“Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Kifuatiliaji,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Personal Study Tracker
Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi
Andika madhumuni yako ya kujifunza Kiingereza.
Madhumuni: Ninataka kujifunza Kingereza kwa sababu:
Unaweza kuboresha uwezo wako wa kujifunza kwa kufuatilia juhudi zako na kuweka malengo. Tumia “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi” ili kufuatilia juhudi zako. Baada ya kila somo, weka lengo rahisi. Sherehekea maendeleo yako; kila juhudi hukusogeza karibu zaidi na lengo lako.
Juhudi Ndogo
Juhudi ya Wastani
Juhudi Kubwa
“Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi” kinachoweza kuchapishwa
Example
Mfano
Lesson |
Study the Principle of Learning |
Memorize Vocabulary |
Practice the Patterns |
Practice Daily |
My Goal |
---|---|---|---|---|---|
Lesson 1 | Study the Principle of Learning
| Memorize Vocabulary
| Practice the Patterns
| Practice Daily
| My Goal Soma Utangulizi. Kamilisha sehemu ya “Kujifunza Binafsi” kwa ajili ya somo la 2. |
Lesson 2 | Study the Principle of Learning
| Memorize Vocabulary
| Practice the Patterns
| Practice Daily
| My Goal Soma kanuni ya kujifunza kabla ya somo. |
Lesson 3 | Study the Principle of Learning
| Memorize Vocabulary
| Practice the Patterns
| Practice Daily
| My Goal Ninaposali, nitatumia maneno ya msamiati mpya wa Kiingereza. |
Study Suggestions
Mapendekezo ya Kujifunza
Fikiria kutumia mapendekezo yaliyo hapo chini ili kuboresha kujifunza kwako.
Study the Principle of Learning
Soma Kanuni ya Kujifunza
-
Sali. Anza na maliza kujifunza kwako kwa sala. Mwombe Mungu akusaidie kuelewa na kutumia kanuni hii.
-
Msikilize Roho. Kuwa makini na mawazo na hisia zako, hata kama zinaonekana hazihusiani na kile unachokisoma. Andika mawazo na hisia zako. Fanya kile ambacho Roho anakualika kufanya.
-
Andika maneno na virai vyenye mwongozo. Unaweza kupata maneno na virai fulani ambavyo vinahusika kibinafsi, kukupa mwongozo na kukuhamasisha. Viandike mahali utakapoviona. Viweke kwenye kioo chako au kwenye simu yako.
-
Tumia kanuni ya kujifunza. Fikiria jinsi unavyoweza kutumia kanuni ya kujifunza, nukuu na maandiko katika maisha yako. Andika kile unachojifunza unapotumia kanuni ya kujifunza.
-
Soma zaidi. Soma maandiko au mahubiri ya mkutano mkuu yanayohusiana na kanuni ya kujifunza.
-
Jifunze msamiati mpya. Chagua baadhi ya maneno kutoka kwenye kanuni ya kujifunza ambayo unataka kujifunza kwa Kiingereza. Angalia maneno. Zungumza na wanafunzi wengine kuhusu kile maneno na virai vinamaanisha kwao.
Memorize Vocabulary
Kariri Msamiati
-
Fokasi kwenye maana na matamshi. Fanya mazoezi ya kurudia maneno kwa sauti na kufikiria maana ya neno. Jifunze matamshi ya kila neno na ufanye mazoezi mpaka ulitamke vizuri. Endelea mpaka unapoweza kusema neno kwa kujiamini na kujua kile linachomaanisha.
-
Fanya mazoezi kwa kadi za kunyanyuliwa. Tumia kadi za muhtasari (au aplikesheni) ili kutengeneza kadi za kunyanyuliwa. Andika neno kwenye upande mmoja na maelezeo, tafsiri au picha kwenye upande ule mwingine. Marudio ni muhimu katika kukariri msamiati.
-
Fanyia mazoezi maneno katika sentensi. Fanyia mazoezi kusema neno unalojifunza katika sentensi. Unaweza kutumia mipangilio ya sentensi ili kufanyia mazoezi maneno unayojifunza.
-
Tumia neno. Fikiria hali ambapo ungeweza kutumia neno hilo katika maisha yako ya kila siku. Fanyia mazoezi hali hiyo mpaka unapoona ni kawaida kutumia neno hilo. Unapokwenda kazini, shuleni, dukani au sehemu zingine, tumia maneno katika akili yako unapoelezea vitu.
-
Tambua maneno. Tafuta na sikiliza kwa ajili ya maneno mapya unapoendelea na shughuli za siku yako. Unaweza kujifunza kutoka kwenye sinema, maonyesho ya runinga, vitabu, podikasti au nyimbo. Andika maneno mapya.
-
Jifunze zaidi. Tumia kamusi ili kujifunza zaidi kuhusu maneno mapya. Jifunze maana, aina za maneno, sehemu za neno, matamshi na mifano ya sentensi.
-
Fanya Marejeo. Chukua muda kila mara kufanyia marejeo maneno uliyojifunza hapo awali. Hii itakusaidia kuona ni kiasi gani umejifunza na haujasahau maneno.
Practice the Patterns
Fanyia Mazoezi Mipangilio
-
Fokasi kwenye maana na ufasaha. Fanyia mazoezi kurudia sentensi kutoka kwenye mpangilio kwa sauti na ufikirie maana ya sentensi hiyo. Endelea mpaka unapoweza kusema sentensi hiyo bila ukakasi, kwa kujiamini na kujua kile inachomaanisha.
-
Jirekodi mwenyewe. Jirekodi mwenyewe ukiuliza na kujibu maswali kwenye simu yako. Sikiliza rekodi na kuwa msikivu kwa ufasaha wako na matamshi yako.
-
Fanya mazoezi na mwenzako. Fanya mazoezi na rafiki yako ukitumia mipangilio ya kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kufanya mazoezi ana kwa ana au kwenye simu. Fanya mazoezi ukitumia mipangilio ya kuandika ujumbe kwa rafiki.
-
Fikiria na zungumza kuhusu mipangilio. Je, unagundua nini kuhusu jinsi gani Kiingereza hutumika? Je, ni kwa jinsi gani Kiingereza ni sawa na lugha yako? Je, ni kwa jinsi gani Kiingereza ni tofauti na lugha yako? Je, ni kwa jinsi gani ungeweza kutumia mpangilio kutoka kwenye somo katika hali tofauti?
-
Tumia nyenzo zingine Vitabu vya sarufi, aplikesheni, tovuti na wanafunzi wengine wanaweza kukusaidia kujifunza zaidi kuhusu mipangilio ya sarufi za Kiingereza.
-
Tambua mipangilio. Tafuta na sikiliza kwa ajili ya mipangilio unayojifunza wakati unaposoma na kusikiliza Kiingereza.
Practice Daily
Fanyia Mazoezi Kila Siku
-
Weka utaratibu. Panga lini na wapi utakapojifunzia kila siku na ufanye hivyo. Ili kukumbuka, andika lengo lako katika kauli ya “lini”. Kwa mfano, “Wakati mimi , nina .” Hapa kuna baadhi ya mifano: “Wakati nikiwa kwenye basi, mimi nitafanya marejeo ya msamiati.” , “Wakatii nikipika chakula cha jioni, mimi nitaelezea kile ninachofanya kwa Kiingereza.”; na “Wakati nikisali, mimi nitasema mengi ninavyoweza kwa Kiingereza
-
Fanya shughuli za kila siku kwa Kiingereza. Tafuta njia za kubadili lugha yako ya asili kwa Kiingereza katika shughuli zako za kila siku. Kwa mfano, wakati wa kusikiliza muziki, sikiliza kwa Kiingereza. Mawazo mengine: tazama sinema kwa Kiingereza au zilizo na maandishi ya Kiingereza, badilisha mipanglio ya simu yako kwa Kiingereza na usome maandiko kwa Kiingereza.
-
Soma. Soma mara nyingi uwezavyo kwa Kiingereza. Soma maandiko, mahubiri ya mkutano mkuu, majarida, blogi, habari na taarifa zingine kwa Kiingereza.
-
Sikiliza. Sikiliza kwa makini sana kadiri uwezavyo. Sikiliza podikasti, maandiko, hotuba, mawasilisho, video, maonyesho ya Runinga au sinema.
-
Zungumza. Tafuta marafiki, familia au wafanyakazi wenza na ufanye mazoezi ya kuzungumza nao. Shiriki kile ambacho umekuwa ukijifunza na kutenda ili kufanyia mazoezi Kiingereza. Unda kundi la mazungumzo na utume mihutasari ya sauti.
-
Andika. Tafuta fursa za kuandika kwa Kiingereza. Anza kuandika shajara ya kila siku au unda kundi la mazungumzo. Tumia sentensi na msamiati unaojifunza.
-
Kamilisha shughuli za somo. Fanya shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect.