“Habari Binafsi,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 3,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 3
Personal Information
Lengo: Nitajifunza kuuliza na kujibu maswali kuhusu habari binafsi.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Take Responsibility
Wajibika
I have the power to choose, and I am responsible for my own learning.
Nina uwezo wa kuchagua, na ninawajibika kwa ajili ya kujifunza kwangu mwenyewe.
Wewe ni mtoto wa Mungu na unao uwezo wa kuchagua na kutenda kwa ajili yako mwenyewe. Uwezo huu huitwa haki ya kujiamulia. Lehi nabii katika Kitabu cha Mormoni, anatufundisha kwamba sisi si kama mawe, tunasubiria mtu fulani atubadilishe na kutuhamisha. Sisi ni mawakala ambao tunaweza kuamua kwa ajili yetu wenyewe nini tunaamini, nini tutafanya, na ni nani tutakuwa. Lehi alifundisha:
“[Mungu] na ameumba vitu vyote, … vitu vya kutenda na vitu vya kutendewa. … Kwa hivyo, Bwana Mungu amemruhusu mwanadamu kujitendea mwenyewe” (2 Nefi 2:14, 16).
Unaweza kuchagua kujifunza na kuwa bora. Mwalimu wako na wanafunzi wengine katika kikundi chako cha mazungumzo wanaweza kukusaidia, lakini mwishoni, ni chaguzi zako ambazo zitakuwa na matokeo makubwa juu ya kujifunza kwako. Unaweza kujitendea mwenyewe katika kufanya mazoezi ya Kiingereza kila siku. Wakati matatizo yanapojitokeza, tafuta suluhisho. Umepatiwa haki ya kujiamulia—uwezo kutoka kwa Mungu wa kutenda. Unaweza kuwajibika kwa ajili ya kujifunza kwako wewe mwenyewe.
Ponder
-
Inamaanisha nini kuwa “wakala” na kuwajibika kwa ajili ya kujifunza kwako mwenyewe?
-
Je, ni vitu gani ambavyo vinafanya iwe vigumu kujifunza Kiingereza kila siku?
-
Je, unaweza kufanya nini ili kujitendea na si kutendewa unapojifunza Kiingereza kila siku?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno mapya katika mazungumzo au katika ujumbe unaotuma kwa mtu ambaye anajua Kiingereza.
their |
yao |
name@email.com |
jina@baruapepe.com |
@ (at) |
@ (kwa) |
. (dot) |
. (nukta) |
When is … ? |
Ni lini … ? |
Nouns 1
anniversary |
maadhimisho |
birthday |
siku ya kuzaliwa |
Nouns 2
address |
anwani |
|
barua pepe |
phone number |
nambari ya simu |
Days
January 1st |
Januari 1 |
February 2nd |
Februari 2 |
March 3rd |
Machi 3 |
April 4th |
Aprili 4 |
May 5th |
Mei 5 |
June 6th |
Juni 6 |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: When is your (noun 1)?A: My (noun 1) is (day).
Examples
Q: When is your birthday?A: My birthday is July 8th.
Q: When is his anniversary?A: His anniversary is April 3rd.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali.
Q: What is your (noun 2)?A: My (noun 2) is ().
Examples
Q: What is your email?A: My email is adam@email.net.
Q: What is their address?A: Their address is 1000 Central Parkway.
Q: What is his phone number?A: His phone number is 706-863-9400.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Piitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanyia mazoezi mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila mtu. Chukueni zamu.
Example: Mei
-
Birthday: July 1
-
Phone Number: 832-351-9721
-
Address: 278 Main Street
-
Email: mei@email.net
-
A: When is Mei’s birthday?
-
B: Her birthday is July 1st.
-
A: What is Mei’s email?
-
B: Her email is mei@email.net.
Image 1: Hugo
-
Birthday: October 9
-
Phone Number: 919-345-3986
-
Address: 620 Oak Road
-
Email: hugo@email.com
Image 2: Mari
-
Birthday: August 2
-
Phone Number: 208-377-1984
-
Address: 966 Sunny Drive
-
Email: mari@email.net
Image 3: Jean
-
Birthday: March 7
-
Phone Number: 356-225-8786
-
Address: 22 First Street
-
Email: jj@email.com
Image 4: Talia
-
Birthday: January 10
-
Phone Number: 660-743-5522
-
Address: 1620 Pine Road
-
Email: talia5@email.net
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Fanya igizo la kila hali. Mtu mmoja ni mwenza A. Mtu mwingine ni mwenza B. Badilishaneni nafasi.
Example
Hali: Mwenza A hufanya kazi katika uwanja wa ndege. Mwenza B anakaguliwa kwa ajili ya safari ya ndege. Mwenza A anahitaji jina la mwenza B, siku ya kuzaliwa na nambari ya simu.
-
A: Hello! Welcome to the airport. What is your name?
-
B: My name is Maria.
-
A: When is your birthday?
-
B: My birthday is January 2nd.
-
A: OK. And what is your phone number?
-
B: My phone number is 208-991-4433.
-
A: Thank you!
Situation 1:
Mwenza A ni daktari. Mwenza B yuko hospitalini. Daktari anahitaji jina na mgonjwa, siku ya kuzaliwa, nambari ya simu, anwani na barua pepe.
Situation 2:
Mwenza A na mwenza B, wako kwenye kituo cha treni. Mwenza B anaanza mazungumzo na anaomba nambari ya simu na baruapepe ya Mwenza A
Situation 3:
Mwenza A ni bosi. Mwenza B ni mwajiriwa mpya. Bosi anahitaji jina, nambari ya simu, anwani na barua pepe ya mwajiriwa mpya.
Situation 4:
Mwenza A ni katibu wa chuo kikuu. Mwenza B ni mwanafunzi mpya anayejisajili katika madarasa katika chuo kikuu. Katibu anahitaji jina la mwanafunzi mpya, siku ya kuzaliwa, nambari ya simu na barua pepe.