“Machi 10–16: ‘Nimeona Dhabihu Zenu katika Utiifu’: Mafundisho na Maagano 129–132,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Mafundisho na Maagano 129–132,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Novemba 10–16: “Nimeona Dhabihu Zenu katika Utiifu”
Mafundisho na Maagano 129–132
Kupitia Joseph Smith, Bwana alifunua baadhi ya siri kutoka milele. Ukuu wa Mungu, utukufu wa mbinguni, na ukubwa wa umilele vinaweza kuonekana vinafahamika katika nuru ya injili iliyorejeshwa, hata kwa akili finyu kama zetu. Mafunuo katika Mafundisho na Maagano 129–32 ni mfano mzuri. Je, Mungu yukoje? Yeye “ana mwili … wenye kushikika kama wa mwanadamu.” Mbinguni kukoje? “Uhusiano ule uliopo miongoni mwetu hapa utakuwepo miongoni mwetu kule” (Mafundisho na Maagano 130:22, 2). Hakika, moja ya kweli zenye shangwe zaidi kuhusu mbingu ni kwamba inaweza kujumuisha uhusiano wetu wa kifamilia tunaouthamini sana, kama utatiwa muhuri na mamlaka sahihi. Kweli kama hizi zinaweza kufanya mbinguni kuhisiwe kuwa sio mbali sana—kutukufu na bado kunafikika.
Lakini tena, wakati mwingine Mungu anaweza kututaka tufanye mambo ambayo hayaleti faraja kabisa na hayawezi kufikiwa. Kwa Watakatifu wengi wa mwanzo, ndoa ya wake wengi ilikuwa moja ya amri kama hizo. Ilikuwa ni jaribu kali la imani kwa Joseph Smith, mke wake Emma, na karibia kila mmoja aliyeipokea. Kuweza kupita jaribu hili, walihitaji zaidi ya hisia zenye kufaa kuhusu injili iliyorejeshwa; walihitaji imani kwa Mungu ambayo ilikwenda mbali zaidi ya hilo. Amri haipo tena leo, lakini mfano wa uaminifu wa wale walioiishi bado upo. Na mfano huu unatushawishi sisi tunapotakiwa kufanya “dhabihu zetu wenyewe katika utii” (Mafundisho na Maagano 132:50).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Mungu anataka kuwainua watoto Wake.
Kuna mambo mengi tusiyoyajua kuhusu kuinuliwa au maisha katika daraja la juu kabisa la ufalme wa selestia—aina ya maisha ambayo Mungu anaishi. Mengi ya haya yanaweza kuwa kupita uwezo wetu wa sasa wa kuelewa. Lakini Mungu ameshafunua vidokezi vichache vyenye thamani, na vingi katika hivyo vinapatikana katika Mafundisho na Maagano 130–32. Unaweza kusoma ukiwa na maswali kama haya akilini: Ninajifunza nini kuhusu Mungu? Ninajifunza nini kuhusu maisha baada ya mauti? Je, taarifa hii kuhusu uzima wa milele hubariki vipi maisha yangu kwa sasa?
Ona pia “Mioyo Yetu Ilishangilia Kumsikia Yeye Akiongea,” katika Ufunuo katika Muktadha, 277–80.
Mafundisho na Maagano 130:20–21; 132:5
Mungu anawabariki watu ambao hutii sheria zake.
Ni kwa jinsi gani ungeelezea, kwa maneno yako mwenyewe, kitu ambacho Bwana anafundisha katika Mafundisho na Maagano 130:20–21 na 132:5? Tafakari jinsi gani kanuni hii imeonyeshwa katika maisha yako.
Wakati mwingine, hata tunapokuwa watiifu kwa Mungu, baraka tunazozitumainia haziji mara moja. Ni kwa jinsi gani unaweza kudumisha imani na tumaini lako wakati hili linapotokea? Tafuta utambuzi katika ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Uhusiano Wetu na Mungu” (Liahona, Mei 2022, 78–80).
Ona pia 1 Nefi 17:35; Mafundisho na Maagano 82:10.
Mafundisho na Maagano 132:13–21
Baba wa Mbinguni amefanya iwezekane kwa familia kuwa za milele.
Kupitia Nabii Joseph Smith, Bwana amerejesha ukweli kwamba uhusiano wa ndoa na familia unaweza kuwa wa miliele. Unaposoma Mafundisho na Maagano 132:13–21, tafuta vifungu vya maneno ambavyo vinakusaidia uelewe tofauti kati ya kile “kitakachodumu” milele na kile ambacho hakitadumu. Unafikiri inamaanisha nini kwa uhusiano wa ndoa kuwa “kwa njia ya [Bwana]”? (mstari wa 14).
Katika ujumbe wake “Kwa Sifa za Wale Wanaookoa” Rais Dieter F. Uchtdorf anatofautisha uhusiano wa ndoa ya milele na vitu vya “kutupwa” (Liahona, Mei 2016, 77–78). Je, tofauti hii inakufundisha nini kuhusu jinsi ya kulea—au kujitayarisha kwa ajili ya—uhusiano wa ndoa? Fikiria kuhusu uhusiano wa familia yako—sasa na katika siku zijazo—unaposoma ujumbe wa Mzee Uchtdorf. Je, unapata nini hapo ambacho kinakupa tumaini katika Kristo kwa ajili ya uhusiano wako wa kifamilia?
Rais Henry B. Eyring alishiriki ushauri huu alioupokea alipokuwa na wasiwasi kuhusu hali ya familia yake: “Wewe ishi tu ukiwa mwenye kustahil ufalme wa selestia, na mipangilio ya kifamilia itakuwa ya ajabu kuliko unavyoweza kufikiria” (katika “Nyumbani Mahali Roho wa Bwana Anaishi,” Liahona, Mei 2019, 25). Je, Ushauri huu utakusaidiaje wewe au mtu unayemjua?
Ona pia “Familia Huwa za Milele,” Nyimbo za Dini, na. 176; Topics and Questions, “Marriage,” Maktaba ya Injili.
Mafundisho na Maagano 132:1–2, 29–40.
Ndoa ya wake wengi inakubalika kwa Mungu iwapo tu Yeye mwenyewe ameamuru.
Watu wengi waliosoma Agano la Kale bila shaka walistaajabu kuhusu Ibrahimu, Yakobo, Musa, na wengine wakioa wake wengi. Je, watumishi hawa wa Bwana walifanya uzinzi? Je, Mungu aliidhinisha ndoa zao? Joseph Smith alikuwa na maswali kama hayo. Tafuta majibu Mungu aliyotoa katika Mafundisho na Maagano 132:1–2, 29–40.
Ndoa kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja ni kiwango cha Mungu cha ndoa (ona kichwa cha habari cha sehemu kwenye Tamko rasmi 1; Yakobo 2:27–30). Hata hivyo, kumekuwa na nyakati ambapo Mungu alikuwa amewaamuru watoto Wake kuwa na ndoa ya wake wengi.
Miaka ya mwanzo ya Kanisa lililorejeshwa ilikuwa moja ya vipindi hivyo vya kipekee. Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu ndoa ya wake wengi miongoni mwa Watakatifu wa mwanzoni, ona “Mercy Thompson na Ufunuo juu ya Ndoa” (katika Ufunuo katika Muktadha, 281–93); Watakatifu, 1:290–92, 432–35, 482–92, 502–4; Topics and Questions, “Plural Marriage in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints,” Maktaba ya Injili; “Why Was It Necessary for Joseph Smith and Others to Practice Polygamy?” (video), ChurchofJesusChrist.org.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Mafundisho na Maagano 130:2, 18–19; 132:13,19
Baba wa Mbinguni ananitaka nifokasi juu ya mambo ya milele.
-
Ni nini Mafundisho na Maagano 132:13 inatufundisha kuhusu vitu vya ulimwengu? Pengine wewe na watoto wako mngeweza kupaki sanduku au begi la mgongoni kwa vitu vinavyowakilisha vitu ambavyo, kulingana na Mafundisho na Maagano 130:2, 18–19; 132:19, tunaweza kuvichukua pamoja nasi kwenye maisha yajayo.
Mafundisho na Maagano 130:20–21; 132:5, 21–23
Mungu ananibariki ninapotii sheria Zake.
-
Pengine kulinganisha kuliko rahisi kungeweza kuwafundisha watoto wako kuhusu kutii amri za Mungu. Kwa mfano, ungeweza kuwaomba wakupe maelekezo ya kutembea kuelekea mahali fulani, kama kwenda shule au kwenye jengo la Kanisa. Je, ni kitu gani hutokea tunapokuwa hatufuati maelekezo? Halafu mngeweza kusoma Mafundisho na Maagano 130:21 na linganisheni maelekezo haya na amri ambazo Mungu ametupatia.
-
Mnaweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu utii, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47), na mtafute maneno katika Mafundisho na Maagano 130:20–21 na 132:5 ambayo ni sawa na yaliyo katika wimbo huu. Je, ni kwa namna gani Mungu anatubariki sisi wakati tunapojitahidi kushika amri Zake?
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wana miili isiyokufa ya nyama na mifupa.
-
Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 130:22 pamoja, wewe na watoto wako mngeweza kuangalia picha ya Yesu Kristo na kuonyesha kwenye macho Yake, mdomo Wake na sehemu zingine za mwili Wake. Watoto wako wanaweza kuonyesha kwenye sehemu sawa na hizo za miili yao. Waeleze kwa nini ni muhimu kwako wewe kujua kwamba miili yetu iko kama miili ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Baba wa Mbinguni amefanya iwezekane kwa familia kuwa pamoja milele.
-
Wasaidie watoto watafute mifano ya vitu ambavyo havidumu milele—chakula ambacho huharibika, maua ambayo hunyauka, na vinginevyo. Kisha angalieni kwenye Mafundisho na Maagano 132:19 kwa pamoja na mtafute vifungu muhimu kama “agano lisilo na mwisho” “kuunganishwa,” “milele yote,” na “milele na milele.” (Ona pia “Sehemu ya 55:Ufunuo kuhusu Ndoa,” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 198, au video inayohusiana katika Maktaba ya Injili.) Ungeweza pia kuangalia picha ya familia yako na shuhudia kwamba Bwana amefanya iwezekane, kupitia ibada na maagano ya hekaluni, kwa familia kudumu milele.