“Somo la 11: Shughuli Zangu,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 11,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 11
My Activities
Shabaha: Nitajifunza kuzungumza kuhusu kile mtu anafanya kwa sasa na utaratibu wao wa kila siku.
Personal Study
Jiandae kwa ajili ya kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ
Tumia imani katika Yesu Kristo.
Jesus Christ can help me do all things as I exercise faith in Him.
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya vitu vyote ninapoonyesha imani Kwake.
Nefi, alikuwa nabii katika Kitabu cha Mormoni. Alipokuwa kijana, Nefi na kaka zake waliamriwa kuchukua kitabu kitakatifu. Kitabu hiki kilikuwa muhimu kwa sababu kilifundisha kuhusu mpango wa Mungu na kazi ya Yesu Kristo. Kitabu kilimilikiwa na mtu mwovu aliyeitwa Labani. Nefi na kaka zake walijaribu kukiomba. Labani alisema hapana. Nefi na kaka zake walijaribu kukinunua. Labani alisema hapana na kupora fedha zao zote. Baada ya kushindwa mara mbili, kaka za Nefi walikasirika na walitaka kuacha.
Nefi aliwatia moyo kaka zake kwa kusema: “Twendeni tena Yerusalemu, na tuwe waaminifu kwa kuzishika amri za Bwana; kwani tazama yeye ni mkuu kupita ulimwengu wote” (1 Nefi 4:1).
Tumaini la Nefi katika Mungu lilimsaidia kujaribu mara ya tatu. Mara hii, kwa msaada wa Mungu, alifanikiwa kukipata kitabu kitakatifu. Uzoefu wa Nefi hutufundisha kwamba kujaribu na mara zingine kushindwa ni sehemu ya kutenda jambo gumu. Kujifunza lugha mpya ni vigumu na kunahitaji mamia ya masaa. Labda wewe umejaribu kujifunza Kiingereza hapo awali, na haikwenda vizuri. Labda ulikosa mkutano wako wa kila wiki, au ulisahau kujifunza. Jaribu tena wakati unaposhindwa. Unapotumia imani katika Yesu Kristo, Yeye anaweza kubadilisha kushindwa kuwa ufanisi.
Ponder
-
Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama Nefi na kuendelea kujaribu wakati tunaposhindwa?
-
Ni kwa jinsi gani imani yetu katika Yesu Kristo inatusaidia kujifunza kutokana na kushindwa kwetu?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kutumia maneno mapya katika mazungumzo au katika ujumbe unaoutuma kwa mtu ambaye anajua Kiingereza.
now |
sasa |
Verbs/Verbs + ing
come home/coming home |
njoo nyumbani/ anaenda nyumbani |
do homework/doing homework |
fanya kazi ya masomo nyumbani/ kufanya kazi ya masomo nyumbani |
eat dinner/eating dinner |
kula chakula cha jioni/kula chakula cha jioni |
exercise/exercising |
fanya mazoezi/kufanya mazoezi |
get ready for bed/getting ready for bed |
Jiandae kulala/kujiandaa kulala |
go to bed/going to bed |
nenda kulala/kwenda kulala |
make lunch/making lunch |
tengeneza chakula cha mchana/kutengeneza chakula cha mchana |
pray/praying |
sali/kusali |
relax/relaxing |
pumzika/kupumzika |
take a nap/taking a nap |
lala kidogo/kulala kidogo |
take a walk/taking a walk |
tembea/kutembea |
visit my friends/visiting my friends |
tembelea marafiki zangu/kuwatembelea marafiki zangu |
watch movies/watching movies |
angalia sinema/kuangalia sinema |
work/working |
kazi/kufanya kazi |
Time
morning |
asubuhi |
afternoon |
mchana |
evening |
jioni |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali.
Q: What are you doing now?A: I am (verb + ing).
Examples
Q: What are you doing now?A: I am relaxing.
Q: What are they doing now?A: They are making dinner.
Q: What is he doing now?A: He is visiting his friends.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kufanya shughuli ya 1 na ya 2 za kikundi cha mazungumzo kabla ya kikundi chako kukutana.
Q: When do you (verb)?A: I (verb) in the (time).
Examples
Q: When do you work?A: I work in the morning.
Q: When do they eat dinner?A: They eat dinner in the evening.
Q: When does she do homework?A: She does homework in the afternoon.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Pattern
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi ya mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu watu katika kila picha wanafanya nini sasa hivi. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example 1: Igor
-
A: What is Igor doing now?
-
B: He is eating lunch.
Example 2: Hua and Bao
-
A: What are Hua and Bao doing now?
-
B: They are cooking dinner.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu lini wewe unafanya shughuli iliyoko katika kila picha. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: When do you do homework?
-
B: I do homework in the evening.