“Desemba 8–14; ‘Tunaamini’: Makala za Imani na Matamko Rasmi 1 na 2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Makala za Imani na Matamko Rasmi 1 na 2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Desemba 8–14: “Tunaamini”
Makala za Imani na Matamko Rasmi 1 na 2
Tangu Ono la Kwanza la Joseph Smith, Mungu ameendelea kuliongoza Kanisa Lake kwa ufunuo. Katika baadhi ya hali, ufunuo huo umejumuisha mabadiliko kwenye sera na utendaji wa Kanisa. Matamko Rasmi 1 na 2 yalitangaza aina hii ya ufunuo—moja liliongoza kwenye kumalizika kwa ndoa ya wake wengi, na jingine lilifanya baraka za ukuhani zipatikane kwa watu wa rangi zote. Mabadiliko kama haya ni sehemu ya kile inachomaanisha kuwa na “kanisa la kweli na lililo hai” (Mafundisho na Maagano 1:30), likiwa na nabii wa kweli na aliye hai, anayeongozwa na Mungu wa kweli na aliye hai.
Lakini ukweli wa milele haubadiliki, ingawa uelewa wetu wa ukweli huo unabadilika. Na wakati mwingine ufunuo unatupa mwangaza wa ziada juu ya ukweli. Makala za Imani zinatimiza dhumuni hili la kufafanua. Kanisa limejengwa imara juu ya ukweli wa milele lakini linaweza kukua na kubadilika “kulingana na mapenzi ya Bwana, likikidhi rehema Zake kulingana na hali za watoto wa watu” (Mafundisho na Maagano 46:15). Kwa maneno mengine, “Tunaamini yale yote ambayo Mungu ameyafunua, na ambayo sasa anayafunua, na tunaamini kwamba bado Yeye atayafunua mambo mengi makuu na muhimu yahusuyo Ufalme wa Mungu” (Makala ya Imani 1:9).
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Makala za Imani zina kweli za msingi za injili iliyorejeshwa.
Zingatia mbinu hii ya kujifunza Makala za Imani: Kwa kila makala ya imani, tengeneza “somo fupi” ili kuelezea kitu unachoamini. Somo lako hilo fupi lingeweza kujumuisha andiko linalohusika, picha, wimbo wa dini, au wimbo wa watoto, au uzoefu binafsi kuhusu kuishi ukweli ambao makala ya imani hiyo inaufundisha.
Je, ni tofauti gani kweli hizi zinaleta katika uhusiano wetu na Baba yetu wa Mbinguni na Yesu Kristo? Makala za Imani zimeboreshaje kujifunza kwako injili au zimekusaidiaje kushiriki injili na wengine.
Ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Makala za Imani,” Maktaba ya Injili,” L. Tom Perry, “Mafundisho na Kanuni Zilizopo katika Makala za Imani,” Liahona, Nov. 2013, 46–48; “Chapter 38: The Wentworth Letter,” katika Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith, 435–47.
Makala ya Imani 1:9; Matamko Rasmi 1 na 2
Kanisa la Yesu Kristo linaongozwa kwa ufunuo.
“Tunaamini kwamba [Mungu] bado atayafunua mambo mengi makuu na muhimu yahusuyo Ufalme wa Mungu” (Makala ya Imani 1:9). Ukiwa na kanuni hii akilini, rejelea Matamko Rasmi 1 na 2, na tafuta maneno na vifungu ya maneno ambavyo vinaimarisha imani yako katika ufunuo unaoendelea. Ni kwa jinsi gani mafunuo haya yamegusa maisha yako? Ni kwa jinsi gani yamesaidia kazi ya ufalme wa Baba wa Mbinguni kuendelea?
Je, ni ushahidi gani unaouona kwamba Kanisa linaongozwa “kwa mwongozo wa kiungu kutoka kwa Mwenyezi Mungu” leo? (Tamko Rasmi 1). Labda unaweza kurejelea moja au zaidi ya jumbe za mkutano mkuu wa hivi karibuni, ukitafuta jinsi gani Bwana analiongoza Kanisa Lake—na maisha yako. Ujumbe wa hivi karibuni kutoka kwa Rais wa Kanisa unaweza kuwa mahali pazuri pa kuanzia.
Unaweza kufanya nini kama wewe au mtu unayempenda anahangaika kuelewa au kukubali kitu ambacho Bwana anafundisha kupitia manabii Wake? Je, Kwa nini una shukrani kwa ajili ya nabii?
Ona pia Amosi 3:7; 2 Nefi 28:30; Allen D. Haynie, “Nabii Aliye Hai kwa ajili ya Siku za Mwisho,” Liahona, Mei 2023, 25–28; Topics and Questions, “Prophets,” Maktaba ya Injili; “Asante Mungu kwa Nabii,” Nyimbo za Dini, na. 11.
Kazi ya Mungu lazima iende mbele.
Katika “Dondoo kutoka Hotuba Tatu za Rais Wilford Woodruff kuhusu Manifesto” (mwisho wa Tamko Rasmi 1), ni sababu gani nabii alizitoa kwa Bwana kusitisha zoezi la ndoa ya mitala? Hii inakufundisha nini kuhusu kazi ya Mungu?
