Hadithi za Maandiko
Familia ya Joseph Smith


“Familia ya Joseph Smith,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)

“Familia ya Joseph Smith,” Hadithi za Mafundisho na Maagano

1805–1817

Familia ya Joseph Smith

Familia ya imani

Joseph Smith na familia yake wakifanya kazi pamoja shambani kwao.

Joseph Smith alizaliwa Desemba 23, 1805, kaskazini mashariki mwa Marekani. Baba yake pia aliitwa Joseph. Jina la mama yake lilikuwa Lucy. Alikuwa na kaka na dada wengi. Familia ya Joseph walikuwa wakulima. Walimwamini Mungu na walipendana.

Joseph Smith—Historia ya 1:3–4

Joseph Smith akiwa mvulana mdogo. Mguu wake wa kushoto umefungwa bandeji. Mama yake ana wasiwasi kumhusu yeye.

Wakati Joseph alipokuwa kijana mdogo, alipata ugonjwa uliosababisha tatizo katika mguu wake. Ulimuuma sana. Familia ya Joseph ilijaribu kumsaidia ahisi vizuri, lakini mguu wake bado uliuma sana. Madaktari walijaribu kutibu mguu wake, lakini hawakuweza.

Saints, 1:7

Joseph Smith akiwa kitandani. Kaka yake anapiga magoti pembeni ya kitanda. Mama yake anazungumza na daktari wake hapo nyuma.

Madaktari walisema walihitaji kukata mguu wa Joseph ili kuokoa maisha yake. Lakini mama yake asingewaruhusu. Aliuliza kama kulikuwa na njia nyingine yoyote ya kumsaidia Joseph. Madaktari waliamua kukata sehemu ya mfupa katika mguu wake. Joseph alijua hii ingeumiza, lakini alikuwa na imani kwamba Mungu angemsaidia.

Saints, 1:7

Daktari wa Joseph Smith anampa pombe kwa ajili ya upasuaji wa mguu wake. Joseph anakataa. Baba yake anamshikilia.

Madaktari walitaka kumpa Joseph pombe anywe ili kutia ngazi maumivu. Lakini Joseph alisema hapana. Alitaka tu baba yake amshikilie.

Saints, 1:7

Mama wa Joseph Smith anaondoka chumbani wakati daktari akijiandaa kufanya upasuaji.

Joseph alimwomba mama yake aende nje. Hakutaka amwone katika maumivu makali wakati madaktari wakikata ndani ya mguu wake.

Daktari akifanya upasuaji kwenye mguu wa Joseph Smith. Baba yake anamshikilia ili kumpa msaada.

Baba yake Joseph alimshikilia wakati madaktari wakikata sehemu mbaya za mfupa kwenye mguu wake. Hii iliumiza sana, lakini Mungu alimsaidia Joseph kuwa jasiri. Baada ya miaka michache, mguu wa Joseph ulipata nafuu, lakini bado uliuma kwenye kutembea.

Saints, 1:6–7

Joseph Smith na familia yake huko New York. Wanafanya kazi wakigema miti ya mishira

Wakati Joseph alipokuwa na umri mkubwa, familia yake ilihamia jimbo la New York. Familia ya Joseph ilikuwa masikini. Walifanya kazi kwa bidii ili kuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya familia yao. Joseph alikuwa mtoto mwema. Alikuwa na furaha na alipenda kucheka na kuburudika.

Saints, 1:5–9

Familia ya Joseph Smith ikiwa imekaa pamoja kwa utulivu kwenye meza ya chakula cha jioni.

Familia ya Joseph walimpenda Yesu Kristo. Walisali na kusoma Biblia pamoja. Lakini wazazi wa Joseph hawakuwa na uhakika wa kanisa lipi wanapaswa kujiunga nalo. Usiku mmoja, mama yake Joseph, Lucy, alisali na kumwambia Mungu kwamba alitaka kupata Kanisa la kweli la Yesu Kristo. Mungu alijibu sala yake na akaahidi angelipata.

Saints, 1:10–11