“Utangulizi,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Utangulizi,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Introduction
Utangulizi
Welcome to EnglishConnect!
Karibu kwenye EnglishConnect!
EnglishConnect huleta watu pamoja ambao wanatafuta kupanua fursa zao kupitia kujifunza Kiingereza. Sisi sote tunatokea katika asili tofauti na kuongea lugha tofauti. Tunaweza kuwa na uwezo wa Kiingereza wa viwango tofauti, lakini pamoja tunaweza kufikia malengo yetu.
Why Are You Learning English?
Je, ni kwa Nini Wewe Unajifunza Kiingereza?
Kuwa na dhumuni dhahiri kunaweza kukusaidia kufokasi na kuwa na motisha. Acha tufikirie kwa nini wewe unajifunza Kiingereza. Je, wewe unatumaini la kupata ajira bora? Je, unahitaji kujifunza Kiingereza ili kuendeleza elimu yako? Chukua muda kuandika sababu zako za kujifunza Kiingereza.
Ninataka kujifunza Kiingereza kwa sababu:
Kujifunza Kiingereza kunaweza kuongeza fursa zako za elimu, ajira, huduma na urafiki. EnglishConnect inaweza kukusaidia kufikia malengo yako.
What Is EnglishConnect?
EnglishConnect ni Nini?
EnglishConnect ni mpango wa kipekee wa kujifunza Kiingereza unaotolewa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. EnglishConnect imesanifiwa ili kukusaidia wewe kukuza ujuzi wa Kiingereza katika mazingira ya imani, urafiki na ukuaji. Hiyo humaanisha hautafanya hivyo peke yako. Utajifunza pamoja na wengine na kusaidiana na kuhimizana. Pia utaweza kukuza imani yako kwamba Mungu anaweza kukusaidia kujifunza.
EnglishConnect inajumuisha madaraja mengi. EnglishConnect 1 na 2 zinawasaidia wanafunzi kukuza ujuzi wa msingi wa Kiingereza. EnglishConnect 3 inawaandaa wanafunzi kwa ajili ya nafasi za elimu—hasa BYU-Pathway Worldwide. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu BYU–Pathway katika byupathway.org. Jifunze zaidi kuhusu EnglishConnect katika englishconnect.org.
What Makes EnglishConnect Unique?
Ni nini Huifanya EnglishConnect kuwa ya Kipekee?
Katika EnglishConnect, tunakuza ujuzi wa Kiingereza katika mazingira ya imani, urafiki na ukuaji.
Faith
Imani
Katika EnglishConnect, tunajifunza kwa kusoma na kwa imani. Kila somo huanza na kanuni ya kujifunza. Hizi ni kanuni za kiroho ambazo zinatusaidia sisi kumtegemea Mungu kuongeza uwezo wetu kwa kujifunza. Imani uliyonayo kuhusu uwezo wako wa kujifunza utakuwa na matokeo makubwa kwenye juhudi na matokeo yako. Kanuni za kujifunza zinaweza kukusaidia wewe kuelewa uwezekano wako halisi na uwezo wa Mungu wa kukusaidia. Zifuatazo ni kanuni utakazojifunza:
Kanuni za kujifunza ni kauli za kweli. Unaweza kusema kauli hizi kwako mwenyewe wakati unapohitaji motisha au kuhimizwa. Unapotumia kanuni hizi, uwezo wako wa kujifunza utaongezeka. Utajua kwamba kwa msaada wa Mungu, unaweza kufikia malengo yako.
Fellowship
Urafiki
Sehemu muhimu ya uzoefu wa EnglishConnect ni kujifunza pamoja na wengine. Makundi ya EnglishConnect wanapendana, wanasaidiana na kuinuana. Mikutano yako ya kikundi ni mahali salama pa kufanya mazoezi ya kuzungumza na kufanya makosa. Kushiriki katika kundi la EnglishConnect kunaweza kukusaidia kubaki kuwa na motisha na kujenga marafiki.
Growth
Ukuaji
EnglishConnect ni zaidi ya mpango tu wa kujifunza Kiingereza. Bila kujali pale unapoanzia, uzoefu utakaopata utakusaidia kuwa mwanafunzi bora. Utapata fursa za:
-
Kufanya mazoezi ya Kiingereza kila siku.
-
Kufuatilia maendeleo yako.
-
Kujifunza pamoja na wengine.
-
Kusali kwa Mungu kwa ajili ya msaada wa kufikia malengo yako.
What Will I Do in EnglishConnect?
Je, Nitafanya Nini katika EnglishConnect?
Katika EnglishConnect, utajifunza binafsi, utafanya mazoezi ya kuzungumza pamoja na kikundi na utafanya mazoezi ya kila siku. Kila somo katika kitabu cha kiada cha mwanafunzi wa EnglishConnect limegawanywa katika sehemu mbili—“Kujifunza Binafsi”na “Kikundi cha Mazungumzo.”
Personal Study
Kujifunza Binafsi
Sehemu ya “Kujifunza Binafsi” hukuandaa kwa ajili ya kundi lako la mazungumzo. Katika “Kujifunza Binafsi,” utakamilisha shughuli zifuatzo:
Study the Principle of Learning
Jifunze Kanuni ya Kujifunza
Kila somo linajumuisha kanuni ya kujifunza. Hizi ni kanuni za kiroho ambazo zinakusaidia kufanya ubia na Mungu katika kujifunza Kiingereza. Kabla ya kundi lako la mazungumzo, soma kanuni ya kujifunza, tafakari maswali na uandike mawazo yako.
