“Somo la 12: Muda na Kalenda,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 12,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 12
Time and Calendar
Shabaha: Nitajifunza kuzungumza kuhusu muda na kalenda
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Take Responsibility
Wajibika
I have the power to choose, and I am responsible for my own learning.
Nina uwezo wa kuchagua, na ninawajibika kwa ajili ya kujifunza kwangu mwenyewe.
Wewe ni wakala; una nguvu ya kuchagua na kutenda kwa ajili yako mwenyewe. Kila mara tabia yetu ni kuwasubiri viongozi, walimu, au wengine kutuambia nini cha kufanya. Tunataka wao watupe maelekezo ya hatua kwa hatua. Mungu anatutaka sisi tuelewe kwamba kama watoto Wake tuna nguvu ndani yetu ya kufanya chaguzi na kusonga mbele.
Yeye anaelezea kwa watoto Wake “yawapasa kujishughulisha kwa shauku katika kazi njema, na kufanya mambo mengi kwa hiari yao wenyewe, na kutekeleza haki nyingi; Kwani uwezo u ndani yao, ambamo wao ni mawakala juu yao wenyewe.” Na kadiri wanadamu watakavyofanya mema hawatakosa thawabu zao” (Mafundisho na Maagano 58:27–28)
Uwezo u ndani yako. Unaweza kuwajibikaji kwa ajili ya kujifunza kwako. Kama mwalimu ni mgonjwa na hawezi kuja, unaweza kuchagua kufanya mazoezi pamoja na wanafunzi wengine. Kama hauelewi kitu fulani, unaweza kuomba msaada. Kama unahitaji mawazo kwa ajili ya jinsi ya kujifunza vyema, unaweza kuwauliza wanafunzi wengine katika kikundi chako nini kinachofanya kazi kwao. Una uwezo wa kuchagua na kutenda Kwa Mungu, wewe unaamua utajifundisha nini na kuwa.
Ponder
-
Je, unaamini jukumu lako ni lipi kama mwanafunzi?
-
Unaweza kufanya nini ili kuwajibika kwa kujifunza kwako wewe mwenyewe?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kujifunza maneno zaidi ambayo unaweza kutumia katika mipangilio. Fikiria kutumia kamusi au mfasiri au kumuuliza rafiki.
date |
tarehe |
day |
siku |
time |
muda |
at |
mnamo |
on |
mnamo |
Time
noon |
saa sita mchana |
midnight |
saa sita usiku |
five o’clock/5:00 a.m. |
kumi na moja kamili/11:00 alfajiri |
five thirty/5:30 p.m. |
kumi na moja na nusu/11:30 jioni |
Days
Sunday |
Jumapili |
Monday |
Jumatatu |
Tuesday |
Jumanne |
Wednesday |
Jumatano |
Thursday |
Alhamisi |
Friday |
Ijumaa |
Saturday |
Jumamosi |
Saturday, January 1st |
Jumamosi, Januari 1 |
Verbs
clean the house |
safisha nyumba |
get the mail |
pata barua |
wash the dishes |
osha vyombo |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: What time is it?A: It’s (time).
Examples
Q: What time is it?A: It’s five o’clock.
Q: What day is it?A: It is Sunday.
Q: What day is it?A: It’s February 5th.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kitumia mipangilio katika mazungumzo na rafiki. Ungeweza kuzungumza au kutuma jumbe.
Q: When do you (verb)?A: I (verb) on (day).
Examples
Q: When do they clean the house?A: They clean the house on Monday.
Q: When do you get the mail?A: I get the mail at noon.
Q: When does he wash the dishes?A: He washes the dishes at 5:30 p.m.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali.
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
New Vocabulary
Is it Friday, June 9th? |
Je, ni Ijumaa, Juni 9? |
Tazama kalenda. Chagua siku. Usimwambie mwenzako ni siku gani umechagua. Uliza na ujibu maswali ili kukisia siku hiyo. Chukueni zamu.
Example
-
A: What day is it?
-
B: It’s Wednesday.
-
A: Is it Wednesday, June 7th?
-
B: No.
-
A: Is it Wednesday, June 14th?
-
B: Yes, it’s Wednesday, June 14th.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Part 1
Uliza na ujibu maswali kuhusu ni lini unafanya kitu fulani. Tumia msamiati kutoka kwenye somo hili na somo la 11. Sema mengi kadri uwezavyo. Chukueni zamu. Badilishaneni wenza na mfanye mazoezi tena.
Example
-
A: When do you wake up?
-
B: I wake up at 7:00 a.m.
-
A: When do you visit your friends?
-
B: I visit my friends on Saturday at 5:30 p.m.
Part 2
Uliza na ujibu maswali kuhusu ni lini unasherehekea matukio muhimu. Zungumza kuhusu matukio muhimu kwenye orodha hii au fikiria juu ya matukio mengine muhimu. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.
New Vocabulary
anniversary |
kumbukizi |
celebrate |
sherehekea |
holiday |
sikukuu |
Matukio Muhimu
-
Siku yako ya kuzaliwa
-
Siku ya kuzaliwa ya mwanafamilia
-
Kumbukizi
-
Sikukuu yako pendwa (Krismasi, Siku ya Uhuru, Mwaka Mpya)
Example
-
A: When do you celebrate your sister’s birthday?
-
B: I celebrate my sister’s birthday on December 10th.