“Somo la 8: Vitu vya Kawaida vya Kila Siku,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 8,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 8
Everyday Common Items
Shabaha: Nitajifunza kutumia hiki, kile, hivi na vile kuuliza kuhusu vitu vya mtu.
Personal Study
Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Press Forward
Songa Mbele
With God’s help, I can press forward even when I face obstacles.
Kwa msaada wa Mungu, ninaweza kusonga mbele hata wakati ninapokabiliana na vikwazo.
Sisi sote tunakabiliana na changamoto katika maisha. Wakati mwingine changamoto zetu hufanya iwe vigumu kutimiza malengo yetu. Nefi, nabii na kiongozi katika Kitabu cha Mormoni, alipatwa na changamoto nyingi. Alitumia maisha yake yote kuwafundisha na kuwatumikia watu wake. Alijua wangekabiliana na changamoto ngumu, na alitaka kuwasaidia wao kujua jinsi ya kuwa thabiti. Nefi alifundisha:
“Usonge mbele ukiwa na imani imara katika Kristo, ukiwa na mg’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote” (2 Nefi 31:20).
Wewe pia unaweza kusonga mbele. Ili “Kusonga mbele ukiwa imara katika Kristo” humaanisha unaweza kuendelea kujaribu, ukimtumainia Yesu Kristo, hata wakati mambo yawapo magumu. Ukitumainia kwamba Yeye atabariki juhudi zako hata wakati mambo ni magumu au wakati umefanya makosa. Kwa mfano, labda umetambua kwamba wewe unafanya makosa wakati wewe unajaribu kuzungumza Kiingereza. Labda umekuwa na wakati mgumu kukumbuka maneno mapya. Wakati wewe unasonga mbele na kufanya mazoezi kila siku, ukimtumainia Yeye kuwa atakusaidia kujifunza. Bila kujali changamoto unazokabiliana nazo, unaweza kusonga mbele kwa imani.
Ponder
-
Ni njia gani ambazo unaweza “kusonga mbele” katika kujifunza Kiingereza?
-
Nini hukusaidia kuendelea kujaribu wakati mambo ni magumu?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutengeneza kadi za kuandikiapo ili kukusaidia kukariri maneno mapya. Unaweza kutumia karatasi au aplikesheni.
not |
siyo |
this/these |
hiki/hivi |
that/those |
kile/vile |
Nouns
book/books |
kitabu/vitabu |
chair/chairs |
kiti/viti |
clock/clocks |
saa/saa |
computer/computers |
kompyuta/kompyuta |
key/keys |
ufunguo/funguo |
notebook/notebooks |
daftari/madaftari |
pen/pens |
kalamu/kalamu |
pencil/pencils |
penseli/penseli |
phone/phones |
simu/simu |
table/tables |
meza/meza |
wallet/wallets |
pochi/pochi |
watch/watches |
saa ya mkononi/saa za mkononi |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: What is this?A: This is a (noun).
Examples
Q: What is this?A: This is a watch.
Q: What are these?A: These are pencils.
Q: What is that?A: That is a key.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kuelewa sheria katika mipangilio. Fikiria kuhusu jinsi Kiingereza kinavyofanana na au ni tofauti na lugha yako.
Q: Is this my (noun)?A: Yes, it is.
Examples
Q: Is this your book?A: No, it is not.
Q: Are those her keys?A: Yes, they are.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2.
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kila kitu katika picha. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: What are those?
-
B: Those are books.
-
A: Are those your books?
-
B: No, they are not my books.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Chagua vitu vitano katika chumba. Vionyeshe kwa mwenzako Uliza na ujibu maswali kuhusu kila kitu. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: What is that?
-
B: That is a phone.
-
A: Is it your phone?
-
B: Yes, it is.