Memorize Vocabulary
Kariri Msamiati
Jifunze maana na matamshi ya kila neno. Tumia msamiati kufanyia mazoezi mipangilio. Unaweza pia kuangalia maneno ya msamiati ambayo yanaweza kutumika katika mpangilio.
Practice the Patterns
Fanyia Mazoezi Mpangilio
Anza kwa kukariri mipangilio ya sentensi. Kisha tumia mipangilio ili kutengeneza maswali na majibu yako mwenyewe. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari kwa maneno mengine kutoka kwenye orodha ya msamiati. Endelea kufanya mazoezi kwa sauti mpaka unapoweza kutumia mipangilio kwa kujiamini kwa kuuliza na kujibu maswali.
Conversation Group
Kikundi cha Mazungumzo
Sehemu ya “Kikundi cha Mazungumzo” hujumuisha shughuli utakazotumia kujifunza pamoja na wengine. Katika “Kikundi cha Mazungumzo,” unakamilisha shughuli zifuatzo:
Discuss the Principle of Learning (20–30 minutes)
Jadili Kanuni ya Kujifunza (dakika 20–30)
Katika kikundi chako, someni na mjadili kanuni ya kujifunza. Hii ni fursa ya kushiriki na kujifunza kutoka kwa wengine.
Activities
Shughuli
Katika shughuli za 1, 2 na 3, tumia msamiati na mipangilio ya sentensi ili kuwa na mazungumzo yenye maana. Shughuli hizi hukusaidia kupiga hatua kutoka kwenye mazoezi ya marudio hadi kubuni mazungumzo yako mwenyewe. Kila shughuli hukuandaa kwa ajili ya shughuli inayofuata.
Activity 1: Practice the Patterns (10–15 minutes)
Shughuli ya 1: Fanyia Mazoezi Mipangilio (dakika 10–15)
Katika shughuli ya 1, pitia tena msamiati na mipangilio uliyojifunza katika kujifunza binafsi. Lengo lako ni kutumia mipangilio ili kusema na kuelewa maswali na majibu rahisi.
Activity 2: Create Your Own Sentences (10–15 minutes)
Shughuli ya 2: Buni Sentensi Yako Mwenyewe (dakika 10–15)
Katika shughuli ya 2, fokasi katika kutumia mipangilio kwa kubuni sentensi zako mwenyewe. Kuwa mbunifu. Lengo ni kutumia mipangilio kubuni maswali na majibu mengi kadiri unavyoweza.
Activity 3: Create Your Own Conversations (15–20 minutes)
Shughuli ya 3: Buni Mazungumzo Yako Mwenyewe (15–20)
Katika shughuli ya 3, fanya mazoezi ya mazungumzo katika hali halisi ya maisha. Malengo yako ni kuwa na mazungumzo ya maana ukitumia Kiingereza ulichojifunza.
Evaluate (5–10 minutes)
Tathmini (dakika 5–10)
Mwisho wa kila kikundi cha mazungumzo, tathmini maendeleo yako kwenye shabaha ya somo. Tumia “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi” ili kutathmini juhudi zako katika kujifunza binafsi, na kuweka malengo ya kuboresha. Chukua muda kusherehekea maendeleo yako na juhudi zako.
Daily Practice
Mazoezi ya Kila Siku
Ili kujifunza Kiingereza, unahitaji kukuza tabia ya kufanya mazoezi kila siku. Kama nyongeza ya muda wa kujifunza uliopangwa, tafuta njia ya kubadili shughuli zako za kila siku kwa kufanya shughuli za Kiingereza. Kwa mfano, wakati wa kusikiliza muziki, sikiliza kwa Kiingereza. Wakati unapoangalia sinema, angalia kwa Kiingereza au weka maandishi ya Kiingereza. Wakati wowote unaposubiria mahali fulani, fanya mazoezi ya mazungumzo ya Kiingereza katika akili yako. Wakati unaposali, sema mengi unavyoweza kwa Kiingereza. Kitu muhimu cha mazoezi ya kila siku ni kutumia Kiingereza katika shughuli za kawaida.
Pia unaweza kukamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources na katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect.
Unapokamilisha shughuli za kujifunza binafsi kwa ajili ya kila somo na mazoezi ya kila siku, utajifunza upesi na kujiandaa vyema kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo. Tumia “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi” kilichojumuishwa hapo mwisho wa utangulizi huu kufuatilia juhudi zako na malengo yako.
Remember This
Kumbuka Hili
Unapokamilisha shughuli za kujifunza binafsi, fanya mazoezi ya Kiingereza kila siku, na kushughulika kikamilifu katika kikundi chako cha Mazungumzo, utakuza ujuzi wa kuzungumza Kiingereza. Cha muhimu zaidi, unapotumia kanuni ya kujifunza na kusali kwa ajili ya msaada wa Mungu, Yeye anaweza kukusaidia kufikia malengo yako sasa na katika siku zijazo.