Kujifunza Kiingereza
Somo la 2: Salamu na Utambulisho


“Somo la 2: Salamu na Utambulisho,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)

“Somo la 2,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi

wanaume wawili wakitabasamu

Lesson 2

Greetings and Introductions

Lengo: Nitajifunza kuwasalimia wengine na kusema kule mahali mtu huyo anakotokea.

Personal Study

Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.

ikoni a
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

Tumia imani katika Yesu Kristo.

Jesus Christ can help me do all things as I exercise faith in Him.

Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya mambo yote ninapoonyesha imani Kwake.

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Mungu alimtuma Yesu, kutufundisha na kutusaidia. Yesu hutufundisha jinsi ya kuishi kweli kwenye kile tunachotaka kuwa kama watoto wa Mungu. Yesu ana uwezo wa kutusaidia kushinda udhaifu wetu na changamoto zetu. Yeye alitufundisha:

“Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” (Mathayo 17:20).

Unaweza kuhisi kwamba kujifunza Kiingereza ni mlima mkubwa—kazi isiyowezekana. Lakini unapofanya hata kiasi kidogo cha imani katika Yesu Kristo, imani yako itakuwa. Imani yako inayokua katika Yeye itakusaidia kushinda changamoto zako.

Yesu akizungumza na Mariamu

Ponder

  • Ni baadhi ya changamoto gani unazoweza kukabiliana nazo katika kujifunza Kiingereza?

  • Ni baadhi ya njia gani unazoweza kukuza imani yako katika Yesu Kristo?

ikoni b
Memorize Vocabulary

Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Mungu atakusaidia kukumbuka kile unachojifunza unapofanya vyema kujifunza.

I

Mimi

you

wewe

we

sisi

they

wao

he

yeye

she

yeye

I am/I’m

Mimi ni

you are

wewe ni

we are

sisi ni

they are

wao ni

he is

yeye ni

she is

yeye ni

How are you?

“Hujambo?”

Nice to meet you.

“Nafurahi kukutana nawe.

country

nchi

what

nini

where

wapi

Adjectives

fine

vyema

OK

SAWA

Nouns

Japan

Japani

Kenya

Kenya

Mexico

Mexico

ikoni c
Practice Pattern 1

Kiingereza kina mipangilio mingi. Kwa mpangilio mmoja na maneno machache ya msamiati, unaweza kuunda idadi kubwa ya sentensi! Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”

Q: How are you?A: I’m (adjective), thanks.

Questions

swali la mpangilio wa 1 hujambo

Answers

jibu la mpangilio wa 1 Mimi kivumishi, asante

Examples

wanawake wawili wakizungumza baada ya darasa

Q: How are you?A: I’m fine, thanks.

Q: Hi, how are you?A: I’m OK, thanks.

ikoni d
Practice Pattern 2

Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Kama kitu fulani kinachanganya, sali kwa ajili ya msaada na uendelee kufanyia kazi. Mungu atakusaidia.

Q: Where are you from?A: I’m from (noun).

Questions

swali la mpangilio wa 2 unatokea wapi

Answers

jibu la mpangilio wa 2 mimi natokea nomino

Examples

mwanaume mzee akitabasamu

Q: Where are you from?A: I’m from Mexico.

Q: Where are they from?A: They are from Japan.

Q: Where is she from?A: She is from Kenya.

ikoni e
Use the Patterns

Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.

Additional Activities

Kamilisha shughuli za somo na upimaji mtandaoni kwenye englishconnect.org/learner/resources au katika Kitabu cha Kazi cha EnglishConnect 1.

Act in Faith to Practice English Daily

Unahitaji kuwa thabiti, mazoezi ya kila siku ya kuzungumza lugha mpya. Kuwa na lengo kunaweza kukusaidia. Lengo lako halihitaji kuwa lenye utata. Kwa kweli, malengo rahisi kwa kawaida yanafaa sana kwa sababu yatakusaidia wewe kukuza desturi ya kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Endelea Kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku. Tumia “Kifuatiliaji chako cha Kujifunza Binafsi.” Pitia tena lengo lako la kujifunza na utathmini juhudi zako.

Conversation Group

Discuss the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ

(20–30 minutes)

Yesu akizungumza na Mariamu

ikoni ya 1
Activity 1: Practice the Patterns

(10–15 minutes)

Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.

Fanya mazoezi mpangilio wa 1 na mwenzako:

  • Fanya mazoezi kuuliza maswali.

  • Fanya mazoezi kujibu maswali.

  • Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.

Rudia mpangilio wa 2

ikoni ya 2
Activity 2: Create Your Own Sentences

(10–15 minutes)

Part 1

Jitambulishe mwenyewe kwa mwenzako Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.

Example
  • A: Hi! How are you?

  • B: I’m OK, thanks.

  • A: My name is . I’m from . What’s your name?

  • B: My name is . I’m from .

Part 2

Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila mtu. Chukueni zamu.

Example: Talia, Samoa
msichana akitabasamu akiwa ufukweni
  • A: What’s her name?

  • B: Her name is Talia.

  • A: Where is she from?

  • B: She is from Samoa.

Image 1: Marco, Italy

mwanaume akitabasamu akiwa na shati la hudhurungi

Image 2: Nat, Canada

mwanamke akitabasamu akiwa na shati jeusi

Image 3: Sam, Mexico

mwanaume mzee akitabasamu

ikoni 3
Activity 3: Create Your Own Conversations

(15–20 minutes)

Fanya Igizo. Mwenza A anachagua kuwa mtu mmoja kutoka kwenye orodha. Mwenza B anauliza maswali. Ili kupata kumjua Mwenza B. Badilisha nafasi.

  • Greta, Germany

  • Louis, France

  • Ji Hoon, Korea

  • Li Min, China

  • Luna, Peru

  • Pia, Chile

  • Dima, Russia

  • Avi, India

  • Kisi, Ghana

Example

  • A: Hi! How are you?

  • B: I’m fine, thanks.

  • A: My name is Avi. What’s your name?

  • B: My name is Kisi. I’m from Ghana. Where are you from?

  • A: I’m from India. Nice to meet you, Avi.

Evaluate

(5–10 minutes)

Tathmini maendeleo yako juu ya malengo na juhudi zako za kufanyia mazoezi Kiingereza kila siku.

Evaluate Your Progress

I can:

  • Greet someone and ask how they are.

    Msalimie mtu na umuulize hali yake.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Introduce myself and say where I’m from.

    Jitambulishe mwenyewe na usema kule unakotokea.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha
  • Ask people’s names and where they are from.

    Waulize watu majina yao na kule wanakotokea.

    uso wa kawaida, uso wa kuridhika, uso wa furaha

Evaluate Your Efforts

Tathmini juhudi zako za:

  1. Kusoma kanuni ya kujifunza.

  2. Kukariri msamiati.

  3. Kufanyia mazoezi mipangilio.

  4. Kufanya mazoezi kila siku.

Weka lengo. Fikiria mapendekezo ya kujifunza katika “Kifuatiliaji cha Kujifunza Binafsi.”

Shiriki lengo lako na mwenzako.

Act in Faith to Practice English Daily

Anza leo ili kuongeza imani yako. Kupitia imani yako, Yesu Kristo ataongeza uwezo wako wa kuhamisha milima katika maisha yako [ona 1 Nefi 7:12] ingawa changamoto zako za kibinafsi zinaweza kuonekana kama Mlima Everest” (Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 102–3).