Njoo, Unifuate
Novemba 17–23: “Jitayarisheni kwa Ujio wa Bwana Harusi”: Mafundisho na Maagano 133–134


Mafundisho na Maagano 17–23: ‘Jitayarisheni kwa Ujio wa Bwana Harusi’: Mafundisho na Maagano 133–134,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 133–134,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

mchoro wa wanawali kumi

Wanawali Kumi, na Jorge Cocco

Novemba 17–23, Jitayarisheni kwa Ujio wa Bwana Harusi”

Mafundisho na Maagano 133–134

Katika mwaka 1833, kundi la wahuni walivamia na kuharibu kiwanda cha kupiga chapa cha Kanisa. Miongoni mwa kazi zilizokuwa zikiendelea kupigwa chapa wakati huo ilikuwa ni Kitabu cha Amri—jaribio la kwanza la Kanisa la kukusanya mafunuo ya Mungu kwa siku za mwisho na kuyaweka katika juzuu moja. Wahuni hao walitawanya kurasa zilizokuwa hazijafungwa, na ingawa Watakatifu shupavu walihifadhi baadhi yake, ni nakala chache tu zisizokamilika za Kitabu cha Amri zinajulikana kuwa zilipona.

Kile tunachojua sasa kama sehemu ya 133 ya Mafundisho na Maagano ilitakiwa kuwa ni kiambatisho kwenye Kitabu cha Amri, kama mahali pa mshangao mwishoni mwa mafunuo ya Bwana yaliyochapishwa. Inaonya juu ya siku ijayo ya hukumu na inarudia wito unaopatikana kote katika ufunuo wa siku za leo: Ukimbie ulimwengu, kama ulivyofananishwa na Babilonia. Jenga Sayuni. Jitayarisheni kwa ajili ya Ujio wa Pili. Na sambazeni ujumbe huu “kwa kila taifa, na koo, na lugha, na watu” (mstari wa 37). Mipango halisi kwa ajili ya Kitabu cha Amri haikuweza kukamilishwa, lakini ufunuo huu ni ukumbusho na ushahidi kwamba kazi ya Bwana itasonga mbele, “kwani atauweka wazi mkono wake mtakatifu … , na miisho yote ya dunia itauona wokovu wa Mungu wao” (mstari wa 3).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 133:4–14

Yesu Kristo ananiita mimi niikatae Babilonia na nije Sayuni

Kinyume cha kiroho cha Sayuni ni Babilonia—ni mji wa kale ambao kote katika maandiko ni ishara ya uovu na utumwa wa kiroho. Unaposoma Mafundisho na Maagano 133:4–14, fikiria jinsi Mwokozi anavyokuita wewe “tokeni … katika Babilonia” (mstari wa 5) na “enendeni … nchi ya … Sayuni” (mstari wa 9). Je, unaitikiaje wito Wake? Unajifunza nini kingine kuhusu Sayuni kutoka kwenye ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Njooni Sayuni”? Liahona, Nov. 2008, 37-40).

(Mafundisho na Maagano 133:1–19, 37–39).

ikoni ya seminari
Ninaweza kujitayarisha sasa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Zote mbili sehemu ya 1, dibaji ya Bwana kwenye Mafundisho na Maagano, na sehemu ya 133, kiambatisho cha kwanza kwenye Kitabu cha Amri, zinaanza na ombi linalofanana kutoka kwa Bwana: “Sikilizeni, Enyi watu wa kanisa langu” (Mafundisho na Maagano 1:1; 133:1). Labda mngeweza kujifunza Mafundisho na Maagano 133:1–19, 37–39 na kuorodhesha jumbe ambazo Bwana anakualikeni “mzisikilize” (sikieni na kutii) mnapojitayarisha kwa ajili ya Ujio Wake wa Pili. Kipekee, unaweza kuorodhesha mambo anayotaka wewe uyafanye ili (1) kujitayarisha wewe mwenyewe na (2) kusaidia kuutayarisha ulimwengu kwa ajili ya kurudi Kwake. Je, unajifunza nini kutokana na orodha hizi?

Rais Russell M. Nelson alishiriki kweli muhimu kuhusu ulimwengu utakuwaje wakati Mwokozi anapokuja—na jinsi ya kujitayarisha. Tafuta kweli hizi katika ujumbe wake “Mustakabali wa Kanisa: Kuutayarisha Ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi” (Liahona, Apr. 2020, 6–11). Je, unajisikia kushawishika kufanya nini—au kuendelea kufanya—ili “kuutayarisha ulimwengu kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi”? (“Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni,” Maktaba ya Injili).

Ona pia Mathayo 25:1–13; Russell M. Nelson, “Zikabili Siku za Usoni kwa Imani,” Liahona, Nov. 2020, 73–76; “Enyi Wana wa Bwana,” Nyimbo za Dini, na. 26; Topics and Questions, “Second Coming of Jesus Christ,” Maktaba ya Injili.

Mafundisho na Maagano 133:19–56

Ujio wa Pili wa Yesu Kristo utakuwa wa shangwe kwa wenye haki.

Unaposoma maelezo ya kurudi kwa Mwokozi katika mistari 19–56, ni kitu gani unakipata ambacho unakitazamia kwa hamu kuu? Ni maneno gani au virai vinaelezea upendo wa Bwana kwa ajili ya watu Wake? Fikiria kuandika uzoefu wako binafsi wa “ukarimu wa Bwana [wako], na yote ambayo ameyaweka juu [yako] kulingana na wema wake” (mstari wa 52).

