“Somo la 6: Familia,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 6,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 6
Family
Shabaha: Nitajfunza kuzungumza kuhusu ni watu wangapi wako katika familia.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: You Are a Child of God
Wewe ni Mtoto wa Mungu
I am a child of God with eternal potential and purpose.
Mimi ni mtoto wa Mungu aliye na uwezekano na kusudi la milele.
Mungu ni Baba wa roho zetu, kwa hiyo tunamwita Yeye Baba wa Mbinguni. Baba yako wa Mbinguni anakupenda. Yeye anakutaka uelewe utambulisho wako wa kweli na uhusiano wako na Yeye. Kupitia manabii Wake, Mungu hutufundisha sisi asili yetu ya kweli. Paulo, nabii katika Biblia, alifundisha:
“Roho mwenyewe anashuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu” (Warumi 8:16).
Mafundisho ya Paulo ni ya kweli kwako. Wewe ni binti au mwana wa Baba wa Mbinguni mwenye upendo. Unao uwezekano wa milele. Mungu ana kusudi kwa ajili ya maisha yako. Unapomuomba Mungu, Yeye anaweza kukusaidia kuona wewe ni nani na wewe unaweza kuwa nani. Wakati wowote unapokuwa na shaka kuhusu uwezo wako wa kujifunza Kiingereza, kumbuka kwamba wewe ni mtoto wa Mungu. Yeye anakupenda na anataka kukusaidia ukue na uendelee. Wakati wewe unaposali na kuomba msaada Wake, Yeye atakusaidia kujifunza.
Ponder
-
Ni kwa jinsi gani ungeelezea uhusiano kati ya baba mwenye upendo na mtoto wake?
-
Ni jinsi gani kujua wewe una Baba wa Mbinguni mwenye upendo kunagusa hisia zako kuhusu wewe mwenyewe?
-
Ni kwa jinsi gani unaweza kukuza uhusiano wako na Baba wa Mbinguni?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Fikiria hali ambapo ungeweza kutumia neno hili katika mazoezi yako ya kila siku.
family |
familia |
have/has |
ina/ana |
How many … ? |
Ngapi … ? |
There are …/There is … |
Kuna …/Kuna … |
Numbers
1 – one |
1 – moja |
2 – two |
2 – mbili |
3 – three |
3 – tatu |
Nouns
husband |
mume |
wife |
mke |
father (dad) |
baba |
mother (mom) |
mama |
brother/brothers |
kaka/akina kaka |
sister/sisters |
dada/akina dada |
child/children |
mtoto/watoto |
daughter/daughters |
binti/mabinti |
son/sons |
mwana/wana |
boy/boys |
mvulana/wavulana |
girl/girls |
msichana/wasichana |
person/people |
mtu/watu |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: How many (noun) are in your family?A: There are (number) (noun) in my family.
Examples
Q: How many people are in Sam’s family?A: There are four people in his family.
Q: How many sisters are in your family?A: There are two sisters in my family.
Q: How many sons are in your family?A: There is one son in my family.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kutumia mipangilio katika mazungumzo na rafiki. Ungeweza kuzungumza au kutuma ujumbe
Q: How many (noun) do you have?A: I have (number) (noun).
Examples
Q: How many children do you have?A: I have six children.
Q: How many brothers does she have?A: She has three brothers.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Piitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila familia. Sema mara nyingi uwezavyo. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
New Vocabulary
who is |
huyu ni |
Example: Yuka
-
A: Who is Yuka?
-
B: Yuka is the mother.
-
A: How many people are in Yuka’s family?
-
B: There are six people in her family.
-
A: How many children does Yuka have?
-
B: She has three children.
-
A: How many daughters does Yuka have?
-
B: She has two daughters.
-
A: How many sons are in her family?
-
B: She has one son.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Uliza na ujibu maswali kuhusu watu katika familia yako. Sema mara nyingi uwezavyo. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: How many people are in your family?
-
B: There are six people in my family.
-
A: How many sisters do you have?
-
B: I have three sisters.
-
A: How many children does your sister have?
-
B: She has six children.