“Malaika Moroni Anamtembelea Joseph Smith,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Malaika Moroni Anamtembelea Joseph Smith,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
1823
Malaika Moroni Anamtembelea Joseph Smith
Kujifunza kuhusu kitabu kitakatifu
Miaka mitatu ilipita tangu Ono la Kwanza la Joseph Smith. Joseph alihisi vibaya kuhusu baadhi ya makosa aliyokuwa ameyafanya tangu wakati huo. Alijiuliza jinsi Mungu alivyohisi kumhusu.
Joseph Smith—Historia ya 1:28–29; Saints, 1:20
Usiku mmoja, baada ya kila mtu kulala, Joseph aliamua kusali. Mungu alikuwa amejibu sala zake hapo awali, na Joseph alijua angezijibu tena.
Joseph Smith—Historia ya 1:29; Saints, 1:21–22
Wakati Joseph alipokuwa akisali, mwanga ulijaza chumba. Joseph alimwona malaika amesimama angani kando ya kitanda chake. Malaika alisema kwamba jina lake lilikuwa Moroni. Mungu alikuwa amemtuma. Alisema Mungu alikuwa amemsamehe Joseph na alikuwa na kazi kwa ajili yake kufanya. Watu ulimwenguni kote wangejua kuhusu Joseph na kazi ambayo Mungu alimpa.
Joseph Smith—Historia ya 1:30–33
Moroni alisema kulikuwa na kitabu kilichotengenezwa kwa kurasa za dhahabu au mabamba. Kilizikwa katika kilima karibu na nyumbani kwao Joseph. Kitabu hicho kilihusu watu ambao waliishi Amerika miaka mingi iliyopita. Walijua kuhusu Yesu Kristo na injili Yake. Moroni alisema Mungu angemsaidia Joseph kutafsiri kitabu hicho ili watu waweze kukisoma.
Joseph Smith—Historia ya 1:34, 46
Moroni alimtembelea mara tatu usiku ule na tena siku iliyofuata. Joseph alimwambia baba yake kile alichokuwa amekiona. Baba yake Joseph alikuwa na furaha. “Lilikuwa ono kutoka kwa Mungu,” alimwambia Joseph.
Joseph Smith—Historia ya 1:35–50; Saints, 1:22–25
Joseph alikwenda kwenye kilima na kupata mabamba ya dhahabu chini ya mwamba mzito. Alipoyafikia, aliwaza kuhusu yalikuwa na thamani kiasi gani cha fedha. Moroni alikuja na kumwambia Joseph kwamba hakuwa tayari kuchukua mabamba. Alimwambia Joseph kurudi mahali hapa kila mwaka hadi atakapokuwa tayari.
Joseph Smith—Historia ya 1:51–54; Saints, 1:25–27