Kwa taarifa zaidi kuhusu chimbuko la kihistoria la Tamko Rasmi1, ona Watakatifu, 2:602–15; “Mtumishi na Manifesto,” katika Ufunuo katika Muktadha, 323–31; Topics and Questions, “Plural Marriage and Families in Early Utah,” Maktaba ya Injili.
Ninaweza kumwamini Bwana, hata wakati ninapokuwa sina uelewa mkamilifu.
Hatujui kwa nini kutawazwa katika ukuhani na ibada za hekaluni hazikupatikana kwa waumini wa Kanisa wenye asili ya Kiafrika kwa wakati fulani. Hata wakati tunapokabiliwa na maswali magumu yasiyojibika kuhusu sera hiyo, Watakatifu wengi wa Siku za Mwisho Weusi walimtumainia Bwana (ona Mithali 3:5) na wakabaki waaminifu Kwake maisha yao yote. Kujifunza kuhusu imani yao na uzoefu kunaweza kuwa ya kuvutia kwako. Haya ni baadhi ya maelezo yao, yanayopatikana kwenye history.ChurchofJesusChrist.org:
-
“In My Father’s House Are Many Mansions” (hadithi ya Green Flake)
-
“You Have Come at Last” (hadithi ya Anthony Obinna)
-
“Break the Soil of Bitterness” (hadithi ya Julia Mavimbela)
-
“I Will Take It in Faith” (hadithi ya George Rickford)
-
“Long-Promised Day” (hadithi ya Joseph W. B. Johnson)
Unaposoma Tamko Rasmi 2, unajifunza nini kuhusu mchakato wa Bwana wa kuongoza sera za Kanisa Lake? Tafakari jinsi ulivyojifunza kumwamini Bwana hata wakati huna uelewa mkamilifu.
Ona pia 2 Nefi 26:33; “Kuwa Shahidi wa Uaminifu,” katika Ufunuo katika Muktadha, 332–41; Topics and Questions, “Race and the Priesthood,” Maktaba ya Injili; Ahmad Corbitt, “Insha Binafsi juu ya Mbari na Ukuhani,” sehemu 1–4, history.ChurchofJesusChrist.org; BeOne.ChurchofJesusChrist.org.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Ninaamini katika injili ya Yesu Kristo.
-
Zingatia kutafuta nyimbo za dini au nyimbo za watoto ambazo zinaweza kuwasaidia watoto waelewe moja au zaidi ya Makala za Imani. Pengine wanaweza kukusaidia kuchagua nyimbo za dini na nyimbo zingine. Wasaidie watoto wako waone jinsi nyimbo hizo zinavyohusiana na Makala za Imani.
-
Wewe na watoto wako mngeweza kufanya kazi pamoja kuandika maswali ambayo watu wanaweza kuwa nayo kuhusu injili ya Yesu Kristo au Kanisa la Lake. Kisha mngeweza kufanya kazi pamoja kujibu maswali hayo mkitumia Makala za Imani. Tunaweza kwenda wapi kwingine tunapokuwa na maswali kuhusu injili?
Makala ya Imani 1:9; Matamko Rasmi 1 na 2
Bwana analiongoza Kanisa Lake kupitia nabii Wake.
-
Ili kuwasaidia watoto wako waelewe makala ya tisa ya Imani, labda ungeweza kutoa seti ya maandiko na picha ya nabii aliye hai (au toleo la hivi karibuni la gazeti la Liahona). Waombe wanyanyue maandiko juu unaposoma maneno “yote Mungu aliyoyafunua” na picha au jarida unaposoma “yote ambayo sasa anayafunua” (Makala ya Imani 1:9). Je, ni kwa nini tunawahitaji wote, manabii wa kale na wa sasa?
-
Watoto wako wanaweza kujifunza jinsi maneno ya manabii yanavyotuongoza sisi kwa kufuata maelekezo ya kutengeneza kitu, kama vile chakula au mwanasesere. Unaweza kulinganisha hili na maelekezo ambayo Yesu Kristo anatupatia sisi kupitia nabii. Je, ni baadhi ya mambo gani Bwana ametufundisha sisi kupitia nabii Wake aliye hai leo?
Matamko Rasmi 1 na 2
Manabii hutusaidia tuyajue mapenzi ya Baba wa Mbinguni.
-
Pengine kuona jinsi maandiko ya kale yanavyohusiana na ufunuo wa sasa kungeweza kuwasaidia watoto wako waelewe Matamko Rasmi. Unaweza kuwaomba wasome Matendo ya Mitume 10:34–35 na Yakobo 2:27–30 na waalike waamue ni andiko gani linahusiana na Tamko Rasmi 1 (ambalo liliongoza kwenye kusimamisha ndoa za wake wengi) na ambalo linahusiana na Tamko Rasmi la 2 (ambalo lilitangaza kwamba kutawazwa katika ukuhani na ibada za hekaluni zinapatikana kwa watu wa rangi zote). Toa ushuhuda wako kwamba Bwana hufunua mapenzi Yake kwa manabii wa kale na wa sasa.