“Somo la 10: Utaratibu wa Kila Siku,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 10,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 10
Daily Routines
Shabaha: Nitajifunza kuzungumza kuhusu utaratibu wa kila siku wa mtu.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: You Are a Child of God
Wewe ni mtoto wa Mungu
I am a child of God with eternal potential and purpose.
Mimi ni mtoto wa Mungu aliye na uwezekano wa kuwa na kusudi la milele.
Wewe ni binti au mwana wa Mungu. Yeye anayo mengi sana anayotaka kukusaidia wewe ujifunze. Yeye anataka kukusaidia wewe ufikie uwezo wa milele. Wakati mwingine hii inaweza kuonekana kama haiwezekani. Katika Biblia, tunasoma kuhusu msichana aliyeitwa Mariamu. Malaika alimtokea na kumwambia kwamba angekuwa mama wa Yesu Kristo, Mwokozi wa kila mmoja. Angeweza kumlea Mwana wa Mungu hapa ulimwenguni kama mtoto wake mwenyewe. Pengine Mariamu alihisi kuzidiwa na kile Baba wa Mbinguni alichomtaka yeye afanye na kuwa, lakini malaika alimwambia:
“Hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu” (Luka 1:37).
Kwa Mungu, lisilowezekana huwa linalowezekana. Mariamu akawa mama wa Mwana wa Mungu. Kama vile Mariamu, Mungu anataka kukusaidia wewe ufikie uwezekano wako na kutimiza madhumuni yako katika maisha. Sali Kwake na muulize Yeye kitu ambacho Yeye anataka wewe ufanye. Fuata mawazo na hisia unazopokea kutoka kwa Roho Wake. Yeye atakuongoza. Pengine unahitaji kujifunza Kiingereza ili upate elimu au ukidhi mahitaji ya familia yako. Kumbuka kwamba “kwa Mungu hakuna lisilowezekana.” Kwa Mungu, wewe unaweza kujifunza Kiingereza. Kwa Mungu, wewe unaweza kufikia uwezekano wako wa kuwa wa milele.
Ponder
-
Unahisi Mungu anataka wewe ufanye nini?
-
Wakati Mungu anapokualika wewe kufanya mambo ambayo unafikiria hayawezekani, ni kwa jinsi gani unaweza kuchagua kutenda kwa imani?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno kutoka kwenye sehemu ya “Memorize Vocabulary” katika mazoezi yako ya kila siku.
daily routine |
utaratibu wa kila siku |
Nouns
morning |
asubuhi |
afternoon |
mchana |
evening |
jioni |
Verbs
brush my teeth/brushes his teeth |
sugua meno yangu/husugua meno yake |
clean the house/cleans the house |
safisha nyumba/husafisha nyumba |
do my hair/does her hair |
chana nywele zangu/huchana nywele zake |
exercise/exercises |
zoezi/mazoezi |
get dressed/gets dressed |
vaa nguo/huvaa nguo |
get ready/gets ready |
jitayarishe/hujitayarisha |
go to bed/goes to bed |
nenda kalale/huenda kulala |
go to school/goes to school |
nenda shule/huenda shule |
go to the store/goes to the store |
naenda dukani/huenda dukani |
go to work/goes to work |
Nenda kazini/huenda kazini |
make breakfast/makes breakfast |
tengeneza kifungua kinywa/hutengeneza kifungua kinywa |
make the bed/makes the bed |
tandika kitanda/hutandika kitanda |
shave/shaves |
nyoa/hunyoa |
take a shower/takes a shower |
oga/huoga |
wake up/wakes up |
amka/huamka |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: Do you (verb) in the (noun)?A: Yes, I (verb) in the (noun).
Examples
Q: Do you exercise in the morning?A: Yes, I exercise in the morning.
Q: Does he make breakfast in the morning?A: No, he makes the bed in the morning.
Q: Does she brush her teeth in the evening?A: Yes, she brushes her teeth in the evening.
Q: Do you go to the store in the morning?A: No, I go to the store in the afternoon.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kutambua mipangilio hii wakati wa mazoezi yako ya kila siku.
Q: What do you do before you (verb)?A: Before I (verb), I (verb).
Examples
Q: What do you do before you make breakfast?A: Before I make breakfast, I exercise.
Q: What does he do after he gets ready?A: After he gets ready, he goes to the store.
Q: What does she do after she makes breakfast?A: She goes to work.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2.
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu shughuli katika kila picha. Chukueni zamu.
Example
-
A: Do you brush your teeth in the morning?
-
B: Yes, I brush my teeth in the morning.
-
A: What do you do after you brush your teeth?
-
B: After I brush my teeth, I get dressed.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Part 1
Mwenza A ni mtu mashuhuri. Mwenza B anamhoji mtu mashuhuri kuhusu utaratibu wake wa kila siku. Sema mengi kadri uwezavyo. Badilishaneni nafasi.
Example
-
A: Do you make your bed in the morning?
-
B: No, I don’t make my bed in the morning.
Part 2
Chagua wanafamilia watatu. Uliza na ujibu maswali kuhusu utaratibu wa kila siku wa kila mtu. Sema mengi kadri uwezavyo. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: What does your sister do before she goes to work?
-
B: Before she goes to work, she does her hair.