezo tulio nao kwa ajili ya kufanya mema, siyo tu katika kuwasaidia masikini bali katika kuokoa nafsi. Juhudi za pamoja zitakamilisha kupita kipimo zaidi kuliko inavyoweza kukamilishwa na nguvu binafsi za kufaa sana. …

“Katika kuwahudumia masikini, Muungano wa Usaidizi wa Wanawake una kazi zingine za kufanya zaidi ya kutuliza tu matakwa ya kimwili. Umasikini wa akili na ugonjwa wa moyo, pia vinahitaji umakini; na mara nyingi onesho la ukarimu —maneno machache ya ushauri, au hata ukunjufu na kushikana mikono kwa upendo kutaleta mema mengi na kupewa shukrani zaidi kuliko mfuko wa dhahabu. …

“Wakati Watakatifu wanapokusanyika kutoka mbali, ni wageni kwa kila mtu, na wanakuwa kwenye hali ya kupotezwa na wale wanaowangojea kuwadanganya, Muungano wa [Usaidizi] unapaswa kuharakisha katika kuwaangalia [hao], na kuwatambulisha kwenye jumuiya ambayo itawasafisha na kuwainua, na juu ya yote kuwaimarisha katika imani juu ya Injili, na kwa kufanya hivyo, wanaweza kuwa vyombo katika kuwaokoa wengi.

“Itahitaji juzuu nyingi ambazo zitahitajika kufafanua majukumu, fursa na wajibu ambavyo huja katika uwepo wa macho ya Muungano. … Iendeeni (chini ya maelekezo ya askofu wako) kwa utulivu, kwa uhuru, kwa nguvu, kwa kuungana na kwa sala, na Mungu atavika taji juhudi zenu kwa mafanikio.”

Muhtasari

  1. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 451.

  2. Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2017), 7.

  3. Joseph Smith, in Sarah M. Kimball, “Auto-biography,” Woman’s Exponent, Sept. 1, 1883, 51.

  4. “Female Relief Society,” Deseret News, Apr. 22, 1868, 81.