Njoo, Unifuate
Sauti za Urejesho: Ubatizo kwa ajili ya Mababu Zetu, “Mafundisho yenye Utukufu”


“Sauti za Urejesho: Ubatizo wa Mababu Zetu, ‘Mafundisho yenye Utukufu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Ubatizo kwa Ajili ya Mababu Zetu, ‘Mafundisho yenye Utukufu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho

Ubatizo kwa ajili ya Mababu Zetu, “Mafundisho yenye Utukufu”

mchoro wa kisima cha ubatizo katika Hekalu la Nauvoo

Mchoro huu unaonyesha kisima cha ubatizo cha Hekalu la Nauvoo kikiwa juu ya ng’ombe kumi na mbili.

Phebe na Wilford Woodruff

Portrait engraving of Orson Pratt

Phebe Woodruff alikuwa akiishi karibu na Nauvoo wakati Joseph Smith alipoanza kufundisha kuhusu uwezekano wa kubatizwa kwa ajili ya wale walioishi hapo awali. Aliliandika hilo kwa mume wake, Wilford, ambaye alikuwa akihudumu misheni huko Uingereza:

“Kaka Joseph … amejua kwa njia ya ufunuo kwamba watu katika kanisa hili wanaweza kubatizwa kwa ajili ya jamaa zao wowote waliokufa na hawakuwa na fursa ya kuisikia injili hii, hata kwa ajili ya watoto wao, wazazi, kaka, dada, mababu, wajomba, na mashangazi. … Mara tu wanapobatizwa kwa ajili ya marafiki zao wanafunguliwa kutoka kifungoni na wanaweza kuwadai katika ufufuko na kuwaleta kwenye ufalme wa selestia—mafundisho haya yamepokelewa kwa uchangamfu na kanisa na wanasonga mbele kwa wingi, baadhi wanakwenda kubatizwa karibu mara 16 … katika siku moja.”

Wilford Woodruff baadaye alisema juu ya kanuni hii: “Mara tu niliposikia juu ya hilo roho yangu iliruka kwa furaha. … Nilisonga mbele na nilibatizwa kwa ajili ya jamaa zangu wote waliokufa nilioweza kuwafikiria. … Nilihisi kusema haleluya wakati ufunuo huu ulipokuja ukitufunulia juu ya ubatizo kwa ajili ya wafu. Nilijisikia kwamba tulikuwa na haki ya kushangilia katika baraka za Mbingu.”

Vilate Kimball

Portrait of Vilate Kimball.

Kama Dada Woodruff, Vilate Kimball alisikia kuhusu ubatizo kwa ajili ya wafu wakati mume wake, Heber, alipokuwa mbali akihubiri injili. Alimwandikia:

“Rais Smith amefungua somo jipya na tukufu … ambalo limesababisha uamsho mkubwa katika Kanisa. Ambalo ni, kubatizwa kwa ajili ya wafu. Paulo analizungumzia, katika Wakorintho wa kwanza sura ya 15 mstari wa 29. Joseph amepokea maelezo yake kamili zaidi kwa njia ya Ufunuo. … Ni fursa ya Kanisa hili kubatizwa kwa ajili ya ndugu zao wote ambao walifariki kabla ya injili hii kuja; hata kurudi nyuma mpaka kwa Babu wa babu na Bibi zao … Kwa kufanya hivyo, tunatenda kama mawakala kwa ajili yao; na kuwapa wao fursa ya kujitokeza katika ufufuo wa kwanza. Anasema watakuwa na Injili itakayohubiriwa kwao … lakini hakuna kitu kama hicho cha roho kubatizwa. … Tangu utaratibu huu umekuwa ukihubiriwa hapa, maji yamekuwa yakiendelea kusumbuliwa. Wakati wa mkutano kulikuwa wakati mwingine kuanzia Wazee nane mpaka kumi katika mto kwa wakati mmoja wakibatiza. … Ninataka kubatizwa kwa ajili ya Mama yangu. Niliazimia kungoja mpaka utakaporudi nyumbani, lakini mara ya mwisho Joseph alipozungumza juu ya swala hili, alishauri kila mtu kuwa tayari na kutenda, na kuwakomboa marafiki zao kutoka kifungoni haraka iwezekanavyo. Kwa hiyo nafikiri napaswa kusonga mbele wiki hii, kwa vile kuna idadi ya majirani wanaosonga mbele. Baadhi tayari wamebatizwa mara kadhaa zaidi. … Hivyo unaona kuna nafasi kwa ajili ya wote. Je, haya si mafundisho matukufu?”