Yesu akionyesha ukarimu kwa mwanamke

Maelezo kutoka Mponyaji, na Kelsy na Jesse Lightweave

Mafundisho na Maagano 134

“Serikali zimewekwa na Mungu kwa manufaa ya mwanadamu.”

Mahusiano ya Watakatifu wa mwanzo na serikali yalikuwa magumu. Wakati Watakatifu walipolazimishwa kutoka Jackson County, Missouri, mnamo 1833, waliomba msaada kutoka kwa serikali za mitaa na serikali ya kitaifa na hawakupokea msaada wowote. Wakati huo huo, baadhi ya watu nje ya Kanisa walitafsiri mafundisho kuhusu Sayuni kumaanisha kwamba Watakatifu walikataa mamlaka ya serikali za kidunia Mafundisho na Maagano 134 iliandikwa, kwa sehemu, ili kufafanua msimamo wa Kanisa juu ya serikali. Sehemu hii inapendekeza nini kuhusu jinsi Watakatifu wa Bwana wanavyopaswa kujisikia kuhusu serikali?

Unapojifunza sehemu ya 134, fikiria kutafuta kanuni za serikali na wajibu wa raia. Ni kwa jinsi gani mawazo haya yaliweza kuwa msaada kwa Watakatifu wa mwanzo? Ni kwa jinsi gani yanatumika pale unapoishi?

Ona ppia Makala za Imani 1:11–12; Topics and Questions, “Religious Freedom,” Maktaba ya Injili.

ikoni ya 03 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 133:4–5, 14

Bwana ananitaka nikae mbali na uovu katika ulimwengu.

  • Wewe na watoto wako mngeweza kuorodhesha baadhi y sehemu na hali ambazo Bwana anataka sisi tukae mbali nazo? Kisha mngeweza kulingaisha sehemu hizo na hali kwenye mapitio ya ufafanuzi wa “Babeli, Babilonia” katika Mwongozo wa Maandiko (Maktaba ya Injili). Wangeweza pia kusoma Mafundisho na Maagano 133:4–5, 14. Je, inamaanisha nini “tokeni … katika Babilonia”? (mstari wa 5). Unaweza pia kutengeneza orodha kama hiyo ya sehemu na hali ambazo Bwana anatualika sisi twende na kulinganisha orodha hiyo na mapitio ya ufafanuzi wa “Sayuni” katika Mwongozo wa Maandiko.

Mafundisho na Maagano 133:19–21, 25

Yesu Kristo atakuja tena.

  • Watoto wako wanaweza kufurahia kuigiza inakuwaje kujitayarisha kwa ajili ya kitu, kama mashindano ya mchezo, mgeni muhimu, au sikukuu pendwa. Kwa nini maandalizi ni muhimu? Kisha someni pamoja Mafundisho na Maagano 133: 17–19, 21 na waalike watoto wako kutafuta kitu ambacho Bwana anatualika sisi tujitayarishe kwa ajili yake. Ungeweza kuwaonyesha watoto picha kutoka kwenye muhtasari wa wiki hii na waulize watoto wako wanajua nini kuhusu Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Kitu gani kingine tunachojifunza kutoka mistari 19–25, 46–52? Je tunaweza kufanya nini ili kujiandaa kwa ajili ya tukio hili la shangwe?

  • Ungeweza kuficha picha mbalimbali au vitu vinavyoonyesha vitu tunavyoweza kufanya ili kujitayarisha kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo (kama vile kusoma maandiko, kushiriki injili, au kuzihudumia familia zetu). Acha watoto wako wazitafute picha hizo au vitu na kuzungumzia kuhusu namna gani kufanya vitu hivi kunatusaidia sisi kuwa tayari kumlaki Mwokozi wakati Atakaporudi.

  • Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu Ujio wa Pili, kama vile “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83). Shiriki upendo wako kwa ajili ya Mwokozi na hisia zako kuhusu kurudi Kwake.

Mafundisho na Magano 133:52–53

Yesu Kristo ni mwenye upendo na mkarimu.

  • Wewe na watoto wako mngeweza kutazama picha ambazo zinaonyesha kwamba Yesu ni mwenye upendo na mkarimu. (Kwa mfano, ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 4247.) Yesu amefanya kitu gani kingine ili kuonyesha upendo Wake na ukarimu? Someni pamoja Mafundisho na Maagano 133:52, na wasaidie watoto wako wafikirie juu ya njia ambazo wanaweza “kutaja ukarimu wa upendo wa Bwana wao” kwa watu wengine.

    Christ Healing the Sick at Bethesda
Yesu akiwa na mtoto

Maelezo kutoka Katika Nuru Yake, na Greg Olsen

Fundisha mafundisho ya wazi na rahisi. Bwana anafundisha injili Yake kwa “uwazi” na “urahisi” (Mafundisho na Maagano 133:57). Maneno haya yanapendekeza nini kwako kuhusu kufundisha injili kwa familia yako au darasa?

Mafundisho na Maagano 134:1–2

Bwana ananitaka nitii sheria.

  • Watoto wako wangeweza kuorodhesha masharti au sheria wanazotii. Je, maisha yangekuwaje kama kusingekuwa na mtu anayetii sheria hizi? Kisha ungeweza kusoma Mafundisho na Maagano 134:1–2 pamoja nao, ukiwasaidia waelewe neno lolote au kifungu cha maneno wasichokielewa. Je, ni kwa nini Bwana anatutaka tutii sheria? (Ona pia Makala ya Imani 1:12).

Kwa ajili ya mawazo zaidi ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

Yesu akiwa amevaa joho jekundu

Kristo katika Joho Jekundu, na Minerva Teichert

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto