Njoo, Unifuate
Desemba 1–7: “Ono la Ukombozi wa Wafu”: Mafundisho na Maagano 137–138


“Desemba 1–7: ‘Ono la Ukombozi wa Wafu: Mafundisho na Maagano 137–138,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 137–138,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Yesu Kristo akifundisha katika ulimwengu wa roho

Maelezo kutoka Kristo Akihubiri katika Ulimwengu wa Roho, na Robert T. Barrett

Desemba 1–7: “Ono la Ukombozi wa Wafu”

Mafundisho na Maagano 137–138

Mafunuo yaliyoandikwa katika Mafundisho na Maagano 137 na 138 yametenganishwa kwa zaidi ya miaka 80 na maili 1,500 (kilomita 2,400). Sehemu ya 137 ilipokelewa na Nabii Joseph Smith mnamo mwaka 1836 katika Hekalu la Kirtland, na sehemu ya 138 ilipokelewa na Joseph F. Smith, Rais wa sita wa Kanisa, mnamo mwaka 1918 katika Jiji la Salt Lake. Lakini kimafundisho, maono haya mawili ni ya bega kwa bega. Yote mawili yanajibu maswali ambayo watu wengi—ikijumuisha manabii wa Mungu—wanakuwa nayo kuhusu maisha baada ya kifo. Joseph Smith alijiuliza kuhusu hatma ya kaka yake Alvin ambaye alifariki dunia pasipo kubatizwa. Joseph F. Smith, ambaye alikuwa amewapoteza wazazi wake wote wawili na watoto 13 kwa vifo visivyotarajiwa, siku zote alikuwa akifikiria kuhusu ulimwengu wa roho na kujiuliza kuhusu kuhubiriwa kwa injili huko.

Sehemu ya 137 inatoa mwangaza wa kuanzia juu ya hatma ya watoto wa Mungu katika maisha yajayo, na sehemu ya 138 inafungua pazia hata kuwa wazi zaidi. Kwa pamoja, mafunuo yote mawili yanashuhudia juu ya “upendo mkuu na wa ajabu unaodhihirishwa na Baba na Mwana” (Mafundisho na Maagano 138:3).

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 137; 138:30–37, 57–60

ikoni ya seminari
Watoto wote wa Baba wa Mbinguni watapata fursa ya kuchagua uzima wa milele.

Alvin Smith, kaka mpendwa wa Nabii Joseph, alifariki dunia miaka sita kabla Mungu hajaresha duniani mamlaka ya kubatiza. Uelewa wa kawaida miongoni mwa Wakristo katika miaka ya 1836 ulikuwa kwamba kama mtu alikufa bila kubatizwa, mtu huyo asingeweza kwenda mbinguni. Joseph alijiuliza kuhusu wokovu wa milele wa Alvin kwa miaka mingi—hadi alipopokea ufunuo huu katika Mafundisho na Maagano 137.

Watu wengi leo wana maswali kama haya. Je, Ni kwa nni Mungu atake ibada na maagano wakati watu wengi sana kamwe hawana fursa ya kuyapokea? Je, unaweza kusema nini kwa mtu ambaye anajiuliza hili? Je, unawezaje kujenga imani yao kwa Mungu na mahitaji Yake kwa ajili ya wokovu? Tafuta kweli ambazo ungeweza kushiriki katika sehemu ya 137 na katika sehemu ya 138:30–37, 57–60. Ungeweza pia kutazama kweli hizi zilizoelezewa katika wimbo wa dini “The Glorius Gospel Light Has Shone” (Nyimbo za Dini, na. 283) na katika ujumbe wa Rais Henry B. Eyring “Kuikusanya Familia ya Mungu” (Liahona, Mei 2017, 19–22).

Unapojifunza na kutafakari, unaweza kuandika misukumo yako kwa kumalizia sentensi hizi:

  • Kwa sababu ya mafunuo haya, ninajua kwamba Baba wa Mbinguni .

  • Kwa sababu ya mafunuo haya, ninajua kwamba mpango wa wokovu wa Baba .

  • Kwa sababu ya mafunuo haya, Mimi ninataka .

Ona pia Watakatifu, 1:232–35.

Mafundisho na Maagano 138:1–11, 25–30

Kusoma na kutafakari maandiko kunaniandaa mimi kupokea ufunuo.

Wakati mwingine ufunuo unakuja hata kama hatuutafuti. Lakini mara nyingi, unakuja kwa sababu tunautafuta kwa bidii na kujiandaa kwa ajili yake. Unaposoma Mafundisho na Maagano 138:1–11, 25–30, fahamu kile Rais Joseph F. Smith alichokuwa anatafakari wakati “macho [yake] ya ufahamu yalipofunguliwa.” Ungeweza pia kulinganisha tukio hili na 1 Nefi 11:1–6; Joseph Smith—Historia ya 1:12–19. Kisha fikiria jinsi unavyoweza kufuata mfano wa Rais Smith. Kwa mfano, je, mabadiliko gani unavutiwa kuyafanya kwenye kujifunza kwako maandiko ili kupokea zaidi ufunuo binafsi?

Katika ujumbe wake “Ono la Ukombozi wa Wafu” (Liahona, Nov. 2018, 71–74), Rais M. Russell M. Ballard alipendekeza njia zingine ambazo kupitia hizo Rais Smith alikuwa amejiandaa kupokea ufunuo huu. Unajifunza nini kutokana na matukio haya? Fikiria jinsi ambavyo Bwana amekuandaa wewe kwa ajili ya uzoefu ulio nao—na jinsi anavyokuandaa sasa kwa ajili ya matukio katika siku zijazo.

Ona pia Watakatifu, 3:202–5; “Ministry of Joseph F. Smith: A Vision of the Redemption of the Dead” (video), Maktaba ya Injili.

2:3

Ministry of Joseph F. Smith: A Vision of the Redemption of the Dead

Nearing death, President Joseph F. Smith receives revelation from God regarding redemption of the dead.

Rais Joseph F. Smith

Joseph F.Smith, na Albert E. Salzbrenner

Mwalike Roho. “Umeona nini ambacho kinachangia katika mazingira ya kiroho ya kujifunza injili? Ni nini kinapunguza mazingira ya kiroho ya kujifunza injili? (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi18). Unapojifunza uzoefu wa Rais Joseph F. Smith katika Mafundisho na Maagano 138:1–11, Fikiria jinsi gani unaweza kuhimiza kutafakari na kualika misukumo ya kiroho kwako wewe mwenyewe na, kama wewe ni mwalimu, kwa watu unaowafundisha.

Mafundisho na Maagano 138:25–60

Kazi ya Mwokozi inaendelea upande mwingine wa pazia.

Rais Russell M. Nelson alifundisha, “Ujumbe wetu kwa ulimwengu ni rahisi na wa dhati: tunawaalika watoto wote wa Mungu kutoka pande zote mbili za pazia waje kwa Mwokozi wao, wapokee baraka za hekalu takatifu, wawe na shangwe ya kudumu, na kustahili uzima wa milele” (“Sote Tusonge Mbele,” Liahona, Mei 2018, 118–19). Tafakari maelezo haya unaposoma Mafundisho na Maagano 138:25–60. Ungeweza pia kuzingatia maswali haya:

  • Unajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu jinsi kazi ya Mwokozi inavyokamilishwa katika ulimwengu wa roho? Kwa nini ni muhimu kwako kujua kwamba kazi hii inafanyika?

  • Je, ni kitu gani kinakuvutia kuhusu wajumbe wa Bwana katika ulimwengu wa roho?

  • Je, ni kwa jinsi gani ufunuo huu unaimarisha imani yako katika mpango wa Mungu wa ukombozi?

Kama unataka kujifunza zaidi kuhusu ulimwengu wa roho, ungeweza kujifunza ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Tumaini katika Bwana” (Liahona, Nov. 2019, 26–29).

Ona pia “Susa Young Gates na Ono la Ukombozi wa Wafu,” katika Ufunuo katika Muktadha, 315–22; “A Visit from Father” (video), Maktaba ya Injili.

3:20

A Visit from Father

President Russell M. Nelson recounts a personal family history story that bears testimony of the importance of temple and family history work for all families.

Kwa mawazo zaidi, ona matoleo ya mwezi huu ya majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

ikoni ya 03 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 137:5–10, 138:18-–5

Watoto wote wa Baba wa Mbinguni watapata nafasi ya kuisikia injili.

  • Ili kujifunza kuhusu ingeweza kumaanisha nini kwa Joseph Smith kuwaona watu kadhaa wa familia yake katika ufalme wa selestia, watoto wako wangeweza kutazama video “Ministry of Joseph Smith: Temples” (Maktaba ya Injili), au ungeweza kusimulia Hadithi za Mafundisho na Maagano, 152–53 (au video inayohusiana katika Maktaba ya Injili). Pengine mngeweza pia kuzungumza kuhusu mtu fulani mnayemjua ambaye alikufa bila nafasi ya kubatizwa. Mafundisho na Maagano 137:5–10 inatufundisha nini kuhusu mtu huyo?

    2:3

    Ministry of Joseph Smith: Temples

    Joseph Smith establishes temple work as an essential purpose for the Saints of God.

    2:17

    Chapter 39: The Kirtland Temple Is Dedicated: January–March 1836

  • Zingatia kutumia picha ya kaburi la Mwokozi (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 58, au Picha za Biblia, na. 14) na picha mwishoni mwa muhtasari huu ili kuwafundisha watoto wako mahali ambako roho ya Yesu ilienda wakati mwili Wake ulipokuwa katika kaburi. Kisha mnaweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 138:18–19, 23–24, 27–30 ili kujifunza kuhusu Yesu alifanya nini wakati alipokuwa huko. Aliwatembelea akina nani? Aliwaamuru wafanye nini? Kwa nini alifanya hili?

    The body of the crucified Christ being wrapped in white burial cloth (presumably by Joseph of Arimathaea and Nicodemus) in preparation for entombment. Several men and women are gathered around the crucified body. They are mourning the crucifixion.
  • Ungeweza pia kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii ili kuwasaidia watoto wako walinganishe kitu ambacho wamisionari wanafundisha kweye upande huu wa pazia (ona, kwa mfano, Makala ya Imani 1:4) na kitu ambacho wamisionari wanafundisha katika ulimwengu wa roho (ona Mafundisho na Maagano 138:33). Je, nini kinafanana katika mistari hii, na nini ni tofauti? Je, hii inatufundisha nini sisi kuhusu Baba wa Mbinguni na mpango Wake?

mtoto akisoma maandiko

Kuyatafakari maandiko kunamwalika Roho Mtakatifu.

Mafundisho na Maagano 138:1–11

Ninapoyatafakari maandiko, Roho Mtakatifu anaweza kunisaidia niyaelewe.

  • Wewe na watoto wako mnaposoma Mafundisho na Maagano 138:1–11 pamoja, ungeweza kuwaalika wajifanye wao ni Rais Joseph F. Smith na wafanye matendo ambayo yanaenda sambamba na maneno katika mstari wa 6 na wa 11. Ungeweza pia kuwaonyesha picha ya Rais Smith (iko moja katika muhtasari huu) na elezea kwamba alikuwa Rais wa sita wa Kanisa. Ungeweza pia kuzungumzia kuhusu wakati ambapo ulitafakari kitu katika maandiko na Roho Mtakatifu akakusaidia ukielewe kitu hicho.

  • Zingatieni kuimba pamoja wimbo kuhusu kujifunza maandiko, kama vile “Search, Ponder, and Pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109). Je, wimbo huu unasema tunapaswa kufanya nini ili kuyaelewa maandiko?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

Yesu Kristo katika ulimwengu wa roho

Waliopewa mamlaka, na Harold I. Hopkinson.

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto