“Bwana Anamtuma Oliver Cowdery,” Hadithi za Mafundisho na Maagano (2024)
“Bwana Anamtuma Oliver Cowdery,” Hadithi za Mafundisho na Maagano
1828–1829
Bwana Anamtuma Oliver Cowdery
Kujifunza jinsi Mungu anavyozungumza nasi
Joseph na Emma waliendelea kutafsiri Kitabu cha Mormoni. Kazi ilikuwa ngumu, na pia iliwabidi wafanye kazi katika shamba lao. Joseph aliomba kwamba Baba wa Mbinguni angemtuma mtu kumsaidia kutafsiri Kitabu cha Mormoni.
Saints, 1:56, 58
Mbali sana huko New York, Oliver Cowdery, mwalimu kijana wa shule, alikuwa akiishi na wazazi wa Joseph Smith. Oliver aliwafundisha wadogo zake Joseph wa kiume na wa kike.
Saints, 1:58–59.
Oliver alisikia kuhusu Joseph na mabamba ya dhahabu. Alikuwa mdadisi. Alizungumza na wazazi wa Joseph. Walimwambia Oliver kwamba Joseph alikuwa akifanya kazi ya Mungu.
Saints, 1:59
Sasa Oliver alikuwa mdadisi zaidi. Wazazi wa Joseph walimwambia Oliver kwamba alipaswa kusali na kujua mwenyewe kama ilikuwa kazi ya Mungu. Hivyo usiku mmoja, Oliver alisali kwa moyo wake wote. Mungu alimpa amani akilini mwake. Oliver alijua kwamba Joseph Smith alikuwa mtumishi wa Mungu. Alihisi kwamba alipaswa kumsaidia Joseph.
Saints, 1:60
Wakati mwaka wa shule ulipomalizika, Oliver alikwenda kukutana na Joseph na Emma. Joseph na Oliver walichelewa kulala wakizungumza kuhusu mabamba ya dhahabu na kazi ya Mungu.
Saints, 1:60
Oliver alisema angeandika wakati Joseph akitafsiri. Alipenda kile alichokuwa akijifunza kuhusu Yesu. Pia alikuwa na maswali na alitaka imani imara.
Saints, 1:61
Kupitia Nabii Joseph, Bwana alimpa Oliver ujumbe. Alimwambia Oliver akumbuke usiku aliokuwa amesali. Mungu alikuwa amempa amani. Ni Mungu pekee aliyejua kuhusu sala hii. Imani ya Oliver ikawa imara zaidi. Aliendelea kumsaidia Joseph, na Bwana alimfundisha mambo mengi kuhusu jinsi Mungu anavyozungumza nasi.
Mafundisho na Maagano 6:14–24; 8:1–3; 9:7–9; Saints, 1:62–64