“Somo la 15: Kazi na Ajira,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi (2022)
“Somo la 15,” EnglishConnect 1 kwa ajili ya Wanafunzi
Lesson 15
Jobs and Careers
Shabaha: Nitajifunza kuuliza na kujibu maswali kuhusu kazi ya mtu.
Personal Study
Jiandae kwa ajili kikundi chako cha mazungumzo kwa kukamilisha shughuli A hadi E.
Study the Principle of Learning: Exercise Faith in Jesus Christ
Tumia imani katika Yesu Kristo.
Jesus Christ can help me do all things as I exercise faith in Him.
Yesu Kristo anaweza kunisaidia kufanya mambo yote ninapoonyesha imani Kwake.
Wanafunzi wa Yesu Kristo walikuwa kwenye mashua. Upepo ulikuwa mkali, na mawimbi yalikuwa makubwa. Katikati ya hili, walimwona Yesu akitembea kuja kwao juu ya maji. Mmoja wa wanafunzi Wake, Petro, alimuuliza Yesu kama angeweza kutembea kukutana na Yeye juu ya maji. Yesu alimwalika Petro kufanya kitu kilichoonekana kama hakiwezekani.
Biblia hutuambia kile kilichofuatia: “Na wakati Petro aliposhuka kutoka kwenye mashua, alitembea juu ya maji, kwenda kwa Yesu.
“Lakini alipoona upepo mkali, aliogopa; na kuanza kuzama, alipiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
“Na mara moja Yesu akanyoosha mkono wake, na akamshika, na akamwambia, Ewe mwenye imanihaba mbona uliona shaka?” Mathayo 14:29–31.
Hapo mwanzo, Petro alitenda kwa imani, na kimiujiza alianza kutembea juu ya maji. Lakini wakati alipoacha kumtazama Yesu na kuanza kuutazama upepo, yeye alianza kuzama. Kama vile Petro, kama unafokasi juu ya uoga wako, unaweza kutaka kuacha. Badala yake, wewe unaweza kufokasi kwa Yesu. Kujifunza lugha mpya inaweza kuonekana haiwezekani. Tumainia kwamba Yesu Kristo anaweza kukusaidia kufanya mambo ambayo yanaonekana hayawezekani.
Ponder
-
Ni baadhi ya njia gani unaweza kufokasi imani yako katika Yesu Kristo wakati unapozidiwa au kuvunjika moyo?
-
Ni kwa jinsi gani imani yako katika Yesu Kristo imekua tangu ulipoanza EnglishConnect?
Memorize Vocabulary
Jifunze maana na matamshi ya kila neno kabla ya kikundi chako cha mazungumzo. Jaribu kujifunza maneno zaidi ambayo unaweza kutumia katika mipangilio. Fikiria kutumia kamusi au mfasiri au kumuuliza rafiki.
Verbs
build |
jenga |
clean |
safi |
deliver |
peleka |
design |
sanifu |
help |
msaada |
manage |
simamia |
own |
miliki |
sell |
uza |
serve |
hudumu |
Nouns
business/businesses |
biashara/biashara |
building/buildings |
jengo/majengo |
computer/computers |
kompyuta/kompyuta |
customer/customers |
mteja/wateja |
employee/employees |
mfanyakazi/wafanyakazi |
product/products |
bidhaa/bidhaa |
warehouse/warehouses |
bohari/mabohari |
Adjectives
challenging |
enye changamoto |
engaging |
kushughulikia |
fast-paced |
mwendo kasi |
meaningful |
enye maana |
stressful |
enye shinikizo |
Practice Pattern 1
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka kwa kujiamini uweze kuuliza na kujibu maswali. Unaweza kubadilisha maneno yaliyopigiwa mstari na maneno katika sehemu ya “Memorize Vocabulary.”
Q: What do you do for work?A: I (verb) (noun).
Examples
Q: What do you do for work?A: I manage a business.
Q: What does he do for work?A: He sells computers.
Q: What do they do?A: They design buildings.
Practice Pattern 2
Fanya mazoezi ukitumia mipangilio mpaka uweze kwa kujiamini kuuliza na kujibu maswali. Jaribu kuelewa sheria katika mipangilio. Fikiria kuhusu jinsi Kiingereza kinavyofanana na au ni tofauti na lugha yako.
Q: Do you like to (verb) (noun)?A: Yes, it’s (adjective).
Examples
Q: Do you like to manage a business?A: Yes, it’s challenging.
Q: Does he like to sell computers?A: Yes, it’s fast-paced.
Q: Does she like to manage a warehouse?A: No, it’s stressful.
Q: Do they like to help customers?A: Yes, it’s engaging.
Use the Patterns
Andika maswali manne unayoweza kumuuliza mtu. Andika jibu la kila swali. Yasome kwa sauti.
Conversation Group
Activity 1: Practice the Patterns
(10–15 minutes)
Pitia tena orodha ya msamiati pamoja na mwenzako.
Fanya mazoezi mpangilio wa 1 na mwenzako:
-
Fanya mazoezi ya kuuliza maswali.
-
Fanya mazoezi ya kujibu maswali
-
Fanya mazoezi ya mazungumzo ukitumia mipangilio.
Rudia mpangilio wa 2
Activity 2: Create Your Own Sentences
(10–15 minutes)
Tazama picha. Uliza na ujibu maswali kuhusu kazi ya kila mtu. Chukueni zamu.
Example: Paul
-
A: What does Paul do for work?
-
B: He delivers products.
-
A: Does Paul like to deliver products?
-
B: Yes, it’s fast-paced.
Activity 3: Create Your Own Conversations
(15–20 minutes)
Chagua wanafamilia watatu. Uliza na ujibu maswali kuhusu kazi ya kila mtu. Tumia mpangilio na msamiati kutoka kwenye somo hili na somo la 14. Sema mengi kadiri uwezavyo. Chukueni zamu.
New Vocabulary
fix |
rekebisha |
airplane |
ndege |
airport |
uwanja wa ndege |
Example
-
A: Where does your brother work?
-
B: He works at an airport.
-
A: What’s his job?
-
B: He’s a mechanic.
-
A: What does he do for work?
-
B: He fixes airplanes.
-
A: Does he like to fix airplanes?
-
B: Yes, it’s challenging.