Phebe Chase

Picture of Phoebe Carter Woodruff, wife of Wilford Woodruff, circa 1840.

Mara baada ya kisima cha ubatizo kukamilika katika Hekalu la Nauvoo, ubatizo kwa ajili ya wafu ulifanywa mle badala ya mtoni. Phebe Chase, mkaazi wa Nauvoo, alimwandikia mama yake kuhusu hekalu, akielezea kisima cha ubatizo kama mahali ambapo “tunaweza kubatizwa kwa ajili ya wafu wetu na kuwa waokozi juu ya Mlima Sayuni.” Aliendelea kuelezea kwamba katika kisima hiki, “nimebatizwa kwa ajili ya mpendwa baba yangu na marafiki zangu wote waliokufa. … Sasa nataka kujua majina ya baba na mama yako ili kwamba niwaweke huru, kwani natamani kuwafariji Wafu. … Bwana amezungumza tena na kurejesha utaratibu wa kale.”

Sally Randall

Katika kuwaandikia marafiki zake na familia kuhusu ubatizo wa wafu, Sally Randall alikumbuka kufariki kwa mwanae George:

“Oo, muda wa majaribu ulioje ambao ulikuwa kwangu na inaonekana kwamba bado siwezi kupatanishwa nao, lakini … baba yake amebatizwa kwa ajili yake na imekuwa jambo tukufu kwamba tunaamini na kupokea utimilifu wa injili kama inavyohubiriwa sasa na tunaweza kubatizwa kwa ajili ya marafiki zetu wote waliofariki na kuwaokoa kwa kadiri ya tunavyoweza kupata ufahamu kuwahusu.

“Ninataka ungeniandikia majina stahiki ya wote tunaohusiana nao ambao ni wafu kurudi nyuma kwa mababu na mabibi kwa kiwango chochote. Ninakusudia kufanya kile ninachoweza kuwaokoa marafiki zangu na ningekuwa na furaha kuu kama baadhi yenu mngekuja na kunisaidia kwani ni kazi kubwa kwa mmoja kuifanya peke yake. … Nategemea utafikiri haya ni mafundisho mageni lakini utayaona kuwa ni ya kweli.”

Muhtasari

  1. Barua ya Phebe Woodruff kwa Wilford Woodruff, Okt. 6, 1840, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jiji la Salt Lake; matamshi na tahajia vimebadilishwa.

  2. Wilford Woodruff, “Remarks,”, Deseret News, Mei 27, 1857, 91; alama za uandishi zimeboreshwa.

  3. Barua ya Vilate Kimball kwenda kwa Heber C. Kimball, Okt. 11, 1840, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jiji la Salt Lake; tahajia na alama za uandishi vimeboreshwa.

  4. Barua ya Phebe Chase, isiyo na tarehe, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jiji la Salt Lake; tahajia na alama za uandishi vimeboreshwa. Wakati Watakatifu kwa mara ya kwanza walipoanza kufanya ubatizo kwa ajili ya wafu, watu binafsi wakati mwingine walibatizwa kwa niaba ya mababu wa jinsia zote. Baadaye ilifunuliwa kwamba wanaume wanapaswa kubatizwa kwa ajili ya wanaume na wanawake kwa ajili ya wanawake.

  5. Barua ya Sally Randall, Apr. 21,1844, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jiji la Salt Lake; tahajia na alama za uandishi vimebboreshwa.