“Martin Harris Anamsaidia Joseph,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Martin Harris Anamsaidia Joseph,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
1828–1829
Martin Harris Anamsaidia Joseph
Kujifunza kumtumaini Bwana
Siku moja, wakati Joseph na Emma wakiishi Pennsylvania, rafiki aliyeitwa Martin Harris alikuja kuwatembelea. Martin alimiliki shamba kubwa huko New York. Alijua kuhusu kazi ya Joseph na mabamba ya dhahabu. Alikuwa amemsaidia Joseph hapo kabla, na sasa alitaka kujua kama kulikuwa na mengi zaidi ambayo angeweza kufanya ili kusaidia.
Saints, 1:49
Joseph na Emma walikuwa na shukrani. Watu wengi walidhani Joseph alikuwa akidanganya. Ilikuwa vizuri kuwa na rafiki kama Martin ambaye aliamini mabamba ya dhahabu yalikuwa halisi.
Saints, 1:49
Wakati Joseph akitafsiri mabamba, Martin aliandika kile alichokisema. Martin alikuwa na shauku ya kumsaidia Bwana katika kazi hii kuu.
Saints, 1:50
Mke wa Martin, Lucy, hakuwa na furaha. Hakuamini kwamba Joseph alikuwa kweli na mabamba ya dhahabu. Alidhani Joseph alikuwa akimlaghai Martin. Alitaka Martin arudi New York na aache kumsaidia Joseph.
Saints, 1:49–50.
Lakini Martin aliendelea kufanya kazi na Joseph. Alidhani kwamba kama Lucy angeweza kusoma kile walichokuwa wanakifanyia kazi, angeamini pia. Alimuuliza Joseph kama angeweza kuchukua kurasa walizokuwa wametafsiri kwenda nazo New York ili kumwonyesha mkewe. Joseph alisema kwamba angesali na kumuuliza Mungu.
Saints, 1:50–51.
Bwana alimwambia Joseph kutomruhusu Martin achukue kurasa. Martin alimwomba Joseph asali tena. Joseph alisali na kupata jibu lile lile. Lakini Martin alitaka sana kumwonyesha mkewe kurasa, na Joseph alitaka kumsaidia rafiki yake. Joseph alisali kwa mara ya tatu. Wakati huu Mungu alimwambia Joseph angeweza kuamua cha kufanya.
Saints, 1:51
Joseph alimwambia Martin kwamba angeweza kwenda na kurasa hizo New York, lakini angeweza kuzionyesha kwa wanafamilia fulani pekee. Na alihitaji kuzirudisha kurasa hizo ndani ya wiki mbili. Martin alikubali na kuondoka na kurasa.
Saints, 1:51
Wakati Martin alipokuwa ameondoka, mtoto alizaliwa kwa Joseph na Emma. Lakini mtoto alifariki, na Emma akawa mgonjwa. Emma na Joseph walikuwa na huzuni sana.
Saints, 1:51–52.
Joseph alikuwa na wasiwasi kuhusu Emma. Pia alikuwa na wasiwasi kuhusu Martin. Wiki mbili zilikuwa zimepita, na Martin hakuwa amerudi. Emma alikuwa na wasiwasi pia.
Saints, 1:52
Emma alimwambia Joseph aende New York kumtafuta Martin. Joseph alikutana na Martin nyumbani kwa wazazi wake. Wakati Joseph alipomuuliza Martin kuhusu kurasa, Martin alihuzunika sana. Alisema kurasa zilikuwa zimepotea. Alitafuta kila mahali lakini hakuweza kuzipata.
Saints, 1:52–53
Joseph alihuzunika sana na kuogopa. Alijua alikuwa amekosea kumruhusu Martin achukue kurasa. Alirudi nyumbani na kumwambia Emma kilichotokea. Malaika Moroni alikuja na kuchukua mabamba ya dhahabu. Alisema kama Joseph angekuwa mnyenyekevu na kutubu, angeweza kurudishiwa mabamba na kutafsiri tena.
Mafundisho na Maagano 3:5–11, 10:1–3; Saints, 1:53–54
Kwa wiki nyingi, Joseph aliwaza kuhusu kile alichokosea. Alisali na kuomba msamaha. Mungu alimsamehe. Alimwambia Joseph kwamba kurasa zilikuwa zimeibiwa na watu ambao walikuwa wanajaribu kusitisha kazi ya Mungu. Lakini hakuna anayeweza kuisitisha kazi ya Mungu. Mungu alikuwa na mpango wa kuifanya kazi Yake iendelee.
Mafundisho na Maagano 3:1–10; Saints, 1:54–55
Moroni alimrudishia Joseph mabamba. Mungu alimwambia Joseph na Martin kwamba kama wangekuwa wanyenyekevu na kumtumaini Yeye, wangeweza kuendelea kusaidia katika kazi Yake katika njia nyingi. Wangeweza kusaidia kuleta Kitabu cha Mormoni ulimwenguni. Kitabu hiki kingewasaidia watu kila mahali watubu na kuamini katika Yesu Kristo.
Mafundisho na Maagano 3:16–20; 5:21–35; Saints, 1:56–57